Tangu jana ilipotolewa hii rasimu nimepiga kelele sana juu ya muundo wa serikali tatu. Haijaniingia akilini ilikuwaje wanasheria wetu wabobezi kwenye hii tume wakaja na rasimu ya namna hii. Kwanza wamewachanganya wananchi kwa kudhani serikali sasa itakuwa ndogo, wakati huo wananchi wameshindwa kuelewa kwamba rasimu hii ni mzigo mzito na ni namna ya ulevi wa kisiasa kujitengenezea madaraka.
Jana tayari wenzetu wametoa matamko, kwamba wao wanataka serikali yenye madaraka kamili, kwamba hata hayo mambo saba yaliyobaki wataendelea kuyadai hadi watakapopata madaraka kamili. Maana yake ni kwamba, kelele za muungano zitaendelea hata baada ya hii rasimu kama itapitishwa (serikali tatu) wanataka serikali yao yenye madaraka kamili.
Hawa wanatoka kwenye chama ambacho most likely kinaweza kushika madaraka zanzibar wakati wowote (rejea historia za chaguzi zilizopita) kwa hiyo hawataacha kudai, wataendelea na kelele zao, na kwa hakika kama watakuwa madarakani, watashinikiza kujiondoa kwenye muungano ili wawe na madaraka kamili.
Inawezekana tume ya jaji haikuzingatia maoni halisi ya wazanzibar wengi, badala yake maoni yao yalimezwa na yale ya wabara ambao siku zote wamekuwa wakitaka serikali tatu. Ikaonekana wengi wanataka serikali tatu.
Mtanzania yeyote anayeitakia mema nchi yetu hawezi kutetea mfumo wa serikali tatu. Binafsi maoni yangu ni kwamba, ama serikali moja, au tuuvunje muungano tubaki na mahusiano ya kawaida ya undugu.
Najua wanasiasa wetu hili limewafurahisha sana maana fursa za kisiasa zitaongezeka sambamba na kuendeleza mashindano ya kutafuna nchi. Maana sasa kutakuwa na majogoo matatu pale juu huku kila moja likininginia juu ya watendaji wake.
Nakubaliana na wewe mkuu. Hawa jamaa wametudangaya. Kwamba mawaziri 15, wabunge 75!!!! Hawa mawaziri 15 ni wa muungano, wa bara ama wa zanzibar ama vyote???? Kuna bunge la muungano, bunge la bara na baraza la wawakilishi. Hii mizigo yote ya nini? Bila kuwa na katiba ya Bara , kama ambavyo kuna katiba ya Zanzibar tayari; itakuwa makosa kupitisha katiba ya muungano!!! Lazima hizi katiba zote zifanyike SAMBAMBA, ili wananchi kama wanapiga kura wajue wakifanyacho!!!!!!!