Umeongea vitu Junius. Wapi pa kuanzia? Si CCM si CUF wote wanawazonga watu wetu. Matokeo yake wanazidi kudhalilika na umasikini.
 

Kweli mkulima maana hata huelewi kama ule umeme unauzwa na haupelekwi bure.
Ama kwa mafuta mtatoa ngonjera nyingi ,lakini hamgaiwi hata tone itawabidi na nyinyi mununue kama mnavyotununulisha umeme ,wanasema titi four teti ,ndio maana yake.
 
Na ya madini je? Kwa nini husemi ni ya pamoja. Muungano sawa - lakini usivunjike, mwenye hasara zaidi ni wewe na Wa-tanganyika wenzio.Lakini sisi (Wazanzibari) lazima tuwe pamoja kudai ile iliyo haki yetu na tulinde maslahi yetu kwanza , halafu na tulumbane katika CUF na CCM ( CCM Zanzibar)
 
Sawa na yaishe. sasa na tuikubali sheria ya Mzanzibari-kama ilivyo. Inamkubali Mzanzibari mwenye asili ya Uafrika (Bara) na inamkubali Mzanzibari mwenye asili ya Comoro, Uarabuni, Uhindini, Uzunguni na popote pale.Hakuna Mzanzibari aliye bora au zaidi ya wengine- wote ni sawa. Kama ni historia ni hao Wazalaendo Washirazi wa kudai hiyo - lini mumewaona wakidai? sasa isitokee watu wakadai kuwa wao eti ni Wazanzibari kuliko wale wanaotoka Mwarumango au kule Sengerema eti kwa sababu tu wanapiga matuta ya viazi..
 
Imechukua miaka mingi kwa SMT kuanza kuanza kuipatia SMZ mgao kutokana na misaada inayoingia nchini kwa jina la muungano. Na mgao wa sekta wa madini katika SMZ utachukua miaka mengine kibao ili japo Zenj waweze kufaidika nayo.

Dawa ni tit for tat, wakae na madini yao yenye mikataba mibovu na Zenj wawe na mafuta yao ambayo yatakuwa na faida kwa wananchi wake. Kwani tumeshasoma jinsi hao Wabara walivyokwenda mkenge kwenye madini yao!
 
Na michango ktk SMT je SMZ itaanza basi kulipia lini?

Yaani Bunge, Polisi, Jeshi, Mambo ya Nje, Elimu ya Juu n.k??

Including pia deni umeme wa TANESCO!
 
Na michango ktk SMT je SMZ itaanza basi kulipia lini?

Yaani Bunge, Polisi, Jeshi, Mambo ya Nje, Elimu ya Juu n.k??

Including pia deni umeme wa TANESCO!
SMT waweke mambo yao wazi na uone kama SMZ itashindwa kulipia na waache ubabe wao! SMZ imechoka kuburuzwa na kwa kuonyesha hilo, mafuta tunayatia kibindoni, na huko Bara mtanusa harufu tu! Safari hii si harufu ya marashi ya karafuu bali ni harufu ya mafuta!
 

Kama huna cha kuandika ni bora ukasoma na kuguna tu. Suala la mafuta na ubaguzi linakujaje? Suala la mafuta mwenzake ni umiliki wake na kama Wazanzibari kudai kumiliki mafuta yao ni ubaguzi basi ubaguzi huo ulianzwa na wale walioamuwa madini na gesi yao kumiliki wao wenyewe.
 


Unajuwa kuwa huo umeme ulipoletwa kwa msaada ulikusudiwa kwa Muungano?
Halafu hilo unalolisema ni sawa naile nyimbo ya Dr. Remi ya kilio cha samaki.
Sijuwi unaweza ukafanya hesabu na kusema mwananchi wa kawaida wa Zanzibar anafaidika na nini kutoka hiyo Serikali ya Muungano? Barabara ,Hospitali, Viwanja vya ndege, mashule, na huduma za kilimo ni vitu vya wazi vinavyowasaidia wananchi wa kawaida na hivi vinalipiwa na Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano haitowi peni. Wakati huohuo ushuru wa Bandari, ndege na visa za Watalii na uvuvi wa Bahari kuu vinachukuliwa na Serikali ya Muungano na kurejesha kasma kwa Zanzibar. Kwanini kasma au hasa kwanini wakusanye wao, kisingizio mchango wa shughuli za Muungano. Shughuli zenyewe za Muungano huduma 99% zinakwenda Bara na 1% ndio zinawafikia watumishi wa Zanzibar walio kwenye Idara za Muungano.
Sasa kwa hesabu yako hizo pesa za Almasi na gesi zinasaidia vipi Zanzibar?
 

