Jemima Mrembo
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 2,864
- 8,328
Tutaangushwa na Tulia, mpuuzi sana yule Betina. Dawa ni kufyeka msituTukiungana na wote tukawa na kauli moja hakuna linaloshindikana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tutaangushwa na Tulia, mpuuzi sana yule Betina. Dawa ni kufyeka msituTukiungana na wote tukawa na kauli moja hakuna linaloshindikana.
Nyie wazandiki wa CCM haya hamuambiani mkiwa ndani, mnakuja kuyalilia hapa JFNa wala hatuna uwezo wa kujitawala. Bora wao kukiwa na Rais wa Tanzania kutoka bara,still Zanzibar wanajitawala.Inauma eti hatuna haki ya kufanya kazi hospital za Zenj za Serikali na Taasisi zozote zile za Serikali ya Zenj ila wao haki wanayo.#Tanganyikaexit
Bilaaa Shakaaa ✍️✍️✍️Tukiungana na wote tukawa na kauli moja hakuna linaloshindikana.
Watakufa na kipi zaidi ya kuuana tu?Wazanzibari wanachokipenda khasa khasa ni muungano usiwepo kabisa kila mmoja afe na chake
Ni kwa sababu ndo matakwa ya makubaliano ya mungano ya 1964.kwanini nchi ya Tanganyika itoweke na nchi ya Zanzibar iwepo?
Ardhi ya Tanzania ni eneo lote la Jamuri ya Muungano wa Tanzania. Tatizo ni nchi kubwa kuungana na nchi ndogo ikiwa na lengo la kuidhibiti hiyo nchi ndogo kwa visingizio kadhaa.Kwanini nchi ya tanzania iwe kwenye ardhi ya nchi ya Tanganyika bila kuijumlisha ardhi ya nchi ya Zanzibar wakati udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa?
Ndivyo ilivyo kwani ndivo alivyotaka NyerereAu huu muungano ulikuwa wa kubadili jina la Tanganyika na kuwa tanzania maana jina la zanzibar lipo?
Kama nchi haipo ila ardhi bado ipo. Ni wakati sasa kuibadilisha hiyo ikawa Tanganyika, ila hili linaweza kufanyika iwapo tu moja kati ya mambo yafuatayo yatafanyika:Nauliza tena, Nchi ya tanganyika ipo wapi?
Mamangu nawe hujui. Akili za kuambiwa changanya na zako. Lakini pia msiba wa kujitakia hauna kilio.Na wala hatuna uwezo wa kujitawala. Bora wao kukiwa na Rais wa Tanzania kutoka bara,still Zanzibar wanajitawala.Inauma eti hatuna haki ya kufanya kazi hospital za Zenj za Serikali na Taasisi zozote zile za Serikali ya Zenj ila wao haki wanayo.#Tanganyikaexit
Unasemaje very selifish wakati muundo huo ulitka kwenu? Very stupid peopleVery selfish people.
Unazungumzia rais yupi mzawa? Huyu aliyepo na baadhi ya wengine waliopita ni Watanganyika, waliowekwa na Watanganyika kuitawala Zanzibar.Zanzibar Ina raisi wake tena ni mzawa ,viongozi wote wa Zanzibar ni wazawa na haitakaa itokee raisi wa Zanzibar asiwe mzawa .
Kama yupiii ambaee ni mtanganyika aliyewahi kuwa Rahisi Zanzibar???Unazungumzia rais yupi mzawa? Huyu aliyepo na baadhi ya wengine waliopita ni Watanganyika, waliowekwa na Watanganyika kuitawala Zanzibar.
1. Mhe. Aboud Jumbe MwinyiKama yupiii ambaee ni mtanganyika aliyewahi kuwa Rahisi Zanzibar??
Ulitoka kwetu wapi wewe Mzenji mla urojo? Huu muungano ni wa kidwanzi tu. Na nyinyi wazee wa kupenda mteremko ndiyo mnao ufurahia siku zote.Unasemaje very selifish wakati muundo huo ulitka kwenu? Very stupid people
Sijawahi kukuelewa P. Mayalla. Ndio maana so far bado unatambia kusoma Ilboru na kupata daraja la kwanza na kusoma Sheria. Hii ni sawa.Mkuu MKWEAMINAZI, kwanza kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako hili, kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
Pili nikurekebishe hii opening statement yako ya "Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", it should be "Mwaka 1964 nchi iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, iliungana na nchi iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", kwasababu nchi hizi zote mbili sasa hazipo!.
Hii ni kweli, na ndicho kilichopo!. Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu muungano now, than any other times, kwasababu ni Mama Samia, ndiye aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika, wala nchi ya Zanzibar, kilichopo ni nchi moja tuu ya Tanzania!. Zanzibar sio nchi!.
Nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
Zanzibar hii iliyopo sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani!.
Sii kweli nchi ya Tanzania iko kwenye ardhi ya iliyokuwa Tanganyika, nchi ya Tanzania ni eneo lote la iliyokuwa Tanganyika na eneo lote la iliyokuwa Zanzibar!.
