Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Ndiyo serekali moja,lakini safari hii iitwe zantania,makau makuu yawepo zanzbr,tanganyika isiwe na mamlaka yoyote,zantania ndio ishughulikie mambo yote ya nje.
 
... Kama ninge kuwa na ID kama ya invisible Robot' hii thread ningeipa kipaumbele, na kuiwekea neno "Sticky"

...kibaya zaidi hata wadau wanakibilia kwenye hoja nyingine zisizo kuwa na mashiko...
 
Tukifuata mfumo wa Serikali Moja, faida zake zitakuwa kama ifuatavyo:

(1) Tutadumisha Muungano na kuonekana JAMUHURI YA MUUNGANO TANZANIA kweli.
(2) Gharama za uendeshwaji wa Serikali zitapungua tutakuwa na Raisi Mmoja tu na si vingenevyo, Serikali itasimamiwa vizuri.

Note: 1.Serikali mbili hazitakiwi kabisa bcoz itawabagua watu wa upande mmoja wa serikali na kuonekana imemezwa na serikali ya Muungano

2. Serikali tatu ni kupeana Madaraka na vyeo tu si vingnevyo. haitadumisha muungano na Gharama za Uendeshwaji utakuwa mkubwa zaidi.

Solution: serikali moja

...NDIYO "Serikali moja"
NUKUU kutoka kwenye hoja ya Mh. mmoja kama ilivyo nakiliwa kutoka kwa wadau mbalimbali;-

...kama Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 Tukapata Tanzania. baada ya miaka50 ya majaribio tulitegemea huu muungano ukomae na kuwa serikali moja, ili tutamke kwa jeuri kuwa kuna nchi moja, Taifa moja, serikali moja, bunge moja, na dola moja. kwa hiyo ifikapo 26/4/2013 tungeizika zanzibar rasmi kama tulivyoizika tanganyika miaka hamsini iliyopita. Kama tutarudi kwenye serikali tatu au kuendelea na serikali mbili, mimi naona hakuna haja ya muungano, hapo ndoa imeshindikana hapo kila mmoja arejee kwa wazazi wake.

...Binafsi naona dhahiri mapendekezo ya katiba mpya ya muungano imedhamiria kuvunja muungano wenyewe!
Serikali moja INATOSHA!

...serikali iwe moja , rais mmoja, nchi moja, sarafu moja kama mliweza kuunganisha vyama kwanini isiwezekane serikali moja?
Kama wazenji hawataki basi wasepe zao sisi hatutaki walalamishi na tumechoka na ngonjera zao.
...Hivi ndugu yangu ... unaona unatenda haki kutetea serikali mbili? Sina imani na mtu yeyote anayesema tubaki hivi hivi Mhe. Kwa upande wa Uchumi ni serikali moja, ila mnawaogopa wazenji kwa kukubaliana nao ati serikali mbili!!!
iwe serikali moja. Tatu mbili hapana.

...mkuu uko juu, tunahitaji Tanzania MOJA yenye serikali moja, nchi moja, Taifa moja, bunge moja, na dola moja:
- Rais moja
- Makamu wa rais mmoja
- Waziri Mkuu mmoja
- Baraza la mawaziri moja
- Katiba Moja
- Uwakilishi wa UTAIFA mmoja
- Kila kitu mfumo mzima uwe kwenye kofia moja,KWA SASA NDIYO DAWA pekee.

... mtake msitake kama si serikali moja basi, hapana kwenda kwenye serikali tatu.

...Mie Tanganyika kwanza vinginevyo ibaki hivi hivi serikali mbili maana wengine tulishajizoelea na muundo huu kutokana na watu wa bara kumezwa na serikali ya muungani wakati wenzetu upande wa pili wana serikali yao pia ni beneficiary wa serikali ya muungano, mistake ilishafanyika tukawa na serikali mbili badala ya moja.

