Muungano ukivunjika na Zanzibar itavunjika

Muungano ukivunjika na Zanzibar itavunjika

Zanzibar ilikuwepo kabla ya muungano na ilikuwa haitegemei kitu kutoka Tanganyika.
Hujui kwamba Tanganyika ndio iliitoa Zanzibar mikononi mwa sultani la sivyo Zanzibar ingekuwa bado chini ya mwarabu katili.
 
Sijui umesoma historia ya wapi lakini pia kumbuka kwamba hizo bandari munazoringia zote zilikuwa sehemu ya ukanda wa maili kumi wa pwani chini ya utawala wa Zanzibar.
Bila Tanganyika Zanzibar mtateseka sana kwani hata chakula chenu sehemu kubwa inatoka Zanzibar.
 
Kwa wanaojua kanuni za uharibifu, huwa hauachii mahali au kwenye kitu kimoja.

Nyerere aliwahi kuulinganisha na kula nyama ya binadamu. Ailaye haachi. Sijui ukweli wa dhana hii.

Hata hivyo, ukiwasikia wanaohanikiza tuvunje muungano, unapata wasiwasi nao.

Mfano, juzi mtu mmoja aitwaye Jussa alisikika akisema tuuvunje na kugawana mbao. Haya ni mawazo mafupi hasa kwa upande wa visiwani ambao watu wengi hujidanganya kuwa muungano ukivunjika watakuwa kama Dubai kwa vile wameonja harufu ya mafuta. Ni uchoyo na upofu mtupu.

Muungano ukivunjika, yafuatayo yanaweza kutokea:

Mosi, wapemba nao watataka kujitenga na waswahili weusi ili wawe karibu na ndugu zao waarabu ambao huwa wanawaabudia japo waarabu wanawaona kama watumwa wa kawaida.

Pili, Tanganyika italazimika kuwatimua wazenj wote ili warejee kwao na Zenj itajibu mapigo japo hatua hii itazua tatizo jingine.

Tatu, kama idadi ya Wazenji wote walioko bara watatimuliwa, Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuwatosheleza kimaisha hata kama ingekuwa na hayo mafuta ambayo haina uzoefu wa kuya-manage sawa na nchi nyingine za kiafrika.

Nne, Zenj itakumbwa na tishio la mapinduzi toka kwa migawanyiko yake ya asili baina ya waliofanya mapinduzi na waliopinduliwa ambavyo kimsingi, ndiyo sababu kuu iliyoisukuma kuungana na Bara.

Tano, Zenj itakuwa na tishio la usalama kutokana na kutokuwa na jeshi lake na vyombo vingine vya ulinzi. Hivyo, italazimika kuendelea kutegemea Tanganyika hata kama ni kinafiki.

Sita na mwisho, Zenj itatumia fedha nyingi kuagiza bidhaa toka Tanganyika katika fedha za kigeni jambo ambalo litaathiri vibaya uchumi wake.

Unaweza kuongeza madhara mengine na faida kama zipo.
Kwanza Pemba na Zanzibar wakigawana mbao Wala hakuna shida,pili sheria za Kimataifa xitawakinda Wazanzibar walioko Bara kama ilivyokuwa Kwa Sudan na South Sudan,sana sana watalipia resident permit basi..

Mwisho hata Tanganyika watu wa Mikoani hatutakubali jasho letu kujenga Dar pekee.
 
Kwamba Tanganyika itabaki salama?
Wale wanaowachukia wazanzibari Kwa sababu ni waislam unafikiri chuki Yao itaishia Kwa wazanzibari?
Waislam wapo Zanzibar tu?

Aliekwambia Zanzibar vyakula vitapanda bei nani?lazima kununua Tanganyika?au Tanganyika ndo nchi pekee inazalisha vyakula duniani?

Aliekwambia nchi zikivunjika lazima Raia wafukuzwe nani??
Kila Mtanzania aliezaliwa baada ya mwaka 1964 huku Tanganyika ana haki ya kuchukua Uraia wa Tanganyika...
Zanzibar ..watapiga hatua kubwa Sana ...billa kuzuiwa na watanganyika

..kuna chuki za aina nyingi.

..kuna chuki dhidi ya Waislamu.

..kuna chuki dhidi ya Wakristo.

..kuna chuki za kikabila, za rangi, jinsia, kiuchumi, etc.

..jambo la msingi ni kuweka mfumo unaotoa HAKI kwa kila raia.

..hili jambo lionekane kwa vitendo na sio maneno-maneno.

..kwa muda mrefu viongozi wamekuwa wanasisitiza amani, huku wakifumbia macho haki.
 
Ndiyo.nimekaa miaka mitano.wakati nataka kununua ardhi nikakerwa na lugha zao mbaya hadi nikahama.ardhi nikanyimwa.wakasema machogo yahee hawaruhusiwi kupata ardhi huku
Ahaa sawa kiongozi nashkuru kwamajibu napia pole sana kukubaguliwa
 
Usiwakee watu maneno midomoni hakuna wenye hizo hisia za kipumbavu labda wewe ndiye mwenye nazo!

Uongozi ukienda mrama unapaswa uambiwe ukweli acheni kuingiza mambo ya kijinga jinga kutafuta sympathy za wasiojielewa.
Utakuwa umeusahau waraka wa maaskofu wewe.
 
Muungano haukupata baraka ya wenye nchi. Ni kama vile ndoa ya kulazimishwa. Lilikuwa ni takwa la Nyerere na Karume.

Pengine wananchi wangeshirikishwa, wangeweza kutoa maoni yao. Wananchi ndiyo wenye nchi. Wasikilizwe!

Kwani wenye nchi wanasemaje kuhusu Muungano?
Sasa leo baba yenu nawashirikisha rasmi
 
Mkuu ulisoma wapi na kwa sasa unafanya shughuli gani?

Ulichoandika unakielewa kweli?
Ulichoandika kinaweza au unaweza kukitumia uweze kuisaidia jamii ya kijijini kwako huku bsra au familia yako?

Nina wasiwasi unaishi bure na unakula bure huko uliko.
Hujui usemalo mwanangu. Kama kusoma ni deal, nimesoma sana tu ndani na nje ya nchi na ninaishi maisha safi ya kujitegemea na kuwasaidia wengine wengi tu. Laiti kungekuwa na namna ya kuonana uso kwa uso, ungeramba viatu vyangu academically na katika maisha ya kawaida ya ukwasi ya binadamu tena maskini na mjinga kama wewe. Sijaona hoja yoyote kwenye utumboo ulioandika hapa.
 
Back
Top Bottom