Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
mtu wa pwani

yalosemwa waloongea yanatosha,muda wa actions umefika no matter wat.

sometime ili uhuru upatikane lazima wengine wakubali familia zao zikae VIZUKA n.k.

warejee ktk maongezi gani tena jamani?

acha ajenda irejeswhe kwa wananchi waamue wanavyotaka.

na kama CUF watashindwa kuamua hilo,basi wafanye yafuatayo:

-CHAMA KIVUNJWE,seif aendelee kupata mafao yake ya smz.
-abubakar na wenzake waendelee kunenepeana kula per diem za smz ktk baraza la wawakilishi.
-ile ofisi yao ya mtendeni,wawakodishe kikundi cha TAARAB CHA NADI IKHWAN SWAFAA wafanyie mazoezi jioni.
-juma duni na wenzake warudi IFM wakoembe kuwa lecturers.

KHALAS.

Sadakta. Yarabi Mwenyezi Mungu ateremshe rehma zake. Tuanzie na familia ya kwako Mheshimiwa kuiwekea vizuka. Amin.
 
Bongo maendeleo hayatapatikana hivi hivi hata siku moja jamani, mimi nawambia tuingie msituni jamani, tutakaokufa poa tu, ili mradi vita ikiisha heshima itakuwa imerudi na maendeleo yataanza upya kwa kuijenga nchi
Tumechoka sasa looooooooooooooooo

Haya mambo ya kuingia msituni sidhani kama kuna mtu anayahitaji sasa hivi mkuu. Utapata wapi silaha, utazigawa vipi kwa watu, na kisha baada ya vita utazikusanya vipi na kuzirudisha kwenye gala la silaha?

Hii kwa mtizamo wangu sio viable solution! Kuna mengine mengi yanaweza kufanyika zaidi ya hili. Hata hivyo unaweza kukusanya watu taratibu kama unaweza na kuanza kazi. Ukimaliza vita kama utakuwa bado hai, rudi hapa kwenye meza ya majadiliano ili kusaini mkataba wa amani?! .... kwani usiende moja kwa moja kwenye meza ya mkataba wa amani?
 
Hivi Karume ndie kikwazo au ni Kikwete? (au wote kwa pamoja?). Kuna kila sababu ya kuanzisha kampeni za nguvu ili wale ambao ni vikwazo wanyimwe viza za kuingia nchi za Ulaya na Marekani. Kama Kenya walilazimishwa kwanini isiwe Tanzania?
 
Chama Cha Majambazi (CCM) sio chama cha kuaminika hata kidogo, siku zote watatumia kila aina ya njia za ulaghai na udanganyifu ili waendelee kutawala. Nadhani Wazanzibar wameshavumilia vya kutosha na kuendelea kukubali huu upumbavu unaoletwa na CCM itakuwa ujinga mwingine. Sitoshangaa CCM wakiitisha hizo kura za maoni halafu wakaiba tena hizo kura na kuweka matokeo wanayotaka wao. Yaani ni usanii mtupu unaoendelea ambao uunaongozwa na Msanii Mkuu Jakaya Kikwete.

Maneno yako Mkuu ni sahihi kabisa - huo ndio ukweli wa mambo ulivyo CCM hawana nia wala adhima ya kufanya mabadiliko ya kisiasa Znz na Tanzania kwa ujumla na wataifikisha nchi hii pabaya - la kujiuliza ni wapi utaanza moto kuwaka na matokeo yake yatakuwa nini?
 
Vipi yakhe sasa wewe ulitaka awe dikteta. Awazuwie wajumbe kutoka Zanzibar wasiseme, pale, maoni ya wanaowawakilisha. If peoples power fahamu tu iko pande zote. Usiione hiyo iliyoko CUF tu bali CCM-Zanzibar nako pia iko na ndiyo kubwa (the latent people's power). Ni vyema kuwasikiliza kama hawataki mseto wanataka nini na siyo kuwashurutisha (kuwalazimisha) katika jambo ambalo linagusa maslahi na maisha yao ya kila siku. Kwani solution huko ni mseto tu. Jee, hakuna njia mbadala?

Nafikiri hii issue wengi wetu tunaona ni katika njama za CCM kutafta sababu ya kutokupatikana Muafaka kutokana na historia na matukio la jambo lenyewe kwani hawana ustaarabu wa kutimiza miadi - kama ni kura ya maoni kwa nini wapoteze muda wa karibu miaka miwili na hela za Taifa kufanya mazungumzo na mwisho waseme wanataka kurud kwa wananchi - toka lini CCm ikafanya hivyo katika maamuzi yake?

Kusema CCM Znz ni majority ni uongo na ndio maana kukatokea huu mzozo - wewe mwenyewe unajua kuwa uchaguzi wa mara zote ulikuwa na dosari nyingi tu baadhi yao zikiwa kutumia nguvu , uandikishaji wa wapiga kura wasiostahiki , kunyimwa haki ya kupiga kura wafuasi wa CUF nk na yote hayo matkeo yake ikawa ni ushindi wa tafauti ya asilmia izozidi 4.5. Sasa majority hiyo ni kwa mtazamo wa CCM tu.

