Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Pakacha said:
Kaka yangu na bado Tanzania Mainland (Kwa wewe siyo Tanganyika) ina madini mengi tu ardhini, pamoja na mafuta pamoja na gesi kibao pamoja na ardhi nzuri ya kilimo. Kwa nini isikubali hii rajuwa iliyoko Zenj watumie wale Waswahili kule peke yao ambao hawana chochote kile chengine cha kutegemea (karafuu ishaanguka ).

Pakacha,

..binafsi i am of the opinion kwamba Zanzibar wamiliki mafuta yanayopatikana ktk eneo lao by 100%.

Jasusi said:
Lakini si makubaliano ya mwungano yaliondoa mipaka. Nini manaa ya "a one sovereign republic?" That is what we were supposed to become, no?

Jasusi,

..Muungano uliondoa mipaka, pia uliondoa u-Tanganyika, lakini haukuondoa u-Zanzibari.

..kama wa-Zanzibari wangekuwa wanaona kwamba wao ni wa-Tanzania, kama ilivyo kwa wa-Tanganyika, sidhani kama matatizo haya yangekuwepo.

..nadhani hilo ndilo tatizo kuu la huu Muungano and it is too late kulirekebisha.
 
Last edited:
Hivi iweje watu waseme kwamba madini ni ya Tanganyika na si ya muungano..harafu watake mafuta ya wenzetu?

Unless niambiwe kwamba tunagawana madini....Ohh I nearly forgot..akina Lowassa na Karamagi wanagawana na akina Nahodha na KARUME. Vinginevyo hawa jamaa wana haki zote za kung`ang`ania mafuta yao. Sadly, sijui kama watakuwa any better than they are now. Maana kwa bandari na utalii walivyonavyo..kama kweli wangekuwa serious wangekuwa wameshakuwa Mayote ya Bongo! Otherwise Its ridicurous and a shame....chako chako..chake chenu..wapi na wapi jamani

Caveat: Uchimbaji wa hayo mafuta usiingilie territorial sovereignty ya JAMHURI YETU. Kifupi continental shelf yetu ibaki intact. Kwa sababu uhai wa Jamhuri yetu una transcend mimi na wewe, mzanzibari na mzanzibara!

Kisheria kuna tatizo hapa. Maana kama mafuta yatachimbwa baharini, bahari ni ya TANZANIA na wala si ya Zanzibar. Na hata signatory wa Law of the Sea Convention ni TANZANIA na wala si Zenji... Anyway ngoja wataalam wa law of the Sea wamwage vitu hapa. Ila uelewa wangu ni kwamba zile neutical miles za Tanzania zina extend beyond ZANZIBAR as such Tanzania itawashinda wazenji kwa Legal arguments. Ila kwa hoja za kawaida tuu..wazenji wana haki zoooote za kufaidi mafuta yao.
 
Kuna Watanzania na Wazanzibar.
Kuna Tanzania Bara na Zanzibar.
Kuna Tanzania pia kuna Zanzibar.
Tatizo kubwa lililopo ni kwamba hakuna Watanganyika hakuna Tanganyika pia hakuna Tanzania Visiwani.
Kuto kuweko kwa serikali ya Tanganyika ndilo Tatizo kubwa linalo yumbisha muungano.

Serikali ya Tanzania imeshindwa kufanya kazi zake zote ndani ya mipaka ya Tanzania. Sehemu moja ya Tanzania haijisikii wala haijivunii U tanzania kwa sabau ya kero nyingi.

Serikali ya Tanganyika kamwe haiwezi kufufuka, naamini kwa dhati baada kuweka kero zote hadharani na kuzijadiri bila uficho wala mizengwe ya KiCCM, siku ina kuja ambayo tutakuwa na serikali ya Tanzania yenye uwezo wa kufanya shughuli zake ndani ya mipaka ya Tanzania bila mawaa.
 
