Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Mwanakijiji naona unataka kurefusha maneno.
Kwanza jiulize kwa nini serikali tatu nini kimetatiza?(Wazanzibar)
wanasemaje waznz pamoja na kuwa na serikali?(Tanganyika inatunyonya sisi tulikuwa na kiti chetu UN mwaka 1963 tunakitaka).


Sasa leo mwanakijiji anataka kuwaambia kuwa vunjeni SMZ na hamtakuwa na rais tena znz bali gavana wa jimbo hili?wataelewa lugha hii?
sasa hakuta kuwa tena na nchi inayoitwa znz bali TZ yenye rais mmoja na makao yake ni dodoma na gavana wa jimbo hili atamtii na kumuheshimu rais wa tz kama kiongozi wa nchi? wataelewa?

Labda lugha ya busara upendekeze muungano ufe kila nchi iwe na serikali moja.
 
...Sioni namna ya Wazanzibar kuridhia mfumo wowote wa Muungano, hivyo Nasema NDIYO kwa Serikali tatu kwa sababu moja kubwa, hii ni njia rahisi na ya wazi kuelekea kwenye serikali moja ya Jamhuri ya Tanganyika...

Serikali moja ndo jibu. Utakuwaje na nchi ndani ya nchi. Tunawalea tu hawa wala urojo. Tikumbali tu haya matakwa yao, next wanaomba kiti UN na kuvunja muungano. Kisha wataanza na watu wa Kigoma kuomba wawe nchi. Tuwe na serikali moja au tuendelea tulivyo au tuachiwe Jamhuri yetu ya Tanganyika.
 
Mi nahitaji sserikali yangu ya Tanganyika irudi, hawa wazanzibar mi hata sijui wanafaida gani, kwanza ni wabaguzi hatuwataki waende kwao kila mtu anabaki na nchi yake
 
Poem Africas plea captures Zanzibars feelings on union.

You meddle, interfere
in my affairs
as if they were yours
and you were me

You are unfair unwise
foolish to think
that i can be you
talk, act
and think like you

God made me me
He made you you
For God's sake
Let me be.
 
mzee mwanakijiji, naomba nitofautiane kabisa na wewe, kwanza hebu fikiria ukija na wazo la serikali moja wazanzibari watareact vipi! ndio utakuwa mwanzo wa kuanzishwa vikundi vya revolution struggle! umeshalifikilia hilo?

kwa sasa tuu na muundo uliopo wa serikali mbili kuna kundi linaona limemezwa! je itakuwaje pindi litakapo mezwa kwe na kuwa na serikali moja? si tutakuwa tunajitangazia vita?

kwa upande wangu naona kwa uhuru na usalama wa pande zote mbili serikali tatu itawapa amani wazanzibari! na hata huku kwetu pia! hebu zama ufikiri kiundani kidoogo

Nakubaliana na wewe 100%.
Kupendekeza nchi moja ni next to impossible. Tume imejaribu kushika mawili - kuwafurahisha wazanzibar na wakati huo huo kulinda Muungano. Wamefunika kikombe mwanaharamu apite. Halafu wanaruhusu nchi wanachama kuwa na mahusiano na hata kukopa kutoka nchi au mashirika ya nje. Is this possible?

Kwa hiyo, mimi namshauri mzee wangu mwanakjiji akubali kuwa hoja yake haitawezekana kwa 100%. Haitawezekana hata kwa bunduki upande wa Zanziabar maana wanaotakiwa kuagiza askari pamoja na askari wote hawataki Muungano sawia. Labda kama mzee mwanakijiji anataka tuwavamie Wazanzibar kimabavu.

Anayetetea muungano kwa upande wa Zanzibar kwa sasa ni Dr Shain na mawaziri wachache sana - na wamezidiwa, yeye ndo inaonekana amewakana wenzake kwenye kudai Zanzibar HURU. Na kuna tetesi kuwa ameahidiwa kitu 2015 ktk serikali tarajiwa ya Muungano.
 
...tanganyika huru haiepukiki,kwanza zanzibar wameshajitenga,kilichobaki ni maandishi tu ya vitabuni, na naomba mchakato wa kuunda katiba ya bara uanze rasmi ili tupate katiba ya bara mapema kabla ya 2015...
 
Mzee Mwanakijiji bila hata kumung'unya maneno, Huu ulioleta hapa ni USANII wa kisiasa. Kwa vile watanzania wengi nao ni bendera fuata upepo ili mradi fulani kasema jambo, basi wengi wanakubaliana na wewe.

Unajaribu kujenga hoja ambayo unafahamu kabisa kwamba haitapata jibu katika mabaraza ya katiba au bunge la katiba, siamini kama hujui hiki anachojaribu kukijengea hoja bali ninaamini unajenga hoja for the sake of argument with damn all.