Na ni kufuatia kitendo kile cha kuchanganya udongo, ndio kuizi fuse nchi zote mbili kuwa nchi moja, hivyo muungano wetu ni muungano wa milele!, hauwezi kuvunjwa kwa namna yoyote, kwasababu ili kuuvunja huu muungano wetu adhimu, ni lazima kuuchukua ule udongo ulio changanywa na kuutenganishe, kitu ambacho haiwezekani!.
Ndio maana hata ule unaitwa ni mkataba wa muungano, The Articles of the Union between Tanganyika and Zanzibar, ule sio mkataba, ni makubaliano ya kuungana milele!, Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
Hapana, Tanganyika ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara, ila jina la Zanzibar lilibaki kwasababu ya utawala wake wa ndani tuu lakini Zanzibar sio nchi!.
Usiendelee kuuliza tena, nchi ya Tanganyika haipo!, na nchi ya Zanzibar pia haipo, kilichopo ni nchi moja ya Tanzania!.
Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,
1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.
2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.
Muungano wetu ni very unique, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao on one side ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, at the same time ni muungano wa federation wenye serikali mbili.
Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni head of state, head of the government and CinC.
Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar.
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa!.
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, ni kwaajili ya Zanzibar tuu, lakini mabadiliko hayo hayatambuliwi na katiba ya JMT.
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee na ya kudumu ya kuondoa kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja!.
P
We chogo we; huo muundo wa muungano ulitoka kwa Nyerere baada ya kuona Zanzibar imemshinda kuitupilia mbali kama ambavyo alipenda. Alipoona imemshinda ndo akaamua kuidhibiti kwa kuungana nayo. Nyerere ni Mtanganyika, hivyo nikisema ulitoka kwenu ni kwasababu hiyo, au nasema uongo ndugu zangu?.Ulitoka kwetu wapi wewe Mzenji mla urojo? Huu muungano ni wa kidwanzi tu. Na nyinyi wazee wa kupenda mteremko ndiyo mnao ufurahia siku zote.
Huyo Mayala, kiukweli ni intelligently brainwashed, anapinda pinda na tawala,Sijawahi kukuelewa P. Mayalla. Ndio maana so far bado unatambia kusoma Ilboru na kupata daraja la kwanza na kusoma Sheria. Hii ni sawa.
Lakini nadhani matarajio ya jamii ni kuona application ya ulichokisoma effectively. Sawa divission one Ilboru, so what!?
Hapo juu umekataa kuwa hakuwà na nchi ya Tanganyika iliyoungana na nchi ya Zanzibar....!
Ila kulikuwa na nchi ya "Jamhuri ya Tanganyika" na "Jamhuri ya Zanzibar" zikaunda Tanzania.
Sasa kwa hoja yako hiyo kuna nchi inaitwa Tanzania?
My take tukishamaliza shule na vyuo uko... kinachofuata sasa ni application ya tulichosoma na kuleta outcome katika jamii. Sio tena kutambia division one halafu application zero.
Mkuu nimekuwa nikirudiarudi kwamba Zanzibar kuwa nchi hayahitaji katiba ya JMT kutambua madam makubaliano ya muungano yanatambua hilo.hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, ni kwaajili ya Zanzibar tuu, lakini mabadiliko hayo hayatambuliwi na katiba ya JMT.
Kuuana kivipi?Watakufa na kipi zaidi ya kuuana tu?
Kelele zote hizo hazikuwepo wakati Tanganyika imevaa koti la Tanzania, leo Zanzibari ndio imevaa koti la Tanzania 🇹🇿 ndio mnaikumbuka Tanganyika yenu, tulieni sasa zamu yao kukuongozeni.Nilitarajia muungano ule ungezifuta nchi zote mbili yaani nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika ili kuwe na nchi moja tu ya Tanzania. Kinachoshangaza kwa muungano huu ni uwepo wa nchi ya Zanzibar na kutoweka kwa nchi ya Tanganyika.
Hebu ulizia vizuri huu mfumo wa Muungano uliopo umetoka huko kwenu ulibuniwa na mwanasheria mkuu wa tanganyika wa wakati huo akitwa Roland Broun kwa kufaata mfumo wa Muungano wa uingereza na Iland ya kaskazini ndio hivoUlitoka kwetu wapi wewe Mzenji mla urojo? Huu muungano ni wa kidwanzi tu. Na nyinyi wazee wa kupenda mteremko ndiyo mnao ufurahia siku zote.
Nyinyi Mizanzibari vichwa flat ni kama mikupe tu kwa nchi yetu ya Tanganyika. Kwa nini msijitoe kwenye huo muungano na kuunda Taifa lenu huru? Maana kila siku ni kudeka deka tu na kupenda kubebwa kama watoto wachanga.We chogo we; huo muundo wa muungano ulitoka kwa Nyerere baada ya kuona Zanzibar imemshinda kuitupilia mbali kama ambavyo alipenda. Alipoona imemshinda ndo akaamua kuidhibiti kwa kuungana nayo. Nyerere ni Mtanganyika, hivyo nikisema ulitoka kwenu ni kwasababu hiyo, au nasema uongo ndugu zangu?.
Mimi sijawahi kufurahia na sitofurahia kwa namna tunavyoendeshana. we chogo litambue hili kwani pingine unazungumza mambo usiyoyajua. Kama hujui jambo uliza, usikurupuke, watu watakuona mjinga.