Muungano huu sasa unathibitika kuwa haukuwa wa maridhiano, matokeo yake ni haya sasa Zanzibar Kudai rasilimali yake ya Mafuta kuyamiliki pekee, mie napata wasi weasi mkubwa sasa kuwa yote yalioanzishwa ndani ya Muungano huu kuwa hayakupata ridhaa ya Wananchi na ndilo kosa kubwa lililofanywa na viongozi wakuu wawili Nyerere na Karume walijichukulia mamlaka yaliokuwa sio yao ijapo ni9a zao zilikuwa ni nzuri lakini mwelekeo lazimishi ulikuwa nje ya msitari.

Hakuna haja yakuvutana yawe yapo au yasiwepo hayo mafuta waachiliwe wenyewe Wazanzibari wayatafute na wakiyapata na wayachimbe kwa maslaha ya watu wao.

Udugu wetu wa damu usivurugwe na mali
 
Masanja said:
Hivi iweje watu waseme kwamba madini ni ya Tanganyika na si ya muungano..harafu watake mafuta ya wenzetu?

Masanja,

..hivi unafikiri wa-Tanganyika wakisema madini ni suala la muungano, basi wa-Zanzibari watabadilisha mawazo na kukubali mafuta pia yawe ya muungano?

..sijayafuatilia vizuri mapendekezo ya Consultant aliyeletwa, lakini sitashangaa kama ameelekeza madini na nishati yawe masuala ya Muungano.

..nadhani ustawi wa Zanzibar utakuwa na manufaa kwa wa-Tanganyika. Zanzibar inaweza kugeuka Dubai na wa-Tanganyika tukapata nafasi za kujimwaya-mwaya huko kwa kazi za u-dobi, u-yaya, au hata kubeba zege.
 
Kuna Watanzania na Wazanzibar.
Kuna Tanzania Bara na Zanzibar.
Kuna Tanzania pia kuna Zanzibar.
Tatizo kubwa lililopo ni kwamba hakuna Watanganyika hakuna Tanganyika pia hakuna Tanzania Visiwani.
Kuto kuweko kwa serikali ya Tanganyika ndilo Tatizo kubwa linalo yumbisha muungano.

Serikali ya Tanzania imeshindwa kufanya kazi zake zote ndani ya mipaka ya Tanzania. Sehemu moja ya Tanzania haijisikii wala haijivunii U tanzania kwa sabau ya kero nyingi.

Serikali ya Tanganyika kamwe haiwezi kufufuka, naamini kwa dhati baada kuweka kero zote hadharani na kuzijadiri bila uficho wala mizengwe ya KiCCM, siku ina kuja ambayo tutakuwa na serikali ya Tanzania yenye uwezo wa kufanya shughuli zake ndani ya mipaka ya Tanzania bila mawaa.

Madela Wa- Madilu,

Bara wako watu 40 millions na Visiwani wako only 1 million!

Saa zote Visiwani wataona wanaonewa tu!!
 
..nadhani ustawi wa Zanzibar utakuwa na manufaa kwa wa-Tanganyika. Zanzibar inaweza kugeuka Dubai na wa-Tanganyika tukapata nafasi za kujimwaya-mwaya huko kwa kazi za u-dobi, u-yaya, au hata kubeba zege.
wawaachie mafuta yao.....after 5 years tuanze kukimbilia zenji kubeba box....
 
Wazanzibar kama wanataka hayo mafuta yawanufaishe wao Wazanzibar peke yao na si Watanzania wote tuwaachie tu hayo mafuta, kwanza wafahamu dunia sasa hivi inayakimbia mafuta ya kuchimbwa polepole na badala yake inawekeza katika green energy, baada ya muda si mrefu mafuta yatazalishwa kwa nafaka n.k, Kule Tanganyika kuna ardhi kubwa na ya kutosha ya kulima hizo nafaka, je ikifika hatua hiyo Wazanzibari mtataka vyote vilivyo bara na viswani?. Chao Chetu , Chetu Chetu!

hii inanikumbusha lile shairi kwenye DIWANI YA MLOKA

"Kuku akipata nyama hukimbia ale peke"
"Japo watamuandama wenzie waishike"
"Kuitupa hakubali mdomoni idondoke"

"Palipo na ubinafsi hapakosi kuwa choyo"
"na upeke wa nafusi na chuki katika moyo"
"Haukosekani wivu maringo pia tamaa"
"Kadhalika na ubovu wa moyo usiofaa"
 
Mzalendo Halisi said:
Bara wako watu 40 millions na Visiwani wako only 1 million!