Kama serikali mbili imetushinda tujaribu serikali moja vinginevyo tuikatae mapema na sie tuwe na Tanganyika yetu na zanzibar ibaki kivyao maana serikali tatu ni uzushi tu wakati huo huo bado tena tupo kwenye shirikisho la Afrika mashariki. Kwani kama la serikali mbili au moja limeshindikana tukivunja muungano kuna shida gani hasa ukizingatia zanzibar na Tanganyika tuna uhusiano wa kiasili hata kama tutakuwa nchi tofauti bado tunaweza tukaendeleza uhusiano wetu, mbona Kenya watu wanaingia na wanafanya tu shughuli zao kama kawa kama vile upo Dar tofauti ni kwamba unaingia na passport tu na bado hotel unalipa kwa rate zile zile (hapa kuna tofauti gani na mtu ambae anaishi Mwanza akaenda kwa shughuli binafsi Dar akafikia hotel akafanya yaliyompeleka na kurudi zake ndivyo hivyo na Zenji itakavyokuwa)

*MWISHO WA KUNUKUU*

Sticky
 
Wakuu naomba mnisikilize:

Siungi mkono muungano wa serikali mbili kwa sababu hata tukisema tutatue kero za muungano wa haina hiyo leo; kesho zitakuja nyingine na nyingine. Kwa kifupi kero zake ni endelevu!

Mimi nadhani kilichotufanya tuungane kwanza ni kutaka kuonesha njia kwa mataifa mengine ya Afrika. Kuonesha njia ambayo baadaye ingetufikisha pale ambapo Afrika nzima ingekuwa moja. Nyerere alikuwa na haki na wajibu wa kuipoteza Tanganyika ili kuidhihirishia Afrika na dunia imani yake kwenye Muungano wa Afrika! Kipindi kile ilikuwa ni sifa kubwa sana kupigania Umoja wa Afrika.

Sababu ya pili ilikuwa ni ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwa wakati ule!

Sababu zote hizo hapo juu hazina mashiko tena kwenye zama hizi za ubepari! Sasa kwa nini tuendelee kuishi imani zisizokuwepo!

Ikumbukwe kuwa zile juhudi za kuliunganisha bara la Afrika zilikufa hata kabla hazijafika mbali kwa sababu wengi wa waliokuwa wanaamini kwenye umoja wa Afrika walitoweka na mawazo yao!

Hata zile juhudi za kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki hazina uhai tena. Sisi ni mashuhuda wa kifo chake kitakatifu; tunasubiria tu kitangazwe rasmi siku za usoni!

Nauliza maswali hapa: Ni kwa nini kuwepo na muungano ambao mshirika mmoja anakubali kupoteza ili kumwokoa mwingine? Hata kwenye ndoa haiwezekani ndugu ni lazima walete chokochoko mwenzi mmoja akitoweka!
Eti serikali tatu haiwezekani kwa sababu Zanzibar haina uwezo! Ni kwanini nchi ijione haina uwezo wakati ilitafuta uhuru wake ili ijiendeshe?

Kama kujiendesha kwake ni kwa kutegemea taifa lingine haioni kuwa ina uhuru wa bendera tu?
Kama Zanzibar wa hofu wakiungana rasilimali zake kama mafuta n.k zitapotea; je, Tanganyika yenye gesi, mafuta, wanyamapori, makaa ya mawe, madini ndiyo iendelee kujitoa sadaka???! Basi Tanganyika itakuwa ni nchi nzuri sana ya kuishi kwa sababu haina hofu ya kuishiwa rasilimali!

Endapo atajitokeza mtu wa kuainisha pasipo shaka mipaka ya mapato na matumizi baina ya Tanzania Bara, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitafarijika sana! Nasema hivi kwa sababu ninachokiona mimi ni kuwa chochote kipatikanacho Tanzania Bara ni faida ya wote na cha Zanzibar ni kwa faida ya Zanzibar tu pekee.

Je, hii inaonesha kuwa Tanzania Bara inajiamini kuwa yenyewe ndiyo yenye uwezo wa gharamia serikali ya muungano na inaona fahari kufanya hivyo?! Au labda kuna masuala mengine Tanzania Bara inanufaika nayo ambayo sisi wananchi hatujui!
Je, Zanzibar nayo inaona fahari tu kuhudumiwa kila kitu kwenye muungano na wala haioni kuwa Tanzania Bara imebeba jukumu zito? Na je Zanzibar isipotimiziwa mambo kadhaa watakuwa radhi kulalamika ilhali wamebebwa katika mambo mengi?

Nionavyo mimi kama tatizo ni gharama za kuendesha serikali tatu ambazo ndo halali ni sharti tutafute mfumo wa kudumu kutatua tofauti zetu! Tukumbuke kuwa upande mmoja wa muungano umeingia gharama kubwa kuhudumia serikali ya muungano kwa zaidi ya miaka 49 sasa! Au iaonekana Tanganyika hajichoka kulea muungano na Zanzibar nayo haijachokaa kubebewa!

