Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hujakosea bwana watu wasikulaumu!Hii JF naona imekuwa ni jukwaa la watu kuponda tu bila hata kuanalyse mambo kwa kina!Hata Kama mada Hijaendana na title still kuna vitu vya msingi kwenye topic pia content vya kuweza ku discuss. Imekuwa kama ni jambo la Uhaini watu kuhoji status eidha ya Tanganyika au zanzibar kwenye Muungano.Hata mkataba ulionzaisha muungano ukihoji upo wapi utafungwa!Mimi naona kuna Masuala ya muhimu ya kujadili Muungano kwa ujumla si katika nia ya kutaka Kuvunja muungano bali katika nia ya kujaribu kujenga na kuweka mambo wazi kiasi kwamba Tusije tukakabidhi next Generation unstable union ambayo itafall after few yrs!Look how america united,or East& west German or united Kingdom!Tatizo letu ni wazembe wa kufikiri!Kama hatutaweza kutatua matatizo yanayokumba Muungano kwa sasa,tukuwa tunachezea Mustakabali wa Muungano wetu na jamii ambayo tumekuwa ndugu tangu miaka 1600 iliyopita!

hata kama ni kuvunja muungano ni sawa tu! Kama uliungwa basi waeza vunjwa tu... Hasa maelewano tu na kila mmoja akiridhika na hasa ikichukuliwa kwamba kila mmoja ameshakuwa na kukomaa! Tanganyika na Zanzibar ni watu wazima sasa 40's yrs of age!
 
Kuna kila dalili ya mbunge fulani kuleta hoja juu ya muungano. Wasiwasi wangu ni kama hoja hiyo itapita maana wakati wa G55 bunge lilikuwa la CCM pekee. Kwa hivi sasa kuunga hoja ya upande mwingine ni sawa na kusaliti chama.
 
Zilikuwa ni sauti za chini chini zilizosikika hapo awali kuhusu matatizo katika muungano, lkni sasa kilio kimekithiri mpaka 'mkuu wa kaya' kudiriki kuunda wizara ya kushughulikia kero za Muungano.Hata hivyo kila uchao malalamiko ya kila upande;yaani Zanzibar na Tanganyika yanazidi kuongezeka!

Wazanzibar wana malalamiko kem kem kuhusu kuukataa Muungano vivyo hivyo kwa Tanganyika!Kwa mfano Zanzibar kuna wanaodai kuwa wametawaliwa na ukoloni Tanganyika na Tanganyika nao kuna wanaodai kuwa wamechoka kuwabeba wazanzibari!

Ukweli uko wapi wanajamvi? Ni wazi kuwa kero zipo,lakini nani anaumia zaidi katika muungano huu na nini kifanyike?Ni lipi lengo la waasisi wa Muungano huu na je limefikiwa?Ungekuwa wewe ni mwenye mamlaka na mwenye maamuzi ya mwisho ungefanya nini?

Naomba tutumie busara zaidi katika kujadili hili kwani huenda ikaleta kwani wigo wa JF ni mpana na hupitiwa na wengi,mimi sipo bongo kwa sasa ila kuna wageni hupenda kuangalia jinsi Watanzania tujadilivyo mambo yetu!
 
WanaJF na wageni munaotembeleao JF

MUUNGANO UNAPOKUWA NI KERO.

Haya ya kero za muungano ,tumeambiwa yalianza kushughulikiwa siku nyingi zilizopita, in fact, miaka mingi iliyopita.
Hivi sasa kuna kamati ya kushughulikia kero za muungano. Hata kama kamati hii ilianzishwa kwa nia njema lakini sinaimini kama kweli kero za muungano zitatatulika. Kwani kero hizi zina mizizi merefu, au kwa makusudi ziliachwa zikue.
Kwa vile, kero za muungano zimeshajadiliwa na wengi na kwa vile serikali wamekiri kuwa kuna kero katika muungano, mimi niende kwenye kuonesha kwa nini Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kero.

Kuna dhana katika vichwa vya wananchi wa pande zote mbili za Muungano huu.