Tatizo litakuja pale huyo mpiga matuta anapewa upendeleo na kuachwa yule asiejuwa alikotoka yeye na zanzbar na zanzibar tu. Haya ndiyo yanayofanywa kwa makusudi na CCM ili kujilinda na kuondoshwa madarakani. Wasichotambuwa kuwa wengi wa hao wanaotoka Mwanarumango wanamapenzi na kwao walikotoka kuliko Zanzibar. Hili lazima Wazanzibari walitie maanani kwani hawa ndio watakaokuja kupiga kura ya ndio kwenye kura ya kufanya Serikali moja. Tunashindwa kuwaelewa wepi ni wakaazi halisi na wepi ni wanapandikizwa.
 
Na michango ktk SMT je SMZ itaanza basi kulipia lini?

Yaani Bunge, Polisi, Jeshi, Mambo ya Nje, Elimu ya Juu n.k??

Including pia deni umeme wa TANESCO!

SMZ ianze kulipa kitu gani kwa SMT wakati pesa pale bandarini zinachukuliwa kwa kipolo jioni kupelekwa Bara na mwisho a mwezi hukasimiwa fungu na kurudi Zanzibar.
Kule Uwanja wa ndege cheki zinaandikwa kwa jina la Directorate ya anga ya Muungano.
Uvuvi wa bahari ya Zanzibar vibali na malipo yanafanywa Dar es Salaam. Vibali vya Mabenki na shughuli zote za kifedha inafanywa Dar.

Sasa unachotaka Zanzibar wailipe SMT kitu gani ikiwa wao SMT ndio wanaotowa fungu katika mapato YA ZANZIBAR kurejesha zanzibar. Unafikiri kutokana na ulafi na ulalamishi wa wenzetu wangenyamza kimya huku hawapati kitu?
Hili la majeshi, Polisi na mambo ya Siasa ni mbinu tu. Kinachofanyika hasa ni kuwalipa mishahara watumishi ambao wanazitumikia idara a ukandamizaji sawa na kumlipa kibaruwa yeyote aliyetoka nje ya nchi. Kwani Zanzibar inahitaji mjeshi kiasi gani kujilinda? inahitaji polisi wangapi kulinda usalama na ina haja gani ya kuwa na Wabunge ndani ya Bunge ambalo kazi yake ni kuhudumia upande mmoja tu wa Muungano. Hata hilo Bunge lenyewe halina nguvu yoiyote kwa Zanzibar, bado hujaona Kiini Macho chenyewe hapo?
 
Bara tunaungangania na kuendelea kuwagharamia Zanzibar kwa kuwapangia watawala, na kuwapa income support

Zanzibar washatuchoka kwenye hii ndoa of convenience wanaona wao watakuwa bora kuwa kivyao


lakini cha ajabu mikataba ya huu muungano imekuwa siri ya Taifa, watawala wa bara hawapendi kudadisiwa juu yake


na mbaya zaidi after 40 YEARS nadhani its about time tukauvunja kwani HAUKUWEPO, UKAWEPO na UNAWEZA USIWEPO TENA ni contract ambayo inaweza kuvunjwa kama haina faida kwa pande zote mbili
 
GT
Kutokana na point zako hapo juu, jee kwa nini tunaendelea kuubeba muungano?
Nadhani muungano ni moja ya vikwanzo vya maendeleo ya kiuchumi kwa Tanganyika sababu Zanzibar wanataka kuendelea kuwa kama nchi wakati wanastaili kuendeshwa kama mkoa.
 
