Akimtambua kuwa Rais, yale mazungumzo yote hayana maana kwa sababu msingi wake ulikuwa ni kusawazisha uwanja wa mapambano katika uchaguzi. Sasa na wewe inabidi tukuulize, kama Seif atamtambua Karume kuwa Rais, kwa nini wafanya mazungumzo ya mwafaka?
inaonekana umelewa au mawazo yako ni mgando..
Mbowe amegombea uraisi kwa mara ya kwanza mwaka 2005...
Rudi kwenye baa uwaambie wakurudishie pesa yako maana inaonekana wamekuuzia pombe ya kienyeji.
Duh.. lakini hapa kuna vichekesho vya mwaka. Kenya Odinga alisema hamtambui Kibaki kuwa Rais lakini leo hii wanakaa meza moja na mmoja baada ya kutengenezewa cheo (Uwaziri Mkuu) anamuita Kibaki Mr. President. So haya mambo ya never say never ni ya kweli.
Kutomtambua Karume kunafanya mazungumzo yawe rahisi kwa kiasi gani na kwa kiasi gani yanafanya yawe magumu? Endapo kutomtambua kunafanya mazungumzo yawe rahisi basi CUF waendelee na msimamo wao; hata hivyo endapo kumtambua kutarahisha mazungumzo basi CUF hawana budi kufikiria mkakati wao huo.
Tanzania is not only Zanzibar!
But Zanzibar ndio inafanya iwepo Tanzania
...Kuna record yoyote inayoonyesha CUF hawamtambui Karume kama rais wa Zanzibar?...
Mheshimiwa Spika, Chama cha CUF, kimekiuka Katiba, kimekiuka vifungu namba 26, 103 na 104, baada ya uchaguzi halali uliofanyika Zanzibar kwa kutangaza kuwa, hawamtambui Rais wa Zanzibar. Kwa maana hiyo, kwa sababu chama hiki kina Wabunge ndani ya Bunge hili, Wabunge hawa, kwa maoni yangu, si halali kuwemo ndani ya Bunge hili, kwa sababu chama chao kimekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maana hiyo, naomba mwongozo wako na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa Wabunge wa Chama cha CUF, sisemi wa Zanzibar, nasema Chama cha CUF. Kwa sababu Chama cha CUF, ndicho kilichotangaza kutomtambua Rais wa Zanzibar, aliyechaguliwa kihalali na kuwemo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
2008-05-20 16:32:06
Na Sharon Sauwa, Mikocheni
Baada ya Rais wa Zanzibar Bwana Amani Karume kutoa masharti ya kukutana na hasimu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, chama cha CUF kimekuja juu kikidai kwamba kauli za kiongozi huyo ni kejeli tupu na kwamba piga ua galagaza, hakitamtambua kama rais halali wa visiwa hivyo.
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa chama hicho,
Bw. Salum Bimani, ameliambia Alasiri leo asubuhi kuwa, kauli ya Rais Karume kutaka CUF wamtambue kwanza ndiyo akae nao kuzungumzia mgogoro wa kisiasa unaokikabili kisiwa hicho, inaonyesha hana nia ya kumaliza mgogoro huo.
Na wala asitarajie kutambuliwa kwani mida ndio huo unayoyoma na ulaji wake unakoma baada ya miaka miwili ijayo na juzi juzi kwenye mkutano wa hadhara Seifu alisema yeye ndio Raisi halali wa Zanzibar mpaka leo CCM wameshindwa kuipinga kauli ile au hata kuibeza.
Swala hili lina sura mbili, kwa upande wa CUF hawawezi kukubali kumtambua Rais Karume halafu wakajadiliane kuhusu muafaka kwa sababu muafaka unahitajika kutokana na madai waliyo nayo kuwa wamedhurumiwa kwenye uchaguzi. Hivyo basi iwapo watakubali kumtambua then kutakuwa hakuna haja ya muafaka.Madai yao ya msingi yatakuwa yamekufa.
QUOTE]
Muafaka hauna lengo la kushughulikia madai ya CUF, bali una lengo la kuleta mstakabala mzuri kati ya wananchi Pemba na wale wanaoishi Unguja, baada ya uhusiano wao kuonekana kuwa unatetereka kutokana na chokochoko za kisiasa zinazopaliliwa na wanasiasa kwa malengo yao binafsi ya kisiasa au tamaa za kuwania madaraka
Swala hili lina sura mbili, kwa upande wa CUF hawawezi kukubali kumtambua Rais Karume halafu wakajadiliane kuhusu muafaka kwa sababu muafaka unahitajika kutokana na madai waliyo nayo kuwa wamedhurumiwa kwenye uchaguzi. Hivyo basi iwapo watakubali kumtambua then kutakuwa hakuna haja ya muafaka.Madai yao ya msingi yatakuwa yamekufa.
