Mkuu
MKWEAMINAZI, kwanza kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako hili, kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
Pili nikurekebishe hii opening statement yako ya "Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", it should be "Mwaka 1964 nchi iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, iliungana na nchi iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", kwasababu nchi hizi zote mbili sasa hazipo!.
Hii ni kweli, na ndicho kilichopo!. Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu muungano now, than any other times, kwasababu ni Mama Samia, ndiye aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika, wala nchi ya Zanzibar, kilichopo ni nchi moja tuu ya Tanzania!. Zanzibar sio nchi!.
Nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
Zanzibar hii iliyopo sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani!.
Sii kweli nchi ya Tanzania iko kwenye ardhi ya iliyokuwa Tanganyika, nchi ya Tanzania ni eneo lote la iliyokuwa Tanganyika na eneo lote la iliyokuwa Zanzibar!.
Na ni kufuatia kitendo kile cha kuchanganya udongo, ndio kuizi fuse nchi zote mbili kuwa nchi moja, hivyo muungano wetu ni muungano wa milele!, hauwezi kuvunjwa kwa namna yoyote, kwasababu ili kuuvunja huu muungano wetu adhimu, ni lazima kuuchukua ule udongo ulio changanywa na kuutenganishe, kitu ambacho haiwezekani!.
Ndio maana hata ule unaitwa ni mkataba wa muungano, The Articles of the Union between Tanganyika and Zanzibar, ule sio mkataba, ni makubaliano ya kuungana milele!,
Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
Hapana, Tanganyika ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara, ila jina la Zanzibar lilibaki kwasababu ya utawala wake wa ndani tuu lakini Zanzibar sio nchi!.
Usiendelee kuuliza tena, nchi ya Tanganyika haipo!, na nchi ya Zanzibar pia haipo, kilichopo ni nchi moja ya Tanzania!.
Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,
1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.
2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.
Muungano wetu ni very unique, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao on one side ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, at the same time ni muungano wa federation wenye serikali mbili.
Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni head of state, head of the government and CinC.
Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar.
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa!.
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, ni kwaajili ya Zanzibar tuu, lakini mabadiliko hayo hayatambuliwi na katiba ya JMT.
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee na ya kudumu ya kuondoa kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja!.
P