Nonda;6517850]Isaac JK Kama ulifuatilia utoaji wa maoni kuhusu Katiba mpya hawa watu walisema "waachiwe wapumue".
Kwani walifanya jaribio lipi la maana na akili ambalo tunaweza kusema waliamua wapumue?
Je, waliwahi kumwita makamu wa rais arudi kutoka bara, waliwahi kupeleka mswada bungeni au BWL, waliwahi kuzuia wabunge wao kuja Dodoma, waliwahi kuwaita viongozi katika utumishi wa JMT? Jibu ni hakuna.
Pili hao viongozi wanaofanyakazi katika JMT na wale waishio Tanganyika ambao ni wengi kuliko walioko znz, wao siyo wznz na je hawakuona umuhimu wa kupumua.
Kuruka ruka barabarani hovyo siyo njia ya kupumua, ilikuwa ni movement isiyojua inakwenda wapi
]Kwa sababu hadidu rejea alizopewa Warioba na Tume anayoingoza ni kuwa "Muungano ujadiliwe kwa nia ya kuuboresha tu" na sio uwepo wake au kutokuwepo kwake. Wazanzibari waliuona mtego wa JK na walibuni kitu walichokiita "Muungano wa Mkataba".Walipendekeza mamlaka kamili kwa Zanzibar , mamlaka kamili kwa Tanganyika na Muungano wa mkataba
Nonda si kweli! Wazanzibar hawakuwa naakili hiyo.
Wangekuwa nayo basi wasingeweka jitihada, akili na fikra zao katika kutafuta wajumbe kwa uwiano. S
isi tuliona hilo tukaonya kuwa kuna tatizo tukapaza sauti
Kuhusu kupendekeza mamlaka kamili, huwezi kuwa na malaka ukiwa huna vyombo vya ulinzi na usalama.
Hakuna mamlaka kamili kwasababu unamkumbuka Mliberali alikamatwa kama mwizi wa kuku na kusweka ndani.
Unakumbuka mwingine aliitwa na kuambiwa stop,Unakumbuka yule aliyetishia kurudi na ASP kutoka Dodoma alipotoka nje ya ukumbi kuanzia mlinzi wake hadi makanda wa polisi wamehamishwa.
Kuanzia hapo hatujamsikia tena! kwanza lazima uwe na ulizi na usalama kitu ambacho znz haitaki kwasababu haijawahi kuwa na bajeti toka mwaka 1964 na uchumi haurusu. Ndizo sababu za mkataba.
Katika mambo ya mkataba hutamsikia mzanzibar akizungumzia ulinzi na usalama, in fact wanasema wazi wanafaidika na hilo
Katika upokeaji wa maoni kutoka kwa wananchi, Tume ya Warioba ilipata wakati mgumu ilipofanya kazi zake kule Zanzibar na Wajumbe wa Tume walionekana kukerwa na maoni yaliyodai Zanzibar huru,Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa,kufufuliwa kwa Tanganyika na muungano wa mkataba
Katika wajumbe 30, 15 wanatoka znz, sasa unaposema walikereka ina maana hata wajumbe wa znz walikereka.
Wakati mgumu uliletwa na vurugu za wanamapinduzi na waliberali kuchapana makonde si tume.
Hukufuatilia au unapotosha
Kama Tume ingeyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wazanzibari (kitakwimu inasemwa ni asilimia 66) basi Tume ya Warioba ingekuja na mapendekezo ya kuifufua katiba ya Tanganyika na serikali ya Tanganyika na bila ya kupoteza muda, mchakato wa kuandika katiba mpya ya Tanganyika ungeanzishwa
Ndiyo maana tulisimama na kusema tume ilianzia mahali ambapo sipo.
Wazanzibar walikuwa bize wakitaka 50/50. Hao unaosema walitaka Tanganyika ndio hao hao wanaikataa serikali 3 akiwemo muasisi wa serikali 3 Seif Sharif. Asilimia 66 ni bendera fuata upepeo
Tunawalazimisha wazanzibari wawe ndani ya muungano lakini hawautaki muungano, hawataki serikali tatu,mbili au moja. Wameshasema sana wanataka nchi yao na uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao.
