Hili halina ubishi, hata muungano wenyewe una matatizo toka kwenye fundamental pillars zake. Prof. Issa Shivji aliuchambua Muungano na kuuvua nguo katika andiko lake la 'The Legal Basis of Union Between Tanganyika and Zanzibar'. Andiko hili alilitoa mwaka 2004 wakati wa miaka 40 ya Muungano. Andiko hili linapatikana Maktaba Kuu ya UDSM, sehemu ya Sheria
Profesa alizungumzia udhaifu wa Muungano kisheria jinsi ulivyokiuka sheria tangu mwanzo kwa Watanganyika wote kuburuzwa na Bunge la chama cha Tanu na Wanzanzibari wote kuburutwa na Baraza la Wawakilishi la ASP vyombo ambavyo havikuwa na mamlaka. Muungano halali ulitakiwa kuundwa kwa white paper, halafu kuundwa kwa constituent assembly na sio vyama. Badala yake ni Bunge na Baraza la Wawakilishi yalijigeuza Constituent Assembly na kuupitisha Muungano kwa papara. Kilichofuatia ni kuongeza vipengele kwa vipengele kwa njia za kibabe bila kuvipitisha Baraza la Wawakilishi kuridhia.
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado aliyagundua mapungufu hayo ya Muungano
Akakuta Katiba imeweka ribit hakuna namna yoyote, wala mahakama yoyote nchini yenye mamlaka ya kusikiliza shauri lolote la malalamiko ya Muungano. Katika inatamka ni lazima uindwe mahakama ya katiba.
Taratibu za kuundwa mahakama hiyo ni mlolongo mwingine na rais wa Muungano bara ndiye aliyeshika mpini.
Dourado akamshauri Jumbe wakaishitaki Tanzania kwenye UN. Wakatayarisha makaratasi wakajipanga vizuri tuu, wakati huo jamaa wa UT wanaripoti kila kitu kwa Nyerere. Wakati muafaka uliwadia, Jumbe akaitwa Dodoma kwenye CC na NEC, akapata kibano cha nguvu. Dourado akaozea kiziuzini, Jumbe nae kizuizi cha nyumbani. Taifa likatangaziwa kuchafuka kwa hali ya hewa ya siasa za Zanzibar zilizopolekea mabadiliko ya uongozi Zanzibar.
Hizi kelele za Baraza na Nahodha wanauchokoa tena Muungano. Mohamed Seif Khatib ni mkongwe na anaelewa somo, Nahodha ni kinda la juzi tuu, subirini walete azimio hilo muone jinsi watu watakavyopigwa dafrao. Hata Dr. Salmin alitaka kulea chokochoko, alichokipata wapambe wake akina Twahir Ali wanajua kilichowapata na vimbelembele wao kina Castico.
Siasa za Zanzibar ni ngumu, zina shari, jazba, chuki, vijembe, chuki, husda, kibri na kila aina ya ubabe, dawa ikawa ni ubabe tuu na ndicho kitachofuatia katika hili suala la mafuta-alinacha.