Gozigumu,

Bara hulipia ulinzi, usalama, mambo ya nje, elimu ya juu, Bunge, n.k na 4.5% ya pesa ya missaada yote! Pia ukiangalia idadi ya watu kati ya bara na visiwani % ya missada ingebidi iwe ni 2.5% ila Visiwani hupata mara 2!

Gesi ya Songosongo kutumiwa na TANESCO na umeme huu unatumika Unguja na Pemba utafika Mwaka huu!

Je Serikali ya bara ilipe cash SMZ pesa inayotokana na dhahabu au almasi?

Jua pia Visiwani huwa hawachangii ktk serikali kuu kwa mda mrefu na mara nyingi Visiwani wakikwama ktk budget siku zote bara huziba upungufu!

Sasa Visiwani wanataka Free port halafu bidhaa zikifika ziuzwe Bara kwa bei ya Chini?? Hii ni halali?? Kumbuka Visiwani soko ni dogo kwani watu ni wachache tofauti na bara!

Pia Waunguja na Wapemba wako huru kufanya shughuli zao na bishara Kariakoo bila bughudha!
 

Kwani sasa hao Wazanzibari wanakuzuieni nini na kuendelea? Naam kweli huwa wanalilia kile kinachopatikana kwa kupitisha bakuli wakati nyie wenyew hakikutosheni. Wapeni uhuru na wao watembeze bakuli kwa upande wao.
 
Ndoto

Wanadhani muungano ukifika wataendelea kumiriki maduka Manzese kuuza na kununua bilashida na kuzurura kwa uhuru mitaa yote down Town.

Ukweli ni kwamba

Muungano haufi ila utaimarishwa, siku yaja ya kusema kila kitu waziwazi ili kuweka mambo sawa sawa.
 
Hoja ingine,

Kuna waalimu zaidi ya 3,000 wa cheti Visiwani hawana kazi..sasa sijui ni kwa nini bara inasita kuwachukua kwani kuna upungufu wa zaidi ya waalimu 10,000!

Tungeanza na hili pengine maana taabu ya Visiwani ni ukosefu wa kazi!!!
 


Kwenye theory zako umesahau jambo moja kubwa," time factor" kwa hivyo ogolea utakavyo lakini bottom line ni kuwa Wazanzbari wanadai haki yao , pengine zile sifa za amani na haki zimeshakutosheni.
 

wawakilishi na Wazanzibari wanaelewa hilo na ndio maana wanazungumzia MAFUTA YA ZANZIBAR si almasi wala tanzaniteya Tanganyika.
 

Azimio hili alipopewa Nahodha hakuambiwa kuwa alipelke Bungeni bali aipeleke Serikali ya Muungano akipitia kwenye kamati yao ya kero za Muungano.
Cha kutia maaanani hapa kama ni suala la Demokrasia ni kuwa tayari Wazanzibari wameshatowa kauli yao na Zanzibar ni sehemu moja ya Muungano. Busara inatakiwa itumike upande wa pili kusawazisha hili.
 

Wasia kama huu ulitakiwa utolewe kila bpale zanzibar inaponyimwa haki zake lakini ukiletwa saa hizi unakosa mtetezi.
 

Kulikuwa na ulazima wa msururu huo wa malipo? Mambo ya Nje faida kubwa na watumishi wengi ni Bara? Ulinzi zanzibbar wanalindwa dhidi ya nani? Umeme tunalipa hata kama tunadeni.
Yes Visiwani hawachangii Waziri Mkuu na mawairi wengine wanazunguka Tanganyika nzima kwa mwalka mzima wakati kule Zanzibar Rais labda aende kwa mwaliko, sasa hayo yote tulipie sisi Zanzibar wakati mambo yetu tunaendesha kwa fedha zetu. Fikira hapo tungetaka kulipa tungewajibika tulipe kiasi gani? Huu si muungano bali ni mkorogano.
Mpaka hapo tutakapojiridhisha kuwa tunalipa kiasi cha haki kulingana na huduma tunazotumia naunga mkono kuwa tusilipe chochote nanyi mna hiari kama mnavyofanya sasa kuweka watu mnaowataka katika vyombo vya Munungano.
 
