Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Nyerere aliondoa Uchifu Hangaya anarudisha Uchifu acheni kuchezea akili za watu.

Nyerere alisema Uchifu utatugawa na utaleta Ukabila acheni hizo scare tactics dhidi ya Wananchi wenu.
Leo chief mangungo wa pemba yupo mwanza anasikiliza ngoma
 
Nyerere aliondoa Uchifu Hangaya anarudisha Uchifu acheni kuchezea akili za watu.

Nyerere alisema Uchifu utatugawa na utaleta Ukabila acheni hizo scare tactics dhidi ya Wananchi wenu.
Kenya siyo mbali utavuka kwa miguu tu!
 
Kweni tunamjadili Samia au muungano?
Uhalali wa Samia kuwa Raisi unatoka kwenye Muungano. Hivyo kutaka kuujadili muungano halafu ukamkwepa Samia ni tabia ambayo mwandishi Ayi Kwei Armaha anaiita ya Chichi Dodo, kupenda wadudu wala mavi (Maggots) halafu mavi anayachukia. Ukipenda boga penda na ua lake..
 
Natoa tu angalizo

Maana naona Mjadala wa Tanganyika unashika kasi kana kwamba ni Jambo jema kumbe ndio kuharibu zaidi

Muungano ukivunjika na Bandari huna ndio itakuwa nini!!!

Kuweni wenye kutafakari!

cc: Daudi Mchambuzi- Machame
Tanganyika hatuna huo ujinga wa ukabila, ndio maana muhaya anaoa na kuolewa na msukuma , mngoni , n. k, .labda watu wa visiwani ndo Wana huo ujinga. Muungano huu Kama ni mzigo kwa watanganyika hauna umuuhimu Tena Wala Radha tena.kama sisi ni nchi moja iweje Mtanganyika haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar !? Kama sisi ni nchi moja iweje Mtanganyika haruhusiwi kuwa rais wa Zanzibar !!??
 
Uhalali wa Samia kuwa Raisi unatoka kwenye Muungano. Hivyo kutaka kuujadili muungano halafu ukamkwepa Samia ni tabia ambayo mwandishi Ayi Kwei Armaha anaiita ya Chichi Dodo, kupenda wadudu wala mavi (Maggots) halafu mavi anayachukia. Ukipenda boga penda na ua lake..
Tumekuwa tukiujadili muungano hata kabla ya Samia kuwa Raisi wewe ulikuwa wapi? Kama unataka kumjadili Samia anzisha nyuzi yako grow up.

Acha mijadala ya Kisichana.
 
Natoa tu angalizo

Maana naona Mjadala wa Tanganyika unashika kasi kana kwamba ni Jambo jema kumbe ndio kuharibu zaidi

Muungano ukivunjika na Bandari huna ndio itakuwa nini!!!

Kuweni wenye kutafakari!

cc: Daudi Mchambuzi- Machame
Hatuwezi kuwaachia watu wasiokuwa Watanganyika waingie mikataba mibovu kwa ajili yetu. Je muungano sio kitu kinachoweza kuvunjika muda wowote na tukabaki na mikataba hovyo iliyosainiwa na wageni? Mbowe yupo sahihi sana!
 
Katiba mpya iwe ya Serikali tatu ili huu muungano ukivunjika tuwe na Serikali yetu ili isitokee vacuum.
 
Unadhani Ubaguzi analeta mwananchi au yule anayeonesha nepotism na upendeleo...; Upuuzi huu ulianza Awamu iliyopita sasa hivi ni muendelezo....; Watanzania tulikuwa hatuna lolote la kujivunia zaidi ya umoja na Utaifa...

Sasa hivi Imani / Ukabila / Matabaka imekuwa kama sifa ya kujivunia..., In short binafsi nimegeuka kuwa an Uninterested Observer its the beginning of the end; Mbaya zaidi uchawa na Propaganda zimezidi; mtu akisema sio sawa au mbona hakuna usawa anapigwa Propaganda kwamba ni mbaguzi (kumbe anayebagua ni yule anayeonesha upendeleo wa wazi wazi)
 
Tumekuwa tukiujadili muungano hata kabla ya Samia kuwa Raisi wewe ulikuwa wapi? Kama unataka kumjadili Samia anzisha nyuzi yako grow up.

Acha mijadala ya Kisichana.
Wewe huna akili kabisa, hata Raisi angekuwa baba yako ni lazima angejadiliwa tu pale linapokuja suala la muungano. Hivyo Raisi Samia atajadiliwa tu, atake au asitake. Vipengele muhimu katika muungano ni hivi vifuatavyo: Aina ya Muungano, Madaraka ya Raisi na jinsi pande zote mbili za muungano zitatoa wagombea, Mgawanyo wa Rasilimali, Uraia, Ulinzi na Usalama.

Sasa wewe endelea kukaza fuvu kama punguani wakati kwao kule Zanzibar haya mambo yanazungumzwa kila siku tena kwa uwazi kabisa. Watanganyika shida yenu kubwa ni ujinga, unafiki, kuendekeza siasa uchwara na nidhamu ya woga.

Samia is incompetent and an existential threat to the stability of the Union.... Bank on it!!
 
Ni kweli kabisa. Tukianza kubaguana hatutakaa tuache mpaka nchi isambaratike kabisa.

Lakini kuna maamuzi viongozi wanafanya inapelekea watu kutoa maneno makali sana.

Hili la bandari linashangaza sana, kwenye mambo mengine ya maendeleo tunakumbushana kushirikiana na wenzetu wa visiwani. Ila la Dp World (ambalo tumeambiwa lina manufaa makubwa) hatuwashirikishi. Watu wanafikia conclusion gani? Utawalaumu?

Hawa viongozi wajitafakari sana, nchi ikisambaratika sijui watajiongoza wenyewe?

Ndio maana kuna viongozi kwa ajili ya kufanya maamuzi kwa maslahi yetu.xx kila kitu wakishirikisha huo mshahara na uongozi wao unafaida gani.
 
Nyerere naye aache mambo yake, mwaka 1963 kabla ya huu muungano mbona katika Tanganyika yetu hakukuwa na mimi Mhaya wewe mchaga . Ile ilikuwa ni fear mingering tu
 
Ndio maana kuna viongozi kwa ajili ya kufanya maamuzi kwa maslahi yetu.xx kila kitu wakishirikisha huo mshahara na uongozi wao unafaida gani.
Maamuzi yenyewe ndio haya sasa ya bandari, kuna uongozi hapo?
 
Muungano wetu mzuri sana lakini Kuna mambo tunaitaji kuelimishwa

1. Kwanini mtanganyika harushusiwi kuwa kiongozi kule Zanzibar?

2. Je mtanganyika anaruhusiwa kumiliki ardhi kule Zanzibar?

3. Je, mwanafunzi anaruhusiwa kusoma kule bila kuwa na resident permit?

4. Kwanini mzanzibar anaruhusiwa kuwa kiongozi huku Tanganyika hususani raisi au waziri?

5. Why bandari ya Dar imekodishwa na si bandari ya Zanzibar?

6. Why gharama za ushuru kule bandari ya Zanzibar ni ndogo compared to DAR port?

7. Je, huwa tunagawana mapato sawasawa
 
Back
Top Bottom