Zanzibar na Tanganyika ni majirani kama ilivyo Kenya. Katiba ya Zanzibar haitambui Mkenya wala Mtanzania bara. Inawatambua raia wake Wazanzibar peke yao daima dumu tena wenye vitambulisho rasmi vya Uzanzibar.
Kutokana na mijadala mingi mitandaoni Muungano wetu ulipofikia kugeuka nyuma ni sawa na reverse ya Boeng 670 angani. Mijadala mingi inagusia suala la mipaka thabiti kwenye masuala ya na yasiyo ya muungano kila upande.
Habari ya mzanzibar kuwa waziri kiongozi kwenye masuala yasiyo ya muungano ya huku bara yasiwepo. Mfano kwa sasa Waziri na Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi wa upande wa Tanganyika wanatokea Zanzibar wakati sio suala la muungano.
Hivyo itapendeza sana Waziri na katibu mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi wakawa watanganyika wenyewe. Wazanzibar wabakie kwenye wizara za masuala ya muungano ambazo ni masuala ya;
Mengineyo yote kila upande uheshimu mipaka ya jirani yake. Ukizingatia kwamba kule Zanzibar kuna SMZ na SMZ ni ya wazanzibar peke yao daima dumu.
Wazanzibar wana vitambulisho viwili, cha Uzanzibar kwa ajili ya Zanzibar na cha Utanzania (NIDA) kwa ajili ya upande wa Tanganyika. Kule Zanzibar NIDA haina umuhimu wowote sio ajira wala chochote.
Kule Zanzibar ni kitambulisho cha Uzanzibar pekee ndio kinatumika kwenye rasilimali na maswala yote ya SMZ.
Wana serikali mbili ya SMZ na JMT.
Wana kitu mara mbili mbili.