Bikirembwe
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 250
- 7
Wote tu ndugu yangu, huyo Kikwete na Pinda aliyekuwa mbele hajulikani. Nchi yetu kwa sasa ina pengo kubwa sana la viongozi na sijui kama tutaweza kulirekebisha hili katika uchaguzi ujao 2010.
Jaji Augustino Ramadhani alitoa opinion kuhusu kama Zanzibar ni nchi au siyo katika kesi iliyoletwa kama ya uhaini. Kama tunaweza kupata nakala ya Kiswahili ya hukumu hiyo tunaweza kupata ufafanuzi wa kimahakama,.[/QUOT
alisema waziwazi kuwa Zanzibar si nchi, hivyo uhaini hauwezi kufanyika huko
Nimetahayari na kufedheheshwa sana na haya Matamshi yako.
Nionavyo mimi huu Muungano wetu ni muungano wa kukidhi haja iliyokuwepo Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar. Waasisi wa Muungano huu walifanya Muungano kwa malengo mawili tofauti. Kwa upande wa Karume alikubali Muungano kwa kutaka usalama wa Dola yake na Nyerere alitaka Muungano akitekeleza ndoto yake ya Kuunganisha Afrika.
Kilichobaki tukae chini kindugu na tuujadili namna ya utaratibu mzuri wa Muungano wetu kutumia mabavu kwa ajili ya ukubwa na utajiri si suluhisho. Binaadamu atafanya kila liwalo apate haki yake na tuone Mifano ya Russia,Canada,na wa karibuni huu wa Belgium(hatukutegemea mambo kama haya kutokea nchi kama Belgium.
VIVA MUUNGANO NA SIO UTAWALA WA TAIFA MOJA KWA JENGINE
Mimi kama Mtanganyika ningependa kujua hasa kwanini nchi hii ina serikali zaidi ya moja hususani ukizingatia ya kwamba serikali nyingine ni kwa ajili ya eneo ambalo ni sehemu ya nchi iitwayo Tanzania.Hiki ni kipengele kimoja cha terms za muungano chenye kuhitaji ufafanuzi wa hali ya juu kwangu mimi binafsi.
Nipo Zanzibar, hivi punde nimetoka kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Dharif Hamad. Ajenda kuu ilikuwa kauli iliyozua mjadala ya Pinda kuwa Zanzibar si nchi.
Maalim amemtaka Pinda awaombe radhi wazanzibari hadharani kwa kauli hiyo ambayo imewahuzunisha, kuwakwaza na kuwafadgaisha wazanznibari wote.
Lakini kikubwa, Maalim ameitumia kauli hiyo ya Pinda kuonyesha kuwa muungano wa sasa unaendeshwa kwa hila za kutaka kuiua Zanzibar. Anasema hili lilianza tangu awali na lilianzishwa na Nyerere ambaye alionyesha kuichukia Zanzibar tangu mwanzo.
Amesema Nyerere alitumia ghilba kumshawishi Karume (Original) akubali Muungano na alipokataa alimtishia kuwa ataondoa askari wake.
Kwa kuwa nchi ilikuwa changa (siku chache baada ya mapinduzi) karume alikubali lakini kwa sharti kwua Zanzibar iendelee kuwa nchi.
Maalim Seif anasema lakini hila za kuiua Zanzibar zilianza wakati huo na ndio maala masuala ya Muungano yameongezeka kutoka 11 ya awali hadi 23 hivi sasa.
Anasema kuongezeka kwa masuala ya muungano kunamaanisha kupungua kwa madaraka ya Zanzibar na hilo haliwezi kukubalika.
Amemtaka Shamsi Vuai kutangaza katika Baraza la Wawakilishi kuwa Zanzibar ni nchi na hiyo itasababisha kuwepo kwa mgororo wa kikatiba. Ameitaka SMZ itangaze mgogoro huo wa kikatiba na CUF itaiunga mkono.
Nadhani Zanzibar ni kama zile US wanaita states ambazo zina utawala wao chini ya magavana, zinatunga hata sheria zao, zinakusanya hata kodi, na bado si nchi. Ziko katika muungano.Mimi nasema na kusisitiza kuwa Zanzibar ni nchi kwa sababu zifuatazo:
1. Ina Raisi
2. Ina baraza la wawakilishi
3. Inayo mahakama
4. Siyo mkoa bali ina mikoa na watendaji wake huteuliwa na raisi wake
5. Ina kiongozi wa serikali ndani ya baraza
6. Uchaguzi mkuu wa raisi na wawakilishi hufanyika kila baada ya miaka mitano na kuapishwa kama katiba yake inavyoelezea.
7. Inayo wimbo wake wa Taifa
Sana kama hayo yote hayatoshi kuitwa nchi, nchi ni nini.
Kelele za vyura bwawani. Kila mtu changu, changu! Iwe nchi, iwe taifa, iwe nini. Cha msingi ni mamlaka gani unayo kwa muundo upi. Wilaya yenye mamlaka na muundo mzuri wa kuleta maendeleo ni ya maana zaidi kuliko nchi au taifa lisilo kuwa na mamlaka yoyote na muundo kiini macho. Hapa dawa ni Wazanzibar tupewe Zanzibar yetu, wadanganyika wapewa Tanganyika yao halafu tukutane katikati kwenye shirikisho la Tanzania. Kama CCM hamtaki na bazara letu na mapinduzi na kamati kuu yenu basi tuunde Shirikisho la MAJIMBO tu hapo.
Asha