QUOTE]
Muafaka hauna lengo la kushughulikia madai ya CUF, bali una lengo la kuleta mstakabala mzuri kati ya wananchi Pemba na wale wanaoishi Unguja, baada ya uhusiano wao kuonekana kuwa unatetereka kutokana na chokochoko za kisiasa zinazopaliliwa na wanasiasa kwa malengo yao binafsi ya kisiasa au tamaa za kuwania madaraka
iwapo CUF wasingekuwa na madai basi kusingekuwa na haja ya muafaka.Muafaka sio baina ya wananchi wa pemba na unguja bali ni baina ya chama cha CUF na CCM.matatizo ya kutokuelewana baina ya wazanzibar hayako katika misingi ya upemba na uunguja bali katika misingi ya party affiliation na misingi ya kihistoria.
excellent explanation.seif anamtambua karume kwamba ni rais wa zanzibar, asichotambua yeye ni kuwa karume ni "raisi halali wa zanzibar aliyechaguliwa kwa kura"
naona watu wamenijia juu mimi; hivi katika ajenda za muafaka kuna lolote linalohusu "kumtambua Rais Karume"? Ni wapi kwenye agenda za muafaka ambako walikuwa CUF wamesema kuwa Karume siyo Rais na hawamtambui?
Endapo wanalalamika kuwa serikali ya SMZ haijateua wapemba wengi, wateuliwe na nani wakati hawamtambua Rais?
Hicho kipengee cha Mwisho kinaweza kuhojiwa pale wanaposema hata Pemba CCM wanakubalika au kwa kiukaribu tunaweza kusema kuwa Pemba wapo CCM wasomi maana iweje Serikali ya Muungano iweze kuopoa akina Omar Ali Juma(mareemu) ,Dr Shein ,Salim Ahamed na wengine tu ambao wapo katika maizara huko Upnde wa pili wa Muungano ? Naamini kabisa kuwa wapo waliompigia kura kule Pemba sasa angalau angeonyesha kuwathamini na kutoa nafasi za unaibu uwaziri na kuwapatia nafasi za uhakika ambazo zinaweza kuwa kigezo cha utawala wake kuwa amejaribu kwa kiasi fulani .lakini wapi unaenda kumsomba mtu na kumpa uwaziri kiongozi jambo ambalo hata wasomi wa Kiunguja limewashitua mtu ambae alikuwa naibu Sheha yaani ni sawa na yule wa chini ya balozi wa nyumba kumi kumi ,Shamsi Vuai Nahoda huyu alikuwa naibu balozi wa nyumba kumikumi kwa sasa wanaita shehia. Na hii ni siasa za akina Karume baba ambae alikuwa wasomi kwake ni tishio.
kuna tetesi kuwa wawakilishi wengi wa CCM ambao ni kama wabunge kiingereza kinawapiga chenga ,hivyo hutumika kama bendera tu na hawawezi kutetea maslahi yao seuze ya Taifa.
Nadhani umefika wakati Tanzania tuwe na mjadala wa kuhusu MAPINDUZI kwa sababu huu ndio msingi wa matatizo yote tunayoyaona hivi sasa Zanzibar.Kuna wale wanaojiona wana haki zaidi ya kuwa watawala kwa sababu wanaamini kuwa somehow kuna ambao hawakushiriki nao au hawatambui umuhimu wa mapinduzi.Ukweli ni kwamba kweli watu wasiotambua umuhimu wa mapinduzi wapo, sasa ili kuwe na uwelewano ni imperative kwa pande hizo mbili kufungua mjadala.
naona watu wamenijia juu mimi; hivi katika ajenda za muafaka kuna lolote linalohusu "kumtambua Rais Karume"? Ni wapi kwenye agenda za muafaka ambako walikuwa CUF wamesema kuwa Karume siyo Rais na hawamtambui?
Endapo wanalalamika kuwa serikali ya SMZ haijateua wapemba wengi, wateuliwe na nani wakati hawamtambua Rais?