Saa zote Visiwani wataona wanaonewa tu!!

Mzalendo Halisi,

..hivi unafikiri Zanzibar wakiambiwa wawe jimbo la USA, ambayo tayari ina mamilioni ya waru, mnafikiri watakataa?

..tatizo Tanganyika ni choka mbaya na ndiyo maana hawaoni faida za kuungana na sisi.
 
Wazanzibari hamtaki kuwaelewa wamehoji na madini yaliyojaa bwerere Bara nayo pia yawe ya Muungano. Na tuzungumze hapa.

Hivi mihela inayopata Zanzibar kutoka Bara mnadhani inatokana na nini? Kuna wakati fulani hata mishahara ya wazenji ilikuwa inatoka bara, na SMZ haichangii uendeshajiw a Serikali ya Muungano ambayo ianhudumia Tz yote, halionekani hili?
 
Hiyo hela inatokana na kodi na tunalipa wenyewe. Nikinywa bia kodi, mtalii akinywa bia (kwetu kule Paje resort) -kodi. Zinakusanywa huko hizo au vipi?
 
Hivi iweje watu waseme kwamba madini ni ya Tanganyika na si ya muungano..harafu watake mafuta ya wenzetu?

Unless niambiwe kwamba tunagawana madini....Ohh I nearly forgot..akina Lowassa na Karamagi wanagawana na akina Nahodha na KARUME. Vinginevyo hawa jamaa wana haki zote za kung`ang`ania mafuta yao. Sadly, sijui kama watakuwa any better than they are now. Maana kwa bandari na utalii walivyonavyo..kama kweli wangekuwa serious wangekuwa wameshakuwa Mayote ya Bongo! Otherwise Its ridicurous and a shame....chako chako..chake chenu..wapi na wapi jamani

Caveat: Uchimbaji wa hayo mafuta usiingilie territorial sovereignty ya JAMHURI YETU. Kifupi continental shelf yetu ibaki intact. Kwa sababu uhai wa Jamhuri yetu una transcend mimi na wewe, mzanzibari na mzanzibara!

Kisheria kuna tatizo hapa. Maana kama mafuta yatachimbwa baharini, bahari ni ya TANZANIA na wala si ya Zanzibar. Na hata signatory wa Law of the Sea Convention ni TANZANIA na wala si Zenji... Anyway ngoja wataalam wa law of the Sea wamwage vitu hapa. Ila uelewa wangu ni kwamba zile neutical miles za Tanzania zina extend beyond ZANZIBAR as such Tanzania itawashinda wazenji kwa Legal arguments. Ila kwa hoja za kawaida tuu..wazenji wana haki zoooote za kufaidi mafuta yao.
Ndio tunasema mazungumzo tena yanayotawaliwa na busara na hekinma yanahitajika katika kujadili hili. Hiyo sheria ya bahari- hiyo ni kasheshe. Kama Zanzibar ingekuwa kivyake na mipaka ipo kungekuwa na vita hapa kugombania mafuta hayo. Sasa hakuna mipaka ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tufikie busara ya kugawa mali hiyo bila ya kuwapunja wenzetu, na wanapohoji kuhusu mali nyengine zilizoko Bara basi waambiwe kuwa watapata mgao huko (kwa kadiri ya udogo wao.) Na la zaidi Serikali ya Jamhuri nya Muungano ingekuwa inafanya miradi ya Maendeleo kule Zenj (kujenga kama hospitali, au barabara) wananchi wakaona ala hii imejengwa na Jamhuri ya Muungano- basi suluhu ipo tu.
 
Ukweli ni mwepesi kabisa, wazanzibar wapewe nchi yao na watanganyika tupewe nchi yetu kwisha.