Mzee mwanakijiji. Wewe unaonekana kuwa ni mtu wa busara labda kidogo tu nikupe tip. Mara nyingi Wazanzibari ni (washairi) wana mtindo wa kusema between the lines. Naamini hoja ya-basi na tufanye kura ya maoni yakhe- ina maana ya kutabanahisha kuwa kauli ya kuwa watu wote wanataka mseto siyo ya kweli, hasa katika mazingira ya viongozi tulionao hivi sasa (pande zote CUF na CCM Zanzibar ambao tunatarajia kuwaweka katika mseto- ukweli nikuwa hawatapikika) Sasa na wasikilizwe wanachama, wapenzi, wafuasi, wapiga debe wa pande zote mbili nini wanataka na iwepo satuwa ya kuleta ufumbuzi wa kweli na wa kudumu utakaokubaliwa na wote. Kama ni people's power basi sehemu kubwa iko kwa wale walio katika upande wa CCM-Zanzibar kwe sababu ndio wengi. Jee na wao waingie barabarani kama hamtawasikiliza? Wajumbe wa CCM Zanzibar wasilaumiwe bure. Walichokifanya ni kueleza kile wanachoamini (au wasichoamini) wanaowawakilisha.

Yote hii ni mbinu ya kuzungushana na kutaka kununua muda ni usanii wa hali ya juu ambao matokeo yake ni kuondoa uvumilivu katika jamii - CCM hamna ustaarabu wa kutafuta maoni ya wananchi na kama utasema hii ndio mara ya kwanza wanabadilka - imani za watu kwa CCM haipo kama wanataka kubadilika kutokana na historia na wakati tulionao kuwahukumu kwa ulaghai na mbinu chafu.
 
CUF msipige makelele mengi kwani CCM nayo wanapata ile haki ya kuyakubali au kuyakataa maamuzi ya kamati kama walivyokubaliana na ndio msimamo wa haki sawa kwa wote.
CUF wameyaona ni mazuri na kuyakubali ila upande wa CCM wamona kuna shortage na hivyo hawakuyaridhia ,sasa tatizo lipo wapi maana hata CUF walikuwa na haki hiyo ya kuyakubali au kuyakataa.
 
Kwani hiyo kamati iliteuliwa na nani kama sio kuwekeana usiku hapa.Wao wamefikia muafaka sasa haya malumbano mengine yametoka wapi.Hizo kura za maoni ni danganya toto.

Kutokana na uroho wa madaraka CCM hawaweze kukubali serikali ya pamoja.

Dalili ninazoziona mimi Muungano unakoelekea sio kuzuri.
 
Kuna haja ya kupata nakala ya hukumu ya kesi ya kutaka kuipindua serikali ya Zanzibar, ambapo majaji katika mahakama ya rufaa waliamua kwamba Zanzibar si dola (Sovereign state). Ukisoma hukumu ile utagundua mambo mengi sana kuhusu, nini maana ya dola, nchi n.k.

hata mimi niliipitia wakati wa kuangalia International law. uamuzi wake ulipindishwa sana na kupita kiasi. any way uamzi huo huo bado unabind maana hakuna uamuzi mwingine ambao tayari ulishaoverule.

ila katika judiciary kuna majaji wenye upeo finyu, timorous soul, na wengine ni upeo mpana bold spirit. hii kesi ilisimamiwa na matimorous souls.

katika historia ya tanzania watu waliojitokeza kuwa bold spirit ni Judge Mwalusanya na Late justice Lugakingira. nina imani serikali ilikuwa ikiogopa kesi zake kupelekwa huko, na katika kesi hii mambo yangekuwa tofauti.
 
Hali ni shwari na itaendelea kuwa shwari - tusiwe na wasiwasi na hilo - kama kawaida CUF watafanya vikao na mwisho watakubali kura ya maoni. CCM washaliangalia zamani hilo na litachukua muda kabla ya kutekelezwa kwani kutakuwa na vikao vya pamoja tena vya utekelezaji wa Kura ya Maoni , hapo litazuka suala la daftari la kutumia kupigia hiyo kura ( kwa vile daftari la sasa CUF wanasema lina kasoro ), utatumika muda kuvutana kwa hili na 2010 itapiga hodi hakujafanyika lolote. Lakini shwari itakuwepo kwani CCM inajua kuwa CUF haina ubavu wa lolote ni wasanii kama wao isipokuwa wao CCM mambo yao huyapanga kwa miaka mingi mbeleni na huwa na njia mbadala kila siku kwa mfano sasa hivi ikiwa CUF hawatakubali na kufanya ghasia itatumika nguvu ya jeshi na lawama itakuwa kwa CUF kwani CCM walikuwa wanataka kurekebisha hali ya Znz ka njia ya demokrasia ya juu kabisa ya kutaka maoni ya wananchi.

