Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Ushasema mbinguni.
Lakini duniani tumekatazwa.
Kutokana na maandiko yetu.
Ila kwenye BIBLIA pia pombe imekatazwa.
Aya ya 10.
Kwanini unabishana na maandiko?View attachment 2066806
Basi Yesu Kristo aliitengeneza hapa Duniani.
Ili kutupa mazoezi tukifika Mbinguni tusiwe tunaishangaa shangaa.
Tunaianzia hapa hapa.

Au unasemaje Rafiki
 
Sasa mbona BIBLIA INAKATAA.
Kuwa walevi hawatauona UFALME WA MUNGU
Basi Yesu Kristo aliitengeneza hapa Duniani.
Ili kutupa mazoezi tukifika Mbinguni tusiwe tunaishangaa shangaa.
Tunaianzia hapa hapa.

Au unasemaje Rafiki
Screenshot_20220103-095204.jpg
 
Alifufua wafu Ila yeye alifufuliwa.
MFUFUA KAFUFULIWA[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Soma ayaaaaa ya 14.
Pia alifufua Wafu.
Hii ni kuonesha anayo mamlaka Mbinguni na Duniani.
Screenshot_20220103-095824.jpg
 
Naona umekaririshwa kuwa alichokitengeneza Yesu ni pombe.
Sasa leo ninakukaririsha kitu kingine, bangi, mirungi, cocaine na heroin ni mimea iliyoumbwa na Mungu, na kwakuwa Mungu aliumba vitu vizuri, vipi kwanini wakuu wa dini waseme haramu?
Nchini Kenya, Ethiopia na Somalia Mirungi sio haramu, ni zao halali la Kibiashara.

Bangi sio haramu Majimbo kadhaa ya Marekani, nchi kadhaa za Ulaya, Malawi na South Africa.

Cocaine na Heroin zina madhara makubwa kiafya na imethibitishwa hivyo ila mimea yake Coca na Opium imetumika miaka mingi kama dawa na vichangamsho kabla ya wahuni kuigeuza unga wa biashara haramu.

Kwa nini sigara imethibitika kuwa na madhara makubwa kuliko bangi lakini haijafanywa haramu hadi sasa?!
 
Kwa hyo yesu alikuwa mlevi au alikuwa mnywaji wa pombe?
Sio Walevi tu.
Na Walafi pia.

Hao wanatumia hizo bidhaa bila kufuata taratibu zake.
Ukivimbiwa Pilau siku ya Iddi ni dhambi.

Wengi mnasahau Ulafi mnakumbuka Ulevi tu.
 
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?[emoji1634][emoji1635][emoji482][emoji481][emoji485]
Tunywe tusilewe.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Ukiondoa kifungu hicho,pia kuna neno linasema "kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi,na sio kimuingiacho".
Tunapenda kutafsiri biblia kwa mtindo wa kuhalalisha matamanio yetu.

Inawezekana tafsiri ya hilo neno ni kuwa maneno uyasikiayo hayana najisi kwako bali yale yanayokutoka wewe halafu sisi tukahamishia hilo fungu kwenye ulabu😂

Tusihalalishe dhambi, tuyafanye kwa chaguzi zetu. Umeamua kuzini zini tu hakuna haja ya kutafuta uhalali HAUPO.
 
Tunaangamia kwa kukosa Maarifa

Mithali23
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari;
Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
na mkayafanye mambo yote kwa kiasi,
 
Ili USIWE mlevi unatakiwa unywe bia kuanzia ngapi?
Au alcohol ngapi imewekwa Kama kipimo yaani ukifika hyo alcohol inakuwa umekuwa mlevi.
Kwani ili mtu usivembewe inatakiwa ule chakula cha kiasi gani?
Kulewa inategemea na uwezo wako wa kuimili pombe/kilevi
 
Back
Top Bottom