Wananchi wa iliyokuwa Tanganyika wanalalamika kuwa "Kajikasehemu kadogo" (wao hawataki kukitambua kasehemu hiki kama nchi), wanafaidika wa muungano, "tunawabeba" "tunawapa umeme bule", "waende zao" "wajikate, watuachie nchi yetu"

Watanganyika(watanzania bara) wanahoji kwa nini waendelee kuubeba mzigo (Zanzibar) ambao hauna faida yoyote kwao, isipokuwa kuwasumbua kila jua linapochomoza asubuhi.

Kwa upande mwengine, Wananchi wa Zanzibar (Wazanzibari) ndio waliokuwa wa mwanzo kupiga kelele, kulalamika kuwa wanabanwa, wanabinywa na muungano(Tanganyika) na kuna njama za kuimeza nchi yao. Wanasikika wakisema "Muungano hautufanyii haki", Wanatubinya", "wanatukandamiza" "wanatutawala" "mkoloni mweusi" , "wanatuchagulia viongozi ambao hatuwataki"

Ukipitia mijadala humu JF na mzalendonet, utakubaliana na mimi kuwa urushianaji wa maneno haya upo kwenye kila ishu inayohusu Muungano na kero zake.

Kambi hizi mbili zinarushiana madongo kama vile mwendawazimu aliyekabidhiwa rungu. Wanadundana kwa hamasa. Imefikia hatua kuwa hakuna anaetowa facts ku-back wanachokisema. Bora mtu aseme tu.

Ukiwa na muda wa kusoma na kutafiti, kuna maandiko mengi ,na tafiti nyingi ambazo zimesheheni facts kuonesha kuwa Muungano wetu una walakini mkubwa, kasoro nyingi. Kuendelea kuzipuuza,"put under the carpet" ni sawa na "Tusipoziba ufa….." au "mdharau donda………………."

Hata wasomi wetu mahiri inafika mahali wanajisahau, wanapozungumzia muungano. Huongozwa zaidi na ushabiki wa sehemu wanazotoka. Inakuwa kama vile ni mechi kati ya Simba na Yanga. Wasomi wetu wangeweza kutusaidia sisi ambao uelewa wetu ni mdogo, na elimu zetu ni ndogo katika suala zima la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hasa kujibu suali jee muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikusudia kuzifuta Nchi za Tanganyika na Zanzibar?
Na kama lengo lilikuwa ni hilo kwa nini Zanzibar ilibakia kuwepo pamoja na vyombo vyake vyote kama dola?

Mpaka hapa, nimeepuka kwa makusudi kutumia jina Tanzania kwa sababu maalum.
Ni kujaribu kumfanya msomaji ajuwe vipi Tanzania imepatikana.
Pitia hapa Uione Tanganyika na Zanzibar zilivyokuwa.

http://unimaps.com/tanzania1886/index.html
http://unimaps.com/tanzania1901/index.html
http://unimaps.com/tanzania/index.html

Kwanza nataka nikushawishi wewe msomaji kuwa Tanzania ni jina la kubuni lililokusudiwa kupunguza urefu wa Tanganyika na Zanzibar. Aliyebuni jina hili alifanya hivi Tan(ganyika) na Zan(zibar). Alipounganisha akapata TanZan. Akaona halina ladha kimatamshi. Alipojikuna kichwa, akatanabahi kuwa nchi nyingi za kiafrika zimeishia na – ia, kama Nigeria, Ethiopia, Namibia, Gambia, Algeria. Kwa hiyo akapata kitia ladha –ia na akakibandika katika Tan-Zan-ia.

Hebu jaribu kulisema jina hili sasa "TanZania".
Jaribu na hili "Zan-Tan-ia".
Kiswahili kina ladha yake, au vipi? Ni wazi neno tanzania lina ladha zaidi kimatamshi kuliko zantania. Muungano wetu na baadae Nchi yetu ingeweza kuitwa , Zantania.
Na sisi utaifa wetu leo ungelikuwa ni uzantania.
Wala hatukupenda kuuita muungano wetu Tangazabar au Zanzinyika, kama walivyofanya Senegambia.

Katika kanuni za kiuandishi, waliolibuni jina hili iliwapasa pia kuindosha herufi kubwa ya Z ili iendane na utashi wa kiuandishi. Wakatupatia, Tanzania yetu. Imependeza au vipi wadau ?
Waliamua kuitupilia mbali kanuni ya Acronymization.

http://www.google.com/dictionary?q=acronymization&hl=en&langpair=en|en&spell=1&oi=spell

Si unajuwa kuna UK, USA, UAE, UN, kulikuwa na USSR, Yugoslavia.

