Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Naona nchi tatu kutokana na jamhuri ya muungano zinatengana

Tuone kati ya pemba, unguja na tanganyika nani watakuwa na maendeleo
 
haya tumeyakubali yote wacheni yatukute, jst tupeni mwanya w kuchomoka tu. dah mijamaa inaboa cjui imeambowa zanzibar ndo moyo wao. mtwana haachi asilie, kila siku mnatupga kampeni izo kwa izo
na hatufaham basi, tuacheni tupumue

serikali tatu, nchi moja, amir jesh moja.
 
serikali tatu ndioooooo
mbona hii ya sasa bado ni ghali?
 
kwa kweli ningekuwa RAISI leo ningetengeneza mazingira watanganyika tubaki wenyewe. Hao mdebwedo siwataki hata kuwasikia. jamaani nendeni zenu huko Zanzibar. Na mmeajiriwa wengiiii Tanganyika sasa mtajazana ofisi gani kwenu huko?
 
Zanzibar ilikuwepo zaidi ya miaka 1000 na hakujawahi kutokea historia ya watu wa unguja na pemba kupigana sisi ni ndugu damu na mila na desturi zetu ni moja na hata siku moja haitatokea sisi kuuwana kama nyie watanganyika:israel:
Tusubiri tuone, Tangu lini mwarabu wa pemba na mtu mweusi wa unguja wakawa ndugu? Ninyi semeni kwamba tangu historia mmekuwa na uhusiano wa Mabwana na watwana. Lakini sio kutuambia ndugu. Kuna mawili: kama sio kuwa na pemba na unguja kama mataifa mawili basi itakuwa ni waarabu wa pemba kuwatawala weusi wa zenji.
 
hyo atakuwa mwalimu ndio amekusomesha vibaya ila endelea kutoka povu wadanganyika ujinga ndio ibada ndio maana mpaka leo maendeleo mnaona kwenye tv na hii ndo sera yenu zidumu fikra za mwalimu.
Yaani na ninyi mnajivuna kwamba mmeendelea kiasi cha kuiona bara haijaendelea? ama kweli nyani halioni _ _ _ _ _ .
 
Hii tabia ya kwa sadala ndio inayoifanya Tanganyika kujifanya mkoloni mweusi kwa Zanzibar, mnapenda mteremko, hamtaki kujituma, mna raslimali mnazikalia. Kwa taarifa yenu wakenya tuu ndio watakaonufaika mukiungana na Kenya, maana wajinga ndio walio wao na nyinyi (tanganyika) wajinga, wakenya ndio wanaouza tanzanite nje kuliko Tanzania, wakenya ndio wenye mlima kilimanjaro na serengeti kwa sababu bado mmelala, na ndio maana Tanganyika yenu ikayayuka bila hata kujijua mnafanya nini, kwa sababu vichwa vyenu povu tupu, kwa hiyo usitegemee mkiungana na kenya mtafaidika ndio watakumalizeni kila kitu kitakuwa chao mpaka gesi ya mtwara. tanganyika itabaki kama Yomba Yomba
Umenena vema kwamba wajinga ndio waliwao. Hii ndio maana Tunaitawala Zanzibar. Nafikiri kwa hapo umeshajua kati ya Tanganyika na Zanzibar nani mjinga na nani mwerevu.
 
Kama nilivyomuelewa jaji Warioba,kuwepo kwa serikali mbili ni kuelekea kuvunja muungano,kuwepo kwa serikali tatu ni kuimarisha muungano. Mimi ni mmoja wa muumini anayekubali serikali tatu, hoja ya kukutaa serikali hazina mashiko. suala la gharama ni uupuzi. demokrasia ni gharama
 
Serikali moja tu Basi!!!

Kama visiwani hawapendi sisi bara hatuwezi tena kuwabeba!

Tumewabeba vya kutosha miaka 50 tayari!
 
Kwa maneno mengine mwanakijiji unatuambia tuseme NO kwa muungano. Ukweli ni kwamba huu muungano umefanya mambo kuwa very complicated. Ndio ambao umewalazimisha kina warioba kushauri serikali tatu. Sio kwa sababu ni option bora sana bali kwa sababu bila hivo muungano utavunjika haraka sana wakati unatakiwa uvunjike pole pole. Tukibaki na serikali mbili inabidi kutumia nguvu mara zote kuiongoza Zanzibar.
 
Ndio hapo sasa mtakapojua,umasikini wa Zanzibar hautokani na Muungano,bali ni kutokuwa na viongozi bora,wenye vision na uzalendo,waliokuzwa chini ya mfumo wa kifisidi wa CCM na wanachi waliopata elimu dhalili,isiyoruhusu kutawala mazingira yao.. Tukishatengana ndio mtaanza kushikana uchawi,punde c punde Unguja republic na Pemba Democratic Republic...
 
