MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 595
Mode tunaomba utuongezee option ya ya serekali moja tafadhali...Bila option ya serikali moja, poll hii ni batil!
Not much I can do from here, I have no option to edit the poll.
Cheers
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mode tunaomba utuongezee option ya ya serekali moja tafadhali...Bila option ya serikali moja, poll hii ni batil!
Mkuu hayo yote yanazungumzika,ili mradi tuu mjadala uwe mpana ili kujitahidi kuziba mianya yote inayoleta migogoro na matatizo katika muungano wetu.Ingawa mie sio mzanzibar ila niliishi zanzibar na ninafanya kazi katika serikali ya mapinduzi,kwa mtazamo wangu serikali moja inaweza kuwa option nzuri zaidi.Tuikarabati katiba yetu ya muungano ili iweze kutoa majibu ya maswali na madukuduku yanayotusimbua,hakuna kusichowezekana.
Habari zenu wana JF,
Tunaomba maoni yenu wana JF kwenye mchakato mzima wa mfumo gani wa muungano watanzania wanaupendelea.
Thanks guys...
Ok, nashukuru kwa ushauri ndugu! Naomba tuendelee na mjadala kuhusu Muungano! Najua watu wanapenda mabadiliko ya mara kwa mara. Wanapenda waone Muungano ukichukua sura mpya, only that! Wengine wanataka wajitwalie madaraka kupitia mabadiliko hayo ya Muundo wa Muungano. Lakini mimi nionavyo hata kama kutakuwa na Tatu, Nne hata zaidi, hakutaondoa matatizo tuliyo nayo! Ni afadhali basi tuwe na Serikali moja kuliko kuzidi kugawanyika! Dunia sasa hivi inazidi kuungana, huku sisi tunazidi kugawanyika kila leo. Tunahitaji basi kurekebisha mind set zetu kama watanzania, tusipelekeshwe na wanasiasa ambao wana "ulterior motives!"
mfumo wa serikali mbili uendelee.
mfumo huu hauna tatizo. matatizo mnayoyaona sasa ni matokeo ya ulegevu wa uongozi. wazanzibari wanapaswa kujisikia kama watanzania zaidi kuliko wazanzibari zaidi. viongozi wa kisiasa wana wajibu wa kuhaasisha umma na sio kuchochea hisia za upande mmoja wa muungano kupuuzwa au kuonewa.
kwa ujumla, watanzania wa bara wamepiga hatua kubwa sana katika kuukubali muungano kwani ni wachache sana bado wana kumbukumbu ya kitu kinaitwa tanganyika, wakati tanzania visiwani kila mtu anajijua kuwa ni mzanzibari! hapo ndio mama wa haya matatizo ya mpasuko wa kisiasa anapozaliwa
tatizo la muungano wa Tanzania si mfumo (unaweza ukawa na mfumo wowote ule wa moja, mbili, tatu, nne hata kumi). Tatizo la Muungano wa Tanzania ni uetekelezaji wa kile kilichokubaliwa (kwa dhati na kwa uwazi). Wewe si unaona hapa kila kitu ni shaghala baghala mpaka samaki wa Magufuli ni shagala bagala. Tunachotakiwa ni kujifunza kuwa waadilifu katika utekelezaji wa tunayokubaliana. Na pahala pazuri pa kuanza kujifunzia ni hapa hapa tulipo. Tujirekebishe. Kama tumeamua kuwepo kwa Zanzibar basi na iwepo Zamzibar (tena iheshimike ndani ya Muungano). Na kama tumeamua kuifuta Tanganyika basi tuwe tumeifuta Tanganyika (isiwemo midomoni mwa watu tena kwa mwamvuli wa Tanzania).Mfumo wa Muungano ninaoupendelea ni;
1. Muungano wa kweli usiwo na ulaghai ndani yakwe!
2. Muungano ambao kila upande una haki sawa katika mambo ya Muungano!
3. Muungano ambao kila upande unajiamulia mambo yake na isiwe Kizota ni ya wote!
4. Muungano ambao ubabe hautowekwa mbele eti kwa vile mmoja ni mdogo na mwengine ni mkubwa!
5. Muungano ambao wananchi wa pande zote watashirikishwa katika kuamuwa uwe wa namna gani, serikali moja, tatu , saba au kusiwe na Serikali ya Muungano
6. Muungano ambao sehemu moja haimnyonyi nyengine kwa vile kila mmoja amepangiwa majukumu yake na anayatekeleza>
7. Muungano ambao watakaoshiriki katika mchakato wawe na daraja moja la uelew(Kisomo) sio kama 1964 mmoja ana elimu ya ukuli.