Kwa hiyo muungano wetu tokea kuzaliwa kwake ulianza kuwa kero. Kero ya jina refu kwa hiyo dawa yake ikawa ni kulifupisha. Na sasa Zanzibar "kasehemu kadogo" hakistahili kuwa nchi, tukifanye mkoa au wilaya. Hii ndio mantiki ya serikali mbili kuelekea moja.

Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kuijenga Afrika Mashariki, na hapa JF tunalalama sana kuwa serikali isituharakishe, isituburuze kututumbikiza huko.Tunahitaji muda kujitayarisha. Tuna hofu kuwa Wakenya na Waganda watatuburuza.

Lakini mantiki hii haifanyi kazi inapotokea kuwa ni wazanzibari(Zanzibar) wanaposema "Muungano(Tanganyika)Unaniumiza!"; "Unaniburuza", "Sivyo hivi tulivyokubaliana"

Leo inapotokea kuwa Zanzibar wana malalamiko yao wajadiliane na nani wakati inasemwa Tanganyika haipo?
Utasikia kuwa Serikali ya Zanzibar inakaa na Serikali ya Muungano kuzungumzia kero.
Unategemea hapo kuwa viongozi wetu wapo serious?
Zanzibar hakuungana na Serikali ya Muungano ,yeye ni sehemu ya Muungano huo. Tanganyika hana tatizo hili, kwani Tanganyika amejifanya kuwa ni kaka kiranja.
Sehemu pekee ambapo Tanganyika au Zanzibar wangepata suluhu na kuhisi kuwa haki imetendeka ni kupitia mahakama ya katiba au international court.
Au ingetokea kuwa Tanganyika au Zanzibar mmoja wao anataka ku-negotiate tena mkataba wa muungano, inapaswa iwepo Tanganyika na Zanzibar. Au mkataba wa kimataifa huwa hauna Exit clause?

Hili la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tulilikoroga tokea mwanzo na haionekani kuwa kuna uwazi, uadilifu, ujasiri na "will" ya kulishughulikia hata baada ya kungunduwa kuwa Muungano wetu una kasoro nyingi. Siku za nyuma tumetumia kuwafukuza uanachama na kuwavua madaraka yote wazanzibari waliokuwa na ujasiri wa kupiga ukelele "unaniumiza"

Tanzania kama nchi na Utanzania kama utaifa.
Kama nimeweza kukushawishi ,at least , kujua kwa vipi tumelipata jina Tanzania basi sasa prepare for a shock! …………..Not really!

Hapa Jf nimesoma katika threads kadha wachangiaji wanalalama kuwa " wenzetu wanajivunia Uzanzibari wao zaidi kuliko Utanzania"

Nimeshawahi kukutana za watu ninaposafiri nje ya Tanzania na huwa ninapowasikia wanazungumza kiswahili huwasalimia na huwauliza wanatokea wapi, huniambia wanatokea Tanzania.
Ninapowadadisi zaidi huniambia " mimi mwenyeji wa zanzibar", "mimi natokea Arusha", mimi natokea Mbeya" nk.

Kwa hiyo wewe ni mzanzibari? Nikimuuliza huonekana akitabasamu na husema , Yap, mimi ni mzanzibari, visiwa vya marashi ya karafuu,

Ama kwa muArusha nikimuuliza kwa hiyo ,wewe ni Mtanganyika? Huonekana hapendezwi na suali langu au hunijibu mimi ni mtanzania au mchaga. Nk.

Kama ambavyo inaonekana katika mifano hii, mimi hujiuliza kuna ubaya gani kwa Mtanganyika kujinasibu/kujivuna na utanganyika wake?
Who did make us feel ashamed of calling ourselves Tanganyikans?
Or at least saying, I come from the Tanganyika part of Tanzania!

Leo kutaja jina halali la Tanganyika, mtu huonekana kama anatenda kosa la jinai. Leo linatumika zaidi Tanzania bara na pia Tanzania visiwani. Wenyeji wa Ukerewe na mafia wao wataitwa wenyeji wa wapi?
Tanzania bara!!?
Hili linaongeza complication katika hali ambayo tayari watu wanatatizika.

