Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Oooohooo.
Leo Paulo amekuwa sio mtume wa YESU?
Si mnasema kuwa yesu alimtokea Paulo akampa utume?
Leo mnakataa maneno ya Paulo[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Sisi kina nani? Mimi nafuata Amri kumi za Mungu, na maagizo ya Yesu. Kama wengine wanamfuata Paulo siwapangii
 
Haya saaa.
Hao wenzio nao waliofata amri kumi za Mungu wameambiwaje hapo?
Sisi kina nani? Mimi nafuata Amri kumi za Mungu, na maagizo ya Yesu. Kama wengine wanamfuata Paulo siwapangii
Screenshot_20220103-093358.jpg
 
Kwani waefeso Wana biblia yao tofauti na yenu?
Au waefeso sio wakristo?
Waefeso ni waefeso. Kama ni wakristo au sio hiyo sio kazi yangu kujua. Mimi nafuata amri za Mungu alizotoa kwa WATU WOTE

Kama waefeso wameambiwa wasinywe Divai haimaanishi wahaya wameambiwa wasinywe RUBISI au wachaga wasinywe MBEGE.
 
Kwa wale wanaosema Divai iliyotumika katika harusi ya Kana sio kilevi naomba walinganishe mistari hii ya Biblia.


Yohane 2:1-25 BHN

Siku ya tatu kulikuwa na harusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo, naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, “Hawana divai!” Yesu akamjibu, “Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado.” Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.” Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha. Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu. Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.” Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi, akamwambia, “Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!”




Mwanzo 9
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; 21akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. 22Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao


Je, Divai aliyokunywa Nuhu na kulewa si hiyo hiyo iliyotumika katika Harusi ya Kana?
 
Basi nipe andiko ambalo limekuruhusu wewe mmatumbi unywe pombe
Waefeso ni waefeso. Kama ni wakristo au sio hiyo sio kazi yangu kujua. Mimi nafuata amri za Mungu alizotoa kwa WATU WOTE

Kama waefeso wameambiwa wasinywe Divai haimaanishi wahaya wameambiwa wasinywe RUBISI au wachaga wasinywe MBEGE.
 
Haya saaa.
Hao wenzio nao waliofata amri kumi za Mungu wameambiwaje hapo?View attachment 2066939
Soma uelewa sio ukalili. Hii amri ilizui watu kutumia vilevi waendapo kwenye ibada (hema ya kukutania ilikuwa ni sehemu maalum iliyo andaliwa kwaajiri ya kuabudia.

“Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
” Waefeso 5:18. Nimeona unaongelea na huu mstari swali ni je neno "ambamo mna ufisadi" kwa kingereza limetumika neno “wherein is excess" umelielewa ama umesoma tu bila kutafakari?
 
Basi nipe andiko ambalo limekuruhusu wewe mmatumbi unywe pombe
Kama ambavyo hakuna lililoninyima kula wali, hakuna pia lililoninyima kupiga ulabu.

Nimeambiwa nisiibe, nisizini, nisishuhudie uongo, niheshimu wazazi nk nk... lakini sijaambiwa nisipige ulabu wala nisije wali.
 
Tunaangamia kwa kukosa Maarifa

Mithali23
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari;
Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Bold.
Usinywe Sana
 
Kwani hizo amri 10 za Mungu zinakuhusu wewe mmatumbi?
Au wana wa Israel?
Kama ambavyo hakuna lililoninyima kula wali, hakuna pia lililoninyima kupiga ulabu.

Nimeambiwa nisiibe, nisizini, nisishuhudie uongo, niheshimu wazazi nk nk... lakini sijaambiwa nisipige ulabu wala nisije wali.
 
Back
Top Bottom