kwa vile sehemu ya watu hawautaki haina maana basi uvunjwe; that is the most simplistic solution. Hakuna njia nyingine ya kushughulikia matatizo yake?

You are absolutely right Mzee mwanakijiji, huu muungano unaonekana kama vile Bara ndio wanao ung'ang'ania wazanzibari hawahutaki. kwa kuwa hautakiwi uvunjwe. Lakini naomba kuuliza hivi kuna mwana JF yeyote yule ambaye anasiri za huu muungano ili atumegee?
 
muungano,has seen its day,its like an epoch which needs to pass out.the powers that be aint ready to make a move for fear of NYERERE arising from his resting place to haunt them

If one dead man can hold 40 million or so living people hostage in a unholy union then we must have some serious mental issues.

There has to be some other plausible reason for the current state of the Union.
 
Mimi naunga mkono kwamba na tuwaache wazenji wajioongoze wenyewe bwana,mimi mpaka leo na elimu na elimu ya ndogo nilyonayo na umri nilionao bado sijaona sisi bara tunaong"ang"ania muungano je unatusaidia nini hasa,zaidi ya kuwa unatulemea tu na wao wanafaidika sana au hawa majisamaki wakubwa kuna kitu wananufaika na waseme basi,ukiuliza wanasema kiusalama kiusalama how?
 
If one dead man can hold 40 million or so living people hostage in a unholy union then we must have some serious mental issues.

There has to be some other plausible reason for the current state of the Union.

Hili ni kweli kabisa...mtu mmoja mtu anaendeleakututawala toka kaburini hii inatisha. Yaani kati ya watu milioni 40 yeye pekeyake tunaambiwa kuwa alikuwa na VISHENI na yote aliyokuwa akiyataka ndio yanatakiwa kubaki kama yalivyo..mfano hii pet project yake ya Muungano ukienda tofauti na mawazo yake utaambiwa MSALITI!



inatisha mjomba
 

hapo ndipo kwenye kiini cha tatizo. Viongozi waliopo bado wanaogopa kumuudhi marehemu na hakuna aliy tayari kuingia kwenye historia kuwa ndiye aliyeuvunja muungano. Hata hao Wazanzibari wanaosema hawautaki, wala hawasemi hivyo waziwazi wawapo hadharani, wanatambulika wka matendo yao na maneno ya kujificha... wanafiki sisi
 
GT
Kutokana na point zako hapo juu, jee kwa nini tunaendelea kuubeba muungano?
Nadhani muungano ni moja ya vikwanzo vya maendeleo ya kiuchumi kwa Tanganyika sababu Zanzibar wanataka kuendelea kuwa kama nchi wakati wanastaili kuendeshwa kama mkoa.
Ukiwaendesha kama Mkoa hapo ndiyo unafanya ukoloni. Lakini kwa majibu ya haraka haraka tu . Tafuta mizani uipe hiyo Tanganyika yako, sasa pima gharama za kuwa na Zanzibar kama jirani- na gharama za kuwa na Zanzibar kama ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano zipi zinazidi nyengine. Halkadhalika na kwa Zanzibar nayo ipime gharma za kuwa na Tanganyika kama jirani na gharama za kuwa na Tanganyika kama mwenza katika Jamhuri moja ni zipi afadhali. Tatizo siyo dhana ya Muungano ndugu yangu, huo unatoa unafuu wa gharama kwa pande zote mbili husika- lakini cha muhimu ni usawa katika Muungano huo, na hilo ndilo wenzetu wa Zanzibar wanalolikumbushia kila mara- Kumbuka tu Muungano wetu ni jambo la pande mbili- sasa ukija na suala la Mkoa - shauri yako msubiri Bwan Mwiba akupashe.
 
kwa vile sehemu ya watu hawautaki haina maana basi uvunjwe; that is the most simplistic solution. Hakuna njia nyingine ya kushughulikia matatizo yake?

Mkuu MMKJ heshima mbele (salute)

Simpo logiki

Wewe na Bibi mmeoana na kuwa kitu kimoja mbele ya baba Askofu, mkakubaliana mtaishi pmj kwa shida na raha.

Baada ya miaka kadhaa; bibi anakwambia HAKUTAKI na MUACHANE ili afanye mambo yake mwenyewe. Njia zote umejaribu ili tu kuhakikisha hiyo ndoa HAIVUNJIKI, bado tu bimkubwa HATAKI kwa ishara na matendo ya kila aina anakuonyesha na UNAYAELEWA.

