Bila option ya serikali moja, poll hii ni batil!
Mode tunaomba utuongezee option ya ya serekali moja tafadhali...
Not much I can do from here, I have no option to edit the poll.

Cheers
 

Ni kweli kila kitu kinazungumzika, lakini unahitaji kuwapatia watu imani wazanzibari kama kweli serekali moja itakuwa ni suluhisho la muungano huu.

Tuletee sababu za msingi kwanini serekali moja iwe ndio suluhisho.Mie napenda kutizama mifano ya watu walioendelea halafu wakati mwengine kuiga yale yaliyo mazuri ili na mie nifikie malengo yangu.

Mfano wa UK, ni mzuri sana kuigwa na kutekelezwa hapa Tanzania.Kila nchi katika muungano huo, ina uhuru wake na kila mwananchi bado anaendelea kutumia uraia wake kwa passport ya UK. (kama sijakosea hapo).

Sasa ni kwanini munafikiria serekali moja ni suluhusiho, wakati hao waliofanikiwa na miungano kama UK hawajafanya hivyo?

Hapa tujue centralization, ni sawa na ujamaa.Yaani nakusudia, kukusanya kila kitu na kukiweka kwenye mamlaka moja unaondosha ushindani na kudumaza uchumi.Kwa akili yangu hili suala la serekali moja aidha limeambatana na akili za kijamaa au dhana potofu ya Tanganyika kuona kama visiwa vya Zanzibar ni sehemu ya eneo lake...au dharau ya kusema nchi ya Zanzibar ifutwe tuu na iwe mkoa!

Katika tatizo moja sugu linazodumaza uchumi wa Tanzania, ni kujikumbizia madaraka.Wenzetu hadi skuli basi zina mamlaka kamili ya kuendesha mambo yake na kuingia sokoni kusaka wanafunzi.Wakati hili ndio kwanza majuzi tuu Tanzania tumeanza, bado kuna maskuli mingi tuu ya serekali hayajashirikishwa katika mchakato wa sokoni na kutafuta wanafunzi.

Sasa ni kwanini tutake kuchukua principle ya serekali moja, badala ya kusema kila mkoa uwe na serekali na mamlaka kamili ya kuendesha maendeleo katika mkoa wake?Same theory applies to Zanzibar, ibakie na serekali yake ya kuendesha mambo yake ya ndani.
 
Muungano huu hautatusaidia chochote kwa vile tunaonekana hatuaminiani. Hata tukiwa na serikali tatu bado tutasumbuana tu kwa kudai proportions ambazo hazitakuwa na maana yoyote. Ni afadhali kila taifa liendelee ki vyake vyake.
 
Habari zenu wana JF,

Tunaomba maoni yenu wana JF kwenye mchakato mzima wa mfumo gani wa muungano watanzania wanaupendelea.

Thanks guys...

Mfumo wa Muungano ninaoupendelea ni;
1. Muungano wa kweli usiwo na ulaghai ndani yakwe!
2. Muungano ambao kila upande una haki sawa katika mambo ya Muungano!
3. Muungano ambao kila upande unajiamulia mambo yake na isiwe Kizota ni ya wote!
4. Muungano ambao ubabe hautowekwa mbele eti kwa vile mmoja ni mdogo na mwengine ni mkubwa!
5. Muungano ambao wananchi wa pande zote watashirikishwa katika kuamuwa uwe wa namna gani, serikali moja, tatu , saba au kusiwe na Serikali ya Muungano
6. Muungano ambao sehemu moja haimnyonyi nyengine kwa vile kila mmoja amepangiwa majukumu yake na anayatekeleza>
7. Muungano ambao watakaoshiriki katika mchakato wawe na daraja moja la uelew(Kisomo) sio kama 1964 mmoja ana elimu ya ukuli.
8.Muungano ambao rasilimali za upande mmoja ziwe ni zao na wanachotakiwa kutowa ni michango iliyokubaliwa.

Kwa kuanzia nafikiri Muungano ungekuwa hivi na masuala ya Serikali ngapi isingekuwa tatizo kwani katika kuutekeleza huo Muungano wa Kitaalamu ndio kutakoamuwa tunakuwa na Serikali ngapi na zinaendeshwa vipi. Hili suwala la kuweka mbele utashi wa mtum au kikundi (Nyerere na hamu ya Serikali moja) ndio uliotufikisha hapa kwani tuliliwanzia la mwisho tukawacha kufanya ya msingi na sasa tunalazimisha mambo yasiyowezekana.
 

