Mzee Mwanakijiji bila hata kumung'unya maneno, Huu ulioleta hapa ni USANII wa kisiasa. Kwa vile watanzania wengi nao ni bendera fuata upepo ili mradi fulani kasema jambo, basi wengi wanakubaliana na wewe.
Unajaribu kujenga hoja ambayo unafahamu kabisa kwamba haitapata jibu katika mabaraza ya katiba au bunge la katiba, siamini kama hujui hiki anachojaribu kukijengea hoja bali ninaamini unajenga hoja for the sake of argument with damn all.
Tume ya Warioba ilipopewa HADIDU ZA REJEA zinazotakiwa kuzingatia mambo fulani, ni wananchi wachache sana walizipinga huku vyama vyetu vyote vya siasa na pressure groups vikiridhia na kuzikubali
Hadidu za rejea ndiyo zimezaa hili "DUDU" la rasimu ya katiba ambayo pamoja na mambo mengine, msingi wake mkuu ulikwa kuwepo na JAMHURI YA MUUNGANO na mfumo wa utawala wa KIJAMHURI katika kipengele cha 9(2)(i) and (iii).
Watanzania wanapiga kelele sasa hivi, walikuwa wapi kuikataa kwanza hii misingi iliyotakiwa izingatiwe wakati hata mchakato wa katiba haujaanza pale iliposema,
Katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika Hadidu za Rejea, Tume itazingatia yafuatayo:-
a) Misingi 9(2)
Tume itaongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo:-
i. kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano;
ii. uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama;
iii. mfumo wa kiutawala wa kijamhuri;
iv. uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
v. umoja wa kitaifa, amani na utulivu;
vi. uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura;
vii. ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu;
viii. utu, usawa mbele ya Sheria na mwenendo wa sheria;
ix. uwepo wa Jamhuri ya Muungano isiyofungamana na dini yoyote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu; na
x. kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na kuboresha masuala hayo 9(3).
Watanzania tunakuwa wanafiki na kama siyo wanafiki basi tunafanya jambo bila kufahamu.
Hili la kutupilia mbali muungano lingefanikiwa kama Tume ya Jaji Warioba ingeachiwa wazi mlango wa maamuzi bila kufungwa kwa kupewa misingi ya kuzingatia.
Kuanza kuilaumu tume ya Jaji Warioba ni kupotoka au kutojua kile unacholaumu na chanzo chake.
Watu wa kulaumiwa ni Rais wa Jamhuri, Rais wa Zanzibar, Technical team ya CHADEMA inayoongozwa na Mh. Tindu Lissu na bila kuwasahau Wananchi wenyewe. Tujiangalie kwanza sisi hasa watu wa Tanganyika kabla kuanza kunyosha vidole kwa watu wengine.
Unachokisema ni sawa na ndege imeisha TAKE OFF halafu unaomba mlango ufunguliwe ili ushuke kwa vile umesahau kitu fulani kukifanya kabla ya kupanda.
IT'S TOO LATE!.
IT'S A LESSON TO BE PROACTIVE