Tusijidanganye; Tanzania ni jina! Nchi ni sisi wananchi! Na wananchi wa pande zote za Muungano wamechoka kulazimishiwa muungano wa serikali mbili! Tunaowaona wanatetea ni baadhi ya watawala ambao muungano uliopo sasa unawanufaisha kwa namna fulani.
Kama wananchi wengi wanadai muungano hauwatendei sasa inabidi tuseme imetosha tutafute kitakachotupa haki na usawa. Na hiki si kingine zaidi ya nchi zote kuungana na kuwa chini ya serikali moja itakayohakikisha kila raia anakuwa na haki sawa na mwenzake bila kujali atokako!

Ingependeza tuwe na serikali tatu kila nchi ijihudumie kwani kila nchi ilidai uhuru ili iwe huru! Lakini watu wanaeneza mawazo hasi ya ukubwa wa gharama!Umaskini na uvivu wa fikra! Ikumbukwe chochote kizuri ni sharti kiwe na gharama yake; tena gharama kubwa!
Kama tunakimbilia unafuu wa serikali mbili tufahamu wazi kuwa nafuu mara zote ni ghali zaidi na mara zote hazidumu!

Muungano wa serikali mbili vilio vya unyonyaji! Muungano wa serikali tatu tunaogopa gharama! Basi muungano unaotufaa ni wa serikali moja. Kama hatuwezi muungano wa serikali moja, muungano wowote ule utakaokuwepo aidha wa serikali mbili, tatu au zaidi hautatuliza kiu ya wananchi! Narudia tena: Tanzania ni jina; nchi ni wananchi!

Nashangaa nchi zenye watu zinaogopa kujiwekea mifumo ambayo itawastawisha na kumaliza chokochoko kwa visingizio visivyoisha! Ina maana pamoja na rasili mali tulizonazo viongozi wetu wanataka kututhibitishia kuwa hawawezi kuweka mifumo ya kuliendesha taifa kwa ustawi!

Hoja ya kuwa kuna udugu wa damu kati ya Tanganyika na Zanzibar ni hoja ya kibaguzi kwani uhusiano wa damu upo pia baina ya Tanganyika na nchi nyingine. Swali hapa: Ni kwa nini tusiungane na Kenya, Uganda, Msumbiji, Burundi, Malawi, Zambia, n.k kwa sababu hata huko wapo watanganyika wana ndugu zao?
Kama hoja ni udugu ni kwanini Zanzibar wanapochagua wabunge wa kuja kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano, upande wa Tanzania Bara nao wasichague wawakilishi wachache kwenye Baraza la Wawakilishi ili kuukuza zaidi huo unaoitwa udugu???
Udugu unaonufaisha upande mmoja zaidi ya mwingine si mzuri jamani! Tuache propaganda. Kama tunaamini umoja ni nguvu utengano ni udhaifu basi tuungane tuwe nchi moja, serikali moja, rais mmoja na Tanzania moja ili tuwe ndugu kweli!

Watasema ni chuki lakini kama hatuwezi kumaliza tofauti zetu kwa kuunda serikali tatu au moja basi ni bora kila nchi ijendee kivyake! Hata Kenya na Uganda ni ndugu zetu lakini hatujaugana nao kutengeneza taifa la kusadikika!

Litakuwa ni kosa sana kuendelea kuwa na muungano ambao upande wa Tanganyika tu ndiyo unaendelea kupoteza historia yake wakati mshirika wake Zanzibar akibakiwa na ziada hata kama ni sawa na wilaya moja ya Tanganyika!

Wakuu; naombeni kuwasilisha hoja!
 
Nionavyo mimi kama tatizo ni gharama za kuendesha serikali tatu ambazo ndo halali ni sharti tutafute mfumo wa kudumu kutatua tofauti zetu! Tukumbuke kuwa upande mmoja wa muungano umeingia gharam kubwa kuhudumia serikali ya muungano kwa zaidi ya miaka 49 sasa! Au iaonekana Tanganyika hajichoka kulea muungano na Zanzibar nayo haijachokaa kubebewa!

Mkuu unaonekana unauwezo wa kuandika lakini upeo wa fikra mdogo sana.

