Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Akimtambua kuwa Rais, yale mazungumzo yote hayana maana kwa sababu msingi wake ulikuwa ni kusawazisha uwanja wa mapambano katika uchaguzi. Sasa na wewe inabidi tukuulize, kama Seif atamtambua Karume kuwa Rais, kwa nini wafanya mazungumzo ya mwafaka?

Bila ya kuleta Siasa za Marekani kwenye ukumbi huu, nillitaka kusema kiufupi tu kwamba ulicho kisema hapo ni doctrine moja ya Obama: anaiambia Marekani ukiweka masharti kwenye majadiliano sasa tunakuja kujadiliana nini?

Binti Maria nadhani hiyo pointi yako ya nguvu. Ina make sense, sio kwa sababu tu Obama nae kasema.
 
inaonekana umelewa au mawazo yako ni mgando..

Mbowe amegombea uraisi kwa mara ya kwanza mwaka 2005...

Rudi kwenye baa uwaambie wakurudishie pesa yako maana inaonekana wamekuuzia pombe ya kienyeji.

Mwafrika wa Kike,
Kuna kipindi unagawa vidonge mpaka unanipa raha. Unanifanya nitamani nikuone maana kuna wakati nashindwa jua majibu haya unayapata wapi. Mbavu sina.

Duh.. lakini hapa kuna vichekesho vya mwaka. Kenya Odinga alisema hamtambui Kibaki kuwa Rais lakini leo hii wanakaa meza moja na mmoja baada ya kutengenezewa cheo (Uwaziri Mkuu) anamuita Kibaki Mr. President. So haya mambo ya never say never ni ya kweli.

Kutomtambua Karume kunafanya mazungumzo yawe rahisi kwa kiasi gani na kwa kiasi gani yanafanya yawe magumu? Endapo kutomtambua kunafanya mazungumzo yawe rahisi basi CUF waendelee na msimamo wao; hata hivyo endapo kumtambua kutarahisha mazungumzo basi CUF hawana budi kufikiria mkakati wao huo.

Ndugu yangu Mwanakijiji,
Hivi ingekuwa wewe ndo mgombea wa CUF au Raila Odinga na unahakika umeshinda lakini unadhulimiwa ushindi wako na Karume au Kibaki,utasemaje? Kwamba sawa bwana nakutambua umeshinda au utasimamisha msuli? Nadhani mambo mengine mtu unahitaji ku-experience kwanza kabla ya kutoa judgement
 
But Zanzibar ndio inafanya iwepo Tanzania

...swadakta!!! duh, leo kuna one-liners humu hatari!...

Maalim akimtambua Karume kuwa rais maana yake amekubali matokeo, na kwamba alishindwa uchaguzi.
 
Duh! yaani Seif hamtambui Karume kama ni rais wa Zanzibar?... Sasa inakuwaje huu muafaka atake kuwa waziri kiongozi ktk serikali inayoongozwa na rais asiyemtambua!..
I mean guys tafadhali sana kila tunapotoa hoja zetu muhimu tuyaweke maslahi ya wananchi mbele..wananchi wa Zanzibar, haya maswala ya kina Raila na Morgan ni uchuro mtupu..
CUF wanaharibiwa sana na huyu mtu nadhani huu niwakati wake kukaa pembeni amwachie Duni na Lipumba..Huyu jamaa nadhani bado ana siasa za kina HezbuLaah.. (Hizbu)
Kuna record yoyote inayoonyesha CUF hawamtambui Karume kama rais wa Zanzibar?..
 
Ndugu wana JF tunahitaji kuwa wa kweli badala ya kuingia kwenye mkumbo wa CCM ingawa wao wanajua nia na lengo.

Seif/Lipumba/Mrema/Cheyo, n.k. si wa kwanza katika kugombea urais miaka mingi katika dunia hii. Angalia rais wa sasa wa Senegal (Wade) alingombea miaka mingapi katika chama cha upinzani mpaka amekuja kushinda? Kumbuka pia waziri mkuu wa India aliyepita kabla ya chama cha Congress kurudi tena madarakani, je aligombea mara ngapi (aliongoza chama chake kwenye uchaguzi mara ngapi)?

Tafadhalini hoja isiwe kwa nini kila wakati anagombea yeye tu bali tuangalie je ana sifa za kugombea??? Tukumbuke kuwa hata JK Nyerere alikaa madarakani miaka mingi kiasi kwamba baadhi ya Watanzania wakafikiria kuwa Nyerere ni title ya urais wa Tanzania, hadi watu wengine wakiuliza nyerere wa sasa hivi ni nani?
Kama Seif or whoever ana earned authourity within his party basi mwacheni agombee kwani inawezekana ndiye anayekiunganisha chama, vinginevyo itakuwa ni suala la kujaribisha kila mtu kugombea urais.

