Mwiba nakujua ati wewe wa Cnanja-mjawiri. Lakini mimi usihofu Bwana ni kindakindaki. Mimi ni Mshirazi -Bwana. Bibi zangu wakifanyiwa shopping Ursine (Kijiji -kipo karibu na Msasani). Sasa kutoka kwao hadi Ursine (kwa kidau cha upondo) ni karibu kuliko kupanda Punda kwenda Zanzibar Mjini. Udumu Muungano
 
 
Last edited:
Mwiba,
Asikushughulishe sana Pakacha wa Kisonge huyu, ila nafikiri kaburi la babu wa babu yake lipo Makunduchi si kama Karume kuna kaburi la baba yake tu Unguja, anapotokea hatupatambuwi, mara Malawi mara Shinyanga, mara Mwanamutapa aaah tabu tu.
 
Junius CCM hawayauzi Ndugu yangu. Acha hiyo. Kuna sera tu ya kuchangia gharama za maji safi, elimu, afya. Kwani wakati ule wa Ukoloni Wazee wetu si walikuwa wakilipa Shilingi Tatu (fixed rate) kwa ajili ya maji Mjini Zanzibar?
kucheka na kulia yote ni makelele.
 
Mwiba,
Asikushughulishe sana Pakacha wa Kisonge huyu, ila nafikiri kaburi la babu wa babu yake lipo Makunduchi si kama Karume kuna kaburi la baba yake tu Unguja, anapotokea hatupatambuwi, mara Malawi mara Shinyanga, mara Mwanamutapa aaah tabu tu.
Junius. Kuchuma karafuu ni hobby. Makunduchi hakuna mkarafuu. . Wazee walikuwa wanakwenda Chanja-mjawiri huko kufanya hobby na wanakaa kambi miezi miwili ,mitatu, hata mitano. Sasa Wapemba damu -damu.
 
KILE AMBACHO MIKOA MINGI YENYE WATU MARADUFU YA WAZANZIBARI inakitarajia kimeanza kufanywa na Wazanzibari baada ya Waswahili huko kuchoka na tabia ya Dar es salaam kutaka kutamalaki juu ya kila jambo hata yale ambayo yangeliweza kufanywa uzuri na eneo au mkoa wenyewe bila kuingiliwa na serikali kuu.

Kuanzia sasa Zanzibar imetangaza rasmi kuwa masuala ya utafutaji, uchimbaji na uendelezaji biashara ya mafuta halitakuwa tena jambo la muungano bali la eneo la Zanzibar kama nchi ndani ya nchi mbili zilizoungana.

Waswahili hao wameamka pia na kutangaza kwamba kuanzia sasa maeneo huru ya kiuchumi au EPZ yatakuwa ni milki ya Waunguja na Wapemba na sio ya Tanzania.

Jambo hili litawawezesha Wazanzibari ambao wamekuwa wakikwamishwa kutokana na kuwekwa kwapani na serikali ya muungano katika kuifanya Zanzibar iwe sawasawa na Dubai, Sharijah au Dohar, kwa maana ya kugeuza kisiwa hicho soko kuu kwa bidhaa toka Uarabuni, Ulaya na Mashariki ya mbali na kisha kuwavutia wananchi wa bara, Zambia, Malawi, Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya kununua vitu toka Zanzibar badala ya kuvifuata mbali. Katika nadharia ya menejimenti ya masoko hii ni kusema Wazanzibari wamegundua kitu kiitwacho fursa ya kipekee na ambayo haifai kucheleweshwa au 'niche' na wameamua kuichangamkia bila kukubali matende ya kuazima toka kwa viongozi wa bara.

Kwa kuwa serikali kuu ya muungano bado inataka kutawala maisha ya kiuchumi na kijamii inaelekea hatua hii ya Zanzibar itapigwa vita kwa ukucha na meno ili Zanzibar isifanikiwe halafu mikoa ya Tanganyika ikataka kuwaiga kwa kutaka kuachiwa na wao uhuru katika masuala yao ya uchumi na kijamii.

Hili hata hivyo litakuwa gumu kwa kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya Tanganyika sio watu wa kuchaguliwa bali watu wanaopandikizwa na chama tawala wawe wana uwezo wa kufanya kazi hiyo au la.
 