Kinacho boa ni Z'bar kila kitu sasa wanataka kufanya kivyao na hawaishi kulalamika. Wana serikali yao wenyewe, bendera yao wenyewe, national anthem yao wenyewe etc which is more than Bara can say. Hivi wana ringia nini haswa? Hata airport ya kimataifa I doubt wanayo. I think as time goes by wazanzibar are getting facts & dreams confused na ever since haya mafuta yagunduliwe ndiyo imekuwa tabu kabisa. Wamekuwa kama watoto wanaotaka kupewa kila kitu wanacho taka. Kwenye vitu vya kwao basi ni vya zanzibar tu vya bara ni vya wote. Hivi umeme wa zanibar unatoka wapi? Si bara? basi nasisi tuseme umeme wakwetu? Ukweli ni kwamba muungano can be a beautiful thing but if one side doesn't want it hata kama stratigically muungano ni muhimu vipi ni bora tuachane. Hata kwenye ndoa mmoja akingangania divorce au sijui afanye mambo yake mwenyewe basi ndoa ita vunjika. The yes or no uestion I have for zanzibar is MNATAKA MUUNGANO YES OR NO? Kama mnautaka basi lets be adults tutafakari cha kufanya kama hamtaki kueni direct siyo kulete mambo ya chini chini.
 
Acheni kuuzunguka mbuyu...wanaoungangania huu Muungano ni BARA its that plain simple

Zanzibar hawautaki na wanaona hauna manufaa kwao

kwa nini hatutaki kua admit hilo?

the issue hapa ni namna ya kuuvunja huo muungano sasa how will we do it kama mikataba ya kuungana inafanya SIRI?
 
Kwa nini tusiweke referrendum? Muungano kuendelea lazima upata asilimia zaidi ya 50 kwa pande zote, peg it with the 2010 general election complete with international observers the works.

Yeah, right. Like CCM can't pull a rabbit out of it's old hat in the midst of international observers.

Wauvunje tu, hauna mpango.Kwanza si wa halali kwa sababu wananchi walishinikizwa tu na zaidi ya nusu hawakuhusishwa hata by proxy ya wawakilishi.
 
kwa vile sehemu ya watu hawautaki haina maana basi uvunjwe; that is the most simplistic solution. Hakuna njia nyingine ya kushughulikia matatizo yake?
 
muungano,has seen its day,its like an epoch which needs to pass out.the powers that be aint ready to make a move for fear of NYERERE arising from his resting place to haunt them
 

Pakacha, unajua Unguja na Pemba ziko ndani ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania. Lakini nyinyi(Wanzanzibari) hamlijui hilo. TPDC ni chombo kinacho shughulikia maswala yote yanayohusiana na maswala ya mafuta yaliyoko Tanzania.

Sasa hicho chombo kingine kinachotoka kuundwa kwa ajili ya mafuta ya Zanzibar kinatoka wapi. Kwa kifupi mikataba yetu ya madini haikuwa mizuri kunatokana na TAMAA za vionozi wetu wakasaini mikataba mibovu. Hakuna kodi ila kuna Royality ya 3% kwa kisingizio kuwa makampuni ya madini hayapati faida.

Sasa tunapokuja kwenye swala la mafuta linakija swala la Tanganyika na Zanzibar, na mnasahau kuwa Zanzibar inaitwa hivyo kwa sababu ya muungano, nje ya muungano hakuta kuwa na kitu kinachoitwa zanzibar, Wapemba watakuja juu na kusema mafuta ni ya kwao kwa sababu ndiko yanapopatika. Mwishoe mtabaki na Unguja na Pemba kila mtu kivyake vyake.

Wanzanzibari jaribuni kutumia hata muda kidogo kufikiri kuhusu swala hili na sio kukurupuka tu na kuanza kusema tuanzishe chombo cha usimamizi wa mafuta ya Zanzibar. Utafiti umefanywa na serikali ya muungano sasa kumeonyesha dalili za upatikanaji, nyie mnaanza kusema mafuta ni ya Visiwani na sio ya Tanzania Bara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…