Kiti kiliondolewa kwa hila za Julius Nyerere pamoja na Bendera, lakini Baada ya miaka karibu ya 40 sasa SMZ imerejesha Bendera kwa Mbwembe na hoi hoi nafikiri hili unalijuwa, ila kwa KITI nakuahidi kiko njiani kurejeshwa.

habari ndiyo hiyoooo
 
..hata mimi napendekeza Muungano huu uvunjwe.

..wa-Zenji wamezidi kutusimanga wakati hawana chochote cha maana wanacho-contribute ndani ya Muungano.

NB:

..IMF walipendekeza wa-Zenj wakatiwe 4.5% ya mapato ya Muungano, sina uhakika kama uchumi wa Zenji unakaribia kiwango hicho ukilinganisha na wa-Tanganyika.
 
unapo -classify Tanganyika na kudai kuoina % ya uchumi wake-Tanganyika iko wapi? hii si ndio kina Bwan Mwiba na wenziwe wanauliza kila siku. Angalia ile ramani ya Visiwa vya CUBA. jiografia ya pale kidogo inashabihiana na jiografia ya Zanzibar na Tanganyika (hususan Dar es salaam) Sasa iulize USA pamoja na ukubwa na ubabe wake, na teknologia yake ya ulinzi na ujasusi inapata shida gani na inagharimika vipi kulinda mpaka pale. sasa fikiria Tanganyika yako itakavyoweza kulinda mpaka kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hizo almasi na dhahabu zenu si zote zitakuwa zinauzwa magendo Zanzibar. sasa mafisadi wenu hamuwaoni na mali yenu hamuioni. Nyiye mtakuwa mmekwisha kabisa, usiombee Muungano kuvunjika.
 
Mnaosema tuwe na referendum kwani wakati Tanganyika na Zanzibar zinaungana waliitisha referendum? Huu mungano uvunjike tuu maana mpaka leo ukiniuliza faida yake kwangu na wananchi wengine wa kijijini kwetu jibu ni kuwa SIJUI.

Kukosa radhi ya moja kwa moja ya wananchi ni moja kati ya vitu vinavyoufanya muungano huu uwe na sura ya ubatili.

Ukitaka kuuvunja vizuri, kupata ridhaa hiyo ya moja kwa moja ya wananchi kutaweza kuondoa shaka kwamba kuvunjwa huku kwa muungano ni halali.

Ama sivyo unakwenda kwenye lawama ile ile na kwamba ukivunja muungano bila ya kura ya maoni, wengine watasema kuvunjwa kwa muungano hakukuwa halali.

Kitu muhimu ni kwamba kama tunaendelea nao au kuuvunja, muungano huu unahitaji baraka za moja kwa moja za wananchi.
 

Pakacha,

..wacha vitisho wewe.

..wa-Tanganyika hawastahili usumbufu na masimango toka kwa wa-Zanzibari day in day out.

..Zanzibar hawana haja na almasi wala dhahabu za Tanganyika, wana mafuta.
 
GT
Kutokana na point zako hapo juu, jee kwa nini tunaendelea kuubeba muungano?
Nadhani muungano ni moja ya vikwanzo vya maendeleo ya kiuchumi kwa Tanganyika sababu Zanzibar wanataka kuendelea kuwa kama nchi wakati wanastaili kuendeshwa kama mkoa.


Game,Wengine hawajui lugha ya Kiswahili tuwavumilie tu ikiwa hawajui maana ya neno Muungano!
 
Ila mimi kubwa linaniuma ni kwa nini kuna tofauti kubwa sana kati ya mishahara ya wafanyakazi wa SMT na SMZ?

As long as hii ni nchi moja basi SMT ingetoa fungu kuziba hii tofauti..maana wote ni nchi moja na Bara wana uchumu mkubwa na watu wengi!!

Yaani ukiwa Mtanzania sekta ya umma Pemba au Mbinga basi mshahara uwe ni mmoja!
 


Hilo halijawa tatizo kwenu kwani nanyi si mna Rais anaehutubia Bunge akitumia masaamatatu na nusu bila ya kutaja maslahi yoyote ya Zanzibar na anapoitaja anaitaja kwa nafsi ya tatu? Si mna Spika wenu wa Bunge anaewasemea watu wa kutoka Mwanza hadi lindi, mna Waziri mkuu wenu anaesughulikia mambo yenu tu na hukutana na Waziri Kiongozi wakajadiliana mnachokiita Muungano?
Hayo yote hayajakuhakikishia kuwa hamna mnalokosa kwa Zanzibar kuwa na vitu vyote hivyo? Kuhusu umiliki wa Rasilimali huo ulikuwa uamuzi wenu wa awali kuwa alienacho afaidi peke yake.
 
kwa vile sehemu ya watu hawautaki haina maana basi uvunjwe; that is the most simplistic solution. Hakuna njia nyingine ya kushughulikia matatizo yake?

