Hilo la Malawi limeisha? Kama bado kwa nini Zanzibar wasidai mipaka ya enzi za Utawala wa Sultani na hasa Mtwara, Bagamoyo na Dar es Salaam?Sasa wewe unaleta mambo ya rais wa Malawi ya outdated Heligoland treaty. Tanganyika inafahamika mipaka yake. Zanzibar ni visiwa vya Unguja na Pemba. This is also known.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Nadhani sasa umefika wakati wa kuwaacha Wanzanzibar wadai nchi yao wenyewe. Hata sisi Watanganyika tunataka nchi yetu, full stop. Hatutaki muungano...
Kwa kweli tokea siku ilipotolewa nilipitia faster na kubaini hayahaya uliyoyasema, hata Tuko alisimama kidete sana kubainisha madudu ya Rasimu hii ilipokuwa ikitangazwa ajabu kuna watu walikuwa wakimuona mwehu. Siamini kama hii tume ilizunguka nchi nzima na kwamba hayo ndiyo mapendekezo ya wananchi, ni kama wamejifungia na kuandika wanavyotaka wao, kwani kila hoja waliyoitoa haina justification yoyote. Jimbo moja wabunge wawili wa jinsia tofauti(kwani tunataka waoane?)! Mambo ya Muungano saba, mawaziri 15, vichekesho; Manaibu waziri kutamkwa katika Katiba? vichekesho maana yake nini kwamba wizara kuwa na wajumbe wawili wa Baraza la Mawaziri? Uhuni. Serikali tatu lakini hakuna mapendekezo ya hizo serikali ziweje, na ziongozwe vipi; yaani wamezunguka nchi nzima wamekuja na mapendekezo ya kurekebisha muungano uliopo? Kwa kifupi wamefanya as if ni Tume ya Kurekebisha Muundo wa Muungano. Sioni majibu ya matatizo na vilio vya watanzaniarasimu hii sijui warioba alijifungia chumbani na mkewe akaitunga au alizingatia maoni yetu? kifupi hii rasimu ni upuuzi na ushuzi wa warioba sio maoni ya wananchi.
Kwa kweli ni upuuzi; as a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?
Kifungu cha maraisi katika rasimu ya katiba yetu inanakera sana.Tutakuwa na maraisi wangapi?Ingekuwa vizuri kama tungekuwa na rais mmoja tu na nchi ya Tanganyika na Zanzibar zingeendeshwa na Mawaziri Viongozi kwa kimombo Chief Ministers
hujaisoma rasimu wewe. Usikurupuke nawe uonekane umeweka post.
Mlivyooana mlipokutana ndivyo mtakavyoelekea mtakapoachana. Halihitaji kuuumiza kichwa hiliHiyo Serikali ya Tanganyika ikipatikana ule ukanda wa Pwani uliokuwa chini ya himaya ya Waarabu ikiwemo Bagamoyo na DSM itakuwa sehemu ya Tanganyika yetu au Zanzibar? King of Zamunda
maoni yangu ni kinyume kabisa na MWANAKIJIJI.. serikali ni jambo lisilokubalika kabisa mbele ya macho ya wazanzibari.Hukutoa maoni yako nini kifanyike notradamme
Heko, yaani uwe unajua 2+2=4, lakini unaweka 3 kwa makusudi ili upate nafasi ya kufanya tena swali hilohilo? Haiwezekani,sawa....lakini why rely on getting results by default rather than structuring it in the first place?
the point is....let's do a correct thing the first time. tuamue sasa tunataka kuwa na serikali ngapi badala ya kusubiri idadi ya serikali kupatikana by default!
mpango wa serkal 3 n ndoto za mchana
Mimi tangu shule ya msingi hadi leo sijaeleweshwa umuhimu wa muungano kwa pande zote mbili - siujui. Muungano kwa jinsi ulivyo una maana ya Changu ni changu peke yangu (Zbar) ile chako (Tanganyika) ni chetu sote (Zbar na Tanganyika). Hii siyo sawa. Bahati nzuri sana wazanzibar ambao Muungano ni wa wote yaani wana haki bara na visiwani ktk mambo mengi ya muungano ndo hao hao wanaodai kujitenga. Sisi wabara au watanganyika tunahofu nini kujitenga au kuunda serikali tatu. Hii ndo maana napenda sera ya Chadema kuhusu Muungano. Wanataka serikali tatu.
Kuna suala la kukinzana kwenye hiyo Rasimu, sehemu mojawapo jamaa wanataja ' Jamuhuri ya Tanganyika' na sehemu nyingine wanataja ' Tanzania Bara' kwa nini tume inakuwa very sensitive inapokwepesha neno 'Tanzania Visiwani' na kuendelea kulinda neno 'Zanzibar'?
Rais wa Muungano atakuwa a very weak president katika kutenda kazi. Katika mfumo wa serikali tatu Tanganyika itaweza kufanya mambo mengi makubwa ambayo yatadhoofisha sana Rais wa Muungano hasa kama itatokea kuwa atakuwa ni Rais kutoka Zanzibar. Zanzibar itaona inazidiwa nguvu kubwa sana na Tanganyika. This is so obvious unless - Kuigawa Tanzania bara katika majimbo mengine ambayo nayo yatajitegemea...
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa