Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
UPO LAKINI HUSIKI WALA HUONI. Zanzibar wamejenga hoja ya kuthibitisha kuwa rasilimali za Bara haziifaidii zanzibar.Pia serikali yako imekwishasema wazi kuwa madini si suala la Muungano ni mali ya Tanganyika ,sasa kama akili yake haina uwezo wa kutia akilini hayo basi itakuwa tatizo.

Gozigumu,

Bara hulipia ulinzi, usalama, mambo ya nje, elimu ya juu, Bunge, n.k na 4.5% ya pesa ya missaada yote! Pia ukiangalia idadi ya watu kati ya bara na visiwani % ya missada ingebidi iwe ni 2.5% ila Visiwani hupata mara 2!

Gesi ya Songosongo kutumiwa na TANESCO na umeme huu unatumika Unguja na Pemba utafika Mwaka huu!

Je Serikali ya bara ilipe cash SMZ pesa inayotokana na dhahabu au almasi?

Jua pia Visiwani huwa hawachangii ktk serikali kuu kwa mda mrefu na mara nyingi Visiwani wakikwama ktk budget siku zote bara huziba upungufu!

Sasa Visiwani wanataka Free port halafu bidhaa zikifika ziuzwe Bara kwa bei ya Chini?? Hii ni halali?? Kumbuka Visiwani soko ni dogo kwani watu ni wachache tofauti na bara!

Pia Waunguja na Wapemba wako huru kufanya shughuli zao na bishara Kariakoo bila bughudha!
 
Hi ninyi, wazenji wamewapa nini mnawanganinia siku zote wee? Zenji ni zigo jamani, masikini Nyerere (RIP) akaacha watu kama wamalawi, wanyaruanda au waburundi ambao niwachap kazi, wanapiga shule fresh akaenda tafuta wapiga maneno matatizo ya ndo za mkeka ndiyo hayo. Waacheni waende zao tutajipange upya, kama zenji itageuka Somalia hilo halituhusu sisi, mombasa ni karibu watakimbilia...Tanganyika shule ipo tukiitumia vyema tunaweza kuwa kama South Korea au hata Japan, kwani Japan wanategemea mafuta? Dhahabu tunachimba, Almas tunachimba, Gas tunachimba, Tanzanite tunachimba, mafuta tulichimba japo mapipa 90, sasa ya nini kungania plots ambazo not even confirmed kama kuna hayo mafuta....eti muungano wetu ni mfano wa kuigwa dunia, we took the wrong people or side of the world. Zenj haina natural resources, it's a weak market so huwezi uza kitu kule, hakuna uzarishaji, hakuna ajira bali wamechukua ajira, tunagawa umeme wakati wenyewe tunauhitaji..Bora ulee kilema au yatima mungu atakukumbuka lakini siyo Zenj, please please, leave them alone we dont need them anyway . Rais bora ni yule atakaye ahidi kuungalia upya muungano...jumba lina nyufa kibao unaishia kuzibaziba, si ubomoe tu ujenge mpya mpaka likudondokee?

Kwani sasa hao Wazanzibari wanakuzuieni nini na kuendelea? Naam kweli huwa wanalilia kile kinachopatikana kwa kupitisha bakuli wakati nyie wenyew hakikutosheni. Wapeni uhuru na wao watembeze bakuli kwa upande wao.
 
Ndoto

Wanadhani muungano ukifika wataendelea kumiriki maduka Manzese kuuza na kununua bilashida na kuzurura kwa uhuru mitaa yote down Town.

Ukweli ni kwamba

Muungano haufi ila utaimarishwa, siku yaja ya kusema kila kitu waziwazi ili kuweka mambo sawa sawa.
 
Hoja ingine,

Kuna waalimu zaidi ya 3,000 wa cheti Visiwani hawana kazi..sasa sijui ni kwa nini bara inasita kuwachukua kwani kuna upungufu wa zaidi ya waalimu 10,000!

Tungeanza na hili pengine maana taabu ya Visiwani ni ukosefu wa kazi!!!
 