Watanganyika wanawatawala waZanzibari au Viongozi wa CCM wanawabana waZanzibari au serikali ya TAnzania inaibana Zanzibar.

Mimi nina ndugu kibao baba zao walizamia Zanzibar miaka wao wamezaliwa huko wanaishi Zanzibar kama kwao. Likizo zote wankwenda Zanzibar. Wamejenga wameoa huko.

Kuna Wazanzibar kibao huko Kwiro na Mahenge hawana hata mpango wa kurudi huko Zanzibar.

Nadhani huu ni Ugomvi wa wale watakao kushika Madaraka na siyo wananchi wenyewe.

Wanajua wazi Zanzibar ikiwa nchi atatoka Rais hapo( au sultan pengine) waziri mkuu na waheshimiwa wengine.
Muungano ni kweli una kero nyingi za kuchefua zinazo fumbiwa macho na kuendelea kufunikwa na kuziacha ziendelee kuvunda na utawala wa CCM.

Kingine ni kwamba wale wenye nasaba na Watawala wa Kikoloni wa Zanzibar wamerudi na wana nguvu kuliko mwaka 1964.
Sasa kwa kupitia kwenye migongo ya Wazanzibari wanadai haki yao ya kutawala tena Zanzibar.
Si unajua tena Mkoloni yeyote heshi kuendelea kunyemelea koloni lake la zamani.

Huenda hizi ni hila za Fisi wa KiOman na sharubu zake.

Bisha?
 

Hakuna cha mbichi wala mbivu, bora hata hizo mbivu zingekuwepo basi, sioni cha kupoteza kwa kuachana na wazenji, after all simnataka kujitenga? kwa hiyo tumeamua piga debe muachiwe nchi yenu kwa hiyo mtusaidie tunao wasupport mjitenge. Inaonekana hasara za muungano zina overide faida zake sasa kuna haja gani ya kuung'ang'ania? Wazenji wa asili ya ubaguzi na siku zote wanakawaida ya kubagua wabara hata katika jamii, sasa huo ufa unazibika na nini na kitu kipo kwenye damu yao? Inawezekana maendeleo duni ya zenji yamesabishwa na leadership ya SMZ lakini wakaamua kutumia tatizo la muungano kama bangusilo...kwa hiyo waacheni nao wajaribu kivyao....Case ya mafuta kama wanayo au hawana is also non of our business, let mainlanders focus on their main problem.....Pia nawashangaa sana wapemba wanao invest kwa nguvu Dar au bara badala ya pemba, wakati huohuo kuna kelele za kuvunja muungano, wabara wamebadirika jamani siyo wale wa zidumu fikra za mwenye cheo....
 

Tutajie kina nani hao?
 


Umesha wahi kusikia Hadithi moja wapo Za mtu aliyekuwa anaitwa firauni?alifika kuwambia watu wake kuwa yeye ndio Mungu wao wakawa wanamtii na kumuogopa sana, lakini chakushangaza ulipofika wakati wake Mungu firauni akafariki .sasa jiulize jee kuna waungu wangapi kama kina firauni ? mwisho ningekushauri soma hadithi za aliyekuwa kiongozi wa Germany Adolf Hitler .happy easter
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, ameungana na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka suala la mafuta liondolewe kwenye muungano ........,Maalim Seif alisema, suala hilo bado lina utata unaohitaji mjadala wa juu zaidi kwa sababu hatima yake inaweza kuwa mbaya zaidi kitaifa.

Naye Dk Salim Ahmed Salim, alisema mgogoro wa mafuta ya Zanzibar unazungumzika hivyo ni vyema viongozi wa pande zote mbili za muungano wakatoa nafasi ya kulitafakari suala hilo ili lisilete madhara kwa Watanzania.
“Hii ni rasilimali ya Watanzania. Nadhani hakuna jambo lisilozungumzika, hivyo ni vyema pande hizi mbili, zikakaa pamoja kuondoa tatizo,” alisema Dk Salim.

Professa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema Zanzibar inajitafutia laana kwa kujiingiza katika mgogoro wa mafuta.

