Tukianza tu kuweka mipaka basi tutakuwa tukizunguka humo kwa humo. Lengo liwe kuwatetea Wazanzibari bila ya kujali kuwa hawa ni Waafrika , Washirazi, Watumbatu au wana asili ya Dubai.
Kwanini? Waafrika hawana tena kwao huko walikotoka Bara, Washirazi hawajui sehemu hasa walipotokea< Watumbatu hawana pahala pa kujinasibu zaidi ya Zanzibar< Wapemba watabaki Wapemba tu na hata hao walio na asili ya Dubai hawana pa kwenda isipokuwa Zanzibar.
Zanzibar Kihistoria ni pahala ambapo watu wa sehemu mbali mbali waliweka makazi na Zanzibar ina bahati kuwa hata katika zama hizi za sasa anakuja huwa anapenda aweke makazi, hivyo kuishi kwa historia si sahihi.
Hili suala la Waafrika kuchukuwa madaraka na kuwaacha Wazanzibari asilia linaletwa na nguvu kutoka upande wa pili wa Muungano na wanafanya hivyo kwa faida zao wanazozijuwa. Wengi wape na ni jukumu la wengi kupigania haki ya kuwa na sauti katika nchi yao lakini kama ulivyosema wanasiasa wanawatumia wananchi kwa uasilia wao kupata manufaa yao.
Well, haya ni matatizo ya ndani ya Wazanzibari lakini kwa sasa wanatakiwa wawe pamoja kukabiliana na tatizo linalowakabili la kunyimwa haki zao kwa kisingizio cha Muungano. Pengine ingekuwa vizuri kama tofauti za Wazanzibari zingetatuliwa kwanza na kupata nguvu ya kuikabili upande wa pili wa MuunganolLAKINI muda huo haupo na hivyo wapambane na kurejesha haki zao kwanza na baadae wakae na kuondosha tofauti zao.