Hili halina ubishi, hata muungano wenyewe una matatizo toka kwenye fundamental pillars zake. Prof. Issa Shivji aliuchambua Muungano na kuuvua nguo katika andiko lake la 'The Legal Basis of Union Between Tanganyika and Zanzibar'. Andiko hili alilitoa mwaka 2004 wakati wa miaka 40 ya Muungano. Andiko hili linapatikana Maktaba Kuu ya UDSM, sehemu ya Sheria

Profesa alizungumzia udhaifu wa Muungano kisheria jinsi ulivyokiuka sheria tangu mwanzo kwa Watanganyika wote kuburuzwa na Bunge la chama cha Tanu na Wanzanzibari wote kuburutwa na Baraza la Wawakilishi la ASP vyombo ambavyo havikuwa na mamlaka. Muungano halali ulitakiwa kuundwa kwa white paper, halafu kuundwa kwa constituent assembly na sio vyama. Badala yake ni Bunge na Baraza la Wawakilishi yalijigeuza Constituent Assembly na kuupitisha Muungano kwa papara. Kilichofuatia ni kuongeza vipengele kwa vipengele kwa njia za kibabe bila kuvipitisha Baraza la Wawakilishi kuridhia.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado aliyagundua mapungufu hayo ya Muungano
Akakuta Katiba imeweka ribit hakuna namna yoyote, wala mahakama yoyote nchini yenye mamlaka ya kusikiliza shauri lolote la malalamiko ya Muungano. Katika inatamka ni lazima uindwe mahakama ya katiba.
Taratibu za kuundwa mahakama hiyo ni mlolongo mwingine na rais wa Muungano bara ndiye aliyeshika mpini.

Dourado akamshauri Jumbe wakaishitaki Tanzania kwenye UN. Wakatayarisha makaratasi wakajipanga vizuri tuu, wakati huo jamaa wa UT wanaripoti kila kitu kwa Nyerere. Wakati muafaka uliwadia, Jumbe akaitwa Dodoma kwenye CC na NEC, akapata kibano cha nguvu. Dourado akaozea kiziuzini, Jumbe nae kizuizi cha nyumbani. Taifa likatangaziwa kuchafuka kwa hali ya hewa ya siasa za Zanzibar zilizopolekea mabadiliko ya uongozi Zanzibar.

Hizi kelele za Baraza na Nahodha wanauchokoa tena Muungano. Mohamed Seif Khatib ni mkongwe na anaelewa somo, Nahodha ni kinda la juzi tuu, subirini walete azimio hilo muone jinsi watu watakavyopigwa dafrao. Hata Dr. Salmin alitaka kulea chokochoko, alichokipata wapambe wake akina Twahir Ali wanajua kilichowapata na vimbelembele wao kina Castico.

Siasa za Zanzibar ni ngumu, zina shari, jazba, chuki, vijembe, chuki, husda, kibri na kila aina ya ubabe, dawa ikawa ni ubabe tuu na ndicho kitachofuatia katika hili suala la mafuta-alinacha.

Kwenye theory zako umesahau jambo moja kubwa," time factor" kwa hivyo ogolea utakavyo lakini bottom line ni kuwa Wazanzbari wanadai haki yao , pengine zile sifa za amani na haki zimeshakutosheni.
 
Baraza la wawakilishi ni sawa na braza la madiwani...jambo likianzia huko mwisho wake bungeni....ati mambo yaliyoamuliwa bungeni mpaka yakubaliwe baraza la wawakilishi!? ebooo!Wale wanatakiwa kutunga sheria za zanzibar kufutatana na katiba ya zanzibar.....ni sawa na bylaws tu. Bunge la Muungano ndiko kunakomalizikia kila kitu.....hata hao wawakilishi wabwateje.
Kama kweli ndugu zetu chokochoko za kuvunja muungano ni kwa sababu ya mafuta....basi vichwa vyao lazima vinawalakini. Hakuna duniani popote kunakuwa-declared uwepo wa mafuta bila ya kuyachimba na ku-flow hayo mafuta...tena ku-evaluate kama kuna comercial quantity.

