Muungano bado una shida nyingi tusidanganyane

Muungano bado una shida nyingi tusidanganyane

Mi nadhani usivunjwe, faida zipo nyingi sana. Na mara nyingi kama sio mara zote miungano ya nchi duniani huwa hairekebishwi bali inarithiwa na kulindwa kwa nguvu zote, USA, UK, China, Spain, nk Ina malalamiko mengi sana lakini ni mwiko kujadili muungano. Hapa kwetu kila siku Kuna upande mmoja ndio unautekenya muungano bila kuchukuliwa hatua, lakini upande mwingine ukiutekenya hatua zinachukuliwa mara moja.
Usitudanganye hawa mwaka juzi walijitoa kwenye muungano na PM wao akaachia ngazi, muungano gani huu ambao wazanzibar pekee wamejaa huku kwetu(kwenye system) sisi kule tunachukuliwa kama watalii au vibarua wao, taja faida 3 ambazo sisi Tanganyika tunazipata? ukizitaja kuanzia tarehe 1-1-2024 hutoniona JF maisha yangu yote. Nchi za wenzetu muungano unapigiwa kura na wananchi na siyo maamuzi ya kamati kuu ya CCM pekee.
 
Nyerere alikuwa mnafiki sana.Aliua Tanganyika kwa maslahi yao
Nyerere alikuwa na akili zilizopitiliza, aliwaza miaka 100 ijayo hakutakuwa na mzamzibar asilia fundamentalists atatawala Zanzibar. Tuendelee TU kusogeleana, kuoana na kuishi pamoja. Siku hizi hata wamasai wanapatikana Zanzibar kwa wingi.. jitahidini sana kila mtanganyika aoe mzamzibar, ikishindikana zaeni nao watoto na kuwasomesha vya kutosha elmu dunia.
 
Wao wako 1m TU, hata wakijazana Huku hawana athari. Kumbuka kuwa kuwa wao hawana jeshi Wala fedha yao. Rais wao lazima achaguliwe huku Dodoma. Hawaruhusiwi kuwa na Rais wao ambae hakubaliki Tanganyika.
 
Nikiwa barabarani naendesha gari, Siti yangu ya mbele alikaa mjukuu wangu wa miaka 11. Mbele yetu kulikuwa na gari Ina namba za Zanzibar kwenye number plate yenye bendera ya Zanzibar. Mjukuu akaniuliza Ile gari mbona Ina namba za tofauti na hizi zetu, ni gari kutoka nchi gani?.

Nikamwambia ni gari kutoka Zanzibar. Akauliza kwani Zanzibar sio Tanzania? Nikamwambia Zanzibar ni Tanzania. Akaendelea kusema kwani T kwenye namba za magari inamaanisha Tanzania au Tanganyika? Nikamjibu inamaanisha Tanzania. Hakuuliza tena, bali nikamuona kama vile hakuridhika na majibu yangu anaona ninamchanganya TU.

Kuna watu ndani ya muungano waliondoa super league ikaonekana ni sawa, Kuna watu walitaka bendara Yao na wimbo wao wa taifa wakaonekana wako sawa TU, Kuna watu wakataka zibaki serikali mbili ya tanzania na ya Zanzibar ikaonekana ni sawa TU. Kuna watu wanafaidi sana ndani ya muungano lakini hawataki kuweka mambo yanavyotakiwa yawe kwa sababu zao TU
Kosa kubwa hili la kihistoria alifanya Nyerere. Lakin muda c mrefu tutafanya kama India kule cashmir
 
muungano ni muhimu sana kiuchumi kuliko hata kisiasa kama ilivyokuwa zamani. Lakini ndani ya nchi moja ni lazima kuwe na magari yenye usajili tofauti? Kama ni lazima serikali ya zanzibar iwepo kwani Tanganyika tusiigawanye kwenye majimbo yanayoshabihiana na uwezo wa serikali ya zanzibar? Yaani tuwe na majimbo yanayomchagua Gavana wao wa jimbo na serikali ya jimbo inayowajibika kwenye serikali ya muungano?
Hii ndio point ya msingi sana, kiutendaji na kiutawala itarahisisha sana. Inakera Rais wa nchi mpaka aende Wilayani Masasi ndio aambiwe changamoto za hospital,maji, umeme nk, wakati pale masasi kuna viongozi chungu nzima na rasilimali zote muhimu, wanachopaswa na full authority ya kujitawala.