Nitakuwa wa mwanzo kuchangia lakini nitatowa maelezo kidogo sana na kwa kifupi ni kama hivi ifuatavyo, hakuna kiongozi yeyote yule umjuwae wewe katika hiyo itwao serekali ya zanzibar mwenye uwezo au hata kusubutu kuja na uwamuzi huo ,kwanini nikasema hivyo kutokana viongozi wengi wa hapa zanzibar wanaelewa vipi wameshika madaraka huku ikiwa serekali kuu inatambuwa undani wa madaraka yao sasa pindi tu wakienda kinyume na matakwa ya serekali halisi (serekali kuu)huambiwa ewe bwana we unaelewa wananchi hawakukuchaguwa kura zako zilikuwa ni hizi na sisi tukawa nawe sasa inakuwaje leo? hupewa uwamuzi wa mambo mawili wakubalie au rejesha kadi yetu, na huo ndio unakuwa mwisho wa hizo kejeli zao msidanganyike kabisa na hayo maneno yao ya hapa na pale sie zanzibar hivi navile javile punda,javile hivi ni unafiki tu huo na kwa kusadikisha hilo wangaliyeni mwisho wao wanaufyata kimnya na ndio pale wanaporudi kule nilikosema ooo chama chetu sie hivi na vile lakini ukweli unabaki pale pale wanaendele kuwa Gari la Ngombe usukani puwa kwa mana nyingine ni sawa na mnyama aliyetiwa (vishwa/wekwa)shemere.
 






wangeanza kwa KumwambI shadya ARUDISHE VIWANJA alivyonyanganya watu na watoto yatima
 

Machinjio ya viongozi woooooooooooooote wa zanzibar ni DODOMA. sasa hakuna mwenye kuwa na jeuri ya kufanya hayo juu. wao wnabaki hewallah bwana
 
KILE AMBACHO MIKOA MINGI YENYE WATU MARADUFU YA WAZANZIBARI inakitarajia kimeanza kufanywa na Wazanzibari baada ya Waswahili.
Mkuu,
Zanzibar haijwahi kuwa mkoa wala haitakuwa mkoa, au ndo ulivyotumwa useme na Moh'd Seif Khatibu(kibaraka wa Tanganyika)
Tumeanza na mafuta yapo mengi yanafuta sasa huyo Samwel Sitta anaeongoza kigarawa cha Ukumbi, anachokiita Bunge atajuwa kuwa kuzimika kwa kibatari hakuzuwii mapambazuko.
 
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetoa msimamo wake rasmi wa kutaka suala la mafuta na gesi asilia liondolewe katika orodha ya mambo ya muungano.

Uamuzi huo wa serikali umetolewa na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoour Yussuf Himid wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2009/10 katika baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar.

Himid alisema wizara yake iliandaa waraka maalumu kupeleka serikalini wenye kumbukumbu namba Nam. 25/2009 na baadae uliwasilishwa katika kikao cha baraza la mapinduzi febuari 27 2009 ikiwa na azma kamili ya kikao hicho kupata dira na msimamo wa serikali ya Zanzibar katika suala hilo nyeti.

Naomba utulivu mkubwa wajumbe maana hili suala ni nyeti naomba musikilize kwa umakini sana” alisema Spika Kificho baada ya kuona wajumbe wa wa baraza hilo kuwa na shauku kubwa ya kutaka kupiga makofi kwa mfululizo.
Himid aliendeleza kusema kwamba baada ya majadiliano hayo ya wajumbe wa baraza la mapinduzi kwa kuzingatia hoja kikao hicho kilipitisha maamuzi matatu mazito.

Akitayataja maamuzi hayo ni pamoja na ardhi ya bahari ya ndani ya Zanzibar (Territorial waters), maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar sura ya kwanza kifungu 2 (1) ni miliki ya Zanzibar katika maeneo hayo, usimamizi, udhibiti na uendeshaji wa shughuli zote zinazohusiana na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia uwe chini ya usimamizi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Pendekezo la pili ni serikali mapinduzi Zanzibar iwe na chombo chake cha kusimamia mambo yote yanayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na mengineyo yanayoandamana nayo.

Na pendekezo la tatu bahari kuu sehemu ya EEZ serikali inashauri baraza la wawakilishi kukubali mashirikiano na serikali ya muungano wa Tanzania kwa aeneo hilo pekee kwa makubaliano maalumu na sio kwa muundo wa sasa wa taasisi na sheria na kwamba Zanzibar itakuwa mshiriki sawa (equal partner) kwa makubaliano yote yatakayofikiwa kwa eneo hilo la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

“Mheshimiwa Spika maelezo ya baraza la mapinduzi niliwasilisha rasmi mapendekezo hayo matatu katika kikao chako tukufu machi 3 mwaka huu kwa kujadiliwa. Maamuzi ya baraza lako kwa kauli moja kukubaliana na na pendekezo la kwanza na la pili. Pendekezo la tatu lilipingwa na badala yake iliamuliwa kuwa ‘usimamizi na uendeshaji wa shughuli za utafiti na uchimbaji wa amfuta na gesi asilia katika ukanda wa Exlusive Economic Zone (EEZ) bado uwe chini ya mamlaka ya serikali ya mapinduzi Zanzibar’” alisema Himid.

Alisema baraza la mapinduzi juni 9 mwaka huu lilijadili waraka maalumu kutoka wizara hiyo kuhusu yatokanayo na kikao cha baraza la wawakilishi cha aprili 3 2009 na kutoa maamuzi yafuatayo.

