Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Kigeugeu,

you have a point,lakini hebu angalia hii ramani hapa na utanielewa zaidi ninachojaribu kuzungumza.


tz_map.gif


ramani ya Tanzania
 
Under age ndugu yangu mimi na wewe tumechoshwa na huu unafiki wa viongozi wetu. Ndo maana tunafika sehemu tunasema labda tukiumia tutapata akili. Kama Karume au wenzake wasingekuwa wanaangalia vitumbua vyao, unafikiri hali isingebadilika? Tatizo ni uongozi unaojali matumbo yao. Wadanganyika na wazanzibari we share common heritage na mahitaji yetu ni yale yale, sema tuu basi tunaangushwa na wale tuliowapa dhamana.

Uzanzibari na utanganyika mimi simo, hizo ni kauli za walioishiwa mawazo, as long as we can forge a common future together, Then our Union will be relevant thousands of years to come as it was fifty years ago when the idea was put on the table.
masanja ,kama wazanzibari na watanganyika kwa pamoja wangeichukua hiyo kauli nilioinukuu hapo juu kutoka kwako ,basi naamini kungekuwa na kuheshimiana baina ya pande mbili za muungano, lakini ! maskini roho zetu! tunachujuana na kunyambuana sie "vibua" huku "papa" na "mzia" (watawala wajeuri wasiojali maslahi ya wananchi) wakitudondoa na kutumaliza kiulaini. twaumizwa na wakubwa na huku chini twaumizana wenyewe kwa wenyewe, inasikitisha ,na sijui lini tutaamka na tumjue adui yetu!
 
under_age,masanja,

mimi napenda watanganyika tujichunguze wenyewe kabla ya kuwalaumu wazenj. hivyo hivyo napenda wazenj wajichunguze kabla ya kulaumu watanganyika.

kuna mengi yako ndani ya uwezo wetu, na hayahusiani moja kwa moja na muungano, ambayo tukiyarekebisha tunaweza kuleta maendeleo, na kupunguza makali ya umaskini.

kwa mfano Wapemba wanaweza kulalamika kwamba SMZ haipeleki maendeleo huko kwao. wakati wanaendelea kuishinikiza SMZ kwanini wasiige mfano wa wananchi wa Kagera kwa kuchangia maendeleo yao?

kama kuna jamii iliyofaidika kiuchumi/kibiashara kwa kufunguliwa kwa milango ya biashara basi ni Wapemba. sasa kwanini Pemba kumeendelea kudorora kimaendeleo?

Tukirudi kwa hawa viongozi wetu. Dr.Anna Tibaijuka ame-pledge kutafuta wafadhili kwa ajili ya shule ya wasichana Kagera. What has Dr.Salim Salim done for the development of Pemba?

Tumejijengea utamaduni mbaya wa viongozi kutokuchangia/kuhimiza maendeleo vijijini kwao kwa kusingizia wao ni waadilifu, au viongozi wa kitaifa.
 
JJoka kuu unayosema ni kweli tupu, lakini hebu tuangalie wale wanaokula kodi zetu kwa jina la kuwatumikia wananchi. Kama jamaa alivyoandika hapo juu, ukifikiria sana inafrustrate tunavyoumizana. kifupi kila mtu anajiangalia yeye sasa unashindwa tofautisha kampuni binafsi na taifa letu sote! Aggghhhh....
 
JK tatizo sio wawakilishi au vingenevyo, tatizo ni ubinafsi wa viongozi na watawala wetu. There is enough for every body in Tanzania ila wachache wanazidi kuhodhi kwa manufaa yao.

Nasema tena, mpaka wananchi tutakapozinduka na kuona uzandiki wa watawala wa CCM tutazidi kuumia. na kwa kuwa tumeamua kuikumbatia CCM basi hatuna budi kulipa gharama inayostahili AMBAYO NDO HUU UMASKINI TUNAOLIA NAO KILA SIKU. Kwa hiyo tusilalamike. Kuhusu Zanzibar mimi siwahurumii hawa jamaa kwa sababu na wao ni wanafiki wanaikumbatia CCM na sera zake kwa sababu wachache wananufaika! Nchi ya watu million moja inakosa hata aspirin, harafu unaniambia hiyo ni akili au ni tope? Let them suffer, wakizinduka-as all Tanzanians, then we shall move forward. For now we are enjoying the consequences of our choices!

Noel Njema!

Masanja CCM zanzibar wanaoikumbatia hawashindi uchaguzi, just wanasema tu % ngapi ya ushindi wanataka then ZEC inatangaza, na wala CCM haitoshinda kidemokrasia, ikiwa Dk Salmin alishinda 0.% kwenye uchaguzi wa 1995, huyu wa sasa apate over 70% kwa lipi? mimi silioni mkuu. Bara ndio waamuzi wa nani awe Rais visiwani, na kwa njia yoyote ile ikibidi hata kwa nguvu ya jeshi. Uchaguzi gani wa kiraia then jeshi linakamata Tv na Radio za Serikali, Bandari na Airport. Kama haitoshi magari ya kivita pia yanapatrol mitaani. Na anaeamrisha hayo ni AMIRI JESHI MKUU (MUUNGANO PRESIDENT) coz Rais wa zanzibar hana mamlaka hayo kikatiba.
Naamini hii dhiki Zanzibar ni mpango maalum ili siku moja waseme tunataka SERIKALI MOJA.
It wont happen Sir
 
Kesho ni siku Kuu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Usiku wa kuamkia tarehe 12/01/1964 John Okello na wapiganaji toka Zanzibar na sehemu za bara waliingia Zanzibar na kwa kutumia mtutu wa Bunduki na Majambia wakachora mstari uliokomesha utawala wa Sultani visiwani humo. Utawala uliodumu kwa karne kadhaa. Siyo tu kukomesha utawala wa Sultani bali pia mapinduzi hayo ya umwagaji damu yalikomesha utawala wa Serikali ya Waziri Kiongozi Shamte iliyokuwa imedumu chini ya mwaka mmoja tu.

