Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Tangu jana ilipotolewa hii rasimu nimepiga kelele sana juu ya muundo wa serikali tatu. Haijaniingia akilini ilikuwaje wanasheria wetu wabobezi kwenye hii tume wakaja na rasimu ya namna hii. Kwanza wamewachanganya wananchi kwa kudhani serikali sasa itakuwa ndogo, wakati huo wananchi wameshindwa kuelewa kwamba rasimu hii ni mzigo mzito na ni namna ya ulevi wa kisiasa kujitengenezea madaraka.

Jana tayari wenzetu wametoa matamko, kwamba wao wanataka serikali yenye madaraka kamili, kwamba hata hayo mambo saba yaliyobaki wataendelea kuyadai hadi watakapopata madaraka kamili. Maana yake ni kwamba, kelele za muungano zitaendelea hata baada ya hii rasimu kama itapitishwa (serikali tatu) wanataka serikali yao yenye madaraka kamili.

Hawa wanatoka kwenye chama ambacho most likely kinaweza kushika madaraka zanzibar wakati wowote (rejea historia za chaguzi zilizopita) kwa hiyo hawataacha kudai, wataendelea na kelele zao, na kwa hakika kama watakuwa madarakani, watashinikiza kujiondoa kwenye muungano ili wawe na madaraka kamili.

Inawezekana tume ya jaji haikuzingatia maoni halisi ya wazanzibar wengi, badala yake maoni yao yalimezwa na yale ya wabara ambao siku zote wamekuwa wakitaka serikali tatu. Ikaonekana wengi wanataka serikali tatu.

Mtanzania yeyote anayeitakia mema nchi yetu hawezi kutetea mfumo wa serikali tatu. Binafsi maoni yangu ni kwamba, ama serikali moja, au tuuvunje muungano tubaki na mahusiano ya kawaida ya undugu.

Najua wanasiasa wetu hili limewafurahisha sana maana fursa za kisiasa zitaongezeka sambamba na kuendeleza mashindano ya kutafuna nchi. Maana sasa kutakuwa na majogoo matatu pale juu huku kila moja likining’inia juu ya watendaji wake.

Nakubaliana na wewe mkuu. Hawa jamaa wametudangaya. Kwamba mawaziri 15, wabunge 75!!!! Hawa mawaziri 15 ni wa muungano, wa bara ama wa zanzibar ama vyote???? Kuna bunge la muungano, bunge la bara na baraza la wawakilishi. Hii mizigo yote ya nini? Bila kuwa na katiba ya Bara , kama ambavyo kuna katiba ya Zanzibar tayari; itakuwa makosa kupitisha katiba ya muungano!!! Lazima hizi katiba zote zifanyike SAMBAMBA, ili wananchi kama wanapiga kura wajue wakifanyacho!!!!!!!
 
Mimi nataka serikali moja tu. Serikali ya Tanganyika tu. Nimechoka kusikia kelele hizi. Zanzibar wapewe nchi yao
 
Mkuu tatizo ni kwamba ni vigumu kwa nchi yoyote kuachie hata kipande kidogo cha nchi yake ijitengee. Ndio maana hata Wakenya na Wauganda miaka miwili liyopita waligombea kikisiwa ambacho hakina thamani yoyote. Ni vigumu nchi yoyote kuachie eneo la nchi ijiondoe. Mimi siyo supporter wa muungano ila kama mwanafunzi wa mambo ya siasa na diplomasia naelewa ugumu wa kuiachia Zanzibar. Politically its not an easy thing.
If that is it,

Then they should force one government, one president, one country, one people as says Mwanakijiji,

And if they want federation, they should be governors and no president for Zanzibar, but for the proposed federation, un acceptable.
 
[h=5]Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?[/h]Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi! Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo. Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea. Na maneno mengine mengi.... In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
Nyerere keshapigwa bao na Jumbe. Kilichobaki ni vilio tu vya kuondoa soo! Kwi kwi kwi!!!!
 