Umenishangaza sana kusema kama hatutaki nchi 3 basi iwe moja,

hivi unajua maana ya nchi kama tukiwa na nchi 3 hiyo nchi ya tatu itaitwaje na aridhi yake iko wapi kwani huwezi kuwa na nchi bila aridhi haya twambie aridhi ya tatu iko wapi?.
 
Hesabu ya Nyerere
1+1=2 akimaanisha mbili ni serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano!
Lakini maana halisi ya Muungano wetu ni
1 + 0 = 1 Yaani moja ni serikali ya zanzibar....sifuri ni nchi ya Tanganyika na Jibu ni serikali ya Muungano!

Muungano ulitakiwa kuwa hivi
1 + 1 = 2 yaani moja ni serikali ya zanzibar,moja ingine ni serikali ya Tanganyika na mbili ni serikali ya Muungano ambayo inasimamia mambo ya bara na visiwani!
Naunga mkono serikali tatu!
 
Mkuu unaonekana unauwezo wa kuandika lakini upeo wa fikra mdogo sana.

Umenishangaza sana kusema kama hatutaki nchi 3 basi iwe moja,

hivi unajua maana ya nchi kama tukiwa na nchi 3 hiyo nchi ya tatu itaitwaje na aridhi yake iko wapi kwani huwezi kuwa na nchi bila aridhi haya twambie aridhi ya tatu iko wapi?.
Turudi kama tulivyokuwa 1961.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nadhani tatizo lipo kwenye title...endelea kusoma dhima nzima ya hiyo thread! Don't ever judge the book by its cover but its contents!

Mkuu unaonekana unauwezo wa kuandika lakini upeo wa fikra mdogo sana.

Umenishangaza sana kusema kama hatutaki nchi 3 basi iwe moja,

hivi unajua maana ya nchi kama tukiwa na nchi 3 hiyo nchi ya tatu itaitwaje na aridhi yake iko wapi kwani huwezi kuwa na nchi bila aridhi haya twambie aridhi ya tatu iko wapi?.
 
mtoa mada una hoja ya msingi lakini wanasiasa kamwe hawawezi kukubaliana na wewe, wao wanachoangalia ni ulaji wao na familia zao (tamaa ya madaraka imewajaa) tu, full stop!

jiulize swali kwani tukiwa na serikali moja, bili au tatu mwananchi wa kawaida ananufaika nini!!! shida ya muungano ni wanasiasa ndg yangu, hapa utatolewa baru bure!
 
Kwetu sisi wazbr muungano c lazima,kitu cha lazima kwa upande wetu ni mamlaka kamili ya nchi yetu ikibidi muungano ni wa mkataba na nchi yoyote sio lazima iwe tanganyika,hii ni tofauti na watanganyika ambao wanaamini hawawezi kuishi bila ya muungano na muungano wao ni kwa zanzibar tu kama vile hakuna nchi nyengine duniani,zanzbr kwanza.
 
Heading yako inanipa mashaka unasema unataka muungano wa nchi 3 sasa ya tatu ni ipi, nchi ni mbili tu Tanganyika na zanzibar, hata hiyo ya muungno haitakuwa nchi bali ni shirikisho, sasa tunaposema nchi it means that hiyo ya tatu itakuwa na mipaka yake ipi ? wakati tayari Tanganyika ina mipaka yake na Zanzibar ina mipaka yake, nieleweshe nchi ya tatu unayo sema wewe ni ipi ?

Wakuu naomba mnisikilize:
Siungi mkono muungano wa serikali mbili kwa sababu hata tukisema tutatue kero za muungano wa haina hiyo leo; kesho zitakuja nyingine na nyingine. Kwa kifupi kero zake ni endelevu!

Mimi nadhani kilichotufanya tuungane kwanza ni kutaka kuonesha njia kwa mataifa mengine ya Afrika. Kuonesha njia ambayo baadaye ingetufikisha pale ambapo Afrika nzima ingekuwa moja. Nyerere alikuwa na haki na wajibu wa kuipoteza Tanganyika ili kuidhihirishia Afrika na dunia imani yake kwenye Muungano wa Afrika! Kipindi kile ilikuwa ni sifa kubwa sana kupigania Umoja wa Afrika.

Sababu ya pili ilikuwa ni ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwa wakati ule!

Sababu zote hizo hapo juu hazina mashiko tena kwenye zama hizi za ubepari! Sasa kwa nini tuendelee kuishi imani zisizokuwepo!

