Muujiza wa Tony Kapola: Je aliombea mtungi mkubwa au mdogo?

Ni majuha na hakuna neno lingine zuri zaidi ya hilo! Na ulokole wangu hauna uhusiano kabisa na ujuha wao
 
Dah haya rafikiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Sasa mkuu ndo utuwekee picha ya Tony akiwa anapuliza mtungi🀣🀣🀣🀣🀣
 
Afungue kituo cha gesi sasa
Nitakuwa wa mwisho kukataa kuwa Tony hajihusishi na Money Laundering... mkewe kuropoka kuwa wana magari mengi hadi wanaogopa vyombo vya usalama ilikuwa kiashiria ila Tony akaharibu zaidi kusema kuwa kuna wazee humwita na kumpa magari bure. Akaenda mbali zaidi kwa kudai naye huwa anagawa magari bure.
 
Mudawote my friend naifahamu miujiza kindakindaki kuanzia ile ya Kilingeni ya kitapeli mpaka ya Kimungu! Kapola ni muhuni na miujiza yake ni ya kitapeli! Unamjua akiwa nabii mimi namjua kindakindaki! Baba yake marehemu namuita mjomba
 
Mudawote my friend naifahamu miujiza kindakindaki kuanzia ile ya Kilingeni ya kitapeli mpaka ya Kimungu! Kapola ni muhuni na miujiza yake ni ya kitapeli! Unamjua akiwa nabii mimi namjua kindakindaki! Baba yake marehemu namuita mjomba
Dah sasa ewe Mshana Jr mna vita vya kifamilia. Ila nafurahi kusikia kuwa kuna miujiza unaijua ya kilingeni na ya kubumba. Kwa Tony nadhani anahitaji elimu ya fedha, maana unajua kuna mtu mwingine anaweza kuwa hata na laki moja tu ila atapiga kelele mtaa wote mjue leo ana laki.
 
"Jana Mimi Luku Iliisha,,Waifu Akanipa Namba Za Kitambulisho Chake Cha Nida,,Nikaziingiza Mara Umeme Huo"....###Ulikuwepo...???###
 
Naam. Hiyo inaitwa imani yenye upofu uliotukuka. Yan unaamini tu bila matendo (jitihada za makusudi) kwamba Mungu atatenda!?? Nani kakudanganya hivo?? Hilo sahau halipo -utakufa njaa, maradhi na umaskini ulokubuhu vitakuandama.
e.g. Huendi kwenye mihangaiko, Huendi na huna juhudi kwenye biashara yako, mtoto humhimizi aende shule na atie juhudi kusoma kwa bidii ....eti Mungu yupo pale atatenda... unajipa upofu na kujidanganya Yesu alisema." ..kazi nitendazo mimi atazitenda..." na unalenga kwamba kwakuwa alitenda miujiza na wewe unakomalia kifungu hicho kwamba na ww utatenda miujiza na kusahau kwamba hata Yesu mwenyewe alifanya kazi e.g. ktk. ujana wake alimsaidia baba yake kazi ya Useremala. Hebu fikiria - si angelifanya muujiza ili baba yake huyo apumzike asiendelee kuhangaika na kujitaabisha na kazi ya kukata mbao, kuchonga fenicha na kuchonga mawe ili kupata riziki ya kila siku??
Wakristo esp. Wakatoliki husema "Ora et labora" = kazi na sala/maombi. Huyo Tony kwa mfano, ikatokea siku waamini-misukule wake wakamstukia wasitoe tena sadaka/michango wakakataa kutapeliwa ndipo "kitaeleweka".
Halafu ukumbuke hata Ibilisi kwa mikono ya wanadamu hufanya miujiza mingi sana - soma Matendo ya Mitume 8:9-11 inayomhusu Simon.
 
Bosi wewe ni moja ya watu wanaoishi kwa jasho sana na utakufa umetoka sana jasho! Hakuna kitu kinaenda bila kuwa na imani na kuamini Miujiza.
 
Hiyo miujiza ya aina hiyo ingekuwa inafanya kazi Nigeria lingekuwa Taifa tajiri zaidi duniani.
Kuna msitari mwembamba sana kati ya mnachoita miujiza na uchawi.
Acheni kutumia ukristo kuficha utapeli, wizi na uchawi kwa kutumia mistari ya biblia.
Nakazia hoja:
Acheni kutumia ukristo kuficha utapeli, wizi na uchawi kwa kutumia mistari ya biblia.
 
Bwana ametenda, jina lake lihimidiwe.... πŸ˜„ πŸ˜„ πŸ˜„

utaskia: "Mti wenye matunda ndo unaopigwa mawe"...
 
Bosi wewe ni moja ya watu wanaoishi kwa jasho sana na utakufa umetoka sana jasho! Hakuna kitu kinaenda bila kuwa na imani na kuamini Miujiza.
Nanukuu : "Hakuna kitu kinaenda bila kuwa na imani na kuamini Miujiza. SIO KWELI - hii ni Potoshi. e.g. Sayansi inadai Proof.
Mfano- Anatinga jambazi ndani ya nyumba yako uck wa manane amebeba silaha halafu ww huchukui hatua yyt kujitetea ww, familia yako na mali zako eti una Imani ya dhati kabisa kwamba kutatokea Miujiza!!?? au Umebanwa na njaa kali halafu kinaletwa chakula na unaambiwa kimewekwa sumu halafu ww unakula tu kwa Imani na Miujiza??
Unaacha kuchukua tahadhari dhidi ya mbu wa malaria, Tahadhari uwapo barabarani, n.k. kwa kutegemea Imani na Miujiza?? Sidhani kama hilo ni sawa.
 
Bwana ametenda, jina lake lihimidiwe.... πŸ˜„ πŸ˜„ πŸ˜„

utaskia: "Mti wenye matunda ndo unaopigwa mawe"...
Etieee! Mwizi/Kibaka anayepigwa mawe, shoga wanaopigiwa kelele kwa tabia hiyo n.k. n.k. wahenga walisema "kwenye msafara wa mamba na kenge wamo"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…