Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
linalowakera wazanzibari sio mafuta , hayo mafuta wanayang'ang'ania wabara zaidi kuliko sie wazanzibari. tunachotaka wazanzibari ni HAKI SAWA KWA WOTE. na naomba muamini kwamba watanganyika mnajiona wajanja lakini bado mnawahitaji wazanzibari kwa kukukomboeni . hamna uwezo wa kuleta mageuzi ndani ya ardhi yenu na hilo lipo wazi kwani mpaka leo ccm inajua fika kwamba haina upinzani ndani ya tanganyika na ndio maana inaushikilia muungano ili iweze kuilinda ccm zanzibar. la kufanya ni kuisupport zanzibar katika mageuzi ili mageuzi ya zanzibar yaweze kuwaamsha watanganyika walio wengi ambao wanaonekana kulala na kulemazwa na siasa za nyerere. mafuta sio big deal, tunaomba uadilifu tu.

ni mzenji halisi-----under age

Mkuu... hii kali!
Naomba somo zaidi kwenye hili... ili kama ni kweli basi tuanze kuhamasishana tupate ukombozi wa wazanzibari.
 
hahaha, siamini ninachosikia, kama kweli hamna mafuta, na kama kweli hawatachimba mafuta, sijui wataongea nini jamani hawa jamaa. hahaha, wanaweza hata kujinyonga. as for us wabara, si tulisikia kuwa kuna mafuta mtwara kule wanakochimba gas, na walishachojoa hadi mapipa karibia kumi. wabara tunayo asilimia hamsini kuchimba mafuta kuliko wazanzibari. pia kule mkuranga je, mnazibay? presence ya gas yenyewe ni tosha kuwa mafuta yetu sisi wabara hayapo chini sana kama wao. na inawezekana muda si mrefu tukachimba. sikui wazenji watadaije sasa hapo, manake wanatuona sisi tutayataka mafuta yao,kumbe na sisi tunayo.

Kuhusu wewe jamaa unayesema kuwa wazanzibari mnatuamsha wabongo kwa mageuzi, sisi wabara tunachotaka ni utawala bora, regardless of chama. iwe ccm,cuf au chadema. hivyo, definition ya mageuzi sio kuing'oa ccm tu, ni kuwang'oa viongozi wabovu na kuweka wale wenye maslahiyetu. mimi sio mwanaccm, lakini, wazenji wengi mnafikiri kuwa kuleta vyama vya fujo kama cuf ndio mageuzi. vyama vya chuki sio mageuzi, ni hasara tupu. poleni kama kweli hakuna mafuta, poleni sana manake sijui kama watu hawatapata bp huko...hahah,na kama wenzenu wakiamua kusema sasa kwasabasbu mafuta hamna ndo tunavunja muungano kusudi tufaidi gas na mafuta na madini ya urenium etc peke yetu sijui mtakuwa wageni wa nani. ni bora kuungana na wakomoro kuliko kuwafuga na kuishi na wazanzibari.
 
Mwanakijiji,

..nakubaliana na wewe kwamba Muungano ni kati ya wananchi wa Zanzibar na Tanganyika. nilikosea hapo mwanzo niliposema ulikuwa kati ya SMZ na serikali ya Tanganyika.

..lakini lazima niongeze kwamba wananchi wanaweza kuuvunja Muungano kwa kutumia mamlaka na vyombo vyao vya sheria, pamoja na wawakilishi wao.

..baada ya kutafakari, naamini Baraza la Wawakilishi linaweza kupitisha muswaada/azimio wa kuvunja Muungano, na serikali ya Mapinduzi ikatekeleza muswaada/azimio huo.

..hapa nazungumzia mazingira kama yale ya hoja ya Tanganyika, ambapo wabunge waliliomba Bunge kupitisha sheria ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

..sidhani kama kuvunja Muungano kunahitaji ulazima wa kupeleka muswada kwenye Bunge la Muungano. nadhani Wazanzibari waendelee kivyao-vyao kuuvunja Muungano, na wa-Tanganyika hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia.
 