Sultanjamshidinexile.jpg.jpg

Sultan Jamshid akiwa uhamishoni​

Kukomesha utawala wa Sultani kulifikisha hatima historia ya ubwana na utwana iliyodumu pia kwa karne kadhaa japo katika kipindi hicho mabadiliko kadha wa kadha ya kisiasa yalianza kuingia visiwani humo. Hata hivyo mabadiliko hayo kwa wengine hayakutosha sana na matokeo yake ni umwagikaji wa damu mkubwa kutoka katika eneo la Afrika ya Mashariki uliofanywa na watawaliwa dhidi ya watawala na wale walioonekana kuhusiana na watawala aidha kwa nasaba au kutokana na nafasi zao.


members_first_govt_zanzibar_1963.jpg.jpg

Hii ni serikali ya kwanza ya Zanzibar chini ya Waziri Kiongozi/Mkuu Shamte

Mapinduzi hayo yaliyochukua karibu saa tisa siyo tu yalimuondoa Sultani na kuipindua serikali ya Shamte bali pia yalisababisha michirizi ya damu katika visiwa hivyo vya karafuu, damu ambayo hadi leo hii inaendelea kuwagawa watu wa visiwa hivyo. Kuna wale ambao wanaapa kwa mapinduzi na kuna wale ambao wanaamini mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni uonevu mkubwa kabisa katika visiwa hivyo na hadi leo hii hawajeweza kusamehe na hawatoweza kusamehe yaliyotendeka usiku ule!

mass_grave_3.jpg.jpg


Kaburi la halaiki la baadhi ya watu waliouawa katika mapinduzi ya Zanzibar

Hivyo wakati wananchi wa Zanzibar wanaadhimisha Mapinduzi hayo na wengine wakiwa wanasherehekea mapinduzi hayo na wapo wale ambao kesho ni siku ya machozi kwao; Hatuna budi kuangalia ishara ya mapinduzi hayo hasa tunapoangalia kinachotokea Kenya leo hii.

Okello.jpg.jpg


John Okello, kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar
Ni kwa kiasi gani watawala wanaweza kuendelea kutawala kwa nguvu hadi kulazimisha umwagikaji damu wa raia wao? Baadhi ya maswali na hoja ambazo ninazifikiria ninapoangalia na kujifunza zaidi kuhusu suala la mapinduzi.

a. Je kulikuwa na njia nyingine yoyote ya wananchi wa visiwa vya Zanzibar kujipatia madaraka ya kuongoza visiwa vyao bila kulazimisha umwagaji damu?

b. Kwa wanaofahamu historia ya utawala wa Kisultani visiwani humo je ulikuwa ni mbaya kiasi cha wananchi kuamua kuinuka dhidi yake na kuukomesha utawala huo?

c. Je ni kwa kiasi gani machungu, na hisia za kisasi zilizotokana na Mapinduzi ya Zanzibari vinazidi kuwagawa wananchi wa visiwa hivyo?

d. Katika kufikia muafaka wa kweli na utakaodumu je kuna ulazima wa Zanzibar kupitia historia yake na kuponya majereha yake ikiwemo kumrudisha Sultani Jamshid na uzao wake na kuwarudishia baadhi ya mali zao endapo watakana Usultani na kukana kumiliki kiti cha Usultani wa Zanzibar na hivyo kuwa Raia wa kawaida tu?

e. Tunapoangalia yanayoendelea Kenya leo hii, ni kwa kiasi gani historia huwa inajirudia yenyewe pale ambapo watu wanahisi kuonewa na watawala wao au wanapoona kuwa kuna kiongozi madarakani ambaye hajatokana na ridhaa yao? Tunaelekea kwenye Mapinduzi mengine?

NB: Picha hizo nne ni kati ya picha 25 za Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zinapatikana kwenye tovuti ya KLH News kwenye eneo la "Pics & Docs". Baadhi ya picha hizo hazijaonwa na Watanzania wengi hivi sasa na kwa mapinduzi ni kama hadithi ya kale!
 
Topic hii tuliwahi kuijadili sana wakati wa summer mwaka jana. Kwa jumla binafsi sikuona sababu ya msingi ya umwagaji damu ule zaidi ya tamaa ya madaraka ya watu waliokuwa ASP. Ingawa vyama vya siasa pale Zanzibar vilikuwa namelngo tofauti kama ilivyo katika siasa zozote, kulikuwa na utaratibu wa kidemokrasia kabisa wa kuindoa serikali madarakani kwa njia ya Kura. lakini ASP walivunja utaratibu ule kwa kuuwa watu wasiokuwa na hatia na kuondoa demokrasi kabisa kutoka visiwani pale.