Nina hofu ndiyo maana hata ndg yetu Kikwete anaonekana kukosa nguvu katika uongozi wa chama kwa sababu wapo wanaoamini kuwa wao ndio wanaokifahamu chama vizuri zaidi kuliko yeye

Inawezekana kukawa na ubaya wa mtu huyo huyo kugombea urais mfululizo lakini pia haipingiki kuwa kuna faida zake kama vile uzoefu wa shughuli shughuli hizo hupatikana kwa kushiriki mara kwa mara. Kumbukeni pia Mwai Kibaki amegombea zaidi ya mara moja na hatimaye akaukwaa urais. Pia akina Raila Odinga wameendelea kuwa viongozi wa vyama vyao na kugombea na hatimaye kuleta upinzani mkubwa kwa rais aliyekuwepo madarakani. Hata Kiongozi wa MDC Zimbabwe ameshagombea mara tatu na kuweza kutikisa siasa za Zimbabwe.

Kwa hiyo naomba tuwe makini tunapoongelea mtu kugombea urais mfululizo ili tusije tukawa tunawasaidia mafisadi CCM pasipo kujua.

Ahsanteni,
 
...Kuna record yoyote inayoonyesha CUF hawamtambui Karume kama rais wa Zanzibar?...

...ndiyo mkuu Mkandara, jikumbushe sehemu ya speech hii ya Mh. Mbunge Hafidh Ali, Tahir CCM jimbo la Dimani wakati akichangia Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2006/2007 Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) 12.July. 2006

Mheshimiwa Spika, Chama cha CUF, kimekiuka Katiba, kimekiuka vifungu namba 26, 103 na 104, baada ya uchaguzi halali uliofanyika Zanzibar kwa kutangaza kuwa, hawamtambui Rais wa Zanzibar. Kwa maana hiyo, kwa sababu chama hiki kina Wabunge ndani ya Bunge hili, Wabunge hawa, kwa maoni yangu, si halali kuwemo ndani ya Bunge hili, kwa sababu chama chao kimekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maana hiyo, naomba mwongozo wako na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa Wabunge wa Chama cha CUF, sisemi wa Zanzibar, nasema Chama cha CUF. Kwa sababu Chama cha CUF, ndicho kilichotangaza kutomtambua Rais wa Zanzibar, aliyechaguliwa kihalali na kuwemo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

source; http://www.parliament.go.tz/bunge/ContrLst.asp?vpkey=1399&pterm=2005-2010&index=16

2008-05-20 16:32:06
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Baada ya Rais wa Zanzibar Bwana Amani Karume kutoa masharti ya kukutana na hasimu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, chama cha CUF kimekuja juu kikidai kwamba kauli za kiongozi huyo ni kejeli tupu na kwamba piga ua galagaza, hakitamtambua kama rais halali wa visiwa hivyo.

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa chama hicho,
Bw. Salum Bimani, ameliambia Alasiri leo asubuhi kuwa, kauli ya Rais Karume kutaka CUF wamtambue kwanza ndiyo akae nao kuzungumzia mgogoro wa kisiasa unaokikabili kisiwa hicho, inaonyesha hana nia ya kumaliza mgogoro huo.

source; http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/05/20/114799.html
 
Swala hili lina sura mbili, kwa upande wa CUF hawawezi kukubali kumtambua Rais Karume halafu wakajadiliane kuhusu muafaka kwa sababu muafaka unahitajika kutokana na madai waliyo nayo kuwa wamedhurumiwa kwenye uchaguzi. Hivyo basi iwapo watakubali kumtambua then kutakuwa hakuna haja ya muafaka.Madai yao ya msingi yatakuwa yamekufa.

Kwa upande wa Rais Karume, ni vigumu kwake kukubali kukaribisha Ikulu wageni wasiomtambua kama Rais.Wasiwasi mwingine unaojitokeza ni kwamba CUF wanaweza kukataa kuheshimu protocol za kukutana na Rais kwa sababu hawamtambui.Sasa protocol ipi itatumika katika kuwakutanisha???

Kwa hiyo ili utatuzi upatikane ni lazima kuwe na compromise.Na ili compromise ipatikane ni vyema mazungumzo yaanze kwa viongozi wa ngazi za chini(without conditions) wa CCM na CUF kabla ya kuwakutanisha Karume na Seif.

Msingi wa utatuzi wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar ni kuwepo kwa political will ya kuupata utatuzi huo.
 
Na wala asitarajie kutambuliwa kwani mida ndio huo unayoyoma na ulaji wake unakoma baada ya miaka miwili ijayo na juzi juzi kwenye mkutano wa hadhara Seifu alisema yeye ndio Raisi halali wa Zanzibar mpaka leo CCM wameshindwa kuipinga kauli ile au hata kuibeza.

Kwani Rais anapatikana kwenye majukwaa ya Mkutano wa hadhara?
 
Swala hili lina sura mbili, kwa upande wa CUF hawawezi kukubali kumtambua Rais Karume halafu wakajadiliane kuhusu muafaka kwa sababu muafaka unahitajika kutokana na madai waliyo nayo kuwa wamedhurumiwa kwenye uchaguzi. Hivyo basi iwapo watakubali kumtambua then kutakuwa hakuna haja ya muafaka.Madai yao ya msingi yatakuwa yamekufa.

