Lucas Julson
Member
- Sep 8, 2014
- 12
- 4
Daaah, tuendelee kula mtori tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wazenji watatia mkorogo kama kawaida yao ili wafanane na waarabu, kwa ubaguzi wa waarabu dhidi ya ngozi nyeusi yaani watauwana.Kwa wanaojua kanuni za uharibifu, huwa hauachii mahali au kwenye kitu kimoja.
Nyerere aliwahi kuulinganisha na kula nyama ya binadamu. Ailaye haachi. Sijui ukweli wa dhana hii.
Hata hivyo, ukiwasikia wanaohanikiza tuvunje muungano, unapata wasiwasi nao.
Mfano, juzi mtu mmoja aitwaye Jussa alisikika akisema tuuvunje na kugawana mbao. Haya ni mawazo mafupi hasa kwa upande wa visiwani ambao watu wengi hujidanganya kuwa muungano ukivunjika watakuwa kama Dubai kwa vile wameonja harufu ya mafuta. Ni uchoyo na upofu mtupu.
Muungano ukivunjika, yafuatayo yanaweza kutokea:
Mosi, wapemba nao watataka kujitenga na waswahili weusi ili wawe karibu na ndugu zao waarabu ambao huwa wanawaabudia japo waarabu wanawaona kama watumwa wa kawaida.
Pili, Tanganyika italazimika kuwatimua wazenj wote ili warejee kwao na Zenj itajibu mapigo japo hatua hii itazua tatizo jingine.
Tatu, kama idadi ya Wazenji wote walioko bara watatimuliwa, Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuwatosheleza kimaisha hata kama ingekuwa na hayo mafuta ambayo haina uzoefu wa kuya-manage sawa na nchi nyingine za kiafrika.
Nne, Zenj itakumbwa na tishio la mapinduzi toka kwa migawanyiko yake ya asili baina ya waliofanya mapinduzi na waliopinduliwa ambavyo kimsingi, ndiyo sababu kuu iliyoisukuma kuungana na Bara.
Tano, Zenj itakuwa na tishio la usalama kutokana na kutokuwa na jeshi lake na vyombo vingine vya ulinzi. Hivyo, italazimika kuendelea kutegemea Tanganyika hata kama ni kinafiki.
Sita na mwisho, Zenj itatumia fedha nyingi kuagiza bidhaa toka Tanganyika katika fedha za kigeni jambo ambalo litaathiri vibaya uchumi wake.
Unaweza kuongeza madhara mengine na faida kama zipo.
Kutakuwa na ukabila mkubwa Sana Tanganyika , nipo nimekaa pale
Mkuu rudi juu usikilize ile video ya Mbunge Ali Kessi. Halafu angalia Bunge linavyoshangiliaKwamba Tanganyika itabaki salama?
Wale wanaowachukia wazanzibari Kwa sababu ni waislam unafikiri chuki Yao itaishia Kwa wazanzibari?
Waislam wapo Zanzibar tu?
Raia wa nchi ya Zanzibar sio mchezo kabisa. Wangebaki na umakamu wa Rais tu kulinda maslahi ya nchi yao pendwa ya Zanzibarkama nini watu wagawane mbao tu hakuna namna 😅
Mkuu rudi hapo juu usikilize ile video ya Mbunge wa Nkasi Ali Kessi. Halafu angalia Bunge linavyoshangilia
Kuna maana moja, kuna reservations na zinapopata ufa hujitokeza
Kama unakumbuka, AH Mwinyi a na mawaziri wake waliipa Zanzibar upendeleo.
Watu walijua lakini hawakuwa na sababu za kulianzisha. Ilipokuja OIC na Loliondo hapa ukatumika ufa wakapatikana wabunge 55! the rest is history. Muulize Jenerali
Rais SSH naye si tofauti. Kuna mambo mengi ya kuipendelea Zanzibar bila kuwajibika
Ikiwa Zbar inapata 1/3 ya mkopo halafu anayerudisha ni Mtanganyika, hapo kuna jema?
Kero za muungano zilziodumu miaka nenda rudi na kamati lukuki zimemalizwa kutoka 26 hadi 2 na wanaojua zimemalizwa vipi ni Wazanzibar .
Mtanganyika hakujulishwa na ni siri. Unadhani Watanganyika wanajisikia uzuri!
Deni la umeme waliotumia Wazanzibar linalipwa na wabeba mizigo wa Manzese, kisa tu 'ameagiza'
Kila jambo limefanywa kwa makusudi kwavile hakuna anayeitetea Tanganyika.
Takwimu za BoT za miaka michache iliyopita zinaonyesha mkoa wa Mwanza unachangia pato kwa Trilioni 10
Mkoa wa Simiyu unaonekana na mkoa mdogo sana wa Kilimanjaro unaonekkana.
Rasilimali zinazoelekezwa huko ni chache kuliko zile zinazokwenda Zbar ambako hakuna mchango kwa mujibu wa BoT na aliyekuwa Gavana Marhum Ben Ndulu
Kwahiyo hili la Bandari ni ufa tu, kuna mengi yanafanywa watu wanayaona wamekaa kimya, haina maana wameridhika. Hivyo liangalie hili jambo kwa jicho pana!
