Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Ila awamu hii, Tanganyika imeingia choo cha kike.
Waswahili tunasema "usiyempenda kaja"
 
Natoa tu angalizo

Maana naona Mjadala wa Tanganyika unashika kasi kana kwamba ni Jambo jema kumbe ndio kuharibu zaidi

Muungano ukivunjika na Bandari huna ndio itakuwa nini!!!

Kuweni wenye kutafakari!

cc: Daudi Mchambuzi- Machame
Si ndivyo mnataka? Nakuhakikishia in case of kuvunjika Muungano tutaanza hapa kuulizana wewe msukuma wewe mchaga huu ni unabii unaoishi.
 
Ni kweli kabisa. Tukianza kubaguana hatutakaa tuache mpaka nchi isambaratike kabisa.
Lakini kuna maamuzi viongozi wanafanya inapelekea watu kutoa maneno makali sana.
Hili la bandari linashangaza sana, kwenye mambo mengine ya maendeleo tunakumbushana kushirikiana na wenzetu wa visiwani. Ila la Dp World (ambalo tumeambiwa lina manufaa makubwa) hatuwashirikishi. Watu wanafikia conclusion gani? Utawalaumu?
Hawa viongozi wajitafakari sana, nchi ikisambaratika sijui watajiongoza wenyewe?
Hiyo bandari iko karibu zaidi Zanzibar kuliko mkoani kwenu kwa maana hiyo km ni ubaguzi hiyo bandari wala haikuhusu. Msitake kuonja sumu ninyi vijana
 
Ila awamu hii, Tanganyika imeingia choo cha kike.
Waswahili tunasema "usiyempenda kaja"
Tanganyika na Zanzibar ziliingizwa Vyoo vya Kike na Nyerere na Karume usitafute mchawi mwingine.

Nyerere alikimbilia kuchanganya mchanga bila kuwauliza Watanganyika hali kadhalika Karume.
 
Tanganyika na Zanzibar ziliingizwa Vyoo vya Kike na Nyerere na Karume usitafute mchawi mwingine.

Nyerere alikimbilia kuchanganya mchanga bila kuwauliza Watanganyika hali kadhalika Karume.
Wewe endelea kuwasingizia wafu ilhali wao waliwaachia nchi ziko salama kabisa, ujinga wenu wa kuendekeza siasa za kijinga-kijinga ndiyo unalitumbukiza hili taifa shimoni. Ukiendelea hivi utalaumu kila kitu kwa Nyerere na Karume wakati umeufumbia macho ukweli mchungu kwamba Raisi Samia hawezi kuvaa viatu vya uraisi. Nchi siyo vicoba
 
Utajua hujui

Mbowe atarudi Malawi
Nyerere aliondoa Uchifu Hangaya anarudisha Uchifu acheni kuchezea akili za watu.

Nyerere alisema Uchifu utatugawa na utaleta Ukabila acheni hizo scare tactics dhidi ya Wananchi wenu.
 
Back
Top Bottom