Nonda,
..suala la kujitambulisha kama Mtanzania au Mtanganyika ni suala ambalo naweza kusema ni la "mafundisho" na "mapokeo."
..binafsi nimezaliwa na kukulia Arusha, lakini wazazi wangu wamezaliwa mkoa mwingine.
..sasa kutokana na mafundisho na malezi ya ndani ya nyumba yetu, leo hii ukiniuliza natokea mkoa gani ktk Tanzania/Tanganyika, bila shaka yoyote ile nitakwambia nimetokea kule walikozaliwa wazazi wangu.
..kutokana na experience yangu hiyo, ndiyo maana nime-conclude kwamba, kwa wenzetu wa-Zanzibari hazikufanyika juhudi zozote zile za kuwaelimisha kwamba baada ya muungano basi ni vema wakachukua identity/utaifa mpya wa TANZANIA.
..naamini pia kuna mambo mengi ya KIHISTORIA na KISIASA yaliyosababisha muungano wetu uchukue sura iliyoko sasa hivi. kwa mfano, kuna tetesi za Wazanzibari kuogopa "kumezwa" kama kikwazo cha kuwa na nchi moja, serikali moja.
Nonda said:
Kweli inawezekana kabisa kuwa muungano wetu unasifiwa sana lakini ukweli unabaki kuwa katika uhai wa muungano wetu hakuna nchi nyengine iliyotamani kujiunga nasi. Ni kwa sababu gani?.
Tumeona Burundi na Rwanda wameona ni bora kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa nini hawakuomba kujiunga nasi tukawa nchi moja wakati tuliwahifadhia watu wao (wakimbizi)? Wao wanajuwa kuwa sisi ni watu wema sana na tunawajali watu wetu, watu wa utulivu na amani.
..kwa kweli kipengele hicho hapo juu sina jibu la uhakika la kukutosheleza. lakini ngoja nijaribu:
..je, tuna uhakika kwamba Rwanda,Burundi, etc hawajaomba kujiunga nasi kutokana na kuona matatizo tuliyonayo sisi, au kutokana na matatizo yao wenyewe, haswa ya viongozi wao?
..is it easy kwa kiongozi aliyekwisha onja madaraka ya Uraisi, akaitumbukiza nchi yake ktk muungano, huku yeye akiwa hana uhakika na nafasi yake ktk muungano huo?
..kwa sababu tunaelewa kabisa kwamba kuna baadhi ya wananchi wa Rwanda na Burundi ambao ilibidi waondoshwe kwa nguvu kuwarudisha nchini kwao.
..binafsi nadhani wakati mwingine haya masuala ya kuunganisha nchi yanahitaji viongozi kuonyesha njia. vilevile zaidi ya viongozi kuonyesha njia kunatakiwa kuwepo na jitihada za makusudi na za muda mrefu kuhakikisha kwamba wananchi wanakubaliana na hatua zilizochukuliwa na viongozi wao. reference nzuri kwa hoja yangu hii ni matatizo yaliyotokea Yugoslavia.
Nonda said:
Pia nakuomba kama unajuwa muungano mwengine wowote wa nchi ambao umezifuta, umeziua nchi wanachama asilia hapa duniani.
..again, sina jibu la uhakika kwa swali lako hili. sijachimba vizuri kujua muungano kama wa USSR au ule Yugoslavia ulikuwa wa namna gani.
..inawezekana ukawa na hoja kwamba hakuna muungano ambao umefanikiwa kuzifuta nchi zilizounda muungano huo.
..lakini haya vilevile ni masuala ya kisiasa na kijamii. kushindwa kwa mataifa mengine kuungana na kuunda utaifa mpya, isiwe kisingizio cha wa-Tanganyika, au wa-Zanzibari, kuukana u-Tanzania. nini kinachotuzuia sisi kuwa wa kwanza, na mataifa mengine kuiga kutoka kwetu?