Mambo haya ya mafuta na matumizi yake n.k yananifanya nikumbuke kisa kimoja cha hekaya za mtu aitwaye Alinacha... kisa hiko watu wengi wanakifahamu kama "ndoto za Alinacha"..
 
..hakuna suala la kujadiliana hapo. Zanzibar wachimbe mafuta yaliyoko ktk eneo lao.

..ifahamike kwamba kuna eneo la bahari kati ya Zanzibar na Tanganyika ambalo tuna-share, kwa maana kwamba haliwezi kuwa defined ni eneo la upande mmoja wa Muungano kwa kuzingatia sheria za kimataifa za bahari.

..utafiti na uchimbaji mafuta ktk eneo la bahari nililolielezea hapo juu ndiyo uwe suala la Muungano.
 
Mimi ndio maana sometimes natamani mafuta yasipatikane Tanzania....hii nishati ni kama laana.....
 
Umenikumbusha kitu ambacho naomba wasomi watusaidie hapa. Kuna ile sheria ya Bahari ambayo ina upendeleo maalum kwa Visiwa. Ukizingatia sheria ile Tanganyika eneo lake la bahari ni Kilomita chache tu ambazo inaweza kufanya bandari na kuvuwa vibua tu, lakini ile exlusive economic zone (katika bahari kuu) imechukuliwa na visiwa vya Zanzibar. Sasa ukiondoa mpaka huo (Yaani ukivunja Tanzania) na kurejesha mpaka wa baharini wa Zanzibar na Tanganyika.Tanganyika haina chake. Ndipo pale Mwalimu Nyerere alipokuna kichwa na kutania kama ana uwezo angehamisha Visiwa vya Zanzibar akavitokomeza mbali - visiwe karibu na Tanganyika. Hakufanya hivyo lakini amejitahidi kuleta Muungano na kufuta mpaka ule wa baharini kati ya Tanganyika na Zanzibar. Msichokone mambo jamani. Watoto wetu wanahitaji kuishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
sasa je Visiwani mafuta yapo??

Au mbuzi ktk gunia bado??
Sasa mbuzi katika gunia kwa nini Mnamshikilia (Wa-Tanganyka) Si muwakubalie tu Wazanzibari kile wasichopendelea kiwemo kwenye Muungano basi wakitoe. Kwanza Makubaliano ya Muungano si Msahafu. Kama kuyabadili kulingana na matakwa ya upande mmoja kwa nini isiwe hivyo.
 
ukisikia uchochezi ndo huo
 

Pakacha,

..inawezekana waliotumbukiza mafuta ktk masuala ya Muungano waliona mgongano unaoweza kutokea kutokana na ukaribu wa Zanzibar na pwani ya Tanganyika.

..lakini pamoja na wasiwasi uliounyesha bado Tanganyika ina eneo kubwa la bahari kuanzia Dar-Es-Salaam kuelekea Mtwara na hakuna sababu ya kukorofishana na wa-Zanzibari.
 
Mambo haya ya mafuta na matumizi yake n.k yananifanya nikumbuke kisa kimoja cha hekaya za mtu aitwaye Alinacha... kisa hiko watu wengi wanakifahamu kama "ndoto za Alinacha"..
Sasa kama mshauri mwelekezi anasema hakuna mafuta, halafu wakati huohuo anasema kama yapo yawe ya muungano, nani anaota ndoto za mchana?ni wazanzibar wanaosema kama yapo yabakiea kwao au smt wanaotaka yawe ya Muungano?
 
waswahili tunamsemo wetu 'lisemwalo lipo kama halipo laja'
 
Siku zote zanzibar ikijitafutia njia za kuganga njaa zake SerikalI ya Muungano imekuwa ni kikwazo tumejiunga na OIC, kutafuta marafiki wanaofanana na sisi , angalau tuombe maji ya kunjwa wenzetu mmetuleta kauzibe , tumejenga bandari yetu tufanye biashara mambo yalishaanza kustawi mmetuletea kauzibe, hayo ya kutuchagulia viongozi mnaowataka nyinyi wala siyasemi, basi hata hichi "kigeleni" kimoja cha mafuta mshaanza longolongo.HE!
 
Pakacha,Junius,

..nadhani huyo Consultant waliyemleta hakuelezwa dhamira halisi ya Wazanzibari.

..matokeo yake ametoa ushauri wa jinsi ya kugawana mafuta, wakati Zanzibar wanataka 100% control ya mafuta yao.
 
Kaka yangu na bado Tanzania Mainland (Kwa wewe siyo Tanganyika) ina madini mengi tu ardhini, pamoja na mafuta pamoja na gesi kibao pamoja na ardhi nzuri ya kilimo. Kwa nini isikubali hii rajuwa iliyoko Zenj watumie wale Waswahili kule peke yao ambao hawana chochote kile chengine cha kutegemea (karafuu ishaanguka ).
 
Sasa kama mshauri mwelekezi anasema hakuna mafuta, halafu wakati huohuo anasema kama yapo yawe ya muungano, nani anaota ndoto za mchana?ni wazanzibar wanaosema kama yapo yabakiea kwao au smt wanaotaka yawe ya Muungano?
Mshauri Muelekezi amefurunda Bwana. Mimi nilifurahi pale pale wawakilishi walipombwatukia katika semina yake pale Zenj.
 
jokaKuu,
Lakini si makubaliano ya mwungano yaliondoa mipaka. Nini manaa ya "a one sovereign republic?" That is what we were supposed to become, no?
 
Tunachotaka kujadili nini mali ya Zanzibar? Ndio mafuta ni bidhaa adimu, na utajiri wake sio mchezo. Lakini sio chetu kwa sasa, labda kwa maongezi iwapo zanzibar watataka. Nimeshasema mwanzo inatakiwa tufike mahali ambapo tuache ubabe, na zanzibar ianze kujiona kama kisiwa chenye nguvu itatusaidia sana katika maendeleo. Sio tuminyaneminyane sisi kwa sisi, hapo bado pemba na unguja!

Hayo maongezi yamafuta kama yakiwekwa vizuri muungano utimarika zaidi, na heshima itapatikana kati yetu. Na sisi wabara tutajifunza uchungu wa kutogawa mali zetu kama peremende! leo tunagawa ardhi, madini, bila kujali chochote. Fununu ya mafuta zanzibar tunakuja na kadi ya usalama! Waachane wazanzibar walinde kilicho chao.
 

Na wka nini Wazanzibariw asikubaliane na wabara kuhusiana na kulifanya suala hilo kuwa la Muungano?
 
Na wka nini Wazanzibariw asikubaliane na wabara kuhusiana na kulifanya suala hilo kuwa la Muungano?
Basi kwanini isiwe serikali ya bara ikawaachia wazanzibar walau "hicho" kidumu kimoja? wakati wao maadini yao na gesi zikabaki kwa kwisha ugomvi. SISI tunakhofu tukileta ushirika mtaitupa rasilimali hii kwa wajanja kama mnavyoyatupa maadini yenu.
 
Na wka nini Wazanzibariw asikubaliane na wabara kuhusiana na kulifanya suala hilo kuwa la Muungano?
Wazanzibari hamtaki kuwaelewa wamehoji na madini yaliyojaa bwerere Bara nayo pia yawe ya Muungano. Na tuzungumze hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…