Kila aliyehoji muundo wa huu muungano alikiona cha moto wakati wa Nyerere. Jumbe aliondolewa kwa kuhoji uhalali wa serikali mbili wakati nchi zilizoungana ni mbili.Siamini kama Nyerere alikuwa mjinga sana kuifuta Tanganyika yake na kuiacha hai Zanzibar, lazima alikuwa na imani fulani ambayo aidha imefeli au inaendelea kufanyakazi kuelekea kwenye lengo kuu la muungano. Lasivyo huu muungano unahojiwa na hata watoto wadogo pia.
Njelu Kasaka na kundi lake walikuwa na hoja za msingi bungeni kutaka serikali ya Tanganyika, hoja zao zilizimwa na Nyerere nje ya bunge, na waziri mkuu wakati huo Malecela akapoteza uwaziri mkuu.
Sioni nia njema aliyokuwa nayo Nyerere zaidi ya kuisaliti Tanganyika.