Kuna wachache tutajua kuwa ni kiini macho tu lakini haitosaidia kitu - hii ndio imetoka na kama kawaida CCM ndio washindi.
 
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ametangaza hivi punde kuwa chama hicho kimeamua kujitoa katika mazungumzo ya kusaka muafaka Zanzibar kwa sababu hakiwezi kukubaliana na ghiliba za CCM katika suala hilo.
Baada ya kujitoa, Hamad amesema kuwa chama hicho sasa kinalirudisha suala hilo kwa wananchi ambao wataamua la kufanya.
Pia CUF imeitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati suala hilo ili kuiokoa Zanzibar isiangamie.
Amesema kilichofanywa na CCM ni usanii mkubwa lakini chama hicho kinafarijika kuwa wananchi sasa wanaelewa ni nani asiyeitakia mema Tanzania.
Nafanya mpango wa kulipata tamko zima ili niwawekee hapa
 
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ametangaza hivi punde kuwa chama hicho kimeamua kujitoa katika mazungumzo ya kusaka muafaka Zanzibar kwa sababu hakiwezi kukubaliana na ghiliba za CCM katika suala hilo.
Baada ya kujitoa, Hamad amesema kuwa chama hicho sasa kinalirudisha suala hilo kwa wananchi ambao wataamua la kufanya.
Pia CUF imeitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati suala hilo ili kuiokoa Zanzibar isiangamie.
Amesema kilichofanywa na CCM ni usanii mkubwa lakini chama hicho kinafarijika kuwa wananchi sasa wanaelewa ni nani asiyeitakia mema Tanzania.
Nafanya mpango wa kulipata tamko zima ili niwawekee hapa

Jitahidi na tamko tuweze kupitia kila neno maana hawakawilii kusema CUF ni wa waarabu na wapenda madaraka .Hawa akina mtambo.
 
Nchi Yetu Ni Huru Na Hawa Cuf Tutapambana Nao Kwa Hoja Na Nguvu Zote Lakini Suala La Muafaka Kwa Sasa Wasahau Tanzania Ina Mengi Ya Kujadili Na Kuyafanyia Kazi Zaidi Ya Huo Muafaka
 
Jitahidi na tamko tuweze kupitia kila neno maana hawakawilii kusema CUF ni wa waarabu na wapenda madaraka .Hawa akina mtambo.

Kimsingi CUF kurudi kwenye meza ya mazungumzo ni kupoteza muda wao, ajenda hiyo wairudishe kwenye mahakama ya wananchi ili watu wenyewe waweze kuamua la kufanya, kwa kweli JK mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar umeshamshinda hivyo anachofanya ni usanii tu, leo hata kama ni siku ya wajinga kama CUF hawakufanya hivyo wao ndio watakua wajinga,
 
Wanalirudisha kwa wananchi - huo si ndio uamuzi wa CCM - ni ule ule usanii kutoka pande zot mbili. Seif siasa haiwezi aliambiwa zamani akatafute msikiti asalishe.
 
Kimsingi CUF kurudi kwenye meza ya mazungumzo ni kupoteza muda wao, ajenda hiyo wairudishe kwenye mahakama ya wananchi ili watu wenyewe waweze kuamua la kufanya, kwa kweli JK mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar umeshamshinda hivyo anachofanya ni usanii tu, leo hata kama ni siku ya wajinga kama CUF hawakufanya hivyo wao ndio watakua wajinga,

NI NGUMU SANA KUKAA MEZA MOJA NA WAASI VIONGOZI WA CUF NI WAASI NA HILO LITAMBULIKE LEO , KESHO NA HATA MILELE HATA WAO WANATAMBUA HILO

SASA TUTAKAAJE MEZA MOJA NA WAASI ?

1 ) WAMESAIDIA KUUWA RAIA KULE PEMBA WAKATI WA UCHAGUZI

2 ) MWEMBECHAI NAPO WANA MKONO WAO

3 ) NA KUNA MENGI MENGI YA KUJADILI HUMU

HAWA NI WAASI HATUWEZI KUKAA MEZA MOJA NA WAASI MPAKA WAO WENYEWE MAAMUE KUWEKA SILAHA CHINI NA WATAMKE KWA MAANDISHI NA KUWEKA SAHIHI HII NCHI NI YA AMANI , UPENDO NA UMOJA ULIOJENGWA NA BABA WA TAIFA AMBAYE ALIKUWA MUASISI NA MWANACHAMA HAI WA CCM
 
Jamani Hiyo Zanzibar Sio Mali Ya Cuf Au Lipumba Au Nani

Zanzibar Ni Moja Ya Nchi Zinazounda Tanzania Na Ni Mali Ya Watanzania

Huyu Anayesema Mambo Sio Shwari Nawasi Wasi Na Uzalendo Wake Anapotosha Watu Kwa Makusudi Kwa Dhamira Zile Zile Changanishi Ambazo Kwa Asili Watanzania Hatuna Hulka Hizo
 
Back
Top Bottom