Ben Mugashe
JF-Expert Member
- Oct 9, 2008
- 999
- 617
Ukifa kabla ya kuona serikali mmoja mpe salaam Mwalimu Nyerere mkumbushe hii sentensi "Watu wazima mnazungumzia serikali tatu maskini kabisa nyie! wakati wazungu wanazungumzia kuunganisha ulaya moja yenye nguvu"
Hakuna Tanzania kama hakuna muungano!! kuna Tanganyika na Zanzibar..serikali moja unayoota ni ya nchi gani kati ya hizi mbili?Niliona katika ndoto yangu nchi zz jiarani zikiingalia Tanzania kwa namna ya kutaka iwe na serikali moja kwanza ndipo wajiunge nayo kufanya nchi kubwa sana yenye nguvu. Nikaona mataifa ya magharibi yakichukia!
Hakuna Tanzania kama hakuna muungano!! kuna Tanganyika na Zanzibar..serikali moja unayoota ni ya nchi gani kati ya hizi mbili?
Na tazama nikaona.....angalia usijekuta unakaribia kutoa kitabu chako cha ufunuo wa kakati.
Kesho ukiota ndoto uko na yule Profesa wa ccm usiache kutuandikia.
Wale wote wanaotaka Tanzania tuwe na serikali Moja yenye kufuata Mfumo wa kuwa na serikali za kimajimbo TUUNGANE na tuifikishe hoja yetu hiyo kwa wananchi kama ndiyo njia pekee ya kuuokoa Muungano wetu. Unguja na Pemba zitakuwa na serikali zao za ndani za kimajimbo na kwa Upande wa Tanganyika majimbo yatagawanywa kwa kufuata mapendekezo yatakayotolewa na wananchi wenyewe.
Wale wote wanaotaka Tanzania tuwe na serikali Moja yenye kufuata Mfumo wa kuwa na serikali za kimajimbo TUUNGANE na tuifikishe hoja yetu hiyo kwa wananchi kama ndiyo njia pekee ya kuuokoa Muungano wetu. Unguja na Pemba zitakuwa na serikali zao za ndani za kimajimbo na kwa Upande wa Tanganyika majimbo yatagawanywa kwa kufuata mapendekezo yatakayotolewa na wananchi wenyewe.
Kigarama kwa nini wewe sio miongoni mwa wanaotakiwa kuheshimu mawazo ya Watanzania????Tujifunze kuheshimu mawazo ya walio wengi,,,wahenga walisema MKATAA WENGI NI MCHAWI...Wananchi wanataka Serikali tatu..Tuheshimu mawazo yao
Kwa mtazamo wangu watanzania tunahitaji muungano wa serikali moja, yaani Zanzibar na bara zote zikubali kusurrender autonomy zake kwa serikali na nchi moja tu ya Tanzania. Nionavyo mimi, serikali mbili ama tatu zitaturudisha kulekule kwenye matatizo ambayo tunapaswa kuyakimbia tena kwa speed ya 250km/h.
Serikali mbili zitaendeleza migogoro na mivutano ileile ambayo tulishaichoka.
Serikali tatu ndo balaa, yaani muundo huu ni sawa na mwanaume aliyeshindwa ndoa ya wake wawili kisha akaamua kuongeza mke mwingine. Kiukweli muundo huu utatugharimu. Kiusalama kwa mfano, nchi washirika wakigoma kuziwezesha wizara zenye dhamana ya usalama nchi imekwisha!, marais wa nchi washirika wakiamua kuuhujumu muungano ni rahisi sana kwenye serikali tatu. Inshort miungano ya serikali mbili au tatu haifai!
Kama ni hivyo basi, dawa ni muungano wa serikali moja. Faida yake kubwa ni kwamba itaimarisha utaifa wetu haijawahi tokea. Pili itaondoa malalamiko ya kila upande wa muungano kuona unakandamizwa na upande mwingine. Kubwa zaidi itatuongezea nguvu mbele ya maadui kwani "umoja ni nguvu"