Sijui!!!. Lakini unahitaji duruso katika somo la sociology na mada ya evolution.Hivyo uelewe kuwa pia wapo Watanzania waliopo Nzega ambao hawana kabisa jamaa yoyote Zanzibar au Pemba au popote pale nje ya Nzega.. Hivyo huyo mwenzio aliyedaI kuwa kwao ni Zanzibar na hana jamaa yoyote nje ya Zanzibar ni sahihi kabisa-na lazima aringie pake na apalilie pake, na ajione nkuwa Mzanzibari zaidi kuliko Mtanzania.

Mh PAKACHA,tatizo letu sisi ni kuanza kujitazama UASILI wetu zaidi ya UTANZANIA wetu,hapa ndio kwenye tatizo,na mimi naichukia sana hii,kwani mbona ukienda DAR,MBEYA etc,huko pande za TANGANYIKA,huwezi kukuta hata mtu mmoja ambae anaweza kukuuliza ati wewe asili yako ni wapi??Lakini huku kwetu tuna hii KITU,,,,inaonekana kama hatukua tayari vile kuingia kwenye MELI hii ya TANZANIA.
 
Inaonekana yanakuumiza sana matokeo ya kule zanzibar .cha kushangaa kwa nini usiwaonee huruwa wale viumbe wanaoishi katika vijiji na maisha yao ni yakubahatisha ukitembelea machozi yatakutoka lakini yale huyaone wewe na inaonesha dhahiri huna huruma kwa watu wako tuwapiganie wale wetu wa vijijini na sio walio mabli nasi kwa kisingizio siasa inaonekana huwasikilizi SMZ wacha kujidanganya unageuka mshumaha .
 
Mgeni huyo huyo akikuambia asilimia 10 ya watu China wanatumia umeme na aslimia 50 Tanzania bado utasema watu wengi zaidi Tanzania wanatumia umeme kuliko China?

Hesabu, ndugu yangu, hesabu!

Basi yaishe, Mkuu. Wazanzibari wengi zaidi watumia umeme kuliko bara!!!!

Labda sisi wasambaa tunahesabu vingine.

Kama unakumbuka hii post
Kuna yale masomo ya hesabu yanaitwa kuainisha.

Una watoto 30, unawagawa katika makundi mawili.
25 unawatuma wakatafute machungwa, wanaporudi hao watoto 25 wamepata machungwa 15.

Kundi la pili watoto watano, wakirudi wamepata machungwa 9

Hayo machungwa sasa yawe umeme unaotumiwa bara na visiwani.

Kundi la kwanza 15 ukigawanya kwa 25 unapata 0.6

Kundi la pili 5 ukigawanya kwa 9 unapata 1.8

Jibu umeshalipata

Shule zetu za kisambaa pia tulikua tunafundishwa kwamba mapeasi 15/25 = 0.6

na mapeasi 5/9 =1.8

Hayo ni mapeasi kwa kule kwetu kwa wasambaa ingekua ni keki, ni watoto wapi wangeshiba kushinda wengine?

Turudi kwenye post yako tena
Mgeni huyo huyo akikuambia asilimia 10 ya watu China wanatumia umeme na aslimia 50 Tanzania bado utasema watu wengi zaidi Tanzania wanatumia umeme kuliko China?

10/100= 0.1
50/100= 0.5
Kama wewe mtanzania mpenda maendeleo katika haya majawabu mawili ungependa uwe kwenye fungu lipi? 0.1 au 0.5?

Kama bado hujaona itabidi nisipoteze muda wangu
 
Labda sisi wasambaa tunahesabu vingine.

Kama unakumbuka hii post

Shule zetu za kisambaa pia tulikua tunafundishwa kwamba mapeasi 15/25 = 0.6

na mapeasi 5/9 =1.8

Hayo ni mapeasi kwa kule kwetu kwa wasambaa ingekua ni keki, ni watoto wapi wangeshiba kushinda wengine?

