Muungano bado una shida nyingi tusidanganyane

Hata Ndoa ya mke na mume inachangamoto nyingi sembuse URT
 
Uvunjwe haraka sn na wazanzibar warudi kwao
Hesabu za milinganyo: Kama Zanzibar yenye watu 1+ milioni lakini in Rais wao, Makamu 2 wa Rais, Mawaziri kadhaa, mikoa 5, wilaya kadhaa, tarafa na kata kadhaa, bunge la wawakilishi, wabunge wa Muungano, nk je, Tanganyika yenye watu 60mil ilipaswa kuwa na makamu wa Rais, mawaziri, mikoa, wilaya na tarafa ngapi?. Cross multiplication.
 
Hata Ndoa ya mke na mume inachangamoto nyingi sembuse URT
Tunapenda atojitokeze mtu mkweli na mwenye hofu ya Mwenyezimungu tunaemuamini atuambie ukweli mtupu ni NINI hasa yalikuwa mawazo/mpango/sababu hasa Mwl Nyerere na Mzee Karume walikusudia kuhusu muungano wa serikali mbili? Je, wote walikuwa na mawazo sawa kuhusu aina hii ya muungano au kulikuwa na mengine ambayo yangefuata? Na kama yalikuwepo ambayo yangefuata ni nani aliyakwamisha yasije na mambo yakabaki kama yaliyo sasa.
 
Alichofanya Nyerere ilikuwa uhaini.
 
Wahafidhina ndani ya Chama na serikali wanaulinda muungano kwa hoja nyepesi sana.

G55.
RIP mchungaji Christopher Mtikila.
muungano ni muhimu sana kiuchumi kuliko hata kisiasa kama ilivyokuwa zamani. Lakini ndani ya nchi moja ni lazima kuwe na magari yenye usajili tofauti? Kama ni lazima serikali ya zanzibar iwepo kwani Tanganyika tusiigawanye kwenye majimbo yanayoshabihiana na uwezo wa serikali ya zanzibar? Yaani tuwe na majimbo yanayomchagua Gavana wao wa jimbo na serikali ya jimbo inayowajibika kwenye serikali ya muungano?
 
Mishahara yao yote inalipwa toka bara pamoja na matumizi yote
 
CDM Wana sera ya majimbo.
 
Huu Muungano ni wa kijinga mpaka basi. Yaani hauna tofauti na zile mbio za mwenge za kila mwaka! Kiufupi hauna faida yoyote ile kwa nchi ya Tanganyika.

I wish ungevunjika hata kesho ili kila upande ujitegemee kwa 100%. Huwezi kuungana na watu wanyonyaji, wabinafsi, kupe na wa watu wa kunung'unika na kudeka muda wote kama Wazanzibari.
 
Alichofanya Nyerere ilikuwa uhaini.
Siamini kama Nyerere alikuwa mjinga sana kuifuta Tanganyika yake na kuiacha hai Zanzibar, lazima alikuwa na imani fulani ambayo aidha imefeli au inaendelea kufanyakazi kuelekea kwenye lengo kuu la muungano. Lasivyo huu muungano unahojiwa na hata watoto wadogo pia.
 
Warioba na Butiku waondoe
 
Wanaongea kiswahili ila matendo na uhalisia tofauti. Muungano ni union. Sasa mbona zanzibar ipo vilevilebna rais na serikali yake?

Labda tuseme Federation. Sasa hapo kiswahili sijui unaitaje. Hapo napo pana shida maanake tulipaswa kila mtu awe na chake ndo tuwe na cha pamoja. Bara sijui tuiteje tulichonacho.

Halafu kuna wato wamekomaaa hawataki liongelewe sembuse kurwkebisha. Hawaoni mapungufu haya ya mfumo?
 
Ikulu, mali, tamaduni na siri za Tanganyika sio siri wala mwiko kwa Mzanzibar lakini Ikulu, mali, tamaduni na siri za Zanzibar ni marufuku kwa Mtanganyika, na jamaa zetu akina Msekwa, Issa Shivj, Ulimwengu na malecela hawakuwa na hofu kuhusu hilo. Nadhani kuna jambo kubwa lilipangwa ambalo halisemwi kamwe.
 
Samahani sana, lakini, wewe na mjukuu wako wote mambumbumbu.
 
Ukwer humweka mtu huru wananchi wa Tanganyika tunao mzigo mkubwa tumebebeshwa isipokua tunaona sawa tu binafsi sijaona faida ya hili jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…