Ikumbukwe kuwa zile juhudi za kuliunganisha bara la Afrika zilikufa hata kabla hazijafika mbali kwa sababu wengi wa waliokuwa wanaamini kwenye umoja wa Afrika walitoweka na mawazo yao!

Hata zile juhudi za kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki hazina uhai tena. Sisi ni mashuhuda wa kifo chake kitakatifu; tunasubiria tu kitangazwe rasmi siku za usoni!

Nauliza maswali hapa: Ni kwa nini kuwepo na muungano ambao mshirika mmoja anakubali kupoteza ili kumwokoa mwingine? Hata kwenye ndoa haiwezekani ndugu ni lazima walete chokochoko mwenzi mmoja akitoweka!
Eti serikali tatu haiwezekani kwa sababu Zanzibar haina uwezo! Ni kwanini nchi ijione haina uwezo wakati ilitafuta uhuru wake ili ijiendeshe?
Kama kujiendesha kwake ni kwa kutegemea taifa lingine haioni kuwa ina uhuru wa bendera tu?
Kama Zanzibar wa hofu wakiungana rasilimali zake kama mafuta n.k zitapotea; je, Tanganyika yenye gesi, mafuta, wanyamapori, makaa ya mawe, madini ndiyo iendelee kujitoa sadaka???! Basi Tanganyika itakuwa ni nchi nzuri sana ya kuishi kwa sababu haina hofu ya kuishiwa rasilimali!

Endapo atajitokeza mtu wa kuainisha pasipo shaka mipaka ya mapato na matumizi baina ya Tanzania Bara, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitafarijika sana! Nasema hivi kwa sababu ninachokiona mimi ni kuwa chochote kipatikanacho Tanzania Bara ni faida ya wote na cha Zanzibar ni kwa faida ya Zanzibar tu pekee.

Je, hii inaonesha kuwa Tanzania Bara inajiamini kuwa yenyewe ndiyo yenye uwezo wa gharamia serikali ya muungano na inaona fahari kufanya hivyo?! Au labda kuna masuala mengine Tanzania Bara inanufaika nayo ambayo sisi wananchi hatujui!
Je, Zanzibar nayo inaona fahari tu kuhudumiwa kila kitu kwenye muungano na wala haioni kuwa Tanzania Bara imebeba jukumu zito? Na je Zanzibar isipotimiziwa mambo kadhaa watakuwa radhi kulalamika ilhali wamebebwa katika mambo mengi?

Nionavyo mimi kama tatizo ni gharama za kuendesha serikali tatu ambazo ndo halali ni sharti tutafute mfumo wa kudumu kutatua tofauti zetu! Tukumbuke kuwa upande mmoja wa muungano umeingia gharam kubwa kuhudumia serikali ya muungano kwa zaidi ya miaka 49 sasa! Au iaonekana Tanganyika hajichoka kulea muungano na Zanzibar nayo haijachokaa kubebewa!
Tusijidanganye; Tanzania ni jina! Nchi ni sisi wananchi! Na wananchi wa pande zote za Muungano wamechoka kulazimishiwa muungano wa serikali mbili! Tunaowaona wanatetea ni baadhi ya watawala ambao muungano uliopo sasa unawanufaisha kwa namna fulani.
Kama wananchi wengi wanadai muungano hauwatendei sasa inabidi tuseme imetosha tutafute kitakachotupa haki na usawa. Na hiki si kingine zaidi ya nchi zote kuungana na kuwa chini ya serikali moja itakayohakikisha kila raia anakuwa na haki sawa na mwenzake bila kujali atokako!

Ingependeza tuwe na serikali tatu kila nchi ijihudumie kwani kila nchi ilidai uhuru ili iwe huru! Lakini watu wanaeneza mawazo hasi ya ukubwa wa gharama!Umaskini na uvivu wa fikra! Ikumbukwe chochote kizuri ni sharti kiwe na gharama yake; tena gharama kubwa!
Kama tunakimbilia unafuu wa serikali mbili tufahamu wazi kuwa nafuu mara zote ni ghali zaidi na mara zote hazidumu!