Yakhee..mafuta yapo atii....wanakula urojo barazani.......Shit!

wawakilishi na Wazanzibari wanaelewa hilo na ndio maana wanazungumzia MAFUTA YA ZANZIBAR si almasi wala tanzaniteya Tanganyika.
 
Asalamu alaykum.

habari za siku nyingi takriban mwezi wa tatu huu sipo mtandaoni kutokana na tatizo nililokuwa likinikabili ambalo nilifanyiwa upasuaji wa mguu hata hivyo nashukuru kwa wale wote ambao wamenifariji kwa njia moja au nyengine kwa kunitakia dua za kheri na sasa nimepona bila ya shaka tupo pamoja katika majadiliano.

Naomba nichangia hii mada ila kwa hakika kilichoandikwa juu kabisa kwamba baraza la wawakilishi hatimae limepitisha mswaada wa suala la mafuta sio sahihi. ama ni kweli wajumbe wa CCM na CUF kwa umoja wao wamependekeza baadhi ya mambo lakini sio mswada ni kuishauri serikali

Kwani hakuna mswaada uliopitishwa kilichokuwa kikijadiliwa katika kikao cha baraza la wawakilishi kwa takriban wiki mbili sasa sio mswaada ni taarifa ya serikali kuhusiana na mapendekezo ya mshauri mwelekezi david reading kutoka uingereza ambayo alipewa kazi ya kuzishauri serikali zote mbili juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na namna ya ugawaji.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi walijadili na mwisho kutoka na maazimio ya baraza na kuishauri serikali ya mapinduzi zanzibar kama ifuatavyo.

Wiki iliyopita, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliwasilisha taarifa katika Baraza ikitaka maoni ya Wawakilishi kuliondoa au kulibakisha suala la mafuta na gesi asilia kwenye mambo ya Muungano.

Mapendekezo mengine ya SMZ ni kuwa, Ardhi na bahari ya ndani ya Zanzibar, maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibat sura ya kwanza 2(1) ni milki ya Zanzibar, katika maeneo hayo usimamizi, udhibiti na uendeshaji wa shughuli zote za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia uwe wa Zanzibar pekee.

Pendekezo la pili ni kuwa , sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo chake cha kusimamia mambo yote yanayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na mengineyo yanayoendana na hayo , chombo hicho kitakuwa sawa na lile Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC).

pendekezo la mwisho kuwa kwa upande wa bahari kuu(EEZ), Serikali inashauri kukubali mashirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa eneo hilo pekee kwa makubaliano maalum na sio muundo wa sasa wa Taasisi na sheria kwamba Zanzibar itakuwa ni mshiriki sawa.

kwa maana hiyo mswada bado hajawasilishwa katika kikao kwanza hadi bunge lijadili na kufikia mwafaka wa suala hili.

Azimio hili alipopewa Nahodha hakuambiwa kuwa alipelke Bungeni bali aipeleke Serikali ya Muungano akipitia kwenye kamati yao ya kero za Muungano.
Cha kutia maaanani hapa kama ni suala la Demokrasia ni kuwa tayari Wazanzibari wameshatowa kauli yao na Zanzibar ni sehemu moja ya Muungano. Busara inatakiwa itumike upande wa pili kusawazisha hili.
 
Wadau naona the way tunavyochangia tunakwenda Nje ya mstari...as if yanayotokea DUNIANI kote hatuyajui au hatuyafuatiliii.....

Bahati Mbaya mtu kama Mwiba unaonekana ni Mtetezi wa CUF, lkn kwa upande mwingine unaharibu image ya CUF kwa Jamii. i do believe members humu JF watamchukilia Mwiba kama mtu binafsi na si MSIMAMO WA CUF.

Unaleta Hoja makini lete hoja, usilete Hoja za Ubaguzi ohh wabara hivi...au Wazenj hivi....?Tunakwenda Wapi? Nini kitatokea leo ikiwa ZNZ ikiwa ALONE, then wapemba na Waunguja nao wagawane Kisiwa...?..wabara nao kila mtu na Mkoa wake...!!!!

Hivi Jamani hatuoni kwanini USA imekuwa powerful country?...Kwanini leo nchi za Ulaya zimekuja na kutengeneza EURO?....waarabu wana GULF nayo ni just nchi 7 tu...