JokaKuu Pascal Mayalla
Nyerere alianza ukombozi wa Zanzibar tangu bado ukiwa Nyani misituni kwenu Congo kabla Tippu Tipp hajakupeni lifti mkakosa soko.Zanzibar ilikuwepo kabla ya muungano na ilikuwa haitegemei kitu kutoka Tanganyika.
Naam hata gharama hii iliotumika kumfukuza Sultani hawajatulipa.Zenj ita twaliwa kwa nguvu kama sehemu ya Bara. Nakuwa kama Kisiwa cha Bara.
Hamna hata udini, Watanzania wanataniana tu, ila kuna wanaopenda kulalamika.Tanganyika ukabila si tatizo. Tatizo letu ni udini
Well said. Watanganyika ambao ni Watanzania hawan platform au uwezo wa kuvunja muungano.As long Wazanzibari hawataki huu Muungano... Tanganyika lazima italipa..gharama ya kulazimisha ndoa....
Sasa basi why tusivunje huu Muungano??
Nyerere alianza ukombozi wa Zanzibar tangu bado ukiwa Nyani misituni kwenu Congo kabla Tippu Tipp hajakupeni lifti mkakosa soko.
Msikilize Waziri wa Sultani anavyomkumbuka Nyerere akiunda vyama ASP akiwa na katibu wake Zuberi Mtemvu huko huko znz enzi za Sultani.
Well said. Watanganyika ambao ni Watanzania na wasio na platform hawana uwezo wa kuvunja muungano.
Kundi la G55 lilijaribu, Nyerere akwaambia kama wanataka kuvunja muungano watoke nje ya chama kwanza kwasababu hiyo si sera ya chama.
Kwasasa Tanzania ndiyo Tanganyika kwa maana kwamba Tanganyika haina mtetezi. Mfano, wakati Rais Hussein Mwinyi anasema Mtanganyika hatapewa ardhi Zanzibar ule ulikuwa Ubaguzi. Hakuna aliyesema akiwemo Rais SSH kwasababu yeye ni muungano hawezi kupingana na Zbar anasimamia umoja wa kitaifa, lakini je, Watanganyika waliridhika? Jibu ni hapana na hilo likabaki moyoni
Juzi Mh Mbowe kaongea vizuri sana akitahadharisha hatari inayokuja kwa umoja wa kitaifa. Yeye alionekana Mbaguzi kwasababu ukiwa Mtanzania hurusiwi kuongelea muungano, ukiwa Mzanzbar unaweza kutukana hata ya nguoni. Katika mazingira hayo Tanganyika itafanyaje?
Wanoweza kuvunja muungano kama wanataka ni Wazanzibar. Ikiwa 2010 walibadilisha katiba, wanaweza pia kupitisha mswada ndani ya BLW wa kura ya maoni. Pili, Wale Wabunge wa Zanzibar wanaokuja Dodoma wasije.
Tatu, Wazanzibar wote wanaofanya kazi ndani ya Taasisi za muungano waondoke. Haya yakitokea yata trigger JMT kuingilia kati na hapo kura ya maoni itaamua
Lakini pia jiulize , je, Wazanzibar hawataki muungano? Maana kuna utata hapo! Ni wapi wasioutaka?
Naam hata gharama hii iliotumika kumfukuza Sultani hawajatulipa.
Hivi unakumbuka kila siku Wazanzibar waliita Watanganyika wajinga. Wanasema eti wanawafundisha kuhusu muungano. Ukweli ni kuwa Watanganyika waliridhika na ukubwa kama Kaka na kuichukulia Zanzibar kwa udogo wake tu, haina maana walikuwa ni wajinga. Mfano, SMZ inaajiri watu 12,000. JMT inaajiri watu 100,000 tu kwa mfano. 21% ya ajira za muungano inakwenda Zbar zaidi ya 21,000. Hii ina maana JMT inaajiri sana kuliko SMZShida Sisi watanganyika tunataka kuvunja Muungano Kwa kuwakomoa wazanzibari...hii itafanya zoezi kuwa gumu kuliko tunavyo dhani...
Mbona tayari tumewasaidia sana! hebu nionyeshe bili yao ya wizara ya ulinzi, mambo ya ndani, nje, na taasisi za muungano. Kwa kutumia mwanya wa kutokuwa na gharama kubwa za mambo makubwa wamejenga taasisi zao. Kwa mfano hakuna taasisi ya muungano isiyo na mbadala Zanzibar! hakuna.Dawa ni kuvunja Muungano Kwa makubaliano Tu ya kuwasaidia wapige hatua ya kuwa Taifa hata Kwa miaka mitano...