Turudi kwenye post yako tena
Mgeni huyo huyo akikuambia asilimia 10 ya watu China wanatumia umeme na aslimia 50 Tanzania bado utasema watu wengi zaidi Tanzania wanatumia umeme kuliko China?

10/100= 0.1
50/100= 0.5
Kama wewe mtanzania mpenda maendeleo katika haya majawabu mawili ungependa uwe kwenye fungu lipi? 0.1 au 0.5?

Kama bado hujaona itabidi nisipoteze muda wangu

Darwin. Hapa unataka kusema nini? Kuwa 0.5 ni kubwa kuliko 0.1? Bila kuangalia 0.1 ya NINI na 0.5 ya NINI? Kwa hesabu zako kwa hiyo 0.5 ya watu milioni 39.4 ni wengi kuliko 0.1 ya watu bilioni moja? Kwa vile 0.5 ni kubwa kuliko 0.1?

Kweli tunapotezeana muda!
 
Mh PAKACHA,tatizo letu sisi ni kuanza kujitazama UASILI wetu zaidi ya UTANZANIA wetu,hapa ndio kwenye tatizo,na mimi naichukia sana hii,kwani mbona ukienda DAR,MBEYA etc,huko pande za TANGANYIKA,huwezi kukuta hata mtu mmoja ambae anaweza kukuuliza ati wewe asili yako ni wapi??Lakini huku kwetu tuna hii KITU,,,,inaonekana kama hatukua tayari vile kuingia kwenye MELI hii ya TANZANIA.
King. Poa moto. Zanzibar ni ndogo. Wacha watu walinde uasili wao. Lakini intergration ni kubwa sana. Hii ni ya kimaumbile. Hata unsingekuwa na Jamhuri ya Muungano- ingetokea tu (Kwa jinsi ya Dar na Mjini Zanzibar zilivyo karibu na social interraction inavyo -apply). Watu kama wewe King (mchanyiko Dar/Pemba, Dar/Unguja,Sengerema/Unguja, Bihamulo/Pemba, Peramiho/ Unguja) ni wengi tu sasa Zanzibar -lakini ni hao wasio na sauti below 15 years). Hiyo inayoendelea ni social factor and power. Sasa, ukiwa na muungano usiwe na muungano-mchanganyiko hauepukiki. Tuulinde Muungano wetu na hatma ya wenetu. Lakini la msingi tuelewane katika haki kwenye Muungano huu. Bara isiididimize Zanzibar- Na Zanzibar isidai yatakayohatarisha Muungano wetu. Sawa.
 
Mwanakijiji,

..baada ya kutafakari, naamini Baraza la Wawakilishi linaweza kupitisha muswaada/azimio wa kuvunja Muungano, na serikali ya Mapinduzi ikatekeleza muswaada/azimio huo.
Endelea na duruso Mkuu. si Baraza la Wawakilishi wala SMZ linaloweza kuuvunja Muungano. Muungano unaweza kuvunjwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa azimio litakalokubaliwa na theluthi mbili ya kura za upande wa Wabunge kutoka Zanzibar, na theluthi mbili ya kura za wabunge wa Upande wa Tanzania Bara. Utaumiza kichwa bure Mzee. Kadiri unayotaka kueleza kuhusu upeo wa Baraza la Wawakilishi na SMZ kuvunja Muungano-Ndivyo unavyoona uhalali wa kuwa na Bunge la Tanganyika na Serikali ya Tanganyika. Unaweza kuweka vyombo vyote hivi katika chombo kimoja kama utatumia "intergration process"- na ukawa na Serikali moja-ambayo ime-intergrate SMZ na Serikali ya Tanganyika (ambayo haioneklani h ivi sasa). Ukawa na Bunge moja la Jamhuri -ambalo litakuwa na Lower Chamber B (ambayo ni Baraza la Wawakilishi "intergrated") na Lower chamber A-Bunge la Tanganyika (intergrated). Mambo yanawezekana lakini watu inabidi wake chini watafakari na kuyapanga.
 