Ndugu yangu nafikiri hakuna jambo la binaadamu lisilo na kasoro lakini binaadamu huwa wanajadiliana na kukubaliana nasi kama tunautaka Muungano basi na tujadiliane na wala tusilazimishane.

Ama hili la kulazimisha Serikali moja nionavyo mimi si Muungano bali itakuwa kumezana. Kuungana unakotaka wewe kungewezekana kama sehemu zote zingelingana lakini mbona tofauti ni sawa na mbingu na ardhi? Hapa lazima kuwepo utaratibu fulani ili kuona kuwa haki inatendeka. Haki hapa inahitajika kulingana na uhusiano wa Kidunia ambao hadhi na haki ya nchi haipimwi kwa ukubwa wa eneo au wingi wa watu bali hupimwa kwa mipaka. Hata kama kaeneo kadogo lakini kina mipaka ni nchi na inakuwa sawa na Bonge la eneo lenye mipaka pia. Sasa dhana ya wengi wa upande mmoja wa Muungano ni kuwa Maadam sehemu moja ni ndogo iweje ipewe hadhi sawa na ile ya pili. Hapa ndipo mnapokosea na ndio chanzo cha maovu mengi dhidi ya wenzenu.
Ama hili la kujidai kuwa nchi ulimwenguni zinaungana badala ya kugawanyika sijuwi umelipata wapi na lina maana wapi? Sijasikia nchi hata moja hata huko ulaya ambayo imegawa soverignity yake kwa Taifa jengine na badala yake mataifa yanaongezeka. Tunajaribu kuwadanganya wasiojuwa kwa kitu chengine kabisa, Kweli kuna majumuiya kama ya Ulaya lakini hii ni majumuiya ya Kiuchumi na wala si ya Kisiasa.
Tunataka Serikali moja kwa Tanzania kwa kisingizio cha kuwa nchi zinaungana duniani, mbona Federation ya Afrika Mashariki tumeikataa iwapo Muungano wa kutawaliwa ni mzuri?
 
Kibunango, uko wapi? Mimi nadhani kuwa wewe ni Mzenjibari na nilitegemea maoni yako hapa. Au unachelea maoni yako yasionekane na Wana-maskani wa Kisiwandui? Toa maoni yako bana au kwa kuwa hii thread haiusiani na mambo ya kikubwa?
 

Mbona kura yako haionekani?

Vyovyote iwavyo, kwa maoni yangu wewe ni mtu mwenyewe mawazo mgando.Kama kungelikuwa hakuna matatizo usingeliona mijadala ya muungano ikiibuka kila leo katika nchi.

Sioni ubaya wowote kwa mzanzibari kujivunia utaifa wake, hata waingereza hadi leo wanajivunia utaifa wao Irish, Scotish, Wales....sasa Tanganyika kuwa hawapendi kutumia utaifa wao ni kosa la Nyerere pengine na wananchi wake kufurahi hilo.

Lakini hii sio hoja ya msingi kusema na wengine wafuate kila Tanganyika inachopendelea.
 
tatizo la muungano wa Tanzania si mfumo (unaweza ukawa na mfumo wowote ule wa moja, mbili, tatu, nne hata kumi). Tatizo la Muungano wa Tanzania ni uetekelezaji wa kile kilichokubaliwa (kwa dhati na kwa uwazi). Wewe si unaona hapa kila kitu ni shaghala baghala mpaka samaki wa Magufuli ni shagala bagala. Tunachotakiwa ni kujifunza kuwa waadilifu katika utekelezaji wa tunayokubaliana. Na pahala pazuri pa kuanza kujifunzia ni hapa hapa tulipo. Tujirekebishe. Kama tumeamua kuwepo kwa Zanzibar basi na iwepo Zamzibar (tena iheshimike ndani ya Muungano). Na kama tumeamua kuifuta Tanganyika basi tuwe tumeifuta Tanganyika (isiwemo midomoni mwa watu tena kwa mwamvuli wa Tanzania).
 
Habari zenu wana JF,

Tunaomba maoni yenu wana JF kwenye mchakato mzima wa mfumo gani wa muungano watanzania wanaupendelea.

Thanks guys...