“Suala la mafuta na gesi asilia liondolewe katika orodha ya masuala yanayojadiliwa na kamati ya kujadilia kero za muungano, masuala yote yanayohusu mafuta na gesi asilia yatolewe katika orodha ya mambo ya muungano na usimamizi na udhibiti wa rasilimali hio katika maeneo yote ya ardhi (on-shore) na baharini (off-shore) yakiwa pamoja na eneo la EEZ ubaki kuwa chini ya seriakli ya mapinduzi zanziabr pekee” alisema Waziri huyo huku akipigiwa makofi kwa sana.

Baraza la mapinduzi pia imeiagiza wizara kuainisha katika sera na nishati udhibiti wa rasilimali ya mafuta na gesi asilia kwa maeneo ya Zanzibar kama ilivyopendekezwa na baraza la wawakilishi ambao ni wawakilishi wa wananchi.

Pia baraza hilo limeagiza wizara iandae mikakati ya kutayarisha sheria ya mafuta na gesi asilia ya Zanzibar ambayo itafuatiwa na kuanzishwa kwa taasisi zitakzosimamia sekta hiyo ambapo wakati huo huo wizara ichukue hatua za dharura za kuimarisha taaluma ya kusimamia suala la mafuta na gesi asilia visiwani hapa.

“Taarifa, taarifa ya mamauzi haya ya serikali ya mapinduzi Zanzibar iwasilishe katika kikao kitakachofuata cha kujadili kero za muungano kinachopelekwa kule ni taarifa ya maamuzi yetu hatwendi kujadili or na aaa hapana tunakwenda kuwasilisha taarifa na baadae hatua kitakachofuata kitaendelea” alisisitiza Himid.

Amesema kazi inayofuata kwa sasa ni utekelezaji wa maelekezo hayo ya baraza la mapinduzi na kuhakikisha kuwa serikali ya mapinduzi inasimamia na kudhibiti sekta ya mafuta na gesi asilia kwa maslahi ya wazanzibari.

Hata hivyo Waziri Himid amewahakikishia wajumbe hao kwamba wizara yake inaendelea na utaratibu wa kuandaa sera ya nishati ya mafuta na gesi asilia ambapo kwa sasa tayari umeshafikia hatua nzuri ya mafanikio.

“Tunahitaji kuwa na sera na sheria ya mafuta itakayozingatia maslahi ya wazanzibari wote na kuwalinda dhidi ya ufusadi wa nje na wa ndani na ubaguzi miongoni mwao katika kuhakikisha malengo yetu kuhusiana na hilo” alimalizia kusema Waziri huyo.

Aliwaambia wajumbe hao kwamba kwa sasa wameshafikia maamuzi ya kusimamia sekta hiyo wenyewe ambapo alisema kufanya haraka katika zoezi hilo kunaweza kusababisha kuibuka makosa yatakayoleta athari za migogoro kama ambavyo baadhi ya nchi za Afrika hutokezea.

Alisema jambo hilo serikali halitaki litokee na ndio maana imeamua kwenda hatua baada ya hatua kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepusha migogoro itakayoweza kuwepo katika suala zima la nishati.




SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG
 
Kwa mujibu wa "bwan Shemej" Mansour Yussuf Himid, anasema kuwa katika kikao kijacho cha kujadili (hizo blah blah) zinazoitwa kero za Muungano, suala hili halitajadiliwa kama ni kero inayotaka ufumbuzi, bali ni itatajwa kuwa ni Msimamo wa baraza la mapinduzi(zamani la Makomandoo) khalas! the union govt will put it in their pipes and smoke it, kwisha habar!!
 
politics za visiwani bwana!

CUF na CCM wanachukiana weee lakini wana one thing in common.....HAWAUTAKI MUUNGANO sema sasa nani atakayesema hilo wazi?

mambo kama haya ndio utapompendea KAMANDOOO yeye kwenye mambo haya alikuwa hana cha nini wala nini


NGANGARI tuuu
 
Waziri(SMZ) DR. Asha Abdallah Juma anasema hata kama yakipatikana kidogo japo saizi ya kigeleni, yatatosha hayo hayo kwa akina mama wa zanzibar kujipaka walau wapendeze, wan'gare babu we khah!
 
Waziri(SMZ) DR. Asha Abdallah Juma anasema hata kama yakipatikana kidogo japo saizi ya kigeleni, yatatosha hayo hayo kwa akina mama wa zanzibar kujipaka walau wapendeze, wan'gare babu we khah!

Interesting.....
 
Waziri(SMZ) DR. Asha Abdallah Juma anasema hata kama yakipatikana kidogo japo saizi ya kigeleni, yatatosha hayo hayo kwa akina mama wa zanzibar kujipaka walau wapendeze, wan'gare babu we khah!
Kwani mafuta yapo huko kwenu. Hivi nani ameshathibitisha kuwa ameyaona? Kazeni kamba kupalilia mikarafuu yenu, piganeni utalii ukunemeesheni badala ya kuwatononoa wawekezaji tu, limeni mpunga mjitosheleze kwa mtee. Acheni kuota mchana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…