Ukweli unabaki kuwa si rahisi kuufuta utaifa wa mtu, wazanzibari wanajivuna ni wazanzibari kwanza kabla ya kuwa watanzania wanapokuwa ndani ya Tanzania.na wanakuwa watanzania wanapokuwa nje ya Tanzania. Wanalazimika kuwa hivyo hata kama hawapendi kwani inawalazimu kutumia pasi za kusafiria za Tanzania.(Pasipoti ya Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar)

Mtikila na wakati fulani kundi la G55 walijikakamua kutaka Tanganyika ndani ya muungano. Matokeo yake tunayajuwa yalikuwaje. Na kilio hiki cha "tuirejeshe Tanganyika yetu" kinasikika kutoka kwa watanzania bara wanapokuwa-fed up na manung'uniko ya wazanzibari.

Tungeendelea kutumia jina la awali, hata kama lilikuwa ni refu, yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haya malumbano ya utaifa yangelikuwa hayapo.Tungepata muda na nafasi ya kushughulikia kero za muungano badala ya muungano wenyewe kuwa ni kero kwa wananchi wa Tanganyika na Zanzibar.

Karibuni .
 
Kuna mambo yananitatiza kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Inashangaza ukiwa na leseni ya uderevya iliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano, haitambuliki nzanzibar. unatakiwa kuombea kibari cha kuitumia ukiwa Zanzibar. Kwa uelewa wangu kibali utolewa kwa wangeni watokao nje ya inchi.

Swali langu kubwa ni kwanini mwajiriwa wa Wizara ya mambo ya ndani (askari wa usalama barabarani-Zanzibar),hasiitambue leseni halali iliyotolewa na mwajiri wake kwa kisingizio cha kuwa haijatolewa Zanzibar?
 
Eti nisaidieni,au Tanganyika ndio Tanzania? Hapana, Tanzania ni acronym ya majina mawili, Tanganyika na Zanzibar. Sasa mbona Zanzibari bado inaishi!!,tanganyika siioni!!

Hata ktk mashindano ya soccer ya challenge yanayoendelea, mbona timu ya Zanzibar jezi zake zimeandikwa ZANZIBAR na timu inaitwa Zanzibar? Timu ya bara inaitwa Kilimanjaro staz, jezi zake hazijaandikwa jina la nchi, Kili staz inawakilisha nchi gani?

Kwa nini zisingeandikwa Tanganyika? Au tanganyika imekufa? Sasa si zingekufa zote Zanzibar na Tanganyika! Au mnaonaje linapokuja swala la pande hizi mbili za muungano kushiriki kila moja kivyake kama ilivyo ktk soccer,tutumie bara kwa upande mmoja na visiwani kwa upande wa pili,hata jezi zionyeshe hivyo.Kuna nini hapa chafichwa?

Mie nabata ushungu.
 
mkuu,

Mkuu usipate tabu katika hili, Kilimanjaro stars inawakilishisha nchi iliyopata uhuru 09,Disemba. lakini ni dhambi, uhaini kuitaja kwa sauti. Na ile timu iliyovaa jezi zilizoandikwa Zanzibar, ni kuwa wazenj wanatushinda sisi huku "Tanzania" kwa uzalendo!
 
Hello chigwiye ukiendelea kuuliza hil swali shauri yako.utaitwa mchochezi au mhaini.Tanganyika ni ziwa eti tuamin hivyo
 
yamejadiliwa sana hapa, utakayoleta ni marudio tu!

Mkuu,

Kuna ubaya gani katika kurudia rudia? Si ndio kukumbushana kwenyewe huko? Unaona hapa kila leo kuna watu wepya wanajiunga na JF. Au kuna topics ni marufuku kuzianzisha?

Pia unajuwa kuwa sisi watanzania ni wasahaulifu sana.Tunasahau vitu, mambo kwa kasi ya ajabu!
 
Nonda,

..mimi ni baadhi ya wale ambao ukiniuliza utaifa wangu natamka kwa fahari kwamba ni Mtanzania.

..nimefikia hapo kwasababu nimezaliwa na kukua wakati nchi hii inaitwa Tanzania.

..wakati tuko shuleni tulifundishwa kwamba Tanzania imetokana na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

..tulifundishwa kwamba Watanganyika na Wazanzibari ni ndugu na ndiyo maana wakaungana na kuunda nchi moja Tanzania.