QUOTE]

Muafaka hauna lengo la kushughulikia madai ya CUF, bali una lengo la kuleta mstakabala mzuri kati ya wananchi Pemba na wale wanaoishi Unguja, baada ya uhusiano wao kuonekana kuwa unatetereka kutokana na chokochoko za kisiasa zinazopaliliwa na wanasiasa kwa malengo yao binafsi ya kisiasa au tamaa za kuwania madaraka
 
iwapo CUF wasingekuwa na madai basi kusingekuwa na haja ya muafaka.Muafaka sio baina ya wananchi wa pemba na unguja bali ni baina ya chama cha CUF na CCM.matatizo ya kutokuelewana baina ya wazanzibar hayako katika misingi ya upemba na uunguja bali katika misingi ya party affiliation na misingi ya kihistoria.
 
Wala cuf msikubali kumtambua mwizi wa ushindi wenu na wazanzibar wote. That is a trap. Mkikubali mmejiua. Endelezeni mapambano. Aluta kontinua.
 
seif anamtambua karume kwamba ni rais wa zanzibar, asichotambua yeye ni kuwa karume ni "raisi halali wa zanzibar aliyechaguliwa kwa kura"
 
naona watu wamenijia juu mimi; hivi katika ajenda za muafaka kuna lolote linalohusu "kumtambua Rais Karume"? Ni wapi kwenye agenda za muafaka ambako walikuwa CUF wamesema kuwa Karume siyo Rais na hawamtambui?

Endapo wanalalamika kuwa serikali ya SMZ haijateua wapemba wengi, wateuliwe na nani wakati hawamtambua Rais?
 
Hicho kipengee cha Mwisho kinaweza kuhojiwa pale wanaposema hata Pemba CCM wanakubalika au kwa kiukaribu tunaweza kusema kuwa Pemba wapo CCM wasomi maana iweje Serikali ya Muungano iweze kuopoa akina Omar Ali Juma(mareemu) ,Dr Shein ,Salim Ahamed na wengine tu ambao wapo katika maizara huko Upnde wa pili wa Muungano ? Naamini kabisa kuwa wapo waliompigia kura kule Pemba sasa angalau angeonyesha kuwathamini na kutoa nafasi za unaibu uwaziri na kuwapatia nafasi za uhakika ambazo zinaweza kuwa kigezo cha utawala wake kuwa amejaribu kwa kiasi fulani .lakini wapi unaenda kumsomba mtu na kumpa uwaziri kiongozi jambo ambalo hata wasomi wa Kiunguja limewashitua mtu ambae alikuwa naibu Sheha yaani ni sawa na yule wa chini ya balozi wa nyumba kumi kumi ,Shamsi Vuai Nahoda huyu alikuwa naibu balozi wa nyumba kumikumi kwa sasa wanaita shehia. Na hii ni siasa za akina Karume baba ambae alikuwa wasomi kwake ni tishio.
kuna tetesi kuwa wawakilishi wengi wa CCM ambao ni kama wabunge kiingereza kinawapiga chenga ,hivyo hutumika kama bendera tu na hawawezi kutetea maslahi yao seuze ya Taifa.
 
Nadhani umefika wakati Tanzania tuwe na mjadala wa kuhusu MAPINDUZI kwa sababu huu ndio msingi wa matatizo yote tunayoyaona hivi sasa Zanzibar.Kuna wale wanaojiona wana haki zaidi ya kuwa watawala kwa sababu wanaamini kuwa somehow kuna ambao hawakushiriki nao au hawatambui umuhimu wa mapinduzi.Ukweli ni kwamba kweli watu wasiotambua umuhimu wa mapinduzi wapo, sasa ili kuwe na uwelewano ni imperative kwa pande hizo mbili kufungua mjadala.
 
Unaposema Mapinduzi lazima uwe unajua ni nani alipinduliwa ?
 
naona watu wamenijia juu mimi; hivi katika ajenda za muafaka kuna lolote linalohusu "kumtambua Rais Karume"? Ni wapi kwenye agenda za muafaka ambako walikuwa CUF wamesema kuwa Karume siyo Rais na hawamtambui?

Endapo wanalalamika kuwa serikali ya SMZ haijateua wapemba wengi, wateuliwe na nani wakati hawamtambua Rais?

Mkuu ! wengi wanakujia juu kwani inaonyesha umehamia upande wa Karume ambaye hata kama hoja yake hii ni kweli lakini wengi wetu unajua kuwa hataki kuhirikiana na CUF katika kulitafutia ufumbuzi hili suala.

Moyoni mwake kama mtoto mwema nataka kutekeleza ahadi ya marehemu baba yake aliyesema kuwa hakutakuwa uchaguzi Znz hadi baada ya mika 50. Kwa hivyo japo uchaguzi unafanyika lakini utawala ni wa waliopindua hadi itimie hiyo miaka. Kwa CCM Znz sio kuwa walimpindua Sultan tu lakini na wote waliokuwa wakimuunga mkono na si siri kuwa tangu zamani wapemba wengi hawakuiunga mkono ASP na hadi sasa hawaiungi mkono CCM.
 
Back
Top Bottom