Nakubaliana nawe kuwa ipo haja ya kuutafutia solution Lakini nakataa kwa nguvu zote kusema kuwa kama itatokea sehemu moja iukatae basi ushindikizwe. Huu ni muungano wa hiari kwa sehemu mbili na iwapo moja ishaona haina faida basi iwe hivyo na si vyenginevyo. Na kutokana na hili nashangaa kwanini zile jitihada za G55 zilizimwa kwa utashi wa mtu mmoja tu.
 

Kwa maana hiyo Zanzibar ni mke katika ndowa hii? Alaa kumbe huu Muungano una mfumo dume? Angalau jitihada za kuwa na uwakilishi sawa kati ya wanawake na wanaume Bungeni umo njiani, basi angalau katika hii ndowa yenu mgempa mke wenu (Zanzibar) haki na uhuru kama mlivyopanga kuwapa jamii ya kike ili kuondowa mfumo dume.
 



Kwa maana hiyo huna hoja utakayotowa ikawa valid kwani umeshakubali kuwa huwezi kutafuta ukweli.
 

Pakacha, Waombe radhi Wazanzibari. Iwapo Muungano imewapa neema na bado wanalalamika basi matusi wanayoporomoshewa ni stahiki yao.
Napenda kuwa umtu wa kusoma tafadhali waulize Wazanzibari walikuwa wapi KINEEMA na wapi waliposasa kishida.
 

Kwa bahati nzuri nyie ndio wenye madaraka ya kufanya hivyo na kama mnajihisi hivyo wafanyieni tu kwani hata sasa si mnawaamulia tu.
 



bona picha unayoichora ni ya kutisha tu? Kwani majirani hawawezi kuishi kwa kushirikiana ? Pengine panapo kuheshimiana majirani hao watashirikiana vizuri kuliko hivi ndani ya Muungano kwani umekosa ile dhana halisi ya usawa wa pande mbili.
 
Ila lawama za Muungano hutoka zaidi Visiwani!

Ila kama ikitoea kuvunjika basi Visiwani wataloose zaidi: The Islands will never be stable, itakuwa kama Komoro!

Halafu licha ya Utalii hakuna chochote cha maana zaidi ya malalamiko!

Watu Wameacha kufanya kazi na sasa kuanza kukaa na kulalamika tu yaani kila siku!

Hii ya kugawana wafuta: je na TANESCO umeme tugawane? na Taarabu tuseme Visiwani wabaki na taarabu zao? Je Zanzibar Stars je itapigia wapi?

Halafu kila mtu ni mtawala: sasa sijui ni nani visiwani anafanya kazi!
 
Last edited:

Hii ingekuwa hivyo kama hii ingekuwa nchi moja lakini kuna Zanzibar inayofanya mambo yake chini ya amri ya Tanzania na kuna Tanzania inayofanya kazi za kuijenga Tanganyika na hivyo hii Serikali ya Muungano ni illussion tu.
 


Usijiumizekichwa kuhusu stability ya Visiwani kwani wao wako stable kuliko nyie.
Matendo ya kuvunja amani yako bara zaidi kuliko Zanzibar na siku mtakayosema hampeleki jeshi kuuwa na kubaka ndio utakuwa mwisho wa maovu hayo kule visiwanoi.
 
Taabu ya Visiwani ni kujilinganisha na Dubai au Omani wakati wenzao wana mafuta!

Dubai au Omani wafanyakazi wengi wanatoka nchi zingine: hii inawezekana kwa utajiri walio nao!

Sasa Visiwani hakuna chochote: may be utalii! Sasa hapo hakuna wa kumtawala!

Ni watu wachape tu kazi, kama eneo dogo waje bara kuna ardhi kubwa!
 

Na Bara tabu yao kujifananisha na Taifa lililoendelea sana hapa Afrika wakati Ufisadi ndio unaowaumiza na wananchi wanakatishwa tamaa na kelele zisizo na hatuwa thabiti za utekelezaji. Bado na kuwa na rasilimali suala la kutembeza bakuli linaanzia Serikalini na hata kwenye NGOs.
Suala la ardhi ni tatizo hilo kwani ukubwa wake haujaunufaisha watu wala kuwatowa kwenye njaa.
 
Kero kubwa ya Muungano kwa watu wa Bara ni Kulia lia kusikoisha toka Visiwani yaani kila siku!

Yaani malalamiko tu! yaani kusema tu wanaonewa siku zote!

Hadi bara wanaona hamna tena jipya hadi na sasa wamezoea!

Hakuna dhambi mbaya kama kila utakachofanyiwa basi utaona unaonewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…