I do believe Muungano una positive na Negative...Muhimu kuangalia mapungufu yaliyopo na kuangalia namna ya kusawazisha Tofauti Iliyopo. Viongozi wa Muungano nao wanataka kuongoza Kibabe ktk wakati watu wanasaka maendeleo....Tukae chini tujadili Muungano uweje...Tunaohubiri Ubara au Uzenji haumsaidii yoyote bali sote tunaonekana majuha.....!!!!

I do believe JK is the right person kuondoa matatizo ya Muungano, Mkutano wa Butiama kuna Genge la watu wamemsaliti.......kama si kusalitiwa kule...Leo hii tungekuwa tumefungua page Mpya kabisa ktk huu Muungano.....Tuna matatizo ya Husda.....kama JK angefanikiwa BUTIAMA...credits zingeenda kwake......hata Miradi Mingi ukiichunguza inafeli si tu kuwa Watendaji hakupewa chochote...lkn wanajua credits za kufanikisha huyo Mtendaji atakuwa Hayumo au Hatajwi............I do hope in the 2nd term atalimaliza hili.......Inshallah.

Wasia kama huu ulitakiwa utolewe kila bpale zanzibar inaponyimwa haki zake lakini ukiletwa saa hizi unakosa mtetezi.
 
Gozigumu,

Bara hulipia ulinzi, usalama, mambo ya nje, elimu ya juu, Bunge, n.k na 4.5% ya pesa ya missaada yote! Pia ukiangalia idadi ya watu kati ya bara na visiwani % ya missada ingebidi iwe ni 2.5% ila Visiwani hupata mara 2!

Gesi ya Songosongo kutumiwa na TANESCO na umeme huu unatumika Unguja na Pemba utafika Mwaka huu!

Je Serikali ya bara ilipe cash SMZ pesa inayotokana na dhahabu au almasi?

Jua pia Visiwani huwa hawachangii ktk serikali kuu kwa mda mrefu na mara nyingi Visiwani wakikwama ktk budget siku zote bara huziba upungufu!

Sasa Visiwani wanataka Free port halafu bidhaa zikifika ziuzwe Bara kwa bei ya Chini?? Hii ni halali?? Kumbuka Visiwani soko ni dogo kwani watu ni wachache tofauti na bara!

Pia Waunguja na Wapemba wako huru kufanya shughuli zao na bishara Kariakoo bila bughudha!

Kulikuwa na ulazima wa msururu huo wa malipo? Mambo ya Nje faida kubwa na watumishi wengi ni Bara? Ulinzi zanzibbar wanalindwa dhidi ya nani? Umeme tunalipa hata kama tunadeni.
Yes Visiwani hawachangii Waziri Mkuu na mawairi wengine wanazunguka Tanganyika nzima kwa mwalka mzima wakati kule Zanzibar Rais labda aende kwa mwaliko, sasa hayo yote tulipie sisi Zanzibar wakati mambo yetu tunaendesha kwa fedha zetu. Fikira hapo tungetaka kulipa tungewajibika tulipe kiasi gani? Huu si muungano bali ni mkorogano.
Mpaka hapo tutakapojiridhisha kuwa tunalipa kiasi cha haki kulingana na huduma tunazotumia naunga mkono kuwa tusilipe chochote nanyi mna hiari kama mnavyofanya sasa kuweka watu mnaowataka katika vyombo vya Munungano.
 
Watanganyika wanawatawala waZanzibari au Viongozi wa CCM wanawabana waZanzibari au serikali ya TAnzania inaibana Zanzibar.

Mimi nina ndugu kibao baba zao walizamia Zanzibar miaka wao wamezaliwa huko wanaishi Zanzibar kama kwao. Likizo zote wankwenda Zanzibar. Wamejenga wameoa huko.

Kuna Wazanzibar kibao huko Kwiro na Mahenge hawana hata mpango wa kurudi huko Zanzibar.

Nadhani huu ni Ugomvi wa wale watakao kushika Madaraka na siyo wananchi wenyewe.