Lakini kuna watoto, ndugu na jamaa wengine wanataka NDOA YENU IENDELEE na kuna wengine wanasema BORA MUACHANE.

JE, BADO UTAENDELEA KUTAFUATA TU KUTAFUTA NJIA NYENGINE
??? 😕
 
Theories zako ni mbovu ndugu yangu. Kwa nini hutoi theory kuwa Wasukuma waje juu na kusema kuwa Madini ya kule Mwanza ni yao na si ya Tanganyika. Wewe nafikiri huwajui Wapemba wasome vizuri zaidi- Ni Wazanzibari halisi.
 
Je huu muungano uko kwenye maandishi yeyote? Je kuna sheria au guidelines zozote kutoka international organisation zinazo-govern formation ya miungano? Kwa nini tuna huu muungano? Mwalimu na Karume walitoa sababu gani juu ya huu muungano?
Haya ni maswali machache ambayo lazima tujiulize kabla ya kuropoka kuvunjwa kwa muungano. Tukicheza vibaya, huu muungano unaweza kutupeleka pabaya as a country. Zanzibar has a great future chini ya muungano kama wakiamua. Sidhani kama wanaweza kujimudu peke yao. Natumia sidhani maana sida economic au social data za ku-support hii and i have no time to research.
 
Ni mpaka ndugu yangu. Kumbuka kuwa ukivunja muungano kuna mpaka pale kati ya Zanzibar na Tanganyika( au niseme kati ya Zanzibar na Dar es salaam) Sasa dar es salaam ndio Tanganyika. Utakabili vipi gharama za kulinda mpaka huo. Huo sio kama ule mpaka wa Mutukula ambako Amini alileta tafrani. Sasa ukikaa Kizimkazi kule kwa rifle tu unakirusha kibomu hadi Magogoni. Wee acha tu.
 
 
hapo ndipo kwenye kiini cha tatizo. Viongozi waliopo bado wanaogopa kumuudhi marehemu na hakuna aliy tayari kuingia kwenye historia kuwa ndiye aliyeuvunja muungano.

Swala sio woga! Alternative vision is problematic. Kiongozi yeyote hawezi kukurupuka tu nakusema navunja muungano! Watu waliozaliwa kuanzia 80's wanajua tanzania ndio tanganyika na zanzibar. Ukitaka kuuvunja lazima utoe sababu tena za msingi kweli kuondoa kivuli cha nyerere na kujenga mwelekeo mpya. Mpaka sasa, sijapata kusikia logic nzito inayoeleza kwanini muungano. Manunguniko yapo, ambayo hata mimi nayaunga mkono, lakini uchambuzi wa iwapo tukitengena kunafaida hizi na zile bado havijawekwa bayana. Until then, the union shall stand, however, solutions for independence for each nation should be respected.
 
Wazanzibari Kwa Uhakika hawataki Muungano kabisa na hilo lieleweke ikiwezekana hata Kesho Uvunjwe kila Mtu awe na Nchi yake kama Ilivyokuwa hapo mwanzo 25.4.1964. Zanzibar ilikuwa ni DOLA Kamili na ilikabidhiwa KITI Chake UN siku moja na KENYA na Kusimamisha BENDERA yake iliopepea katika Umoja huo wa MATAIFA.

Uvamizi wa hila za JULIUS NYERERE ndio Ulioipoteza ZANZIBAR na Kuitumbukiza katika Dimbwi hili la MUUNGANO wa KIFISADI. Muungano huu ni Kichekesho Dunia Nzima haupo kama huu na wala ulofanana na huu, huu sio Muungano Ni UVAMIZI.

Hakuna haja ya Kupigishana kelele Wazanzibari wapewe Nchi yao na Upesi kabla ya kuja kutokea mabishano makali na yawazi ambayo Jumuiya ya Kimataifa itabidi iingilie kati kwa Kuleta Mshauri Mwelekezaji wa Kugawana Nchi na Mipaka yake kabla ya Mika nmichache ijayo.
 
Mnaosema tuwe na referendum kwani wakati Tanganyika na Zanzibar zinaungana waliitisha referendum? Huu mungano uvunjike tuu maana mpaka leo ukiniuliza faida yake kwangu na wananchi wengine wa kijijini kwetu jibu ni kuwa SIJUI.
 