Mkataba wanataka wa nini?
Seif aliulizwa binafasi na Warioba kwanini tusikutane EAC, akasema muungano wetu ni mzuri kuliko wa EAC. Seif ambaye amebeba akili za wznz anasema muungano ni bora hakusema hataki muungano,sasa mznz gani aliyebaki.
Mansour,Moyo, Jusa walisimama na kusema wanataka muungano, mznz aliyekataa ni yupi tena
Tunalazimisha serikali tatu lakini kama ni muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar tu, hautadumu. Kama nchi za Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda zitaruhusiwa kujiunga, huenda Zanzibar watajifunza kitu na kutamani kubakia katika muungano.
Unajichanganya, hapo juu umesema wznz walitaka serikali ya Tanganyika kwa maana walitaka serikali 3.
Chama cha CUF sera yao ni serikali 3 sasa leo kipi cha kuwatetea kuwa waliona zaidi.
Walichokiona ni wajumbe 50/50.Tuliwaambia tusimame pamoja kukataa tume, wao akiwemo mpiga debe mkuu wa znz kupitia BBC Ali Swalehe akakimblia masufuru na 50/50.
Akili ya kuona kilichokuwa kinakuja haikuwepo. Akaingia mliberai huyo ndiye akatumbukiza nyongo kabisa akidai mkataba. Tukasikia kama wa Uswiss, Hong Kong, Bemuda na Nigeria n.k Leo mseme hamtaki muungano, acheni uongo asiyetaka muungano ni Mtanganyika anayewaambia nendeni kwenu hatuwahitaji.
Ikiwana nusu ya znz ipo Tanganyika nguvu ya kukataa muungano ni ya akina Uamsho, wznz wenyewe hawana jeuri hiyo.
Wakati watu wanajadili "usanii" wa Tume ya Katiba mpya, CCM wanacheka sana, wanachekelea sana. Muda wa kuandika Katiba ya Tanganyika na kuiunda na kuisimika serikali ya Tanganyika utafanya uchaguzi mkuu usogezwe mbele au itatumika katiba ya 1977.
Wenzetu mlitaka 50/50 kwamaneno mengi quantity siyo quality
Kwa kweli kinachoendela ni kituko/maigizo tu. Kama Tume imetoa pendekezo la kuanzisha serikali tatu. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuandika katiba ya Tanganyika na kuunda serikali ya Tanganyika. Baadae serikali ya Tanganyika ikae mezani na serikali ya Zanzibar kujadili Muungano kama vile wabia hawa wa muungano walivyofanya 1964
Tuliyoona haya tulisema tume itaingiza watu mkenge, wenzetu mkaendelea na hadithi za Seif na uwiano. Hapo ndipo tatizo lilipoanziaHatukuwa na true partner
Tunatengeneza utata na maumivu tu ya muungano badala ya kuamua kulishughulikia tatizo la muungano na mfumo/muundo wake lililopo mbele yetu kwa ujasiri na kwa kujiamini. Tunateketeza fedha za kodi za walalahoi na pia tunatengeneza matatizo mingine mapya na mazito zaidi.
Hasa rasimu hii inammaliza mznz kabisa. Hakuna mamlaka kamili na utegemezi unafikia kikomo ingawa bado tutabeba zigo la kuendesha serikali. Waambie wznz hii ni fursa pekee kwao kukataa rasimu na muungano. Baada ya hapo ni maumivu. Kama walifanya makosa huko mwanzo warekebishe sasa, tutawasadia sana katika kupata mamlaka lakini lazima wao kwanza watake. Sisi hautingii SMZ,BLW au BLM. Tunawapa mawazo tu, wale walioko Dodoma walete mswaada hilo una uwezo nalo kuwasadia. Knyume chake maumivu makali yanaisubiri znz hasa Tanganyika inaporudi.