Mkuu Mwanakijiji,
Na hili hili la wabunge wawiliwawili (jinsia tofauti) kwa jimbo unalionaje? Mbona kwa wenzetu waliotutangulia kwenye maswala ya demokrasia hatujawahi kusikia upuuzi huu? Kituko tulicholetewa na Warioba hakilingani na gharama tulizowalipa.

Hawa ma-CCM wanawaza uzinzi tu. Ni bora basi kuwe na mbunge wa vipofu, mbunge wa viwete, mbunge wa albino n.k
 
baada ya Tanganyika kuwa huru; unakubaliana na mimi kwamba itapendeza tukibadili jina na kuiita "Jamuhuri ya Tanzanite"? tehe! tehe! tehe!

mkuu, itabidi iitwe Tanganite, na yale madini yabadilishwe jina.
 
Hapana Mzee Mwanakijiji,serikali tatu ndiyo suluhu na isipoweza kutawalika/kuelewana ndiyo mwanzo wa kutengana nao walime vizuri karafuu, maana sijawahi ona tija ya huu Muungano,serikali moja wazanzibar watafaidi sana kama sasa au zaidi.
 
Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?

Hapana Sabini mara Saba.Badala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma.

Na hiki wanachokita Shirikisho la Afrika mashariki kwa mwendo huu itakuwa ndoto

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Mfumo huu ndiyo ungekuwa Muwaarobaini wetu na hatua moja kwenda shirikisho la Afrika mashariki ambapo tungeweza kuwashawishi wenzetu wa Kenya na wengineo kuondoa mipaka ya kikoloni lakini wapi-wazee/Tume chini ya Warioba bado wameturudisha mwaka 1954-1961.

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.

Mkuu MKjj.
Usiache kuleta Elimu hii kupitia Makala kwenye Gazeti ili wazanzibar na watanganyika waelewe kinachoendelea maana nawaonea huruma Wapemba na Unguja na watanganyika mzigo ulioko huko mbele ya safari hawatauweza.
Lakini hiyo haitoshi lazima ujio wa Tanganyika utakuwa na Madhara makubwa kwa Wapemba na Unguja hasa suala la Ardhi na washauri wajiandae !
 
Mkuu Mzee MwanakijijiTunahitaji serikali moja iwe ya kuunganisha na Zanzibar au Tanganyika peke yake, ila we only need one.

Na muhimu zaidi tunahitaji DIKTETA wa kukomesha rushwa na ufujaji wa mali za umma! Nchi zetu masikini kuongelea demokrasia na utawala bora wakati wananchi wana hali ngumu ni mapema sana.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na heshima zote Mzee Mwanakijiji hapo sikubaliani na wewe hata kidogo.

Umetoa sababu zako kwa nini hupendelei tuwe na serikali tatu, kubwa zaidi ni gharama kubwa ya kuziendesha hizo serikali wewe umetumi aneno 'mzigo mkubwa'. Kwa upande wangu mimi ninaona serikali tatu ndiyo njia peke yake itakayotuwezesha watanganyika kubana matumizi ya serikali yetu, na pia kupanga na kufuatilia vizuri matumizi mabaya ya pesa na madaraka yanayofanyika sasa hivi kwa visingizio vya kuwa na Serikali ya Muungano peke yake (kwa huku bara) wakati wenzetu wa visiwani wana serikali yao ya Mapinduzi. Kumekuwa na masuala mengi sana ambayo ukiyachunguza hayahitaji kuwemo kwenye Muungano lakini Serikali ya Muungano inaingia gharama kuyatekeleza kwa ajili ya wenzetu wa upande wa pili wa Muungano.

