Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Watanganyika wameumia sana masikini. hahahaaaaaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.
Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!
Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.
Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.
mkuu CCM wanataka mbili, je na wewe unapendekeza mbili?I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa
Mwanakijiji mbona haukuonekana kutoa maoni kwenye tume ya katiba unaonekana saizi umechelewa.
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa
ndumyana; Unataka muungano uvunjwe kama ambavyo mkoa wenu wa Mbeya utavunjwa vipande viwili, then what???
Umeishapata nafasi ya kuwauliza Prof. Baregu na Jaji Warioba kuhusu hili suala la serikali tatu mpaka unasema itakuwa ni maajabu jinsi ya kufanya kazi.
Mimi nadhani ingekuwa vyema kama ungepata maoni kutoka kwa mwanachama mwenzako Prof. Baregu kupata ufafanuzi zaidi.
Urusi iliposambalitika wengine wamechoka lakini Rusia imebaki Kuwa Tajiri hata ZNZ wakijitoa haitawaathili Bara sana sana Bara atakuwa tajiri kwa kuuza umeme zenji Ada za viza na vibali vya kuishi na kufanya kazi Bara kwani wazenji wote watakuwa Raia wa Nchi Jilani
Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.
Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!
Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.
Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.
Hili linaweza kuwa baya kuliko yote,nimeangaika kutafuta kama kuna nchi duniani yenye mfumo kama huu nimekosa.Huenda Tanzania ikaweka historia kwa jambo la kipuuzi kama hilo.Mpaka hapa tulipo tunatakiwa kupunguza kwani ni gharama sana kuwalipa,unaweza ukaangalia uwiano wa wanawake bungeni duniani kwa kila nchi na Tanzania ikiwa ni ya 20;Women in Parliaments: World ClassificationMkuu Mwanakijiji,Na hili hili la wabunge wawiliwawili (jinsia tofauti) kwa jimbo unalionaje? Mbona kwa wenzetu waliotutangulia kwenye maswala ya demokrasia hatujawahi kusikia upuuzi huu? Kituko tulicholetewa na Warioba hakilingani na gharama tulizowalipa.
Mara zote huwa nashangaa kiburi cha wenzetu wa tz visiwani na ukizingatia wapo 1.6m wachache kuzidi hata shinyanga na jinsi wanavyojiona wana mamlaka juu yetu,,
its time to let them go and i always remember that verse in the bible ''there is a way that seems right to a man but its end is destruction''
we need tanganyika back!!!!we need tanganyika back!!!
Wewe saa zote unafikiria kichama kichama na kisiasa siasa tu. Kwa nini nimuulize kwani mie siwezi kufikiri?
Kijana tunakwenda kujadili mambo serious, usiingizee ukada na uchama kila kona. Nilijuana na Profesa Baregu kwenye taaluma kabla hatujakutana CDM, na siku zote huwa naweza kumkosoa au kumuunga mkono waziwazi bila kificho.
Siyo kila kitu kutazamia unadhani kila kitu tunachofanya tanzania lazima kifanane na mataifa ya nje huo ni utumwa jiamini,jitegemee.Hili linaweza kuwa baya kuliko yote,nimeangaika kutafuta kama kuna nchi duniani yenye mfumo kama huu nimekosa.Huenda Tanzania ikaweka historia kwa jambo la kipuuzi kama hilo.Mpaka hapa tulipo tunatakiwa kupunguza kwani ni gharama sana kuwalipa,unaweza ukaangalia uwiano wa wanawake bungeni duniani kwa kila nchi na Tanzania ikiwa ni ya 20;Women in Parliaments: World Classification