Wanajua wazi Zanzibar ikiwa nchi atatoka Rais hapo( au sultan pengine) waziri mkuu na waheshimiwa wengine.
Muungano ni kweli una kero nyingi za kuchefua zinazo fumbiwa macho na kuendelea kufunikwa na kuziacha ziendelee kuvunda na utawala wa CCM.

Kingine ni kwamba wale wenye nasaba na Watawala wa Kikoloni wa Zanzibar wamerudi na wana nguvu kuliko mwaka 1964.
Sasa kwa kupitia kwenye migongo ya Wazanzibari wanadai haki yao ya kutawala tena Zanzibar.
Si unajua tena Mkoloni yeyote heshi kuendelea kunyemelea koloni lake la zamani.

Huenda hizi ni hila za Fisi wa KiOman na sharubu zake.

Bisha?
 
Sungura alipo zikosa zabibu alitowa maneno kama yako zabibu gani mbichi mbovu haziliki sababu tu amezikosa sasa any way shukurani zangu za zati nazipeleka kwa wabunge mashuhuri waliochagulia kwa imani ya wananchi nitawataja wachache hapa lowasa ,rostam,marehemu Bilal ,chenge (visent) etc wewe mtowa maoni endelea hivyo hivyo by the way usije ukajisahau sana

Hakuna cha mbichi wala mbivu, bora hata hizo mbivu zingekuwepo basi, sioni cha kupoteza kwa kuachana na wazenji, after all simnataka kujitenga? kwa hiyo tumeamua piga debe muachiwe nchi yenu kwa hiyo mtusaidie tunao wasupport mjitenge. Inaonekana hasara za muungano zina overide faida zake sasa kuna haja gani ya kuung'ang'ania? Wazenji wa asili ya ubaguzi na siku zote wanakawaida ya kubagua wabara hata katika jamii, sasa huo ufa unazibika na nini na kitu kipo kwenye damu yao? Inawezekana maendeleo duni ya zenji yamesabishwa na leadership ya SMZ lakini wakaamua kutumia tatizo la muungano kama bangusilo...kwa hiyo waacheni nao wajaribu kivyao....Case ya mafuta kama wanayo au hawana is also non of our business, let mainlanders focus on their main problem.....Pia nawashangaa sana wapemba wanao invest kwa nguvu Dar au bara badala ya pemba, wakati huohuo kuna kelele za kuvunja muungano, wabara wamebadirika jamani siyo wale wa zidumu fikra za mwenye cheo....
 
Watanganyika wanawatawala waZanzibari au Viongozi wa CCM wanawabana waZanzibari au serikali ya TAnzania inaibana Zanzibar.

Mimi nina ndugu kibao baba zao walizamia Zanzibar miaka wao wamezaliwa huko wanaishi Zanzibar kama kwao. Likizo zote wankwenda Zanzibar. Wamejenga wameoa huko.

Kuna Wazanzibar kibao huko Kwiro na Mahenge hawana hata mpango wa kurudi huko Zanzibar.

Nadhani huu ni Ugomvi wa wale watakao kushika Madaraka na siyo wananchi wenyewe.

Wanajua wazi Zanzibar ikiwa nchi atatoka Rais hapo( au sultan pengine) waziri mkuu na waheshimiwa wengine.
Muungano ni kweli una kero nyingi za kuchefua zinazo fumbiwa macho na kuendelea kufunikwa na kuziacha ziendelee kuvunda na utawala wa CCM.

Kingine ni kwamba wale wenye nasaba na Watawala wa Kikoloni wa Zanzibar wamerudi na wana nguvu kuliko mwaka 1964.Sasa kwa kupitia kwenye migongo ya Wazanzibari wanadai haki yao ya kutawala tena Zanzibar.
Si unajua tena Mkoloni yeyote heshi kuendelea kunyemelea koloni lake la zamani.

Huenda hizi ni hila za Fisi wa KiOman na sharubu zake.

Bisha?

Tutajie kina nani hao?
 
Ndoto

Wanadhani muungano ukifika wataendelea kumiriki maduka Manzese kuuza na kununua bilashida na kuzurura kwa uhuru mitaa yote down Town.