Nilikuwa na shaka sana na uongozi wa ASP kwa vile walishindwa hata kuelewana na Shamte wa ZNPPP ambaye baadaye aliamua kuungana na ZNP. Kwenye makubaliano ya Uhuru ya Lanzaster House, chama cha ASP kilikuwa hakiwezi kuweka bayana matakwa yake, kikawa kama vile kinaburuzwa lakini kumbe ni kama kilikuwa na njama zake za kuuwa watu.

Vyama vya ZNPP na ZNP(Hizbu) ambavyo ndivyo vilivyopinduliwa kutoka madarakani havikuwa vya waarabu tu; kulikuwa na waafrika wengi ndani ya vyama vile. Hebu mwangalie yule Shamte aliyepinduliwa na ASP na kufungwa Keko; mtoto wake Baraka Shamte eti alikuwa kada wa CHAMA; nini na wapi hiyo. Ilikuwaje Shamte awe mwarabu lakini mtoto wake awe na Mtanzania safi?

Wanasiasa hao wa ASP watakwambia kuwa aliopinduliwa alikuwa ni Sultani, lakini wapi? Sultani hakuwa na serikali. Hata wakati mkoloni, sultani alikuwapo na wala hakukuwa na tatizo. Wangeweza kumwondoa kikatiba bila kuua watu wengi vile. Kuna Movie niliiweka kwenye ile thread iliyokuwa inaomnyesh a jinsi watu walivyouwawa.

Conclusion: Mauaji yale yalikuwa ni matokeo ua uroho wa Madaraka kama wa Kibaki. Mpaka leo hii, ile sumu iliyoletwa na mapinduzi yale bado inawanyanyasa watoto wa Zanzibar. Ilikuwa kama Bomu la Atomik kule Nagasaki na Hiroshima linavyoendelea kuwasumbua hadi leo.
 
Kichuguu,
Naomba kutofautiana kidogo na wewe kuhusu yale mauaji ya Zbar. Mimi nadhani yalitokana na chuki na ubaguzi uliokuwepo kwa miongo mingi. Nasikia Mwafrika mweusi alikuwa hatakiwi kuonekana kwenye maeneo ya "Waarabu" baada ya saa fulani za siku. Kulikuwepo ubwana na utwana. Niliwahi kumwuliza rafiki yangu mmoja Mzanzibari mwenye asili ya Kiarabu juu ya hali hiyo akakiri kuwa ni kweli ilikuwepo. Sasa hiyo ndiyo iliyosababisha mauaji baada ya waafrika kupindua serikali, kwa mtazamo wangu.
Na kwa Kenya unaweza kutumia analogy hiyo hiyo. Wakikuyu wamehodhi madaraka kwa muda mrefu sana na hawakutaka kuachia makabila mengine. Baada ya wizi wa Kibaki ilikuwa rahisi kwa wakalenjin, wajaluo na wakisii kuwaandamana Wakikuyu kwa mapanga. Very said, I might add.
 
Jasusi ndugu yangu.

Wakati wa summer nililichimba swala hili la mapinduzi kwa kina sana. Inawezekana kweli chuki ya kikabila ilikuwapo, lakini kumbuka pia kuwa waarabu walikuwa wamewaoa waafrika sana.

Mapinduzi yale hayakutokana na ukabila kwa vile yalifanyioka kabla ya mwezi kupita tangu wapate Uhuru. hakuna mwenye ushahidi kuwa serikali ile ilikuwa ya kikabila. Ilikuwa inaongozwa na Shamte ambaye mwanzoni alikuwa anahsirikiana na ASP.
 
Kichuguu,
'Shamte alionekana kuwa kama kibaraka wa Waarabu. Yeye alitaka kuendeleza status quo yaani waarabu waendelee kuwa mabwana na Waafrika watwana wao. Ni kwa nini Shamte aliacha kushirikiana na AFP? That is the question.
 
Jasusi ndugu yangu.

Wakati wa summer nililichimba swala hili la mapinduzi kwa kina sana. Inawezekana kweli chuki ya kikabila ilikuwapo, lakini kumbuka pia kuwa waarabu walikuwa wamewaoa waafrika sana.

Mapinduzi yale hayakutokana na ukabila kwa vile yalifanyioka kabla ya mwezi kupita tangu wapate Uhuru. hakuna mwenye ushahidi kuwa serikali ile ilikuwa ya kikabila. Ilikuwa inaongozwa na Shamte ambaye mwanzoni alikuwa anahsirikiana na ASP.


Kwanini mwafrika siku zote awe na bad deal? Kwani kabla ya Zimbabwe kupata uhuru wake Muzorewa si alikuwa waziri mkuu.

Suala la kuwa mwarabu alioa waafrika sana halina umuhimu. Liberia imeundwa na watumwa waliorudi kutoka marekani. Lakini pamoja na wao kuelewa vizuri mabaya ya utumwa, walichofanya kwanza ni kuwafanya waliowakuta kuwa watumwa na kuendeleza status quo. Kama unaendeleza status quo, one day you will pay the HEAVIEST PRICE.
 
Kwanini mwafrika siku zote awe na bad deal? Kwani kabla ya Zimbabwe kupata uhuru wake Muzorewa si alikuwa waziri mkuu.