MrFroasty,

1: Serikali kuu moja ya muungano (Federal)

Halafu:

Serikali za majimbo 11; serikali za majimbo 9 upande wa Bara na upande wa Visiwani kukiwa na serikali mbili za majimbo (Jimbo la Unguja na Jimbo la Pemba)

Sina la kuongeza.

Amani.
 
tatizo la muungano wa Tanzania si mfumo (unaweza ukawa na mfumo wowote ule wa moja, mbili, tatu, nne hata kumi). Tatizo la Muungano wa Tanzania ni uetekelezaji wa kile kilichokubaliwa (kwa dhati na kwa uwazi)

Pakacha,
Utekelezaji unakuwa mgumu kwa sababu ya matatizo ya mfumo wenyewe wa muungano. Kama ingalikuwa serikali moja, kuna baadhi ya matatizo wala yasingejitokeza. Vivyo hivyo kama tungalikuwa na serikali tatu kuna baadhi ya matatizo tungeyaepuka. Kitendo cha serikali ya JMT kufanya mambo yanayohusu Tanzania pamoja na Tanganyika kinaleta mikanganyiko mingi tunayoishuhudia.
 
SMU. Tanganyika haipo.kwa mujibu wa mfumo wetu. sasa wewe unalazimisha iwepo. Ndipo hapo watu wanapokosea katika utekjelezaji. Na wengine hukosea zaidi kwa kukataa kuwepo kwa Zanzibar (na mambo yake) wakati tumekubaliana iwepo. Tuna matatizo ya kiutekelezaji lakini mfumo wa mbili ni safi tu na unatekelezeka. Nasikitika kuwa hata viongozi wenyewe wakuu (wakiwemo jopo la waasisi) walikuwa wakiteleza katika utekelezaji. Na ndio maana katika miaka ya l980's na l990's kukajitokeza hisia pevu za kuwa na Serikali Moja na pia kuwa na Serikali Tatu (refer sakata la Mzee Jumbe)
 

Mungu wetu hawamjui kwa kuwa Mungu wetu na allah wao ni watu wawili tofauti kabisa. Sasa wanawezaje kumcomment Mungu wetu wasiomjua na hawatamjua ila kwa neema tu.

Ingekuwa vema kama jamaa angesema kuwa Yesu siyo Allah ila ni Mungu wa wakristo
 

Tatizo la Muungano lipo katika hatuwa ya mwanzo ya kuundwa Muungano huo. Haiwezekani matakwa ya watu wawili tu kuwa kigezo cha makubaliano yanayowahusu mamilioni ya watu.
Tatizo linakuja hasa kwa upande wa Zanzibar kwani wao ndio waliopoteza Utaifa wao. Watanganyika kwao jina si kitu wakati wanamiliki kila kitu ambacho Tanganyika ilikuwanacho. Wana uhuru wa kuamuwaq walitakalo liwe la humuhumu ndani au liwe linahusu mahusiano ya Kimataifa wakati Zanzibar waombe ruhusa kwa hao hao Watanganyika.
Sijuwi kwa mantiki gani unasema kuwa wafuatwe yaliyokubaliwa wakati Zanzibar hamna usemi wowote wa yaliyokubaliwa na yanayoamuliwa.
Hapana! Tunataka muundo wa Muungano utakaotuweka pamoja na kwa hadhi moja ili tuamuwe mambo yanayotuhusu sote.
 
Mods tunaomba option ya serikali moja ili poll ikamilike vinginevyo tutakuwa tumeiminya demokrasia na matokeo yatakuwa biased. Mimi na-opt serikali moja lakini siwezi kupiga kura au sina ZaID utambulisho wa ukaazi. Zanzibar uwe mkoa na Pemba uwe mkoa jumla tuwe na mikoa 23. Kusiwe na ma-RC tuwe na Governor.
 

Off point
 
Mungu wetu hawamjui kwa kuwa Mungu wetu na allah wao ni watu wawili tofauti kabisa. Sasa wanawezaje kumcomment Mungu wetu wasiomjua na hawatamjua ila kwa neema tu.

Ingekuwa vema kama jamaa angesema kuwa Yesu siyo Allah ila ni Mungu wa wakristo

Off point..nyie mkoje? muugano na signature wapi na wapi?
 



Ni tabu kupata kila ulitakalo na hiyo ingewezekana ningeomba option ya serikali 25 (kila mkoa na yake) nayo iorodheshwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…