Kama wanamafuta, wachimbe wauze yatakayobaki wajipake, nasi tanganyika tuendelee na harakatizetu za kuwazawadia rasilimali zetu kwa kisingizio cha uwekezaji
 
Asalamu Alaykum.

Naomba kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala la wawakilishi au wajumbe wa baraza la wawakilishi kukutana katika hoteli ya Serena iliyopo Shangani katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Kwanza kwa mujibu wa utafiti wangu mdogo niliofanya leo asubuhi hakuna wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoka Kambi ya upinzani waliokutana katika hoteli hiyo. pia niliwasiliana na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kwa upande wa CCM na wamenipa jibu kuwa hakuna hata mjumbe mmoja aliyekutana na wageni Serena kisha nikawasiliana na baadhi ya mawaziri kama sita wa SMZ na wamenieleza wao hawana taarifa yoyote kuhusiana na kikao au mkutano wa serena.

lakini naweza kuamini kwamba hakuna kikao hicho kilichokaa kati ya wawakilishi na wafadhili kutokana na sababu kadhaa ikiwemo mawaziri wengi hivi sasa wapo Pemba ambao wamefuatana na Rais Karume katika ziara yake akiwemo waziri mawasiliano, na naibu wake, waziri wa elimu na mafunzo ya amali, waziri asiyekuwa na wizara maalumu, na wengine lakini pia hata kama wangekutana kwa serena sio siri maana kwa utaratibu wa SMZ wanazo sehemu za kukutana kwa siri lakini sio hoteli hsa katika eneo la mji mkongwe hakuna siri wala hakuna hoteli ambayo itakuwa siri kwa wazanzibar.

Suala la kuzungumzia issue ya mafuta ni mbili tu kwenye baraza la mapinduzi (baraza la mawaziri) ambapo tayari wameshalijadili na kutoa mapendekezo yake na baadae kupelekwa katika sehemu ya pili ambapo ni baraza la wawakilishi nalo limetoa baraza zake.

Wasia wangu kwa leo ni kuwa tunapoongea jambo ni vyema tukafanya utafiti kabla ya kuliwasilisha ili tujijengee heshima mbele ya jamii lakini pia mbele ya watu wanaosoma maandishi yetu na kutusikiliza. bila ya shaka taarifa zenye uhakika zinakujengea heshima lakini pia zinakuwa umadhubuti na kujiamini kwa ulichokiwasilisha.

Naomba kuwasilisha

karibuni Stonetown kwenye mji wa kihistoria amabo umeingizwa katika hifadhi ya kimataifa na hiyo hoteli ya Serena pia ipo katika mamlaka yangu ya mji mkongwe.
kila la kheri kwa usiku huu.
 
Kwa hakika katiba (original) au makubaliano baina ya Nyerere na Karume walipotia saini zao hayapo. Kiliopo ni kuburuzana na kubabaishana tu. Mimi nawauliza nyooote, yuko mtu anaweza kutuonyesha karatasi ilio andikiwa muungano. Mabwana na mbabibi tusidanganyane bure. zanzibar ni koloni la Tanganyika na kisingizio ni muungano. Muungano haupo kwa kuwa haukuridhiwa na wananchi waliokuwepo wakati ule na ndio maana zanzibar ilitawaliwa kwa "DECREE" mpaka 1977 palipotafutwa ufumbuzi wa katiba. Mengineo ni usanii wa hali ya juu.
 
Kitu kinaachonishangaza sana ni kuwa kwanini zenji wamesimama kidete kutetea suala la mafuta na wamesahau mambo yote yanayonufaisha watu wa pande zote mbili.Sidhani kama watu wote wana picha halisi ya nini mdhara ya kuvunjika muungano. Au ndo strategy ya baadae unguja na pemba kumeguka kuwa nchi mbili?
Nafikiri kwa kuwa zenji wanalia sana na mafuta yao tuwaachie.Watatukumbuka baada ya hayo mafuta kwenda zake
 
Back
Top Bottom