Suala la kuwa mwarabu alioa waafrika sana halina umuhimu. Liberia imeundwa na watumwa waliorudi kutoka marekani. Lakini pamoja na wao kuelewa vizuri mabaya ya utumwa, walichofanya kwanza ni kuwafanya waliowakuta kuwa watumwa na kuendeleza status quo. Kama unaendeleza status quo, one day you will pay the HEAVIEST PRICE.
samahani sikuelewa message yako hapa. Kwa vile wewe ni mgeni kidogo hapa kijiweni, ni afadhali nikuarifu kuwa swala hili tulilijadili kwa kina sana mwezi wa July mwaka jana hapa. Mwarabu kuoa Mwafrika haikuwa ishu kwangu, ila process yote iliyopelekea mapinduzi yale. Kuna chaguzi kadhaa za kidemokrasia zilifanyika. Kuna wakati ASP ilishinda na kuna wakati ilishindwa. Ule Uchaguzi wa mwaka 1963 ASP walishindwa kwa makosa yao kisiasa, na hakukuwa na sababu ya wao kutumia mabavu kuingia madarakanai na kubomoa misingi yote ya demokrasia.
 
samahani sikuelewa message yako hapa. Kwa vile wewe ni mgeni kidogo hapa kijiweni, ni afadhali nikuarifu kuwa swala hili tulilijadili kwa kina sana mwezi wa July mwaka jana hapa. Mwarabu kuoa Mwafrika haikuwa ishu kwangu, ila process yote iliyopelekea mapinduzi yale. Kuna chaguzi kadhaa za kidemokrasia zilifanyika. Kuna wakati ASP ilishinda na kuna wakati ilishindwa. Ule Uchaguzi wa mwaka 1963 ASP walishindwa kwa makosa yao kisiasa, na hakukuwa na sababu ya wao kutumia mabavu kuingia madarakanai na kubomoa misingi yote ya demokrasia.

Message yangu ni simple. Unapokuwa na sheria za mchezo jaribu kizifuata. Uchaguzi wa kwanza ASP walishinda na kwa mujibu wa sheria walitakiwa waunde serikali. Lakini mbinu zilifanyika za kurudi uchaguzi.

Makosa makubwa yaliyofanyika ni ku-manipulate sheria za uchaguzi ku-maintain status quo.

Misingi ya demokrasia sio kurudi uchaguzi kwa mipango ya ku-manipulate ushindi na hayo ndio makosa yaliofanyika.

Kwa upande mwingine inasemekana kwamba mapinduzi yalitakiwa yafanyike kwa sababu walioshinda kinyemela nao walikuwa na mipango ya ku-exterminate wafuasi wa ASP. ASP walichofanya ni kuwahi game.
 
Hao waZenji hawana mpangilio sasa hapo walimwondoa sulutani au waliiondoa serikali iliyopewa Uhuru maana ukitazama hata Nchi za Ulaya zina wafalme na Serikali ,naona hapo walifanya kosa kwani Ufalme ni nembo ambayo hadi hii leo inatumika huko Maulaya.
Pia kuhusu hayo makabuli ya halaiki nasikia hayapo na hiyo si habari ya kweli ni uzushi kuna filam moja The 1964 Zanzibar Massacre: Blacks Slaughtered All Arabs.Hawa jamaa wanamalizana wenyewe kwa wenyewe maana ile picha pale inaonyesha ni wenyewe kwa wenyewe hapa mwarabu pale ndio hadi hii leo bado wanamalizana ,hakuna anaetawala kwa raha ,kila mmoja anamuona mwenziwe ni muarabu ,hii Zenji ilipata Uhuru na haijasikika ikisheherekea Uhuru wake ,wanangoja za kwetu na kuja kujibamiza eti ndio wanasheherekea Siku ya uhuru ,yaani hawaoni hata haya.
Hebu tazama uzushi uliopo ndani ya kideo hii ,halafu leteni maoni yenu kama hii filamu ni ya kweli au ni kupakazia tu.Ili mkoloni mweusi azidi kuwabamiza ndugu zake kwa vitu feki kama hivi.

http://www.youtube.com/watch?v=kT1LCuxXdcg
 
huku tukiendelea kujadili suala hili kwa kina tujue kuwa ASP haikupindua kama chama, na wao hawakuwa na lengo hilo kabla.

wao walikuwa wakipigania kuongezwa nafasi zao katika serikali ya shamte na shamte akasema hawezi kushirikiana na mateka( akikusudia ASP).

na pia ni vyema kujua kuwa huyo anaeambiwa mwarab na mkoloni askari wake wengi walikuwa ni waafrika miongoni mwao ni maruuhum Khamis Darweshi na wengi wengine.

sasa alipokuja mheshimiwa shamte akaanza kuwanyofoa kwa kutaka kuwaweka wazanzibari asili na hapo ndipo hali ikazidi kuharibika.

CCM ilichupia basi kwa nyuma baada kumuona Okello na kundi lake kina said Bavuai na Washoto ni wahuni na hata maneno aliokuwa akizungumza Okello ukiyasoma utagundua ni jinsi gani wasingeweza kuongoza dola. kwa hiyo ASP na UMMA party wakatake advantage.

huo ndio ukweli.

hali hiyo nnaweza kuifananisha na hali ya sasa kenya, mfano kitokezee kikundi ambacho kiaamua kula na kibaki sahani moja na kundi lenyewe haloijajiandaa vyema na baada ya kufanikiwa kushika hatamu wana ODM wayahozi mapinduzi
 
Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya Mapinduzi

Joseph Mihangwa Januari 9, 2008



VISIWA vya Zanzibar vilipata uhuru wa bendera Desemba 10, 1963 kutokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika Julai 8-15, 1963 pale muungano wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People`s Party (ZNPP)-ZNP/ZNPP ulipoibuka mshindi kwa viti 18 katika Bunge dhidi ya viti 13 vya chama cha Afro-Shirazi Party (ASP).