8.Muungano ambao rasilimali za upande mmoja ziwe ni zao na wanachotakiwa kutowa ni michango iliyokubaliwa.
Kwa kuanzia nafikiri Muungano ungekuwa hivi na masuala ya Serikali ngapi isingekuwa tatizo kwani katika kuutekeleza huo Muungano wa Kitaalamu ndio kutakoamuwa tunakuwa na Serikali ngapi na zinaendeshwa vipi. Hili suwala la kuweka mbele utashi wa mtum au kikundi (Nyerere na hamu ya Serikali moja) ndio uliotufikisha hapa kwani tuliliwanzia la mwisho tukawacha kufanya ya msingi na sasa tunalazimisha mambo yasiyowezekana.
Habari zenu wana JF,
Tunaomba maoni yenu wana JF kwenye mchakato mzima wa mfumo gani wa muungano watanzania wanaupendelea.
Thanks guys...
tatizo la muungano wa Tanzania si mfumo (unaweza ukawa na mfumo wowote ule wa moja, mbili, tatu, nne hata kumi). Tatizo la Muungano wa Tanzania ni uetekelezaji wa kile kilichokubaliwa (kwa dhati na kwa uwazi)
SMU. Tanganyika haipo.kwa mujibu wa mfumo wetu. sasa wewe unalazimisha iwepo. Ndipo hapo watu wanapokosea katika utekjelezaji. Na wengine hukosea zaidi kwa kukataa kuwepo kwa Zanzibar (na mambo yake) wakati tumekubaliana iwepo. Tuna matatizo ya kiutekelezaji lakini mfumo wa mbili ni safi tu na unatekelezeka. Nasikitika kuwa hata viongozi wenyewe wakuu (wakiwemo jopo la waasisi) walikuwa wakiteleza katika utekelezaji. Na ndio maana katika miaka ya l980's na l990's kukajitokeza hisia pevu za kuwa na Serikali Moja na pia kuwa na Serikali Tatu (refer sakata la Mzee Jumbe)Pakacha,
Utekelezaji unakuwa mgumu kwa sababu ya matatizo ya mfumo wenyewe wa muungano. Kama ingalikuwa serikali moja, kuna baadhi ya matatizo wala yasingejitokeza. Vivyo hivyo kama tungalikuwa na serikali tatu kuna baadhji ya matatizo tungeyaepuka. Kitendo cha serikali ya JMT kufanya mambo yanayohusu Tanzania pamoja na Tanganyika kinaleta mikanganyiko mingi tunayoishuhudia.
1. "Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." (Yoh. 1:1)
2. "Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa BWANA Mwenye Nguvu utatimiza haya." (Isa. 9:2, 6-7).
tatizo la muungano wa Tanzania si mfumo (unaweza ukawa na mfumo wowote ule wa moja, mbili, tatu, nne hata kumi). Tatizo la Muungano wa Tanzania ni uetekelezaji wa kile kilichokubaliwa (kwa dhati na kwa uwazi). Wewe si unaona hapa kila kitu ni shaghala baghala mpaka samaki wa Magufuli ni shagala bagala. Tunachotakiwa ni kujifunza kuwa waadilifu katika utekelezaji wa tunayokubaliana. Na pahala pazuri pa kuanza kujifunzia ni hapa hapa tulipo. Tujirekebishe. Kama tumeamua kuwepo kwa Zanzibar basi na iwepo Zamzibar (tena iheshimike ndani ya Muungano). Na kama tumeamua kuifuta Tanganyika basi tuwe tumeifuta Tanganyika (isiwemo midomoni mwa watu tena kwa mwamvuli wa Tanzania).
1. "Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." (Yoh. 1:1)
2. "Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa BWANA Mwenye Nguvu utatimiza haya." (Isa. 9:2, 6-7).
Mungu wetu hawamjui kwa kuwa Mungu wetu na allah wao ni watu wawili tofauti kabisa. Sasa wanawezaje kumcomment Mungu wetu wasiomjua na hawatamjua ila kwa neema tu.
Ingekuwa vema kama jamaa angesema kuwa Yesu siyo Allah ila ni Mungu wa wakristo
Mods tunaomba option ya serikali moja ili poll ikamilike vinginevyo tutakuwa tumeiminya demokrasia na matokeo yatakuwa biased. Mimi na-opt serikali moja lakini siwezi kupiga kura au sina ZaID utambulisho wa ukaazi. Zanzibar uwe mkoa na Pemba uwe mkoa jumla tuwe na mikoa 23. Kusiwe na ma-RC tuwe na Governor.
tuendelee na huu huu!...
Mbona kura yako haionekani?
......................................................