SERIKALI MOJA UNAITAKA WEWE
SISI TUNATAKA SERIKALI TATU Tanganyika, Zanzibar na TANZANIA.
Tusubiri kura ya maoni....tuone kila mmoja atapata asilimia ngapi. Atakayeshinda kwa kura nyingi tutakubaliana na matokeo kwamba ni serikali 1; au 2; au 3?
Kura ndio mwamuzi!
 
Nadhani sasa umefika wakati wa kuwaacha Wanzanzibar wadai nchi yao wenyewe. Hata sisi Watanganyika tunataka nchi yetu, full stop. Hatutaki muungano...

Sasa nahisi munaanza kupatwa na akili na kama kutakuwa na watu kama ww wengine wengi tu basi tungalitatua na kuondaosha mazingira na uchafu wote uliopo sasa bila ya jasho wala kuchoka kiakili au mwili na badala yake tungali patwa na furaha na amani ya milile, serekali 3 nikujaribu kuukwepa mshare usipitie nyuma ya kichwa na kutokezea usoni bali tunapeleka uso upite ili utokezee kichogoni, nibora kilaupande wadai nchi yao ilio huru tena bila ya muungano.
 
kwa kweli ningekuwa RAISI leo ningetengeneza mazingira watanganyika tubaki wenyewe. Hao mdebwedo siwataki hata kuwasikia. jamaani nendeni zenu huko Zanzibar. Na mmeajiriwa wengiiii Tanganyika sasa mtajazana ofisi gani kwenu huko?

Hata mm sion la kuwavuta mashati waZanzibari waendelee na muungano, inaonekana Zanzibar na Tanganyika ziko tofaut kiutamaduni, siasa, mitazamo, madaraka, ukubwa, wingi, ufisadi, Mali, & kilakitu, nakuombeni majirani zetu Tanganyika kuweni wamoja na toeni tamko Kuwa "LEAVE Zanzibar ALONE", km midembwedo au yakheee hayo shauri yao, hapo kila fitna za muungano zitakuwa hazip, kuna mswal eti waZanzibari wanaishi wengi, oo wamejenga, ooo wanafanyakazi etc huko nikutapatapa kwa jambo lisilo epukika, mbona EUrope, Asia, America, Africa hususan Africa kusini wapo wengi au nawao pia wafukwuzw maana wao hata muungano hawana?.
 
[h=5]Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?[/h]Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi! Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo. Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea. Na maneno mengine mengi.... In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
KTK NCHI HII KUNA KASUMBA ZA KUTAKA KUZIMA MAWAZO NA MAMBO AMBAYO YAKO OBVIOUS. ETI MUUNDO WA SERKALI 2 NDIO ULIOKUBALIKA. JE ULIKUBALIKA NA NANI KAMA SIYO KUNDI LA WACHACHE? TUJIULIZE WALIFANYA HIVYO KWA FAIDA YA NANI KAMA SIYO USHABIKI WA AFRIKA NZIMA KUUNGANA? TUSIPAKE RANGI NYEUPE HAli ndani tuna rangi nyeusi. kuna mawazo ya ajabu sana eti wazanzibari wanahitaji identity. kwahiyo sisi watanganyika hatuhitaji IDENTITY? KUNA NINI HAPA. IKIWA NA NCHI HUHITAJI IDENTITY HII ANALOGY INANISHANGAZA SANA. NI LAZIMA TURUHUSU MAWAZO YA WATU WOTE SIYO KUTEKWA NA KUNDI LA WATAWALA HAWA WASI NA HURUMA. KWANIN WABONGO WAKIENDA ZENJI WANAONEKANA KUWAKATAA WABARA KWA KUWACHOMEA BIASHARA , MAKANISA, LAKINI WANAPOKUJA BARA KUHEMEA WANAKUWA WAPOLE GHAFLA NA KUUENZI MUUNGANO? MIMI NAPATA SHIDA na unafiki huu wa watu wa zanzibar. kama tumeamua zanzibar kuwa na serkali haina budi tuanzishe yabara pia ili mijadala inayohusu Tanganyika wazenji wasiwe na fursa ya kujadili mambo yetu kama ilivyo wao wanapojadili mambo yao katika BARAZA LAO TUKUFU LA MAPINDUZI na Baraza la Wawakilishi. UTUKUFU WA BARAZA LAO HAUWEZI KUIUA TANGANYIKA NA SISI TUBAKI TUNANG'AA MACHO PIMA , LAZIMA TUFANYE KITU, HUWEZI KUOMBA MTOTO BILA KUSHUGHULIKIA MAMBO YA MSINGI YA KUPATA MTOTO. KWAHIYO NI WAKATI WETU SASA WATANGANYIKA TUIDAI SERKALI YETU, VINGINEVYO KAMA SIYO BASI GHARAMA YA KUIKOSA TANGANYIKA NI LAZIMA IWE NI GHARAMA YA KUIKOSA ZANZIBAR. HATUWEZI KUBAKI NA WATU NDANI YA NCHI MOJA WATAKA IDENTY HALAFU SISI TUNAIZIKA IDENTITY.
 