Kwa ushindi huo, Mohamed Shamte wa ZPPP aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar na Sultan wa Zanzibar Jamshid bin Abdallah Khalfa Harubu alibakia kama Mkuu wa nchi, mwenye mamlaka ya kuteua mrithi (Gazeti la serikali 1963).

Kilichoshangaza ulimwengu ni jinsi Serikali ya Shamte ilivyopinduliwa hima, siku 34 tu toka uhuru wa bendera, yaani Januari 12, 1964 katika mabadiliko sawia ambayo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanayaeleza kuwa ni ya aina yake katika nchi za Kiafrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, ukiondoa Guinea ya enzi za Rais Sekou Toure. Nini na kina nani ‘waliochochea’ mapinduzi hayo?

Wakati kuna majibu ya kutosha juu ya sababu ya Mapinduzi hayo, bado ni kitendawili ni nani aliyaanzisha na kuyaongoza kiasi kwamba suala hili limepata simulizi na tafsiri mbalimbali zinazokinzana na kuacha umma gizani.

Katika makala haya kwa kutumia vyanzo mbalimbali tutaelezea matukio yaa kabla, wakati na baada ya Mapinduzi, kuwawezesha wasomaji kupata angalau picha ya nini kilichotokea ili kuweza kujibu swali “nini na nani alichochea au kuongoza Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ambayo sherehe za miaka 44 ya kumbukumbu yake zinafanyika Jumamosi hii.

Harakati za uhuru Zanzibar kwa sehemu kubwa ziliendeshwa na vyama vikuu viwili –ZNP kilichoundwa Desemba 1955 na ASP kilichoanzishwa Februari 5, 1957.

Kati ya mwaka 1959 na 1963 kuelekea uchaguzi wa Julai 1963, mitafaruku ilizuka miongoni mwa wanaharakati wa vyama hivyo, Mohamed Shante akijiengua kutoka ASP na kuunda chama cha ZPPP ambapo Abdulrahman Mohamed Babu alijitoa ZNP na kuunda Umma Party (UP) chama cha mrengo wa kushoto.

Katika uchaguzi wa Julai 1961, ASP kilipata asilimia 49.9 ya kura zote, ZNP kilipata asilimia 35 na ZPPP asilimia 13.7. Hata hivyo, pamoja na ushindi wa kura ASP, kilishindwa kutamba katika viti vya bunge (LEGCO) kilipopata viti 10, ZNP 10 na ZPPP vitatu.

Uchaguzi huo ambao haukupata mshindi na ulifuatiwa na ghasia, zilizoacha watu 68 wakiuawa na wengine 400 wakiwa majeruhi. Watu 100 walikamatwa hivyo ilibidi urudiwe Julai, 1963, chini ya ulinzi mkali wa askari zaidi ya 100 waliwamo askari wa Kiingereza.


baraza la shamte.jpg
WAZIRI Mkuu Shamte na baraza lake la mawaziri lililopinduliwa.


Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama ifuatavyo muungano wa ZNP/ZPPP viti 18 na ASP viti 13 chama cha umma hakikugombea. Shamte alishauriwa aunde Serikali ya mseto kati ya ZNP/ZPPP na ASP ili kulinda umoja wa kimataifa, lakini alikataa kwa kiburi kwamba hawezi kukubali “kugawana mateka”

Sherehe za uhuru zilifanyika Desemba 9, 1961 zikihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri kutoka nchi 70, akiwamo mwana wa Mfalme (Duke) wa Edinburgh pamoja na Aga Khan. Hakuna kiongozi yeyote wa Afrika aliyehudhuria.

Katika salamu zake za uhuru siku hiyo, Babu wa Umma Party aliwashangaza watu alipomaliza kwa kusema “umma wa Zanzibar na chama chao cha UMMA unasubiri kunyakua madaraka ya nchi saa itakapowadia”. Alikuwa na maana gani?

Serikali ya Shamte ilitoa haraka haraka madaraka makubwa kwa Wazanzibar katika Jeshi la Polisi, ambayo kabla ya hapo yalishikwa zaidi na Wamakonde kutoka Tanganyika na Msumbiji Kaskazini, ambao sasa waliachishwa kazi na kubakia Visiwani kwa uchungu bila kazi.

Mapema Januari 1964 (kabla ya Mapinduzi) Serikali ya Shamte ilikipiga marufuku chama cha UMMA na Babu akawa anasakwa kwa kosa la uhaini kwa kuhutubia mkutano wiki mbili kabla na kumshambulia Sultan na Serikali ya “kibaraka” Shamte. Kwa sababu hiyo alikimbilia Dar es Salaam kukwepa kukamatwa.

Tetesi za Mapinduzi zilianza asubuhi Jumamosi ya Januari 11,1964 ambapo Sultan Jamshid alidokezwa uvumi kwamba kungetokea machafuko siku hiyo usiku au kesho yake lakini kwa kuhakikishwa na waziri wa usalama kwamba huo ulikuwa ni uvumi usio namsingi aliamua kuupuuza.