Muungano wa serikali mbili vilio vya unyonyaji! Muungano wa serikali tatu tunaogopa gharama! Basi muungano unaotufaa ni wa serikali moja. Kama hatuwezi muungano wa serikali moja, muungano wowote ule utakaokuwepo aidha wa serikali mbili, tatu au zaidi hautatuliza kiu ya wananchi! Narudia tena: Tanzania ni jina; nchi ni wananchi!

Nashangaa nchi zenye watu zinaogopa kujiwekea mifumo ambayo itawastawisha na kumaliza chokochoko kwa visingizio visivyoisha! Ina maana pamoja na rasili mali tulizonazo viongozi wetu wanataka kututhibitishia kuwa hawawezi kuweka mifumo ya kuliendesha taifa kwa ustawi!

Hoja ya kuwa kuna udugu wa damu kati ya Tanganyika na Zanzibar ni hoja ya kibaguzi kwani uhusiano wa damu upo pia baina ya Tanganyika na nchi nyingine. Swali hapa: Ni kwa nini tusiungane na Kenya, Uganda, Msumbiji, Burundi, Malawi, Zambia, n.k kwa sababu hata huko wapo watanganyika wana ndugu zao?
Kama hoja ni udugu ni kwanini Zanzibar wanapochagua wabunge wa kuja kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano, upande wa Tanzania Bara nao wasichague wawakilishi wachache kwenye Baraza la Wawakilishi ili kuukuza zaidi huo unaoitwa udugu???
Udugu unaonufaisha upande mmoja zaidi ya mwingine si mzuri jamani! Tuache propaganda. Kama tunaamini umoja ni nguvu utengano ni udhaifu basi tuungane tuwe nchi moja, serikali moja, rais mmoja na Tanzania moja ili tuwe ndugu kweli!

Watasema ni chuki lakini kama hatuwezi kumaliza tofauti zetu kwa kuunda serikali tatu au moja basi ni bora kila nchi ijendee kivyake! Hata Kenya na Uganda ni ndugu zetu lakini hatujaugana nao kutengeneza taifa la kusadikika!

Litakuwa ni kosa sana kuendelea kuwa na muungano ambao upande wa Tanganyika tu ndiyo unaendelea kupoteza historia yake wakati mshirika wake Zanzibar akibakiwa na ziada hata kama ni sawa na wilaya moja ya Tanganyika!

Wakuu; naombeni kuwasilisha hoja!
 
Nadhani umekimbilia heading na si mantiki...hoja ni muundo wa serikali, mbili, tatu au moja!

Huu c muungano ndio maana enzi za mwalimu ilikuwa ukiujadili tu unauliwa,kwa vile kwa sasa hayupo ndio watanganyika mnaamka kutoka ucngizini,c vibaya kuujadili ndio mtapata kuyaona madudu ya dubwana hili,wazbr wanalielewa vizuri dubwani hili bado watanganyika tu kulielewa.
 
Machama mengine yamebaki kumtukana mwenyekiti na jopo lake la katiba mpya.maoni ya wananchi kuyaita ni viongozi wa tume ni opofu!!! kama serikali moja haiwezekani bac tujaribu 3 siyo mbili maana tayari madhaifu ya ni pamoja na kero na uvunjifu wa katibu ya muungan unaofanywa na upande wa pili wa muungano.g56!
 
Good comment, nafikri serikali moja ndio jibu mengine yote ni watu kutafuta ulaji na umashuhuri tu. Wazo mbadala Tanzania ibaki na iwe na raisi mmoja, alafu zazibar iwe na governor wake na Tanganyika, lakini Raisi na baraza lake la mawaziri ndio wanakuwa na mamlaka ya juu kuliko governor
 
Mi nadhani waasisi wa Muungano walikula yamini fulani za kipepo ambapo waliapizana kwa matambiko ya damu!
Watu wazuri kabisa wa kuungana nao walikuwa ni nchi za huku bara ambazo hatuhitaji hata usumbufu wa kupanda majahazi kufika kwao, huku uki'risk maisha kwa hofu ya kuzama baharini!
Aina ya muungano tulio nao unaleta gharama mno kwa bara na wenzetu hawariziki na chochote.
Ninachojiuliza kwanini kusiwe na referrandum ya kuhoji kuwepo au kutokuwepo Muungano kwa Bara na Visiwani ili tukate mzizi wa fitna? Ni nani mwenye hati miliki ya nchi hizi mbili hadi akataze watu kuuliza upya kama wanahitaji Muungano?
 
Back
Top Bottom