King. Poa moto. Zanzibar ni ndogo. Wacha watu walinde uasili wao. Lakini intergration ni kubwa sana. Hii ni ya kimaumbile. Hata unsingekuwa na Jamhuri ya Muungano- ingetokea tu (Kwa jinsi ya Dar na Mjini Zanzibar zilivyo karibu na social interraction inavyo -apply). Watu kama wewe King (mchanyiko Dar/Pemba, Dar/Unguja,Sengerema/Unguja, Bihamulo/Pemba, Peramiho/ Unguja) ni wengi tu sasa Zanzibar -lakini ni hao wasio na sauti below 15 years). Hiyo inayoendelea ni social factor and power. Sasa, ukiwa na muungano usiwe na muungano-mchanganyiko hauepukiki. Tuulinde Muungano wetu na hatma ya wenetu. Lakini la msingi tuelewane katika haki kwenye Muungano huu. Bara isiididimize Zanzibar- Na Zanzibar isidai yatakayohatarisha Muungano wetu. Sawa.

Pakacha,

Dalili zote zinaonyesha kuwa Zanzibar bila Muungano si Zanzibar bali ni Unguja na Pemba. Ni ZPPP/ZNP na Afro Shiraz kwa lugha ya sasa unaweza kusema ni CUF na CCM Zanzibar. Ni Karume na Maalim Seif. Ni Wazanzibari na Wazanzibara! Kama mnajipenda endeleeni kupiga kelele zenu hivyo hivyo kama wazanzibari ndani ya Muungano! Rejea 'miafaka' yote miwili. Hivi eti Zanzibar ilipata uhuru wake lini? Maana yupo mtu anasema ni mwaka 1963 na mwengine anasema ni January 12, 1964. Mimi naongeza naona kuna uwezekano mkubwa Zanzibar bado haijapata Uhuru!
 
Darwin. Hapa unataka kusema nini? Kuwa 0.5 ni kubwa kuliko 0.1? Bila kuangalia 0.1 ya NINI na 0.5 ya NINI? Kwa hesabu zako kwa hiyo 0.5 ya watu milioni 39.4 ni wengi kuliko 0.1 ya watu bilioni moja? Kwa vile 0.5 ni kubwa kuliko 0.1?

Kweli tunapotezeana muda!

Kama yangekua matunda kwenye hesabu yako ya 10 gawanya kwa watu 100 ambayo ulisema umeme china
Na matunda hayo hayo 50 gawanya kwa watu 100 ambayo ni umeme Tanzania.
Niambie utachagua uwe fungu gani?
 
Kama yangekua matunda kwenye hesabu yako ya 10 gawanya kwa watu 100 ambayo ulisema umeme china
Na matunda hayo hayo 50 gawanya kwa watu 100 ambayo ni umeme Tanzania.
Niambie utachagua uwe fungu gani?

Hapa hatuzungumzii matunda hayo hayo. Idadi ya mapeaz China ni tofauti na idadi ya mapeaz bongo! Hii ndiyo basis ya hesabu hizi! Au unataka kusema idadi ya watu China ni sawasawa na watu Tanzania?

Mkuu, naona tukubali kutofautiana.
 
Last edited:
zanzibar ilipata uhuru wake 1963 na ikajiunga na UN mwaka huo huo na ikatawaliwa tena na Tanganyika 1964 mpaka hivi leo sasa wazanzibari wameanza tena kudai uhuru wao kotoka Tanganyika. Index of /files
 
Hapa hatuzungumzii matunda hayo hayo. Idadi ya mapeaz China ni tofauti na idadi ya mapeaz bongo! Hii ndiyo basis ya hesabu hizi! Au unataka kusema idadi ya watu China ni sawasawa na watu Tanzania?

Mkuu, naona tukubali kutofautiana.