Uwajibikaji:
Kwa sasa mkurugenzi wa wilaya au mkoa akizingua labda ametumia rasilimali vibaya, ufisadi nk... sio mkuu wa wilaya/mkoa, naibu waziri Tamisemi, waziri Tamisemi, naibu waziri mkuu, waziri mkuu, makamu wa Rais anayeweza kumtoa, wote wanasubiri mtukufu Rais aamue.. nchi hii ina wakurugenzi wangapi? Wakuu wa wilaya wanagapi? Rais atawezaje kuwamanage wote hawa?

Kwanini tusitengeneze serikali za majimbo? Ambazo zitajitawala zenyewe? Zitumie rasimali zilizopo kila mmoj kujiletea maendeleo..
 
Tukisema ipigwe kura ya kuuvunja muungano. Kule Zanzibar lazima yatatokea machafuko maana ni wanafiki
 
Hesabu za milinganyo: Kama Zanzibar yenye watu 1+ milioni lakini in Rais wao, Makamu 2 wa Rais, Mawaziri kadhaa, mikoa 5, wilaya kadhaa, tarafa na kata kadhaa, bunge la wawakilishi, wabunge wa Muungano, nk je, Tanganyika yenye watu 60mil ilipaswa kuwa na makamu wa Rais, mawaziri, mikoa, wilaya na tarafa ngapi?. Cross multiplication.
Fikiria mwenye kama inawezekana. Zanzibar 1+ milioni Ina rais 1. Kwa cross multiplication zako Tanganyika watu 60 + mil ilitakiwa kuwa na Marais 60!!!
 
Tunapenda atojitokeze mtu mkweli na mwenye hofu ya Mwenyezimungu tunaemuamini atuambie ukweli mtupu ni NINI hasa yalikuwa mawazo/mpango/sababu hasa Mwl Nyerere na Mzee Karume walikusudia kuhusu muungano wa serikali mbili? Je, wote walikuwa na mawazo sawa kuhusu aina hii ya muungano au kulikuwa na mengine ambayo yangefuata? Na kama yalikuwepo ambayo yangefuata ni nani aliyakwamisha yasije na mambo yakabaki kama yaliyo sasa.
💬💭🙏
 
muungano ni muhimu sana kiuchumi kuliko hata kisiasa kama ilivyokuwa zamani. Lakini ndani ya nchi moja ni lazima kuwe na magari yenye usajili tofauti? Kama ni lazima serikali ya zanzibar iwepo kwani Tanganyika tusiigawanye kwenye majimbo yanayoshabihiana na uwezo wa serikali ya zanzibar? Yaani tuwe na majimbo yanayomchagua Gavana wao wa jimbo na serikali ya jimbo inayowajibika kwenye serikali ya muungano?
💭💬🙏
 
Kila aliyehoji muundo wa huu muungano alikiona cha moto wakati wa Nyerere. Jumbe aliondolewa kwa kuhoji uhalali wa serikali mbili wakati nchi zilizoungana ni mbili.

Njelu Kasaka na kundi lake walikuwa na hoja za msingi bungeni kutaka serikali ya Tanganyika, hoja zao zilizimwa na Nyerere nje ya bunge, na waziri mkuu wakati huo Malecela akapoteza uwaziri mkuu.

Sioni nia njema aliyokuwa nayo Nyerere zaidi ya kuisaliti Tanganyika.
🙏
 
Zanzibar ni demu aliyeikata Tanganyika... Ila kwakuwa mwanaume ana asili ya kulazimisha Mambo ..... Basi Zanzibar imeamua kuichuna Tanganyika. Hivi kwa akili za kawaida inawezekana mtu anayetoka kwenye ki-Nchi swa na mkoa wa Tabora anaweza kuwa Rais kwenye Nchi ambayo Ina watu zaidi ya 55+m?.
🤣🤣🤣
 
Say whaaaaat?

Tema mate chini na uwaombe radhi watu wa Tabora!

Zanzibar hailingani hata na wilaya moja ya Tabora

Zanzibar kilomita za mraba 2,462

Sikonge kilomita za mraba 27,873


Zanzibar inaingia Sikonge mara kumi na moja!

Nyerere alikuwa amekunywa chakari siku anatuingiza chaka la Muungano

FBo0diTWUAQtMJU
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom