Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Muungano wetu mzuri sana lakini Kuna mambo tunaitaji kuelimishwa

1.kwa nini mtanganyika harushusiwi kuwa kiongozi kule Zanzibar...
Anaweza. Mbona Ali Hassan Mwinyi na Hussein Mwinyi wameweza kuongoza? Soma historia ya Mwinyi utajua alikozaliwa siyo visiwani bali Kivure pale mkoani Pwani.
 
Kumiliki Ardhi mpaka uwe na kitambulisho cha Mzanzibari.

Sio ngumu kukipata.

Kwa urahisi zaidi vinatolewa ovyo na bure kipindi cha uchaguzi ili wapate kura za watu wa bara ambao huenda wakaipa ssiemu kura, mzenji wa kawaida hata hao wanaovaa kijani hawatoi kura ssiemu.

Vizieni hicho kitambulisho kabla ya uchaguzi mkuu ili mpate kumiliki Ardhi zenji.
 
Anaweza. Mbona Ali Hassan Mwinyi na Hussein Mwinyi wameweza kuongoza? Soma historia ya Mwinyi utajua alikozaliwa siyo visiwani bali Kivure pale mkoani Pwani.
Muongo mkubwa.
Mwinyi ni Mzanzibari, aliongoza Zanzibar kama Mzanzibari, kama aliovyoongoza Mzee Abeid Karume mzaliwa wa Malawi.
Wote wawili na wengine wengi wamepata Uzanzibar kwa sababu nchi imepatikana wakiwa pale pale (Mapinduzi 1964) hivyo waafrika wote waliokuwa kwenye Ardhi hio ndio wananchi.
 
Muongo mkubwa.
Mwinyi ni Mzanzibari, aliongoza Zanzibar kama Mzanzibari, kama aliovyoongoza Mzee Abeid Karume mzaliwa wa Malawi.
Wote wawili na wengine wengi wamepata Uzanzibar kwa sababu nchi imepatikana wakiwa pale pale (Mapinduzi 1964) hivyo waafrika wote waliokuwa kwenye Ardhi hio ndio wananchi.
Muongo wewe. Lakini bado hao si wazanzibari na umekiri mwenyewe.
 
Muongo wewe. Lakini bado hao si wazanzibari na umekiri mwenyewe.
Mzanzibari wa kweli ni Mreno aliekaa miaka 400.
Waarabu na waingereza waliomuweka Sultani feki miaka 130.
Nyie weusi wabana pua wa leo mlioletwa na Tippu Tipp toka unyanini kwenu Congo miaka 50 baada ya Nyerere kuikomboa ZNZ
Hivyo Wareno waje kuchukua visiwa vyao.
 
Muungano wetu mzuri sana lakini Kuna mambo tunaitaji kuelimishwa

1.kwa nini mtanganyika harushusiwi kuwa kiongozi kule Zanzibar?

2.je mtanganyika anaruhusiwa kumiliki ardhi kule Zanzibar?
3.je mwanafunzi anaruhusiwa kusoma kule bila kuwa na resident permit?

4.kwa nini mzanzibar anaruhusiwa kuwa kiongozi huku Tanganyika hususani raisi au waziri?

5.Why bandari ya Dar imekodishwa na si bandari ya Zanzibar?

6.why gharama za ushuru kule bandari ya Zanzibar ni ndogo compared to DAR port?

7.je huwa tunagawana mapato sawasawa
Do you know the meaning of a saying which says yours is mine, and mine is mine!? This is all about the useless Union between Tanganyika and Zanzibar.
 
Zanzibar na Tanganyika ni majirani kama ilivyo Kenya. Katiba ya Zanzibar haitambui Mkenya wala Mtanzania bara. Inawatambua raia wake Wazanzibar peke yao daima dumu tena wenye vitambulisho rasmi vya Uzanzibar.

Kutokana na mijadala mingi mitandaoni Muungano wetu ulipofikia kugeuka nyuma ni sawa na reverse ya Boeng 670 angani. Mijadala mingi inagusia suala la mipaka thabiti kwenye masuala ya na yasiyo ya muungano kila upande.

Habari ya mzanzibar kuwa waziri kiongozi kwenye masuala yasiyo ya muungano ya huku bara yasiwepo. Mfano kwa sasa Waziri na Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi wa upande wa Tanganyika wanatokea Zanzibar wakati sio suala la muungano.

Hivyo itapendeza sana Waziri na katibu mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi wakawa watanganyika wenyewe. Wazanzibar wabakie kwenye wizara za masuala ya muungano ambazo ni masuala ya;
  • Fedha
  • Ulinzi
  • Ndani
  • Nje

Mengineyo yote kila upande uheshimu mipaka ya jirani yake. Ukizingatia kwamba kule Zanzibar kuna SMZ na SMZ ni ya wazanzibar peke yao daima dumu.

Wazanzibar wana vitambulisho viwili, cha Uzanzibar kwa ajili ya Zanzibar na cha Utanzania (NIDA) kwa ajili ya upande wa Tanganyika. Kule Zanzibar NIDA haina umuhimu wowote sio ajira wala chochote.

Kule Zanzibar ni kitambulisho cha Uzanzibar pekee ndio kinatumika kwenye rasilimali na maswala yote ya SMZ.

Wana serikali mbili ya SMZ na JMT.
Wana kitu mara mbili mbili.
 
Hizi bandari zinakuwaje za muungano sasa hadi zifanyiwe maamuzi makubwa na wazanzibari? ikiwa zanzibar wana sheria yao ya bandari ambayo imefanya mkataba wa DP world kutogusa bandari za zanzibar. Hii ina maana kwamba maamuzi yanayofanywa na wazanzibari kwenye swala la bandari za Tanganyika ni batili.​
 
Mtanganyika ana haki gani kule Zanzibar ???
Katiba na kila kitu cha Zanzibar kimemtenga hivyo mtanganyika hatambuliwi na SMZ kwa kila kitu
Kule Zanzibar hakuna muungano kuna Uzanzibar chini ya SMZ
 
Hata kuwa mjumbe wa nyumba 10
Kuwa office attendant wa taasisi zote za SMZ lazima uwe ZAN ID

NIDA mwisho bandari ya bara
 
siku watanganyika watakapojua ukweli huu kupitia utandawazi ndio watapoidai kwa nguvu zote Tanganyika yao ambao itakuwa imeuza kila kitu kuanzia makaa ya mawe ardhi bandari madini na kila kitu
Wakati huo wazanzibar kila kitu chao sio cha muungano na kipo salama saliminj chini ya SMZ kwa maslani mapana ya Wazanzibar peke yao daima dum
 
Kumiliki Ardhi mpaka uwe na kitambulisho cha Mzanzibari.

Sio ngumu kukipata.

Kwa urahisi zaidi vinatolewa ovyo na bure kipindi cha uchaguzi ili wapate kura za watu wa bara ambao huenda wakaipa ssiemu kura, mzenji wa kawaida hata hao wanaovaa kijani hawatoi kura ssiemu.

Vizieni hicho kitambulisho kabla ya uchaguzi mkuu ili mpate kumiliki Ardhi zenji.
Umiliki Ardhi ili iweje?
Eneo lote la ardhi ya Zanzibar ni sawa na wilaya ya Kinondoni, hoja ni kuwa na Ardhi ya kufanyia uzalishaji na kilimo au ilimradi tuu uwe na ardhi zenji?
Mbona sisiwenyewe tunakuja Kutafuta Ardhi Huko bara kwa ajili ya kilimo na uwekezaji kwa sababu ya ufinyu wa ardhi zenji, wewe unaifanya hii kuwa ni hoja, Uko sawa?

Tanganyika Imeikalia Zanzibar haiwezi kujiendeleza kiuchumi kwa mwamvuli wa kupata kwanza ruhusa ya Muungano ambayo ndiyo Tanganyika.
Wakikataa wao tunabaki masikini.
Ndio maana Zenji ni kisiwa Masikini pamoja na Ukubwa wa Bahari yake, Uwepo wa Mafuta na Gesi na mambo ya Bandari.
kizuizi Muungano hawatoi kibali kuendelezwa.
You see the Problem?
 
Wazanzibar mambo yao yako mezani mengine yameshatatuliwa ila Watanganyika mambo yao yapo moyoni,watu namna hiyo wakija kugeuka ni wabaya sana.
 

Attachments

  • VID-20230614-WA0517.mp4
    8.3 MB
Muungano huu sio msahafu unaweza kuvunjwa mm binafsi si muumini wa muungano huu wa hovyo usio na kichwa wala miguu,unavunjikaje au unaendeleaje? Ni kwa watawala kutoa fursa ya kuendesha kura ya maoni-referendum ili kuamua iwapo wanataka kuendelea na muungano huu au la,tatizo kubwa hapa Tz ni watawala kuamua hatma ya nchi badala ya wananchi,Kulifanyika kosa kubwa ni Nyerere na Karume kutuuza bila ridhaa yetu,duniani kote muungano baina ya nchi na nchi huamuliwa au kukataliwa na wananchi,hapa kwetu tunakatazwa kwa nguvu zote kuzungumzia kuvunja muungano ,hili ni kosa kubwa watawala wetu wanalifanya ipo siku Wananchi watapewa fursa hiyo na viongozi wanaojielewa,kwa sasa mlango umefunga na kufuri nzito
 
1. Wametaka kuwagawa kidini lakini mmekataa mkabaki wamoja
2. Wametaka kuwagawa kiitikadi (kivyama) hakika mmegoma mkaungana
3. Wametaka kuwagawa kikanda ; mmegoma

Asanteni sana . Hii nchi ni yetu. Tuilinde mali yetu.

Wamefaulu kutugawa Watanganyika na Wazanzibar. Wote wanaoshabikia kuuzwa ni wazanzibar. Hatuwachukii ila tumezijua rangi zao.

Ukimya wa Chongolo, Dr. Mpango, Majaliwa Majaliwa, Polepole, Bashiru ni furaha kwetu.

Tanganyika imara itajengwa na watanganyika imara.
 
Back
Top Bottom