Jioni ya siku hiyo askri wa kuzuia fujo Kambi ya Mtoni walipewa amri kwenda kuzuia fujo mjini Unguja umbali wa kilomita tatu wakabakia huko usiku huo. Ndipo vikundi vya wananchi viliposhambulia na kuteka Kituo cha Polisi cha Ziwani na kujipatia silaha na hatimaye kushambulia Kituo cha Mtoni kwa uraisi na kuteka silaha nyingi zaidi.

Hadi saa 11.00 alfajiri Vituo vya Ziwani na Mtoni vilikuwa vimesalimu amri, upinzani pekee ukibaki Kituo cha Malindi karibu na bandari ya Unguja.

Wakati huo huo Shamte aliendelea kutapatapa kuomba Uingereza ipeleke majeshi, lakini ombi hilo likakataliwa kwa sababu nchi hiyo haikuwa na mkataba wa ulinzi na Zanzibar. Alitumia ndege ndogo Pemba kuleta silaha lakini ilishindikana kurejea baada ya Uwanja wa Zanzibar kufungwa.

Saa 3.00 asubuhi Sultan Jamshind alitaarifiwa na watu wake kuwa majeshi ya Serikali yalikuwa yameshindwa na kwamba aondoke Zanzibar katika muda wa dakika 10.

Kwa kutumia ulinzi wa Kituo cha Malindi, Jamshid alitoroka jumba la kifalme akaingia kwenye boti iendayo kasi iliyoitwa Salama na kuingia kwenye meli “Seyyid Khalfa” kwenda Mombasa kutafuta hifadhi, lakini Serikali ya Kenya ikamkalia, akageuza njia kuelekea Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumapili ambayo ndiyo ilikuwa siku kwanza ya Mapinduzi machafuko yaliendelea hadi mashambani kwa walalahoi kuwashambulia mamwinyi.

Siku ya kwanza; Jumapili Januari 12:

Asubuhi uvumi ulienea kwamba Mapinduzi yaliendeshwa na vyama vya UMMA na ASP, kwamba UMMA waliratibu oparesheni yote na ASP walitoa askari. Uvumi huo ulisema vijana wa Babu wanashirikiana na washauri kutoka Cuba.



okello.jpg
"Field Marshal" John Okello na wanamapinduzi wenzake.

Jioni ya siku hiyo, mtu mmoja mwenye sauti nzito, alitangaza kwa Kiswahili kupitia Radio Zanzibar na kujitambulisha (bila kutaja jina) kama “Field Marshal” alisema “sasa Zanzibar ni Jamhuri, vyama vya ASP na UMMA vitaunda Serikali mpya, Rais atakuwa Sheikh Abeid Amani Karume”. Katika hali ya kukanganya aliita kwa sauti ya kuamrisha “Karume (popote ulipo) rudi haraka kuchukua nafasi yako”

Inasemekana Karume aliondoka Dar es salaam siku ya Jumamosi kabla ya Mapinduzi kuanza au kushika kasi kwa madai ya kwenda kumweleza Mwalimu Julius Nyerer jinsi Mapinduzi yanavyofanyika na kufuatiwa na Kassim Hanga siku ya Jumapili asubuhi kwa madai ya kwenda kupata bunduki zaidi.

Itakumbukwa kuwa kwamba Babu wa UMMA alikuwa Dar es Salaam tangu alipotoroka huko kukwepa kukamatwa sasa kama wote hawa hawakuweao Zanzibar nani aliongoza Mapinduzi?

Kitu kingine kinachoshangazaa wengi ni kuwa katika orodha ya wajumbe 30 wa Baraza la Mapinduzi iliyotolewa baadaye jina la Okello ni la kwanza lakini Karume halikuwapo hata miongoni mwa majina ya wajumbe 14 wa Kamati ya Mapinduzi (Gazeti la Serikali , Januari 25, 1964).

Usiku siku hiyo Mwalimu Nyerere alionana na Karume Ikulu na kumshauri arudi Zanzibar mara moja baada ya kuona hapakuwa na sababu ya yeye kuwa Dar es Salaam.

Siku ya pili; Jumatatu Januari 13:

Asubuhi “Field Marshal”alijitambulisha kama kawaida kupitia redioni kwa jina la John Okello kisha kwa sauti yenye mamlaka akaendelea kusema: “Sultan amefukuzwa mguu wake hautakanyaga tena ardhi yetu, jumba lake na mali yake itataifishwa” kisha akaiomba Serikali ya Tanganyika ipeleke ndege nzima ya dawa na kuwataka wauguzi wote warudi kazini.

Aliendelea kutamba: “Nitachukua hatua kali, kali mara 88 zaidi, hakuna ruhusa mtu kuacha mke wake atakayefanya hivyo atapata viboko 65; Sultan alikuwa shetani na kibaraka wa mabepari. Mtu atakayejaribu kuwa mnafiki atafungwa miaka 50, atakayeiba hata mche wa sabuni atafungwa miaka minane. Mimi ni Field Marshal naweza kutengeneza mabomu 800 kwa saa moja”

Siku hiyo mchana, Oscar Kambona, Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje wa Tanganyika, alimpigia simu Rais Nyerere kutoka Nairobi kumjulisha kuwa Kenya na Uganda zimeitambua Serikali ya Mapinduzi na kumwomba aitambue pia bila kumeza maneno Nyerere alikataa kwa kuwa hakuwa na hakika kwamba Karume na ASP walikuwa wameshika hatamu na kwamba hakuyapendelea mauaji yaliyokuwa yakiendelea.

