Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Mara zote huwa nashangaa kiburi cha wenzetu wa tz visiwani na ukizingatia wapo 1.6m wachache kuzidi hata shinyanga na jinsi wanavyojiona wana mamlaka juu yetu,,
its time to let them go and i always remember that verse in the bible ''there is a way that seems right to a man but its end is destruction''
we need tanganyika back!!!!we need tanganyika back!!!
 
Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.

Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!

Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.

Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.

Umeishapata nafasi ya kuwauliza Prof. Baregu na Jaji Warioba kuhusu hili suala la serikali tatu mpaka unasema itakuwa ni maajabu jinsi ya kufanya kazi.

Mimi nadhani ingekuwa vyema kama ungepata maoni kutoka kwa mwanachama mwenzako Prof. Baregu kupata ufafanuzi zaidi.
 
ktk ie rasimu sijaelewa kipengele cha wabunge 70, inamaana majombo mengine hayatakuwa na wawakilishi?
 
Mwanakijiji mbona haukuonekana kutoa maoni kwenye tume ya katiba unaonekana saizi umechelewa.

Mbona sababu nilishazitoa kuwa sikuutambua mchakato wa kuandika Katiba Mpya... hauukwa mchakato halali? Sasa hivi naogopa tu kuwa Watanzania kama kawaida hawashtuki wanapokuwa tayari kubambikiziwa kitu...
 
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa

Huu muungano bora tuuvunje tu kila mtu aendelee na maisha yake
 
Last edited by a moderator:
Umeishapata nafasi ya kuwauliza Prof. Baregu na Jaji Warioba kuhusu hili suala la serikali tatu mpaka unasema itakuwa ni maajabu jinsi ya kufanya kazi.

Mimi nadhani ingekuwa vyema kama ungepata maoni kutoka kwa mwanachama mwenzako Prof. Baregu kupata ufafanuzi zaidi.

Wewe saa zote unafikiria kichama kichama na kisiasa siasa tu. Kwa nini nimuulize kwani mie siwezi kufikiri?

Kijana tunakwenda kujadili mambo serious, usiingizee ukada na uchama kila kona. Nilijuana na Profesa Baregu kwenye taaluma kabla hatujakutana CHADEMA, na siku zote huwa naweza kumkosoa au kumuunga mkono waziwazi bila kificho.
 
Hivi hii ndoa ya muungano haina option ya talaka kwani?
 
wazaninzibar mambo ya nje lazima litoke kwenye hiyo rasimu uhamiaji lazima utoke ,uraiya tutakuwa na uraiya wa tanzania huku kila nchi ikiwa na passport

yake

mfano jamuuhuri ya muungano wa tanzania au shirikisho la tanzania tangnyika passport au shirikisho la tanzania zanzibar passport

usjili wa vyama vya siasa kila nchi iasjili vyama vyake lazima litoke

sasa yaliyo baki benk kuu na hili watalijadili kwa kuliboresha sio kuliondowa kabisa

kinyume wazanzibar kuyatowa mambo ya nje basi shida na zogo la muungno halita maliza hadi kufa kwa muungano kupitia mgogoro

kwa kupitia mgogoro wa katiba
 
Urusi iliposambalitika wengine wamechoka lakini Rusia imebaki Kuwa Tajiri hata ZNZ wakijitoa haitawaathili Bara sana sana Bara atakuwa tajiri kwa kuuza umeme zenji Ada za viza na vibali vya kuishi na kufanya kazi Bara kwani wazenji wote watakuwa Raia wa Nchi Jilani

Wakiondoka waZnz Tanganyika mutawamaliza hao mazeruzeru wenu kwa kutafuta utajiri
 
Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.

Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!

Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.

Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.

Rais wa Muungano atakuwa a very weak president katika kutenda kazi. Katika mfumo wa serikali tatu Tanganyika itaweza kufanya mambo mengi makubwa ambayo yatadhoofisha sana Rais wa Muungano hasa kama itatokea kuwa atakuwa ni Rais kutoka Zanzibar. Zanzibar itaona inazidiwa nguvu kubwa sana na Tanganyika. This is so obvious unless - Kuigawa Tanzania bara katika majimbo mengine ambayo nayo yatajitegemea...
 
