Junius Shirikisho ni muwafaka. Laiti Zanzibar ingekuwa angalau inaikaribia Tanganyika. Hivi Junius Shirikisho la Watu (kule kwetu labda Milioni Moja na Nusu) na wenzetu sijui data zao -sifuatilii- (not interested) Lakini United Republic of Tz ina kama 35 Million hivi sasa. sasa Junius wapi umeona Shirikisho la aina hiyo? Hata ukimfufua Babu yangu (Mshirazi, mtu wa sili ya Mrima, jirani wa Wamakunduchi - na amechuma karafuu Pemba) hakubali hilo wazo.
Unajuwa ukiitazama Zanzibar kwa udogo wake tu, unaweza ukaikosesha mambo mengi na ukaona hai-fit katika mwahala mwingi, nikupe mfno, mwaka 1963 punde tu baada ya Zanzibar kupata uhuru kutoka kwa Muingereza, ikawa ni memba wa Umoja wa Mataifa (UN), katika Baraza kuu la Umoja wa mataifa, Waziri Mkuu wa aliechaguliwa kidemokarasia katika uchaguzi wa kidemokrasia, S.K Moh'd Shamte aliiwakilisha bendera na taifa huru la Zanzibar, pamoja na mataifa mengine makubwa kieneo na kimamlaka, lakini Zanzibar ilikuwa sawa katika fursa na haki nyengine kama memba wengine wote,bila kujali udogo wake wa eneo wala idadi ndogo ya watu wake. Kama imeweza ku qualify katika vigezo vya haki na usawa katika duru kama hizo za kimataifa bila kujali hayo unayosema ya udogo wa eneo na uchache wa watu wake, kwanini vigezo hivo vishindwe katika ngazi za kitaifa, ilhali kuna taratibu na sheria tutakazokubaliana kuzifuata kwa matakwa ya wananchi.Kama wazo la serikali tatu au shirikisho ni mufaka ni wananchi watakao pendekeza namna bora ya makubaliano ya utendaji wa serikali hizo , haitakuwa kama mara ya kwanza wakati Nyerere alikuwa na wataaalamu wa sheria, Karume alikuwa na walevi na wahuni tu, hata mwanasheria wa serikali Dourado wakati huo hakujuwa kinaendelea nini,anashtukia tu muungano huo!! tukapigwa bao!!!
Pakacha, fursa hiyo itakuja Mw'mungu akipenda na wazanzibar hawatokubali kuruka kisima mara mbili.