Sikuzungumzia wingi wa watu kwani najua China watu ni wengi kuliko TZ, niliongelea kwamba watumizi wa Zanzibar wametuzidi kushinda bara kutokana nakwamba Zanzibar watu wengi wana umeme.
Kama China wangekua asilimia 10 wanatumia umeme na Bongo asilimia 50 basi bongo tungekua tumewashinda

Na hii ndio njia wanayotumia kuangalia duniani kwamba taifa lipi ni tajiri na taifa lingine ni masikini.

Hio hio ndio wanatumia kwamba Singapore kanchi kadogo ni tajiri kushinda nchi kubwa Brazil.
 
Zanzibar imeanza kuonja makali ya mgao wa umeme baada ya kuzimwa kwa saa 10 jana kufuatia kuharibika kwa mitambo mitatu ya umemeTanzania Bara.

Ofisa Uhusiano Shirika la Umeme Zanzibar, Salum Abdalla, alisema utekelezaji wa mgao umeanza baada ya kupokea taarifa kutoka uongozi wa TANESCO kuwa mji huo umeingizwa katika mgao.

Alisema Shirika limeamua kuweka mgao katika kanda sita kwa watumiaji wa huduma hiyo.

``Hakuna njia nyingine, lazima mgao wa umeme uanzishwe,`` alisema.

Alisema kutakuwepo na kanda sita, ambapo kila kanda itakosa umeme kwa saa tatu. Ratiba hiyo itakuwa ya mzunguko, alisema Abdalla.

Alisema maeneo nyeti kama sehemu wanazoishi viongozi, hakutakuwa na mgao. Alisema Zanzibar inatumia megawati 42 kwa siku.

Mgao huo umesabishwa na kuharibika mitambo ya uzalishaji umeme na kusababisha upungufu wa nishati hiyo kutoka megawati 180 hadi megawati 140.

Pemba haitahusika na mgao huo kwa sababu kisiwa hicho hupata umeme wake kupitia majenereta yanayotumia mafuta ya IDO, yaliyopo Wesha, Wilaya ya Chake Chake, Pemba.

Imefahamika kuwa Zanzibar inaendelea na mipango yake ya kutafuta umeme wa kutumia njia mbadala ikiwemo uzalishaji wa kutumia mawimbi ya bahari na majenereta.

Source: IPPMEDIA
 
Sasa hii ndio nini . Ndio Muungano huu? kama sisi ni wateja baki- tunaonunua umeme wenu- kwa nini mnatukatia? (Wapi misingi ya kibiashara?)
 
Pakacha,

Dalili zote zinaonyesha kuwa Zanzibar bila Muungano si Zanzibar bali ni Unguja na Pemba. Ni ZPPP/ZNP na Afro Shiraz kwa lugha ya sasa unaweza kusema ni CUF na CCM Zanzibar. Ni Karume na Maalim Seif. Ni Wazanzibari na Wazanzibara! Kama mnajipenda endeleeni kupiga kelele zenu hivyo hivyo kama wazanzibari ndani ya Muungano! Rejea 'miafaka' yote miwili. Hivi eti Zanzibar ilipata uhuru wake lini? Maana yupo mtu anasema ni mwaka 1963 na mwengine anasema ni January 12, 1964. Mimi naongeza naona kuna uwezekano mkubwa Zanzibar bado haijapata Uhuru![/QUOTE

Gotee unachanganyikiwa Ndugu yangu. Zanzibar is strong. Imejitayarisha. Lakini Muungano na udumu. Tunabanana hapo hapo, lakini hatukubali usanii.
 
Tujiulize kwanini hadi leo Tanganyika wamekuwa wanulizana eti wewe ni kabila gani hii inaonesha kuwa mabo ya makabila bado yapo katika jamii yao sasa unaposema eti zanzibar wapo hivi na vile unakosea wao ni maumzi ya na sawa na sisi huku Tanganyika tumekuwa na mambo ya kulizana wewe ni kabila gani jambo ambalo halileti faida yoyote
 
Back
Top Bottom