Kwa mujibu wa Okello baadaye alieleza kuwa watu 9,999 waliuwawa lakini kulikuwa na taarifa nyingine za kuwa walikuwa ni 200, japo taarifa za Mzungu mmoja Visiwani zilikadiria watu 6,000 kuwa waliuawa.

Vivyo hivyo katika simu hiyo Kambona alimjurisha Nyerere juu ya Sultan Jamshid kukataliwa kutia nanga Mombasa na kumshauri naye asimruhusu, hata hivyo, Nyerere alimjibu Kambona kuwa hakuwa na ugomvi na Sultan, kwa hiyo, hakuwa na sababu ya kutomruhusu nchini.


karume na okello.jpg
KARUME na John Okello

Karume na Hanga waliondoka Dar es salaam kutokea eneo la “Silver Sands” saa 8.00 alfajiri (saa 24 baada ya Mapinduzi kwanza) kuelekea Zanzibar kwa boti ya Fainzilber na kufika Zanzibar saa 6.30 baadaye eneo la Kizimkazi asubuhi ya Jumanne waliomba na kupata usafiri wa gari la mwalimu mmoja wa shule na kwenda moja kwa moja eneo la Raha Leo na kulakiwa na “Field Marshal” wakala chakula pamoja.

Siku ya tatu; Jumanne Januari 14:

“Field Marshal” John Okello alitangaza kupitia redio kwamba mawaziri wanne wa Serikali ya zamani watanyongwa, lakini Karume alipinga siku iliyofuata (Januari 15) kwamba hakutakuwepo kulipiza kisasi.

Siku hiyo Mwalimu Nyerere alikwenda Nairobi kuonana na Waziri Mkuu wa Kenya, Jomo Kenyatta, kuzungumzia uundwaji wa shirikisho la nchi za Afrika Mashariki. Ni katika ziara hiyo Mwalimu alipoanza kubaini kwamba Jomo Kenyatta hakuwa na shauku ya kuundwa kwa shirikisho hilo ambalo ndoto yake haijatokea kuwa ya kweli hadi leo.

Siku ya nne; Jumatano Januari 15:

Sultan Jamshid aliyekataliwa kutia nanga Mombasa na Serikali ya Kenya alitia nanga Dar es Salaam na kuruhusiwa na Mwalimu Nyerere kukaa nchini hadi alipokamilisha mipango yake ya kukimbilia uhamishoni Uingereza siku nne baadaye.

Siku ya tano Alhamisi Januari 16:

Huku “Field Mashal” Okello akiendelea kutoa matangazo mbalimbali kupitia radio, Karume, Babu na Hanga waliondoka kwa ndege kwenda kuonana na Nyerere kumwomba aitambue Serikali yao na kuomba askari wachache kuweza kurejesha amani na utulivu Visiwani. Siku mbili baadaye askari 300 waliwasili Zanzibar.

Okello pengine bila kufahamu juu ya safari ya Karume, Babu na Hanga, alitangaza redioni kulalamika kwamba alifanya makosa kumteua Karume kuwa Rais kwa sababu hakushiriki hata kidogo katika mapambano, hivyo siku hiyo, Okello alijipa mwenyewe cheo cha Rais na kumtangaza Karume kuwa makamu wake.

Mchana “Field Marshal” Okello alitembelea makao makuu yake yaliyokuwa kwenye Jumba la Manjano, Raha Leo ambako umati mkubwa wa watu ulikuwa ukimsubiri kumwona akiwa amevaa mavazi meusi ya kijeshi, mara alipojitokeza tu umati ulizizima kwa shangwe na kupiga kelele “Jamhuri! Jamhuri!.......”

Siku hiyo Okello alikaribisha wageni wa kimataifa na kwa msaada wa mkalimani alizungumza kwa kirefu habari za maisha yake na jinsi alivyopanga Mapinduzi ya Januari 12 bila kumwambia Karume wa sababu angeyazuia kutokana na ukweli kwamba bado alikuwa na matumaini ya kufika mwafaka na Shamte wa kuunda serikali ya mseto.

Huko nyuma Karume alimtumia Shamte ujumbe mara mbili kumbebeleza akubali lakini Shamte alikataa kata kata akitaka ASP kivunjwe.

Siku ya nane; Jumapili Januari 19:

Siku ya sita na ya saba, Okello aliendelea kutangazia umma juu ya Mapinduzi na matarajio yake kama kawaida lakini siku ya nane aliondoka kwenda Dar es Salaam kama mapumziko kidogo baada ya kazi kubwa. Usiku huo alionana na Mwalimu Nyerere Ikulu na alishauriwa kufanya kazi kwa imani na Rais Karume. Aliporejea Zanzibar siku moja baadaye aliambiwa anatakiwa Dar es Salaam. Nyerere alimkamata Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam na kurejeshwa kwao Uganda.



okello ulinzi.jpg
John Okello akiwa chini ya ulinzi

Kwa hiyo wanaharakati hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 1961 na 1963 na kwamba ASP kilidai kupokonywa ushindi. Lakini swali juu ya nani aliongoza Mapinduzi ya Januari 12 halijapata jibu.