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa

Acha kuaminishwa ujinga, nchi hii ina pesa kuliko unavyofikiri, mianya ya wizi, rushwa, ufisadi, misamaha ya kodi na mengi yanayofanana na hayo yakidhibitiwa, pesa itatosha kuhudumia serikali zote za EAC.

Tatizo sasa hivi hatuna serikali ya kuwatumikia watu, bali tuna genge la mafisadi na wezi ndilo linalotuongoza. Ukitaka kujua pesa zinavyoliwa wafuatilie sasa hivi wafanyakazi wa Halmashauri uone wanavyo funga kasma zao. Wanatunga project hewa wanakomba pesa za miradi benki ili kusiwepo fungu linalorudi hazina. Achana na serikali ya CCM ni balaa!

Nikupe mfano: Mtu mume akioa mtu mke mbona hasemi nimeongeza gharama, na je anaweza akasema tusizae kwanza maana gharama itaendelea kuwa kubwa? Mambo mengine ni kuaminishwa ujinga na magamba, Serikali tatu zije, hata za majimbo zije kwani ndiyo tutadhibitiana wenyewe kwa wenyewe!
 
Mwaka 2007 nilifanya research kuhusu shirikisho la Africa Mashariki katika kumalizia masomo yangu ya elimu ya juu..Ulichosema ndugu Mwanakijiji ni sahihi kabisa. Wengi walikataa hoja za shirikisho lakini tume ile ikiongozwa ( naomba nisimtaje jina) ilitoa majibu tofauti na uhalisia wa wengi.. hapa ni rasimu tuu nachoamini haki ikitendeka hata Muungano utavunjika iwapo suala la serikali 3 litapita. Ukweli lazima tufanye maamuzi kulingana na faida na hasara na ni lazima tufanye uana harakati wakuonyesha ukweli wa mambo. Kama kweli tunauihitaji muungano kwanini tuogope serikali moja? take example of Brazil, USA and other federal Governments. Mbona zina Rais Mmoja nasie ombaomba tung'ang'anie serikali 3? tena wao kila uchao wanaangalia namna yakupunguza ukubwa wa serikali...mAONI YANGU.. TUWE WAKWELI kama kwanza kama wengi wanautaka Muungano au haawataki and we should share facts about viability of such Union1
 
Acha kuaminishwa ujinga, nchi hii ina pesa kuliko unavyofikiri, mianya ya wizi, rushwa, ufisadi, misamaha ya kodi na mengi yanayofanana na hayo yakidhibitiwa, pesa itatosha kuhudumia serikali zote za EAC.

Tatizo sasa hivi hatuna serikali ya kuwatumikia watu, bali tuna genge la mafisadi na wezi ndilo linalotuongoza. Ukitaka kujua pesa zinavyoliwa wafuatilie sasa hivi wafanyakazi wa Halmashauri uone wanavyo funga kasma zao. Wanatunga project hewa wanakomba pesa za miradi benki ili kusiwepo fungu linalorudi hazina. Achana na serikali ya CCM ni balaa!

Nikupe mfano: Mtu mume akioa mtu mke mbona hasemi nimeongeza gharama, na je anaweza akasema tusizae kwanza maana gharama itaendelea kuwa kubwa? Mambo mengine ni kuaminishwa ujinga na magamba, Serikali tatu zije, hata za majimbo zije kwani ndiyo tutadhibitiana wenyewe kwa wenyewe!

This short sited mind... improve your focus
 
Tukifuata mfumo wa Serikali Moja, faida zake zitakuwa kama ifuatavyo:


(1) Tutadumisha Muungano na kuonekana JAMUHURI YA MUUNGANO TANZANIA kweli.
(2) Gharama za uendeshwaji wa Serikali zitapungua tutakuwa na Raisi Mmoja tu na si vingenevyo, Serikali itasimamiwa vizuri.

Note: 1.Serikali mbili hazitakiwi kabisa bcoz itawabagua watu wa upande mmoja wa serikali na kuonekana imemezwa na serikali ya Muungano


2. Serikali tatu ni kupeana Madaraka na vyeo tu si vingnevyo. haitadumisha muungano na Gharama za Uendeshwaji utakuwa mkubwa zaidi.


Solution: serikali moja
 
Back
Top Bottom