Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Kwani muungano unaulazima gani kwa mtanganyika? Hasa mwananchi aliye kijijini?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naunga hoja serikali moja,taifa moja,nchi moja,rais mmoja!!!tueneze wito huu kwa kila mtanzania ili rasimu hii isipite na mapendekezo ya serikali 3
 

sawa....lakini why rely on getting results by default rather than structuring it in the first place?

the point is....let's do a correct thing the first time. tuamue sasa tunataka kuwa na serikali ngapi badala ya kusubiri idadi ya serikali kupatikana by default!
 
liwalo naliwe serikali moja,taifa moja,nchi moja,rais mmoja,huo ndo muungano

Lazima ulikula jongoo ulipokuwa mdogo maana akili zako si sawa sawa za kushikiwa iweje iwe serikali moja na Zanzibar wali - keep their identity ni watanganyika tu ndio waliopoteza identity yao. sasa wana haha na katiba ya Tanganyika kabla ya uchaguzi 2015 ni dhahir ya Tanganyika itakuwa ya kuburuzwa na muda mfupi ujao itakuwa imejaa viraka.
 

Hii nimeipenda. Kiukweli hii ni transition. Kwa wanaosema kuwa wanataka serikali moja hao ndio wanaoutaka muungano kwa dhati. Serekali mbili au tatu huo ni unafiki na kutokuupenda muungano. Kwa hili naungana na "wanafiki" ili tuuvunje kimya kimya kwani wao (wazanzibari) ndio wenye choko choko. I am sure baada ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano Watanganyika tutakaa chini tuandike ya kwetu itakayotusimamia.
 
...Sioni namna ya Wazanzibar kuridhia mfumo wowote wa Muungano, hivyo Nasema NDIYO kwa Serikali tatu kwa sababu moja kubwa, hii ni njia rahisi na ya wazi kuelekea kwenye serikali moja ya Jamhuri ya Tanganyika...

Mimi sitaki muungano. Nataka Tanganyika irudi na Zanzibar iende kwao. Tuungane EA.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Hivi kwanini tuhangaike hivi ,kwanini tusivunje huu muungano .najua raisi anaogopa kashfa lakini huu muungano haubebeki tena
 
Baadhi ya wajukuu wa sultani ni janga kwenye Taifa letu...
Hatupaswi kuwabembeleza...ni bora tuwe na serika
 
Kwa rasimu hii tunahitaji kuwatimua na kuishitaki tume ya Warioba na pia kuwa chunguza kama zimetimia kweli

Nakuunga mkono. Ndiyo hao waliotenga bajeti ya watakaopata UKIMWI na fuel full tank kila siku. Haikubaliki. CAG aingilie mapema. Halafu kila aliposhauriwa Warioba alikuwa akibisha. May be he had a different agenda.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Hiyo Serikali ya Tanganyika ikipatikana ule ukanda wa Pwani uliokuwa chini ya himaya ya Waarabu ikiwemo Bagamoyo na DSM itakuwa sehemu ya Tanganyika yetu au Zanzibar? King of Zamunda
 
Bado naipiti rasimu kipengele hadi kingine.
Kuhusu hili analosema Mwanakijiji kuna ukweli mkubwa sana.

Serikali ya muungano ni kubwa kuliko watu wanavyodhani. Yaani ni katiba ya sasa ambayo imevunjwa vunjwa na kupewa maneno mbadala.

Hii katiba itakuwa mzigo kwa Mtanganyika. Nikiangalia ukubwa wa serikali ya muungano nina uhakika kabisa Zanzibar hawataweza kuchangia gharama za uendeshaji wake na hilo litakuwa zigo la Mtanganyika.

Najaribu kuangalia ukubwa huo naona mambo ya kutisha kidogo. Mfano, endapo bajeti ya serikali ya muungano itakuwa trillioni 1 tu(kitu ambacho hakiwezekani) Zanzibar italazimika kchangia bilioni 500 kwa usawa.
Bajeti ya znz kwa mwaka 2013 ni bilioni 630 na mapato ya znz ni bilioni 120.
Kwa maneno mengine mapato ya znz hayawezi kuendesha kitengo kimoja cha serikali ya muungano.

Katika hali hiyo mzigo anaubeba Mtanganyika kama anavyoubeba sasa hivi.
Kitu kinachoshangaza ni kuwa nafasi zimetolewa kwa uwiano, lakini wakati wa kuchangia uwiano hautakuwepo na zigo atalibeba Mtanganyika.

Nathubutu kusema kuwa serikali ya muungano ni zigo kwa Mtanganyika, mzanzibar yupo tu kwa kudai nafasi na hana mchango wa aina yoyote kama kawaida yake. Tumesema tunataka kutua zigo la misumari

Tutaendelea kuangalia mambo mengine lakini sehemu kubwa ni mzigo kwa Mtanganyika.
 
hapa pana kitu kimejificha, na siku kikiibuka kinaweza kuleta mshangao kwa wengi.... mimi ninaamini kwa dhati kabisa kuwa muungano wetu umewachosha wote(tanganyika/zanzibar) ila tu hakuna kiongozi anayetaka kukubali umfie chini ya uongozi wake. tunashinikizwa kuungana kama jinsi mwalimu alivyoufanyia usanii mkataba wa muungano na kutokuuweka wazi hata kwa KARUME MWENYEWE....... Hatuna haja ya kulinda kwa nguvu muungano ambao pande husika haziko tayari. serikali tatu sio suluhisho na inaweza ikawa ndio muelekeo sahihi wa kuipeleka jamhuri ya muungano wa tanzania mwishoni. na serikali moja ndio janga kabisa kwa wazanzibari, hawawatakubali na watatangaza vita vya wazi(an open war) dhidi ya bara... tujiulize swali la msingi........... KAMA SERIKALI MBILI HAWARIDHIKI, HIYO MOJA WATAIPOKEAJE?????? Kwa sababu itawanyima na kuwaondolea hata kile kidogo walichonacho hivi sasa
 
Nadhani huu ndio wakati muafaka wa kuidai Tanganyika yetu,kwanini mizigo isiyo na ulazima kwetu!!!!!
Hakuna siku wazanzibar watakubali tubaki na serikali moja wavunje yao,hivyo kutaka kuwa na serikali tatu
ni kuwafurahisha wazanzibar na kutuumiza Watanganyika,ifike sasa tuseme NO'
 
Yes! This would be a good starting point. Mimi sitaki muungano. Nataka Tanganyika. Hivi kweli nani aliwahi kuiona ile instrument ya muungano wa 1964? Hawa wazee walikuwa na hoja gani za msingi?


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Reactions: SMU
mi nafikili wale Wapemba pale Kariakoo,muda umefika kuchukua maamuzi magumu....warudi Zanzibar wakaijenge Zanzibar yao....maana kama kujibembeleza tulianza zamani sana...kama ni maji sasa yako shingoni....
 
Hiyo Serikali ya Tanganyika ikipatikana ule ukanda wa Pwani uliokuwa chini ya himaya ya Waarabu ikiwemo Bagamoyo na DSM itakuwa sehemu ya Tanganyika yetu au Zanzibar? King of Zamunda
Sasa wewe unaleta mambo ya rais wa Malawi ya outdated Heligoland treaty. Tanganyika inafahamika mipaka yake. Zanzibar ni visiwa vya Unguja na Pemba. This is also known.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Hukutoa maoni yako nini kifanyike notradamme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…