..pia tulifundishwa kwamba kuna nchi nyingine zilizojaribu kuungana kama sisi lakini kutokana na ubinafsi wakashindwa, kwa hiyo muungano wetu ulikuwa ni kitu cha fahari na mfano kwa nchi nyingine za Kiafrika.

..vilevile tulifundishwa kwamba muungano wetu ni hatua ya kuelekea kuunganisha nchi zote za Kiafrika na kuunda taifa moja la Waafrika.

..binafsi sidhani kama haya majina yana umuhimu sana. wakati unauliza kwanini watu hawaoni fahari kuitwa Watanganyika, wengine wanaweza kwenda mbali na kusema wao walikuwa raia wa Deustch-Ostafrika ile ya wakati wa Mjerumani, na wengine wanaweza kwenda mbali zaidi ya hapo.

..kwa kifupi nadhani Watanganyika tuliukubali Muungano na kila juhudi zilifanyika ktk kuwaelimisha na kuwaaminisha wananchi kwamba muungano wetu na muhimu na kitu cha kuonea fahari.

..kwa upande mwingine inaelekea Zanzibar hazikufanyika juhudi kama hizi za huku bara kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa muungano wetu. hakukuwa na juhudi za kutosha kuhakikisha kwamba Wazanzibar wanachukua utaifa mpya wa Tanzania.
 
Hapa JF kisichotosha ni Mbowe, Slaa Vs Zito!
 
Hakuna la kweli hata moja kati ya haya na nina uhakika kuwa unajuwa hilo sasa!
 
Uliyoyasema ni mazuri tu. Kwa vile umesema umezaliwa katika Tanzania ni vizuri kuisoma historia ya Tanzania imetoka wapi, vipi ilikuja na makusudio yake.

Nina hakika Mkuu, JokaKuu kama una kabila basi pia unajivunia kabila lako, kwa mfano kama wewe ni mzaramo, hutasita kusema wewe ni mtanzania pia ni mzaramo.

Kwa bahati ya kuchanganyika sana kama ilivyo desturi ya watu wa visiwa. watu wa Zanzibar wengi hujitambulisha kuwa wao ni watanzania, lakini pia ni wazanzibari na wakiendelea chini wanasema wao ni watumbatu, wahadimu, wapemba, utaona hapa ukabila wao ni sehemu walizokulia au wazazi wao walizokulia. Dhana ya ukabila Zanzibar haiko sawa na ya huku Tanganyika.
Kwa hiyo, tusiwalaumu kabisa kwa wazenj ,kujitambulisha kama wazanzibari.

Lakini pia kama unakubali kuwa Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi wewe na mimi tunaweza kusema kuwa ni watanzania,watanganyika, wadendereko. Kwangu mimi sioni shida yoyote hapa.

Kweli inawezekana kabisa kuwa muungano wetu unasifiwa sana lakini ukweli unabaki kuwa katika uhai wa muungano wetu hakuna nchi nyengine iliyotamani kujiunga nasi. Ni kwa sababu gani?.
Tumeona Burundi na Rwanda wameona ni bora kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa nini hawakuomba kujiunga nasi tukawa nchi moja wakati tuliwahifadhia watu wao (wakimbizi)? Wao wanajuwa kuwa sisi ni watu wema sana na tunawajali watu wetu, watu wa utulivu na amani.

Pia nakuomba kama unajuwa muungano mwengine wowote wa nchi ambao umezifuta, umeziua nchi wanachama asilia hapa duniani.

Nimesikia Jumuia ya Afrika Mashariki watatoa Pasi ya kusafiria ya pamoja. Unafikiri umoja huu kuna siku utaziua,kuzifuta nchi wanachama wake? Na kama itakuwa hivyo utakuwa tayari kuuacha utanzania na kuwa Mu-east Afrika tu?
 
Comoro wanataka kujiunga na sisi, kama unafuatilia matukio! labda nikuulize tukijiita mtanganyika itatusaidia kujenga zahanati, shule, barabara, nk?
 
Comoro wanataka kujiunga na sisi, kama unafuatilia matukio! labda nikuulize tukijiita mtanganyika itatusaidia kujenga zahanati, shule, barabara, nk?

Mkuu ,
kwani utanzania umetusaidia kutekeleza hayo?
 