Mnaanza mwanzo ,tatizo la Muungano ni kutokuwepo kwa Tanganyika ,hakuna jingine hili ni tatizo sugu ambalo ndilo linalozusha kisirani chote kwa raia kuhoji baadhi ya mambo mambo.

Kutokuwepo kwa Tanganyika ni donda ndugu katika Muungano ,na hata kuuvunja Muungano kunahitaji kuwepo kwa Tanganyika ,sasa cha muhimu ni kujiuliza Tanganyika ipo wapi ? Kwa nini ikaingia mitini na kuiwacha Zanzibar ikiteseka.

Unapotaka kutatua mambo ya muungano au ndoa ni lazima wawepo wanandoa sasa leo yupo mmoja tu ,mwengine hajulikani alipo ,vipi utaweza kuamua mambo ya Muungano huo?

Je huyu Kikwete alikuwa mmoja wa waasisi wa kuidai Tanganyika leo amejinyamazia kimya na kudai kuwa ni mlinzi Mkuu wa Muungano ,jiulizeni ni kitu gani kimemfanya awe mlinzi mkuu na anamtishia mwanandoa mmoja ambae yupo ikiwa atavunja Muungano atakiona.

Zanzibar ,simple ikiwa wataamua kikweli kweli na kudai lazima mwanandoa alieingia mitini arudi la si hivyo ndoa itavunjika na kutoa kipindi cha mwaka mmoja au miezi sita ,basi ijulikane tu kuwa lazima Mwanandoa atajitokeza ili kulinda ndoa hiyo ikiwa anaihitajia.

Je wanaoiongoza Zanzibar wapo tayari kutoa kauli hiyo au ni unafiki tu uliowashika ili kutimiziwa mambo yao na kujiwezesha na kujikita zaidi kiufisadi ,wakijua mafisadi wa bara lazima watekeleze matakwa yao kwani kuwepo kwa jopo hili linaloiongoza Zanzibar kunawasaidia mafisadi wanaoinyonya Tanzania ,hivyo kinachoendelea ni mipango iliyomo ndani ya Serikali ya Mafisadi Tanzania (SMT) na Serikali ya Mafisadi Zanzibar (SMZ).

Serikali hizi mbili hazitoweza kuleta suluhishi la Muungano milele ikiwa mwanandoa Tanganyika hatajitokeza kuzungumza na Mwanandoa Zanzibar kuhusiana na ushirika wao. Mazungumzo haya tunayoyaona ya kushughulikia kero za Muungano zinafanywa na Matapeli wa Tanzania na kumuhusisha Mwanandoa mmoja tu ambae ni Zanzibar ,Serikali ya Mafisadi Tanzania (SMT) ni walioitapeli Serikali ya Tanganyika na kuitia guniani.
 
Mh!!! Muungano wanauhitaji tena wote. Wale wa Zanzibar wanauhitaji na wale wa Tanganyika (kama ipo ) wanauhitaji. sasa ni namna gani tutaishi katika Muungano huu ndio suala la kila siku la kulizungumza (au kulumbana). lakini "we need each other" na tuendelee kuzungumza -how best each of us will benefit. Bila ya Muungano Tanganyika isigekuwa ilivyo hivi sasa na bila ya MuunganoZanzibar (pamoja na malalamiko yake mengi) isingekuwa ilivyo hivi sasa_Namaanisha katika neema.
 
Unaona wewe ulivyopotoka. eti tuvunje Muungano ili waZenj wajiongoze wenywe. Kwani Muungano ulikuwa na maana ya Wazenj waongozwe na WaTanganyika. Wazenj siku zote watajioongoza wenyewe. Na wa Tanganyika watajiongoza wenyewe. Katika Muungano tutaongoza sote kwa pamoja kwa misingi maalum ya mashirikiano.sasa sio suala la kuvunja Muungano ili Wa zenj wajiuongoze wenyewe- lakini ni kuimarisha Muungano ili waZenj wajiongoze wenyewe (kama sasa hawajiongozi wenyewe), Wa Tanganyika wajiongoze wenyewe. Na kwa pamoja tuongoze Tanzania yetu kwa ridhaa na manufaa ya wote wazenj na Watanganyika. Mungu ubariki Muungano. Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
jee una hakika na unayoongea?. Tafadhali define Wazanzibari. Ni wepi hao? Kwani Wazananzibar hawana bendera? Kwani wa Zanzibari hawana kiti UN? Be specific- please.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…