Tunaambiwa kuwa ni Mzee Karume aliyeongoza mapambano, lakini hoja hii imejaa ukingu baridi na maswali tele kwa nini alikimbilia Dar es Salaam kabla au mara Mapinduzi. Kama ilikuwa ni kumjulisha Mwalimu Nyerere juu ya Mapinduzi kama alivyodai kwa nini asingepiga simu?

Kwa nini Nyerere hakuyatambua Mapinduzi mapema na kwa haraka kama zilivyofanya Kenya na Uganda? Kwa nini alimhifadhi Sultan Jamshid kwa chukizo la Karume na wanamapinduzi? Kuundwa kwa serikali ya mseto kati ya ASP na Umma kunaonyesha nini juu ya Mapinduzi? Na kama tutakataa kwamba Okello ndiye aliyeongoza Mapinduzi kwa nini aliruhusiwa “kutamba” kwenye radio ya Serikali (mpya) kwa siku nane mfululizo?

Na kama tutakubali kuwa Okello ndiye aliyeongoza na hatimaye Karume (ASP) na Babu (Umma) wakaunda serikali ya mseto Karume akiwa rais na “Field Marshal “ John Okello akatupwa nje; je, tuseme hatua hiyo yalikuwa Mapinduzi ndani ya Mapinduzi?



source http://raiamwema.co.tz/08/01/09/11.php
 
Na kwa Kenya unaweza kutumia analogy hiyo hiyo. Wakikuyu wamehodhi madaraka kwa muda mrefu sana na hawakutaka kuachia makabila mengine. Baada ya wizi wa Kibaki ilikuwa rahisi kwa wakalenjin, wajaluo na wakisii kuwaandamana Wakikuyu kwa mapanga. Very sad, I might add.

..awali,ilishasemwa kwamba kenya imegawanyika,baada ya yale matokeo.wakamba,wameru na wenzao wachache wa central wakaungana na wakikuyu.na hao uliowataja plus waluya na watu wa pwani[waislam]wakaungana dhidi ya kibaki.

..sasa hiyo ukiunganisha na class war[watu wa hali duni kuchoka hali waliyonayo na kutaka mapinduzi]inaifanya kenya iwe katika vita,ambayo haitaisha mapema kama ambavyo kibaki & company wanavyofikiri kwa kutumia dola itakuwa.mbaya wanaelekea kui-polarize hiyo dola.

..walafi na wenye woga hawaoni chombo kikienda mrama!wamepumbazwa na fikra zao!
 
Huyo Okello hata kama alikuwa na ushujaa na uwezo wa kupanga na kutekeleza mapinduzi, hakika hakuwa na uwezo wa kuongoza serikali wala kushiriki katika serikali yoyote, kama kauli zake zilizoandikwa na Mihangwa hapo juu ni za kweli. Inaelekea jamaa alikuwa "analikoka" bange, sina maelezo mengine kwa mtu mwenye lugha kama hiyo!

Lingine, kama mtu anayeshindwa kwenye uchaguzi (ambao hajalalamikia kasoro zake kama zipo) anaamua kuchukua madaraka kwa nguvu, haya si mapinduzi ni ubakaji. Unabembeleza wee, unakataliwa, unaamua "kupiga ngwala"! Noma sana! Kama rekodi za Mihangwa ni sahihi (sina data za kupingana nazo), basi waasisi wa mapinduzi wataniwia radhi, maoni yangu ndio haya.
 
Huyo Okello hata kama alikuwa na ushujaa na uwezo wa kupanga na kutekeleza mapinduzi, hakika hakuwa na uwezo wa kuongoza serikali wala kushiriki katika serikali yoyote, kama kauli zake zilizoandikwa na Mihangwa hapo juu ni za kweli. Inaelekea jamaa alikuwa "analikoka" bange, sina maelezo mengine kwa mtu mwenye lugha kama hiyo!

Lingine, kama mtu anayeshindwa kwenye uchaguzi (ambao hajalalamikia kasoro zake kama zipo) anaamua kuchukua madaraka kwa nguvu, haya si mapinduzi ni ubakaji. Unabembeleza wee, unakataliwa, unaamua "kupiga ngwala"! Noma sana! Kama rekodi za Mihangwa ni sahihi (sina data za kupingana nazo), basi waasisi wa mapinduzi wataniwia radhi, maoni yangu ndio haya.

..kithuku,neno lenyewe[mapinduzi]linajieleza!
 
Sultani alikuwa ni mkuu wa nchi tu, na serikali iliongozwa na Waingereza na Baada ya Uchaguzi wa July 1963 Sultani alibakia kuwa kiongozi wa nchi ila Serikali iliongozwa na Wazenji wenyewe.
Uchaguzi ulikwenda poa na ASP ikaanguka, hakuna kuibiwa kura wala manung'uniko yoyote, walifeli coz ya sera zao hazikukubalika na wananchi wakati huo.

Mapinduzi ni uonevu tu, na wala hakukuwa na sababu yoyote kufanya hivyo, demokrasia tayari ilishajikita, ilitakiwa ASP wajipange vizuuri tayari kwa uchaguzi unaofuatia.
Kutoka hii 12/1/64 Zanzibar ndio mwanzo wa kupoteza direction yake hadi hii leo, watu wazito wamechinjwa (wasomi), ili tu watawale bila ya kupata oppose yoyote.

Sasa zimwi linatuandama, kila uchaguzi tunapindua!
 
Back
Top Bottom