Comoro wanataka kujiunga na sisi, kama unafuatilia matukio! labda nikuulize tukijiita mtanganyika itatusaidia kujenga zahanati, shule, barabara, nk?

Mkuu Buchanan,

Baada ya Comoro kujiunga nasi, tutabadilisha jina la nchi yetu na utaifa wetu?

Kwa mfano nchi yetu itaitwa Cotanzania? Tanconzania ? Tanzancomia ? Au !!??
 
Nonda,

..suala la kujitambulisha kama Mtanzania au Mtanganyika ni suala ambalo naweza kusema ni la "mafundisho" na "mapokeo."

..binafsi nimezaliwa na kukulia Arusha, lakini wazazi wangu wamezaliwa mkoa mwingine.

..sasa kutokana na mafundisho na malezi ya ndani ya nyumba yetu, leo hii ukiniuliza natokea mkoa gani ktk Tanzania/Tanganyika, bila shaka yoyote ile nitakwambia nimetokea kule walikozaliwa wazazi wangu.

..kutokana na experience yangu hiyo, ndiyo maana nime-conclude kwamba, kwa wenzetu wa-Zanzibari hazikufanyika juhudi zozote zile za kuwaelimisha kwamba baada ya muungano basi ni vema wakachukua identity/utaifa mpya wa TANZANIA.

..naamini pia kuna mambo mengi ya KIHISTORIA na KISIASA yaliyosababisha muungano wetu uchukue sura iliyoko sasa hivi. kwa mfano, kuna tetesi za Wazanzibari kuogopa "kumezwa" kama kikwazo cha kuwa na nchi moja, serikali moja.

Nonda said:
Kweli inawezekana kabisa kuwa muungano wetu unasifiwa sana lakini ukweli unabaki kuwa katika uhai wa muungano wetu hakuna nchi nyengine iliyotamani kujiunga nasi. Ni kwa sababu gani?.
Tumeona Burundi na Rwanda wameona ni bora kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa nini hawakuomba kujiunga nasi tukawa nchi moja wakati tuliwahifadhia watu wao (wakimbizi)? Wao wanajuwa kuwa sisi ni watu wema sana na tunawajali watu wetu, watu wa utulivu na amani.

..kwa kweli kipengele hicho hapo juu sina jibu la uhakika la kukutosheleza. lakini ngoja nijaribu:

..je, tuna uhakika kwamba Rwanda,Burundi, etc hawajaomba kujiunga nasi kutokana na kuona matatizo tuliyonayo sisi, au kutokana na matatizo yao wenyewe, haswa ya viongozi wao?

..is it easy kwa kiongozi aliyekwisha onja madaraka ya Uraisi, akaitumbukiza nchi yake ktk muungano, huku yeye akiwa hana uhakika na nafasi yake ktk muungano huo?

..kwa sababu tunaelewa kabisa kwamba kuna baadhi ya wananchi wa Rwanda na Burundi ambao ilibidi waondoshwe kwa nguvu kuwarudisha nchini kwao.

..binafsi nadhani wakati mwingine haya masuala ya kuunganisha nchi yanahitaji viongozi kuonyesha njia. vilevile zaidi ya viongozi kuonyesha njia kunatakiwa kuwepo na jitihada za makusudi na za muda mrefu kuhakikisha kwamba wananchi wanakubaliana na hatua zilizochukuliwa na viongozi wao. reference nzuri kwa hoja yangu hii ni matatizo yaliyotokea Yugoslavia.

Nonda said:
Pia nakuomba kama unajuwa muungano mwengine wowote wa nchi ambao umezifuta, umeziua nchi wanachama asilia hapa duniani.

..again, sina jibu la uhakika kwa swali lako hili. sijachimba vizuri kujua muungano kama wa USSR au ule Yugoslavia ulikuwa wa namna gani.

..inawezekana ukawa na hoja kwamba hakuna muungano ambao umefanikiwa kuzifuta nchi zilizounda muungano huo.

..lakini haya vilevile ni masuala ya kisiasa na kijamii. kushindwa kwa mataifa mengine kuungana na kuunda utaifa mpya, isiwe kisingizio cha wa-Tanganyika, au wa-Zanzibari, kuukana u-Tanzania. nini kinachotuzuia sisi kuwa wa kwanza, na mataifa mengine kuiga kutoka kwetu?
 
Back
Top Bottom