Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili la serikali tatu ni sawa kwa kuwa muda si muda tutakuwa na akina Yeltsin watakaowaacha akina Gorbachev bila nchi ya kutawala na hivyo Tanganyika kuwa nchi peke yake bila unyonyaji wa Zanzibar na Zinzibar kubakia peke yake bila unyonyaji wa Tanganyika. Juzi nimewasikia wakililia kiti chao UN basi tukimpata Yeltsin wetu nao watakuwa na kiti chao huko UN. Wacha zije lakini tatu hazitadumu.
liwalo naliwe serikali moja,taifa moja,nchi moja,rais mmoja,huo ndo muungano
Afu we mkuda usitake kutuharibia thread kabisa wewe, nenda kwny threads zako za kimbea-mbea
si tayari wako zanzibar?? wafanye referrendum yao, wafuate taratibu na wasikilizwe ili watoke... hakuna haja ya kukaa tunalumbana na kanchi kenye kelele wakati productivity hakuna
mimi naamini kabisa kama zanzibar wangekua na nia ya dhati ya kujiondoa kwenye muungano wangeweza, ila wameishia kupiga perepete ili tu wawe wanapata watakacho, ni kama mtu mwenye gubu
kuhusu serikali tatu, nadhani itasaidia zaidi ile transition ya kuanchana na zanzibar, tutakua na migogoro mingi mno kati ya hizo serikali tatu mwisho tutafanikiwa kutengana.... ni sawa na kusema ndoa ina matatizo basi ulete mama mkwe akae hapo ndani kutatua - NDIO HIYO SERIKALI YA TATU AMBAYO ITAKUA NA MAMLAKA YA KUSADIKIKA ZAIDI, I DONT MIND UKIRITIMBA IF THAT IS WHAT IT TAKES KUVUNJA MUUNGANO
...Sioni namna ya Wazanzibar kuridhia mfumo wowote wa Muungano, hivyo Nasema NDIYO kwa Serikali tatu kwa sababu moja kubwa, hii ni njia rahisi na ya wazi kuelekea kwenye serikali moja ya Jamhuri ya Tanganyika...
wazaninzibar mambo ya nje lazima litoke kwenye hiyo rasimu uhamiaji lazima utoke ,uraiya tutakuwa na uraiya wa tanzania huku kila nchi ikiwa na passport
yake
mfano jamuuhuri ya muungano wa tanzania au shirikisho la tanzania tangnyika passport au shirikisho la tanzania zanzibar passport
usjili wa vyama vya siasa kila nchi iasjili vyama vyake lazima litoke
sasa yaliyo baki benk kuu na hili watalijadili kwa kuliboresha sio kuliondowa kabisa
kinyume wazanzibar kuyatowa mambo ya nje basi shida na zogo la muungno halita maliza hadi kufa kwa muungano kupitia mgogoro
kwa kupitia mgogoro wa katiba
Kwa rasimu hii tunahitaji kuwatimua na kuishitaki tume ya Warioba na pia kuwa chunguza kama zimetimia kweli
Tunataka serikali moja tu
Serikali ya watu wa TANGANYIKA
Hao wengine hatutaki kuwasikia, waende kupika urojo huko kwao
Ni wakati umefika Ng'ombe akatae kunyonywa na kupe mlalamishi.
Hivi kwanza wana faida gani kwa bara hawa wazenji zaidi ya kelele na udini?
Yes! This would be a good starting point. Mimi sitaki muungano. Nataka Tanganyika. Hivi kweli nani aliwahi kuiona ile instrument ya muungano wa 1964? Hawa wazee walikuwa na hoja gani za msingi?Katika mazingira ya siasa za Zanzibar za sasa kwa hakika kutaka serikali moja ni "kulilia mbaramwezi"! - Halitatokea!. "Tulifanya" makosa kutunga sheria inayozuia watu wasitoe maoni yao juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa muungano. Na haya ndio malipo yake!
Tungeanza kwanza kuwauliza watu kama wanataka kuendelea kuungana ama la, kabla ya kuwauliza mfumo wa muungano wanaoutaka. Ukitizama maoni/mapendekezo ya sasa ya baadhi ya wazanzibari, ni wazi hawataki kuendelea na huu muungano na hata watanganyika baadhi yetu hatuoni faida za wazi za muungano huu.
Sasa wewe unaleta mambo ya rais wa Malawi ya outdated Heligoland treaty. Tanganyika inafahamika mipaka yake. Zanzibar ni visiwa vya Unguja na Pemba. This is also known.Hiyo Serikali ya Tanganyika ikipatikana ule ukanda wa Pwani uliokuwa chini ya himaya ya Waarabu ikiwemo Bagamoyo na DSM itakuwa sehemu ya Tanganyika yetu au Zanzibar? King of Zamunda
hapa pana kitu kimejificha, na siku kikiibuka kinaweza kuleta mshangao kwa wengi.... mimi ninaamini kwa dhati kabisa kuwa muungano wetu umewachosha wote(tanganyika/zanzibar) ila tu hakuna kiongozi anayetaka kukubali umfie chini ya uongozi wake. tunashinikizwa kuungana kama jinsi mwalimu alivyoufanyia usanii mkataba wa muungano na kutokuuweka wazi hata kwa KARUME MWENYEWE....... Hatuna haja ya kulinda kwa nguvu muungano ambao pande husika haziko tayari. serikali tatu sio suluhisho na inaweza ikawa ndio muelekeo sahihi wa kuipeleka jamhuri ya muungano wa tanzania mwishoni. na serikali moja ndio janga kabisa kwa wazanzibari, hawawatakubali na watatangaza vita vya wazi(an open war) dhidi ya bara... tujiulize swali la msingi........... KAMA SERIKALI MBILI HAWARIDHIKI, HIYO MOJA WATAIPOKEAJE?????? Kwa sababu itawanyima na kuwaondolea hata kile kidogo walichonacho hivi sasa