Tukiangalia mfano hata jana tu Mbunge Maua Daftari amesema ya kuwa Zanzibar inachangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Muungano. Ninachoona mimi ni kuwa tuwe na serikali tatu lakini kila serikali (ya Tanganyika na ya Mapinduzi) ziweze kujitegemea zenyewe. Wazanzibari wenyewe kila kukicha wanalalamikia Muungano, kuna wanaoona kama 'wanakaliwa kimabavu' na serikali ya Muungano pamoja na kwamba serikali yao inategemea sana kifedha serikali ya Muungano. Ili kuondokana na hii dhana potofu waliyojijengea, ushauri wangu wapewe hiyo serikali yao waiendeshe wenyewe kabisa. Wakiamua kujiunga na OIC wapate misaada wawe huru kufanya hivyo. Wawe na Rais wao mwenye mamlaka kamili nchini mwake na ambaye wananchi wake watamchagua naye atawajibika kwao tu. Wawe na Bajeti yao na fungu lao la pesa lisilokuwa na uhusiano wowote na fungu la pesa la serikali ya Tanganyika. Halafu na serikali ya Tanganyika iwajibike kwa watanganyika peke yetu. Fungu la pesa letu liwe kwa matumizi ya Tanganyika. Halafu tuwe na Serikali ya Shirikisho (Federation). Hapo sasa kila serikali itakuwa na wajibu wa kuchangia kwenye Federal Government. Serikali ya Shirikisho iwe ndogo na yenye ufanisi wa hali ya juu. Hatuhitaji kuwa na mawaziri wengi kwa kuwa masuala muhimu mengi yatakuwa yanahudumiwa na serikali zetu mbili za Tanganyika na Zanzibar.

Na hizo serikali za Tanganyika na Zanzibar ziwe na uhuru wa kupanga sheria zake kutokana na utashi wa watu wake, bila ya kuingiliwa na Serikali ya Shirikisho. Mipaka ya serikali hizo tatu iwekwe bayana ili kila mmoja (viongozi mpaka raia) waelewe mipaka ilipo kusiwe na kuingiliana kwa madaraka. Serikali za mitaa (local governments) zitumike kufanya kazi ndani ya serikali zetu za Tanganyika na Zanzibar, ziweze kukusanya kodi na kupanga matumizi yake bila kuingiliwa na serikali ya shirikisho. Halafu kutoka kwenye hiyo kodi ziweze kutoa fungu kwa serikali ya Shirikisho. Hapo sasa itakuwa bayana wapi pesa inaliwa, wapi wameshindwa kukusanya mapato na ni kwa sababu gani. Kwa mtazamo wangu hata ufisadi utaweza kudhibitiwa vizuri zaidi kwa njia hiyo.

Mungu Ibariki Tanganyika!!!
 
Hoja hii naunga Mkono.

Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?

Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi....

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
 
Haya ni maoni niliyoyaandika kwenye uzi mwingine na nayarudia hapa. Nayaweka hapa bila kupitia posts za wanaJF wengine waliochangia uzi huu.
Kama kweli watu wa Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara wana kweli nia ya kuungana kwa nini wanawekeana vikwazo vya kuungana ...hoo mara serikali tatu mara serikali ngapi !

Kwa nini mnataka kufufua utaratibu utakozidi dololesha uchumi wa nchi na wananchi wa kawaida(maana ndiyo wanabebeshwa mzingo huu)!?

Narudia kama hatuko makini/serious kuungana kama nchi mbili na kuwa na serikali moja....basi twende kama nchi mbili zinazojitegemea huko EAC na AU.

Vinginevyo nitaendelea kuamini wanaolazimisha serikali tatu wanatafuta vyeo ili wajilimbikizie mali.

Na kwa kweli kwa sasa sitaki/sipendi tuendelee na mfumo wa sasa wa serikali ya JMT na SMZ. Ni ama serikali mbili huru ama Serikali moja ya Jamhuri ya Muungano ya Watu wa Tanzania.

Mkiniita kesho na kesho kutwa kuniuliza msimao wangu nitajibu hivi hivi !!
 
...Kuna mara nyingine hoja nyingine husababisha more complications kuliko solutions kwa maswala ya wazi....mojawapo ni hii hoja ya Mwanakijiji...

