Muungano ni kati ya nchi ya Tanganyika na Zanzibar, kama Zanzibar ipo Tanganyika ipo wapi?

Nyie wazandiki wa CCM haya hamuambiani mkiwa ndani, mnakuja kuyalilia hapa JF
 
kwanini nchi ya Tanganyika itoweke na nchi ya Zanzibar iwepo?
Ni kwa sababu ndo matakwa ya makubaliano ya mungano ya 1964.
Kwanini nchi ya tanzania iwe kwenye ardhi ya nchi ya Tanganyika bila kuijumlisha ardhi ya nchi ya Zanzibar wakati udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa?
Ardhi ya Tanzania ni eneo lote la Jamuri ya Muungano wa Tanzania. Tatizo ni nchi kubwa kuungana na nchi ndogo ikiwa na lengo la kuidhibiti hiyo nchi ndogo kwa visingizio kadhaa.
Au huu muungano ulikuwa wa kubadili jina la Tanganyika na kuwa tanzania maana jina la zanzibar lipo?
Ndivyo ilivyo kwani ndivo alivyotaka Nyerere
Nauliza tena, Nchi ya tanganyika ipo wapi?
Kama nchi haipo ila ardhi bado ipo. Ni wakati sasa kuibadilisha hiyo ikawa Tanganyika, ila hili linaweza kufanyika iwapo tu moja kati ya mambo yafuatayo yatafanyika:
1 Kuitishwe bunge la katiba libadilishe muundo wa muungano
2 Uvunjwe muungano uliopo na baadae kuundwe muungano mwingine utaokuwa na nchi za Tanganyika na Zanzbar
3 Uvunjwe muungano uliopo na nchi za Zanzibar na Tanganyika kila moja iwe kwake kivyake.

Chaguo ni la kwenu wenye chungu na nchi
 
Mamangu nawe hujui. Akili za kuambiwa changanya na zako. Lakini pia msiba wa kujitakia hauna kilio.
 
Zanzibar Ina raisi wake tena ni mzawa ,viongozi wote wa Zanzibar ni wazawa na haitakaa itokee raisi wa Zanzibar asiwe mzawa .
Unazungumzia rais yupi mzawa? Huyu aliyepo na baadhi ya wengine waliopita ni Watanganyika, waliowekwa na Watanganyika kuitawala Zanzibar.
 
Unazungumzia rais yupi mzawa? Huyu aliyepo na baadhi ya wengine waliopita ni Watanganyika, waliowekwa na Watanganyika kuitawala Zanzibar.
Kama yupiii ambaee ni mtanganyika aliyewahi kuwa Rahisi Zanzibar???
 
Unasemaje very selifish wakati muundo huo ulitka kwenu? Very stupid people
Ulitoka kwetu wapi wewe Mzenji mla urojo? Huu muungano ni wa kidwanzi tu. Na nyinyi wazee wa kupenda mteremko ndiyo mnao ufurahia siku zote.
 
Sijawahi kukuelewa P. Mayalla. Ndio maana so far bado unatambia kusoma Ilboru na kupata daraja la kwanza na kusoma Sheria. Hii ni sawa.
Lakini nadhani matarajio ya jamii ni kuona application ya ulichokisoma effectively. Sawa divission one Ilboru, so what!?
Hapo juu umekataa kuwa hakuwà na nchi ya Tanganyika iliyoungana na nchi ya Zanzibar....!
Ila kulikuwa na nchi ya "Jamhuri ya Tanganyika" na "Jamhuri ya Zanzibar" zikaunda Tanzania.
Sasa kwa hoja yako hiyo kuna nchi inaitwa Tanzania?
My take tukishamaliza shule na vyuo uko... kinachofuata sasa ni application ya tulichosoma na kuleta outcome katika jamii. Sio tena kutambia division one halafu application zero.
 
Ulitoka kwetu wapi wewe Mzenji mla urojo? Huu muungano ni wa kidwanzi tu. Na nyinyi wazee wa kupenda mteremko ndiyo mnao ufurahia siku zote.
We chogo we; huo muundo wa muungano ulitoka kwa Nyerere baada ya kuona Zanzibar imemshinda kuitupilia mbali kama ambavyo alipenda. Alipoona imemshinda ndo akaamua kuidhibiti kwa kuungana nayo. Nyerere ni Mtanganyika, hivyo nikisema ulitoka kwenu ni kwasababu hiyo, au nasema uongo ndugu zangu?.