Tume ya Warioba ilipopewa HADIDU ZA REJEA zinazotakiwa kuzingatia mambo fulani, ni wananchi wachache sana walizipinga huku vyama vyetu vyote vya siasa na pressure groups vikiridhia na kuzikubali

Hadidu za rejea ndiyo zimezaa hili "DUDU" la rasimu ya katiba ambayo pamoja na mambo mengine, msingi wake mkuu ulikwa kuwepo na JAMHURI YA MUUNGANO na mfumo wa utawala wa KIJAMHURI katika kipengele cha 9(2)(i) and (iii).

Watanzania wanapiga kelele sasa hivi, walikuwa wapi kuikataa kwanza hii misingi iliyotakiwa izingatiwe wakati hata mchakato wa katiba haujaanza pale iliposema,

Katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika Hadidu za Rejea, Tume itazingatia yafuatayo:-
a) Misingi 9(2)
Tume itaongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo:-
i. kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano;
ii. uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama;
iii. mfumo wa kiutawala wa kijamhuri;
iv. uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
v. umoja wa kitaifa, amani na utulivu;
vi. uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura;
vii. ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu;
viii. utu, usawa mbele ya Sheria na mwenendo wa sheria;
ix. uwepo wa Jamhuri ya Muungano isiyofungamana na dini yoyote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu; na
x. kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na kuboresha masuala hayo 9(3).

Watanzania tunakuwa wanafiki na kama siyo wanafiki basi tunafanya jambo bila kufahamu.

Hili la kutupilia mbali muungano lingefanikiwa kama Tume ya Jaji Warioba ingeachiwa wazi mlango wa maamuzi bila kufungwa kwa kupewa misingi ya kuzingatia.

Kuanza kuilaumu tume ya Jaji Warioba ni kupotoka au kutojua kile unacholaumu na chanzo chake.

Watu wa kulaumiwa ni Rais wa Jamhuri, Rais wa Zanzibar, Technical team ya CHADEMA inayoongozwa na Mh. Tindu Lissu na bila kuwasahau Wananchi wenyewe. Tujiangalie kwanza sisi hasa watu wa Tanganyika kabla kuanza kunyosha vidole kwa watu wengine.

Unachokisema ni sawa na ndege imeisha TAKE OFF halafu unaomba mlango ufunguliwe ili ushuke kwa vile umesahau kitu fulani kukifanya kabla ya kupanda.

IT'S TOO LATE!.

IT'S A LESSON TO BE PROACTIVE
 
...tanganyika huru haiepukiki,kwanza zanzibar wameshajitenga,kilichobaki ni maandishi tu ya vitabuni...
baada ya Tanganyika kuwa huru; unakubaliana na mimi kwamba itapendeza tukibadili jina na kuiita "Jamuhuri ya Tanzanite"? tehe! tehe! tehe!
 
baada ya Tanganyika kuwa huru; unakubaliana na mimi kwamba itapendeza tukibadili jina na kuiita "Jamuhuri ya Tanzanite"? tehe! tehe! tehe!
..kweli eeeh, ! kama ivorycoast ..teh teh a.k.a kinanacoast..,
 
Mimi naona unazunguka sana kaka, Tuvunje tuu huu muungano, hivi huu Muungano ni kwa maslahi ya nani? kwanini hawataki kujaribu kujua kwa kura za maoni kama wananchi wa pande mbili hizi bado wanauhitaji muungano ama la, Kwa survey yangu isiyo rasmi inaonyesha Wazanzibar walio wengi hawautaki Muungano na Watanganyika walio wengi hawataki Muungano, je ninani anautaka huu Muungano?

'Via Mobile'
 
Huu ni mwisho wa CCM, maana hata wenyewe yanawageuka mauzauza yao ndio hali inakuwa hivi. Ulisikia wapi jimbo moja wabunge wawili tena kijinsi! Hii ni hatari sana, Tz angalieni CCM inakotupeleka jamani, maamuzi ni yetu!
 
Kiufupi muungano hatu utaki , tunataka tanganyika yetu, let znz go!!
 
Tumechoka kuwabeba wengine.. wajitegemee.. ama tatu ama moja.. mbili basi.
 
jamani mkiungana hamuwezi kutengana? mbona mnaupenda sana muungano huu kunani? kuhusu majimbo kuwa na wagombea wawili wanawake na wanaume bado ni muendelezo wa viti maalumu, jina tu ndo limebadirika, maana watapambana wanawake kwa wanawake, ni vyema kila jimbo moja mbunge mmoja, waache wapambane na wanaume si bado kuwaweka kwenye kundi.
 
Mzee Mwanakijiji
utaandika sana mwaka huu,nilitaka kushangaa usipinge serikali tatu,ningestaajabu sana.Msimamo wa viongozi wa imani yako ni huu wa serikali moja au muungano uvunjike.Msimamo huu umekuja baada ya wznz kujitambua na kustukia hila zenu.Sasa hakuna upenyo wa kupeleka mambo yenu kule.Rasimu ya katiba itaendelea vizuri na hatimaye tutapata katiba tuitakayo.Endelea kuandika utakavyo lakini maoni ya wengi yataamua.Pole mfia dini

Katika makala ya Mwanakijiji hakuna sehemu amezungumzia dini, wewe ndiyo umeingiza mambo ya dini kwenye mjadala, kati yako na MM ni nani mfia dini?
 