...Mimi sielewi kutakuwa na ugumu gani kwa serikali tatu.....wakati ndizo zinaonekana kutoa majibu....haswa kwa wale waliokuwa wanalalamika kutotendewa haki ndani ya muungano(haswa wazanzibar)....

Wewe mwenyewe mwanakijiji umekua mara zooote humu unawaambia wazanzibar wawe free kujiondoa kwenye muungano.....leo wamepewa uhuru wa kujiamulia mambo yao(e.g kujiunga na jumuiya za kimataifa etc)....wewe unaongeza complications zako za sijui majimbo etc etc....I really can't get your logic on this....

....Nilitegemea uwe wa kwanza kupongeza tume on this issue (serikali tatu).....lakini umeonekana kutoridhika na uamuzi huu...this to me is ridiculous....being fair to some important decisions sometimes helps my friend....

...Kuhusu hili la matumizi ya gharama tele kuendesha serikali tatu...well....haya ndio malipo ya democracy....kama mambo yatafanyika kwa usahihi...bila rushwa...na serikali zikapunguza wingi wa mawaziri na viongozi waandamizi...then lazima mambo yataenda.....Tunalalamikia gharama hapa kwasababu tumekua tunaishi kwenye mfumo mbovu wenye matumizi mabaya ya raslimali za nchi ndo maana tunaona huu utakua mzigo.....

....Mchango wako wa kupunguza gharama kwa serikali ya Tanzania/Tanganyika utahitajika sana katika kwanza uundaji wa katiba na pia serikali yenyewe ya TZ bara/Tanganyika......I think its high time for you to come to TZ my brah...to offer your inputs physically.....now that there will be opportunities for many to be leaders in TZ (if they will pass this constitutional draft ofcourse)
 
Kwa viongozi tulionao bila shaka hakuna anaeweza kufungua mdomo wake kushauri kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ivunjwe ili tubaki na serikali moja ya Muungano. Tutazunguka sana ila dawa ni kuivunja hiyo serikali ya Unguja!
 
Serikali tatu hapana! Kila mtu kivyake, hiyo ndo sahihi!
 
Kwa kweli ni upuuzi; as a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?

Mzee Mwanakijiji hii hoja ni zaidi ya upuuzi, huu ni usawa kweli au tunataka kuongeza mzigo kwenye serikali? Kuna maana gani ya kuwa na wawakilishi wa jinsia mbili tofauti katika jimbo moja? Kwenu bungeni wanaenda kuwakilisha jinsia au maoni na matatizo ya wananchi wao? Tunaabudu jinsia au tunataka maendeleo? Huu usawa nao wa kijinsia tusipouangalia vizuri, tunatengeneza bomu lingine la kudidimiza nchi!!! Nimekerwa na hili pendekezo! :heh:
 
Last edited by a moderator:
Nchi moja KELELE hazitaisha, sisi tunataka kuishi kwa starehe bwana. Watu wavivu na wenye wivu hudai mambo ya hovyo hovyo. Cha Muhimu ni kuhakikisha Serikali ya Muungano kwa vile ina mambo 7 tu iwe ndogo sana. Na serikali ya Tanganyika iwe na waziri mkuu tu na kupunguza mrundikano wa vyeo usiojali uhalisia wa kazi zenyewe. Haya tutayakomesha ndani ya Katiba ya Tanganyika. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa wilaya n.k wakae macho.
 
Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?

Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi....

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.

Mzee mwanakijiji na wengine kutokana na mawazo yenu mpo sahihi ila kutokana na hao watu wa Zanzibar mmekosea na hawapo tayari kukubali, cha muhimu katoeni hii elimu Zanzibar ili watoe maoni. kama wao wapo tayari sisi tuwakatalie vya nini yakiwashinda watarudi kwenye muungano mmoja ngoja kwanza wakajitegeme. Mtoto akililia wembe mpe. Sisi uku bara tumechoka na malalamiko ya muungano.
 
Back
Top Bottom