Tunaweza sema Tunavunja Muungano Kwa makubaliano ya kuwasaidia hela kidogo Sana ...hata bilioni 50 kila mwaka Kwa miaka mitano Hadi watakapo stabilize....in return na Sisi tutapata assurance kutoka kwao ya kutotumia "Uhuru wao mpya"kutuhujumu na Kenya mfano au nchi yeyote Ile ingine...
Pata Picha Kenya airways wamehamia Zanzibar baada ya Muungano kufa...Sisi tuko tayari??
Umeongea yote but hutaki kunijibu hoja yangu..Hivi unakumbuka kila siku Wazanzibar waliita Watanganyika wajinga. Wanasema eti wanawafundisha kuhusu muungano. Ukweli ni kuwa Watanganyika waliridhika na ukubwa kama Kaka na kuichukulia Zanzibar kwa udogo wake tu, haina maana walikuwa ni wajinga. Mfano, SMZ inaajiri watu 12,000. JMT inaajiri watu 100,000 tu kwa mfano. 21% ya ajira za muungano inakwenda Zbar zaidi ya 21,000. Hii ina maana JMT inaajiri sana kuliko SMZ
Je, unadhani 21% ni haki? na unadhani Watanganyika hawakujua fursa za Wzbar kwao na na Tanganyika!
Rais Samia alipokwenda kwenye mahafali ya Uhamiaji kule Tanga alisema ''Uhamiaji ni suala la muungano' hivyo Wazanzibar waajiriwe popote kwasababu kule kwao ni padogo wanajuana na inaathiri utendaji.
Hii ilikuwa njia ya ujanja ya kuleta Wzbar bara ili kujenga uhalali wa kuongeza intake. Fikiri kama wana graduate 50 bila kuleta bara next year watahitaji mafunzo !
Kwahiyo hakuna kukomoa ni kwamba Wazanzibar wameansha dude kwa kujua au kutojua, na hili linagharama kwao. Tunaona ya Mbarawa, sasa yataenda hadi taasisi. Kama si za muungano wakae pembeni kwasababu ni wao wanaolalamika kuongezwa mambo ya muungano.
Mbona tayari tumewasaidia sana! hebu nionyeshe bili yao ya wizara ya ulinzi, mambo ya ndani, nje, na taasisi za muungano. Kwa kutumia mwanya wa kutokuwa na gharama kubwa za mambo makubwa wamejenga taasisi zao. Kwa mfano hakuna taasisi ya muungano isiyo na mbadala Zanzibar! hakuna.
Mfano:
Wanavikosi maalumu vya ulinzi
TPA- Wana ZPA
IMO- ZMO
TAA- ZAA
TPDC- ZPDC
TANESCO-ZESCO
TBS(Viwango)- Wana ZBS
TMDA- ZFDA
Baraza la Mitihani- Wana Baraza la Mitihani
HESLB- ZHESL
Bank- ZPB
Orodha ni ndeu sana inaendelea...
Advantage waliyo nayo ni ajira sehemu zote mbili. Mambo ya JMT wanatumia kama sehemu za ajira tu.
Wabunge wao katika kamati walimkatalia Aida Kenani kwa kumwambia suala la Bandari haliwahusu kwa mujibu wa katiba yao. Lakini ni hao hao walikwenda Dubai na India kwa jambo lisilo wahusu kwavile tu wanapata pesa za bure za kodi za Watanganyika.
Hiyo ni mifano michache sana, sasa unataka wasaidiwe nini tena?
Kwasasa wanapata 4.5% ya pato la Tanganyika. Kwa maana madini na hata Bandari zetu.
, magufuli aliwasamehe na Samia amewasamehe. Yaani mbeba lumbesa wa Ubungo au Tandale analipa umeme na ziada kwa ajili ya Wananchi wa Taifa bora la Zanzibar! Unataka wapewe nini zaidi
Kila Tanganyika ikifanya vizuri wanapata zaidi. Ni rahisi kupata msuluhishi wa kimataifa aangalie hisa zao na kuwalipa kuliko ilivyo sasa. Yaani tukilipa kodi zaidi Tanganyika wao wanapata 4.5, achilia ukweli kwamba mikopo wanayopata inalipwa na JMT ambayo ni Tanganyika
Wanahitaji referendum waamue wao kama wanataka muungano au la. Kwa Tanganyika ile population na size of economy yao, Zanzibar haina impact. Wakati ukifika Tanganyika watakuwa na haki ya kulinda masilahi yao, hapo hakuna ubaguzi wala nini
Ipo siku tu utavunjika, ni swala la muda tuWanaotaka kuvunja wataondoshwa KABLA haujavunjika!!!
"Zibaki mbili sio tatu"
Hakuna tatizo kabisa kwasababu Kenya airways wana 'hub' Tanzania. Fuatilia timbwili la wakati wa Kikwete.Umeongea yote but hutaki kunijibu hoja yangu..
Tuko tayari kuvunja Muungano Kwa shari na ikitokea Zanzibar wanaegemea Kenya...mfano Kenya airways waende weka hub Yao pale Zenji...tuko tayari Kwa Hilo Tanganyika?
Au waweke Us military base pale Zanzibar...tuko tayari??