Mkuu saa nyingine politics is about compromise. There are many different interests and sometimes you have to find a middle ground. Huo ndio ukweli. A federal system is usually a system of compromise when there are irreconcilable differences when it comes to power sharing. You cannot always get everything you want but you end up with what you can leave with.

Binafsi I prefer serikali moja ila ni vigumu kuunda serikali moja kwenye nchi mbili zilizo ungano haswa kama upande mmoja tayari una vugu vugu ya kutaka uhuru kamili. Kwa maana hiyo ukisema uwe na serikali moja inabidi uruhusu Wazanzibar waende zao kwa maana hawato kubali serikali moja kwa vile wataona ina nyonya nchi yao.

Pili, tukumbuke hii itakua federal system. Tanganyika na Zanzibar haitakua na raisi nk itaongozwa na gavana. Tofautisha na kama wangeuchukua mfumo wa sasa na kuongeza raisi wa Tanganyika. Serikali inayo ongozwa na gavana na serikali inayo ongozwa na raisi ni vitu viwili tofauti mkuu. I'm sure wewe of all people unaelewa maana ya shirikisho au federal system.

At the end of the day mimi naona this is a fair enough compromise. Kama wenzetu ambao wana taka eneo lao litambulike hawa wezi kubali serikali moja ni heri mara mia basi na Tanganyika iwe na serikali yake.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba wanzanzibari hawataki muungano, wanalazimishwa kwa maslahi ya nani?,
Maoni ya wazanzibar yamezingatiwa katika rasimu?
 
Hivi huyu Ritz ni mtoto wa rais au tu nimeshindwa kumwelewa Mkira aliposema "utawala aw baba yako ukipita HATA wewe na yeye..." ? Nadhani "aw" alimaanisha "wa". Naomba nifahamishwe huenda bado nimo kwenye "mapango" kama jina langu la humu linavyosomeka!
 
Mkuu saa nyingine politics is about compromise. There are many different interests and sometimes you have to find a middle ground. Huo ndio ukweli. A federal system is usually a system of compromise when there are irreconcilable differences when it comes to power sharing. You cannot always get everything you want but you end up with what you can leave with.

Binafsi I prefer serikali moja ila ni vigumu kuunda serikali moja kwenye nchi mbili zilizo ungano haswa kama upande mmoja tayari una vugu vugu ya kutaka uhuru kamili. Kwa maana hiyo ukisema uwe na serikali moja inabidi uruhusu Wazanzibar waende zao kwa maana hawato kubali serikali moja kwa vile wataona ina nyonya nchi yao.

Pili, tukumbuke hii itakua federal system. Tanganyika na Zanzibar haitakua na raisi nk itaongozwa na gavana. Tofautisha na kama wangeuchukua mfumo wa sasa na kuongeza raisi wa Tanganyika. Serikali inayo ongozwa na gavana na serikali inayo ongozwa na raisi ni vitu viwili tofauti mkuu. I'm sure wewe of all people unaelewa maana ya shirikisho au federal system.

At the end of the day mimi naona this is a fair enough compromise. Kama wenzetu ambao wana taka eneo lao litambulike hawa wezi kubali serikali moja ni heri mara mia basi na Tanganyika iwe na serikali yake.

Hapo nyekundu ndio point, kwa nini tunalazimisha muungano?
Unaweza kuniambia ni manufaa gani ya msingi sana ambayo mimi Mtanganyika wa Lyamidati huku Shinyanga ninapata kutokana na Muungano?
Kwa nini tumekubali nchi yetu Tanganyika kupotea, lakini Zanzibar imebaki na hadhi yake?
Tunabembeleza kitu gani?
Je ni kweli sisi watanganyika tunawanyonya wazanzibar ndio maana tunawang'ang'ania?
 
Hapo nyekundu ndio point, kwa nini tunalazimisha muungano?
Unaweza kuniambia ni manufaa gani ya msingi sana ambayo mimi Mtanganyika wa Lyamidati huku Shinyanga ninapata kutokana na Muungano?
Kwa nini tumekubali nchi yetu Tanganyika kupotea, lakini Zanzibar imebaki na hadhi yake?
Tunabembeleza kitu gani?
Je ni kweli sisi watanganyika tunawanyonya wazanzibar ndio maana tunawang'ang'ania?

Mkuu tatizo ni kwamba ni vigumu kwa nchi yoyote kuachie hata kipande kidogo cha nchi yake ijitengee. Ndio maana hata Wakenya na Wauganda miaka miwili liyopita waligombea kikisiwa ambacho hakina thamani yoyote. Ni vigumu nchi yoyote kuachie eneo la nchi ijiondoe. Mimi siyo supporter wa muungano ila kama mwanafunzi wa mambo ya siasa na diplomasia naelewa ugumu wa kuiachia Zanzibar. Politically its not an easy thing.
 
Back
Top Bottom