Ukweli ni kwamba

Muungano haufi ila utaimarishwa, siku yaja ya kusema kila kitu waziwazi ili kuweka mambo sawa sawa.

Umesha wahi kusikia Hadithi moja wapo Za mtu aliyekuwa anaitwa firauni?alifika kuwambia watu wake kuwa yeye ndio Mungu wao wakawa wanamtii na kumuogopa sana, lakini chakushangaza ulipofika wakati wake Mungu firauni akafariki .sasa jiulize jee kuna waungu wangapi kama kina firauni ? mwisho ningekushauri soma hadithi za aliyekuwa kiongozi wa Germany Adolf Hitler .happy easter
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, ameungana na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka suala la mafuta liondolewe kwenye muungano ........,Maalim Seif alisema, suala hilo bado lina utata unaohitaji mjadala wa juu zaidi kwa sababu hatima yake inaweza kuwa mbaya zaidi kitaifa.

Naye Dk Salim Ahmed Salim, alisema mgogoro wa mafuta ya Zanzibar unazungumzika hivyo ni vyema viongozi wa pande zote mbili za muungano wakatoa nafasi ya kulitafakari suala hilo ili lisilete madhara kwa Watanzania.
“Hii ni rasilimali ya Watanzania. Nadhani hakuna jambo lisilozungumzika, hivyo ni vyema pande hizi mbili, zikakaa pamoja kuondoa tatizo,” alisema Dk Salim.

Professa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema Zanzibar inajitafutia laana kwa kujiingiza katika mgogoro wa mafuta.

Aliliambia gazeti hili kuwa jinamizi la rasilimali hiyo, linaweza kuitafuna kabisa Zanzibar kwani haiwezi kujiendesha yenyewe katika suala la mafuta kutokana na kuwa na nguvu ndogo ya kidola.
_________________________________________

Angalia Seifu amesema watu wajadiliane ,na Salim nae amesema hivyo hivyo na Lipumba pia amesema yafanywe majadiliano.

Sasa huyu Profesa Baregu ,hivi hana uelewa kuwa Zanzibar Kimataifa imo ndani ya Tanzania na mhusika wa nguvu za dola ni Tanzania nzima ,Profesa anashindwa kufahamu kuwa Serikali ya Muungano ndio inahusika na ulinzi wa Zanzibar na Tanganyika sasa anaposema Zanzibar ina nguvu kidogo kidola ana maana gani ? Muungano haupo ? Ni Muungano hewa ? au vipi waandhi kama mpo hapa JF hebu muulizeni huyo Mheshimiwa Professor Baregu atufafanulie huo usemi wake ?

Nakubalina nae kwamba inawezekana kabisa kwa majambazi ya kimataifa kutaka kutumia nguvu kuyapata mafuta haya (kama yapo anyway) kwa kuwatumia baadhi ya waliomo ndani ya Serikali kuu aka MAFISADI, lakini pia hujui kwamba ni wajibu wa vyombo vya ulinzi vya dola (Muungano) kuilinda Zanzibar kama ni sehemu ya Tanzania?, vyenginevyo kuna haja gani ya Muungano? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya wanasiasa mafisadi washapiga hesabu za namna ya kujinufaisha kibinafsi na mapato ya mafuta, lakini hili tunaweza kulishughulikia kama nyinyi mnavyoshughulikia raslimali zenu za maliasili na nyenginezo, tena bila ya "kukolimbana".
 
Mwiba,

Wewe unadhani Prof. Baregu ni mganga njaa?? Kwa nini??

Hii habari imetoka ktk magazeti..na magazeti ya tz not so analytical na sina uhakika kama ndo alichooongea Baregu!

Hebu fafanua maana saa ingine lugha yako humu JF huwa huelewaki!
 