Mkuu Mwanakijiji,Na hili hili la wabunge wawiliwawili (jinsia tofauti) kwa jimbo unalionaje? Mbona kwa wenzetu waliotutangulia kwenye maswala ya demokrasia hatujawahi kusikia upuuzi huu? Kituko tulicholetewa na Warioba hakilingani na gharama tulizowalipa.
Hili linaweza kuwa baya kuliko yote,nimeangaika kutafuta kama kuna nchi duniani yenye mfumo kama huu nimekosa.Huenda Tanzania ikaweka historia kwa jambo la kipuuzi kama hilo.Mpaka hapa tulipo tunatakiwa kupunguza kwani ni gharama sana kuwalipa,unaweza ukaangalia uwiano wa wanawake bungeni duniani kwa kila nchi na Tanzania ikiwa ni ya 20;Women in Parliaments: World Classification
 
Mara zote huwa nashangaa kiburi cha wenzetu wa tz visiwani na ukizingatia wapo 1.6m wachache kuzidi hata shinyanga na jinsi wanavyojiona wana mamlaka juu yetu,,
its time to let them go and i always remember that verse in the bible ''there is a way that seems right to a man but its end is destruction''
we need tanganyika back!!!!we need tanganyika back!!!

Sasa ndio ujue watu wa visiwani tofauti na wa shinyanga
 
Wewe saa zote unafikiria kichama kichama na kisiasa siasa tu. Kwa nini nimuulize kwani mie siwezi kufikiri?

Kijana tunakwenda kujadili mambo serious, usiingizee ukada na uchama kila kona. Nilijuana na Profesa Baregu kwenye taaluma kabla hatujakutana CDM, na siku zote huwa naweza kumkosoa au kumuunga mkono waziwazi bila kificho.

Hizo ni fikra zako na mtazamo wako juu yangu halafu huwezi kuniita kijana hunijui wewe hauna ukubwa wa hivyo kuniita mie kijana.

Wewe umesema wamechagua serikali tatu ni maajabu mimi nilitaka kuyajua hayo maajabu.

Kila mmoja wetu ana haki kwenye hili jambo hakuna aliyeleta mambo ya siasa.
 
Mzee mwanakijiji ungewashauri Watanganyika wenzako njia ya kudai Irudi Tanganyika kwanza.
 
Kutoka serikali mbili ni sasa kuwa na serikali moja au serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar bila muungano.
Na hili la wabunge wawili wawili, mwanaumme na mke, ni geni sana katika ulimengu huu hivyo tuelemishwe kwamba halitadhoofisha mambo maendeleo yetu. Muhimu kwangu ni kundi lolote la jamii lisibaguliwe. Kama ni neno "forced" demokrasia tu basi kwa makusudi kabisa tuweke uwakilishi wa (1) watu wa kipato cha chini (mfano wamachinga) ambao mara kwa mara wanyang'anywa bidhaa zao na mgambo (2) wazee (3) wajane (4) waandishi wa habari (4) dini na list hii inaweza kuboreshwa ikaongezeka au ikapungua kidogo.
 
Hata mimi kuhusu hili la Serikali tatu (3) siliungi mkono na miguu. Majukumu ya Serikali ya Muungano yatakuwa yapi ?? Wanasema yatabakiwa na Mambo 7 kati ya Mambo 27 ?? !!! Tunatakiwa kuwa na Serikali Moja, Nchi Moja, Wananchi Wammoja ambao ni Wazalendo, Waadilifu.
 
Hili linaweza kuwa baya kuliko yote,nimeangaika kutafuta kama kuna nchi duniani yenye mfumo kama huu nimekosa.Huenda Tanzania ikaweka historia kwa jambo la kipuuzi kama hilo.Mpaka hapa tulipo tunatakiwa kupunguza kwani ni gharama sana kuwalipa,unaweza ukaangalia uwiano wa wanawake bungeni duniani kwa kila nchi na Tanzania ikiwa ni ya 20;Women in Parliaments: World Classification
Siyo kila kitu kutazamia unadhani kila kitu tunachofanya tanzania lazima kifanane na mataifa ya nje huo ni utumwa jiamini,jitegemee.
 
Back
Top Bottom