Mimi sijawahi kufurahia na sitofurahia kwa namna tunavyoendeshana. we chogo litambue hili kwani pingine unazungumza mambo usiyoyajua. Kama hujui jambo uliza, usikurupuke, watu watakuona mjinga.
 
Huyo Mayala, kiukweli ni intelligently brainwashed, anapinda pinda na tawala,
Ukweli ni kwamba ni muhimu sana kusoma alama za nyakati za misingi ya jamii.

Pengine Mayala anaamini turn ya sasa uliyosababishwa na Tanganyika kutokuwa na kiongozi basi ndio inatoa future ya Tanganyika ya miaka 100 mbele.

Udhaifu wa katiba ya Tanganyika wakati inaingia katika Muungano na hata wakati ikiendelea na Muungano umeifanya ikose kiongozi kwa sasa, jngawa Tanzania kama Jamhuri Unganiko inaye Kiongozi.

Tanganyika kwa sasa haina Kiongozi kwa sababu kiongozi wa Tanganyika lazima atokee Tanganyika kama ilivyo kwa Zanzibar ina kiongozi mwenye asili ya Zanzibar.

Hivyo basi kuwa na akili sana siyo kujitosheleza, ni muhimu ku- appreciate maoni ya wengine.

Mfano wengi huamini hata mwalimu Nyerere angeielewa janja ya Zanzibar kuendelea kuwa semi autonomous archipelago of Zanzibar angeruhusu mchakato wa semi autonomous ya Mainland Tanganyika.
Vile vile hata Magufuli angejua kuwa bunge linalomilikiwa na chama kimoja linaweza kuuzwa kirahisi kuliko lililo na mchanganyiko angeimarisha upinzani kwa kutotishia wananchi kuwa wakichagua mpinzani wakamuombe yeye hela za maendeleo ya jimbo lao.

Hoja hii inalenga kuzibua side adhesive za mayala-like.
 
hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, ni kwaajili ya Zanzibar tuu, lakini mabadiliko hayo hayatambuliwi na katiba ya JMT.
Mkuu nimekuwa nikirudiarudi kwamba Zanzibar kuwa nchi hayahitaji katiba ya JMT kutambua madam makubaliano ya muungano yanatambua hilo.

Katiba ya JMT na ile ya Zanzibar zinahitaji kufuata maelekezo ya makubaliano ya muungano na ndo sababu JMT haijasema lolote.

Nadhani unakumbuka swala la OIC wakati unajifunza kuwa mwandishi.

Zawadini
 
Nilitarajia muungano ule ungezifuta nchi zote mbili yaani nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika ili kuwe na nchi moja tu ya Tanzania. Kinachoshangaza kwa muungano huu ni uwepo wa nchi ya Zanzibar na kutoweka kwa nchi ya Tanganyika.
Kelele zote hizo hazikuwepo wakati Tanganyika imevaa koti la Tanzania, leo Zanzibari ndio imevaa koti la Tanzania 🇹🇿 ndio mnaikumbuka Tanganyika yenu, tulieni sasa zamu yao kukuongozeni.
 
Ulitoka kwetu wapi wewe Mzenji mla urojo? Huu muungano ni wa kidwanzi tu. Na nyinyi wazee wa kupenda mteremko ndiyo mnao ufurahia siku zote.
Hebu ulizia vizuri huu mfumo wa Muungano uliopo umetoka huko kwenu ulibuniwa na mwanasheria mkuu wa tanganyika wa wakati huo akitwa Roland Broun kwa kufaata mfumo wa Muungano wa uingereza na Iland ya kaskazini ndio hivo
 
Nyinyi Mizanzibari vichwa flat ni kama mikupe tu kwa nchi yetu ya Tanganyika. Kwa nini msijitoe kwenye huo muungano na kuunda Taifa lenu huru? Maana kila siku ni kudeka deka tu na kupenda kubebwa kama watoto wachanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…