Mwiba,

Si ulisema mnataka kujitenga? Mnasema kuwa tunawatawala. Inawezekana Prof. alichukulia maneno yanu ya kutaka kujitawala/kutoka kwenye Muungano maana sasa mna mafuta ya kujipaka. Naona hili ndilo aliloliongelea kuwa mkijitenga na muanze kuchimba mafuta basi mmejiingiza kwenye laana wenyewe. Hili wengi mmeambiwa kwa muda mrefu kuanzia maneno ya JKN ya laana ya kutengana kuwa ni sawa na kula nyama ya mtu na hadi juzi mie, Pasco na wengine mmeambiwa hilo. Ila wenzetu mnajifanya kuwa mko very strong katika ulinzi. Haya, siku ikifika twaja wachukua wamasaai wetu na Wakurya wetu na nyie muanze kazi ya ulinzi.

By the way, Mwiba nadikia wauza magari, ni kweli Mnyamwezi wangu? Heri nijue ili nikihitaji moja huku kwetu Sikonge basi nije ninunue kwako maana zimwi likujualo....
 
KUNA LAANA KWA WAZANZIBARI ZAIDI YA LAANA YA KUKOSA KUJITAWALA? Baada ya laana hii tulionayo tuko tayari kwa laana hiyo ya kujiamulia juu ya mafuta. Simlaumu sana Baregu kwani niliwahi kusoma pahala kuwa ili uwe profesa lazima uilimit akili yako kwenye jambo fulani na pengine ndio yanayomsibu huyu Profesa wetu.
 
Professa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema Zanzibar inajitafutia laana kwa kujiingiza katika mgogoro wa mafuta.

Aliliambia gazeti hili kuwa jinamizi la rasilimali hiyo, linaweza kuitafuna kabisa Zanzibar kwani haiwezi kujiendesha yenyewe katika suala la mafuta kutokana na kuwa na nguvu ndogo ya kidola.
_________________________________________

Sasa huyu Profesa Baregu ,hivi hana uelewa kuwa Zanzibar Kimataifa imo ndani ya Tanzania na mhusika wa nguvu za dola ni Tanzania nzima ,Profesa anashindwa kufahamu kuwa Serikali ya Muungano ndio inahusika na ulinzi wa Zanzibar na Tanganyika sasa anaposema Zanzibar ina nguvu kidogo kidola ana maana gani ? Muungano haupo ? Ni Muungano hewa ? au vipi waandhi kama mpo hapa JF hebu muulizeni huyo Mheshimiwa Professor Baregu atufafanulie huo usemi wake ?

Nakubalina nae kwamba inawezekana kabisa kwa majambazi ya kimataifa kutaka kutumia nguvu kuyapata mafuta haya (kama yapo anyway) kwa kuwatumia baadhi ya waliomo ndani ya Serikali kuu aka MAFISADI, lakini pia hujui kwamba ni wajibu wa vyombo vya ulinzi vya dola (Muungano) kuilinda Zanzibar kama ni sehemu ya Tanzania?, vyenginevyo kuna haja gani ya Muungano? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya wanasiasa mafisadi washapiga hesabu za namna ya kujinufaisha kibinafsi na mapato ya mafuta, lakini hili tunaweza kulishughulikia kama nyinyi mnavyoshughulikia raslimali zenu za maliasili na nyenginezo, tena bila ya "kukolimbana".

KUNA LAANA KWA WAZANZIBARI ZAIDI YA LAANA YA KUKOSA KUJITAWALA? Baada ya laana hii tulionayo tuko tayari kwa laana hiyo ya kujiamulia juu ya mafuta. Simlaumu sana Baregu kwani niliwahi kusoma pahala kuwa ili uwe profesa lazima uilimit akili yako kwenye jambo fulani na pengine ndio yanayomsibu huyu Profesa wetu.

Usiniambie mimi, mwambie Mwiba anayesema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Sasa kama mko kwenye Muungano, nani anakutawala? Mnatawaliwa au mko kwenye Muungano? Hebu wewe na Mwiba mkae hapa mtuambie. Mwiba, huo usalama unaoutaka utoke kwenye Muungano, unamaanisha utatoka kwa mkoloni wenu au JWTZ ambalo hata nyinyi mpo? Maji yamezidi unga......
 
Kila muomba ngoma huvutia kwake hivyo ndivyo alivyofanya Baregu,lakini pia inawezekana profesa Beregu He is in medication .
 
Back
Top Bottom