Aliliambia gazeti hili kuwa jinamizi la rasilimali hiyo, linaweza kuitafuna kabisa Zanzibar kwani haiwezi kujiendesha yenyewe katika suala la mafuta kutokana na kuwa na nguvu ndogo ya kidola.
_________________________________________

Angalia Seifu amesema watu wajadiliane ,na Salim nae amesema hivyo hivyo na Lipumba pia amesema yafanywe majadiliano.

Sasa huyu Profesa Baregu ,hivi hana uelewa kuwa Zanzibar Kimataifa imo ndani ya Tanzania na mhusika wa nguvu za dola ni Tanzania nzima ,Profesa anashindwa kufahamu kuwa Serikali ya Muungano ndio inahusika na ulinzi wa Zanzibar na Tanganyika sasa anaposema Zanzibar ina nguvu kidogo kidola ana maana gani ? Muungano haupo ? Ni Muungano hewa ? au vipi waandhi kama mpo hapa JF hebu muulizeni huyo Mheshimiwa Professor Baregu atufafanulie huo usemi wake ?

Nakubalina nae kwamba inawezekana kabisa kwa majambazi ya kimataifa kutaka kutumia nguvu kuyapata mafuta haya (kama yapo anyway) kwa kuwatumia baadhi ya waliomo ndani ya Serikali kuu aka MAFISADI, lakini pia hujui kwamba ni wajibu wa vyombo vya ulinzi vya dola (Muungano) kuilinda Zanzibar kama ni sehemu ya Tanzania?, vyenginevyo kuna haja gani ya Muungano? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya wanasiasa mafisadi washapiga hesabu za namna ya kujinufaisha kibinafsi na mapato ya mafuta, lakini hili tunaweza kulishughulikia kama nyinyi mnavyoshughulikia raslimali zenu za maliasili na nyenginezo, tena bila ya "kukolimbana".
 
Mwiba,

Wewe unadhani Prof. Baregu ni mganga njaa?? Kwa nini??

Hii habari imetoka ktk magazeti..na magazeti ya tz not so analytical na sina uhakika kama ndo alichooongea Baregu!

Hebu fafanua maana saa ingine lugha yako humu JF huwa huelewaki!
 
Mwiba,

Si ulisema mnataka kujitenga? Mnasema kuwa tunawatawala. Inawezekana Prof. alichukulia maneno yanu ya kutaka kujitawala/kutoka kwenye Muungano maana sasa mna mafuta ya kujipaka. Naona hili ndilo aliloliongelea kuwa mkijitenga na muanze kuchimba mafuta basi mmejiingiza kwenye laana wenyewe. Hili wengi mmeambiwa kwa muda mrefu kuanzia maneno ya JKN ya laana ya kutengana kuwa ni sawa na kula nyama ya mtu na hadi juzi mie, Pasco na wengine mmeambiwa hilo. Ila wenzetu mnajifanya kuwa mko very strong katika ulinzi. Haya, siku ikifika twaja wachukua wamasaai wetu na Wakurya wetu na nyie muanze kazi ya ulinzi.

By the way, Mwiba nadikia wauza magari, ni kweli Mnyamwezi wangu? Heri nijue ili nikihitaji moja huku kwetu Sikonge basi nije ninunue kwako maana zimwi likujualo....
 

KUNA LAANA KWA WAZANZIBARI ZAIDI YA LAANA YA KUKOSA KUJITAWALA? Baada ya laana hii tulionayo tuko tayari kwa laana hiyo ya kujiamulia juu ya mafuta. Simlaumu sana Baregu kwani niliwahi kusoma pahala kuwa ili uwe profesa lazima uilimit akili yako kwenye jambo fulani na pengine ndio yanayomsibu huyu Profesa wetu.
 



Usiniambie mimi, mwambie Mwiba anayesema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Sasa kama mko kwenye Muungano, nani anakutawala? Mnatawaliwa au mko kwenye Muungano? Hebu wewe na Mwiba mkae hapa mtuambie. Mwiba, huo usalama unaoutaka utoke kwenye Muungano, unamaanisha utatoka kwa mkoloni wenu au JWTZ ambalo hata nyinyi mpo? Maji yamezidi unga......
 
Kila muomba ngoma huvutia kwake hivyo ndivyo alivyofanya Baregu,lakini pia inawezekana profesa Beregu He is in medication .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…