Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
nnaendelea kuleta machache ili yazidi kuongeza kasi ya mjadala,
na sasa tuangalie vipi jinsi gani muingereza alipoingia visiwani
source: http://www.zanzinet.org/zanzibar/history/historia.html


The Protectorate
After a period of confusing lines of control, Zanzibar was officially declared a British protectorate in 1890; the sultan was retained for ceremonial purposes, but most major decisions were made by the British resident. The British however continued to rule under cover and to the locals it appeared as if the Sultan was in control and their policies of division and rule and of exercising indirect rule created ethnic conflicts among people of Zanzibar and Pemba.

During their rule they encouraged formation of associations based on ethnic lines, which later on were the foundation for the new political parties. The ethnic based census of 1948 that categorized people into Shirazis, Arabs, Indians, and other African tribes formented ethnic tensions that have plagued Zanzibar ever since. The Arab, Indian, Shirazi and African associations that were formed in the 50s have plunged Zanzibar into political conflicts bigger than its size. During this period, the history of Zanzibar witnessed the formation of political parties all fighting for independence from Britain. The Zanzibar Nationalist Party (ZNP), Afro Shirazi Party (ASP) and the Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) are all products of ethnic associations. For example, the ZNP, which was launched by people considered to have no direct descendant to Arabs got a support from the Arab Association. The ASP was a merger between the African Association and the Shirazi Association. The ZPPP was an offshoot of ASP as result of disagreement of ASPs too much lineancy towards African Association. The period was marred by dirty politics and party conflicts that led to scores of politicians changing ranks from one party to another. The Umma Party, which was formed by communist members of the ZNP joined ASP in claiming full independence and became an influential partner of ASP in the early days after independence.
 
Kichuguu,
1. Nafasi ya Sultani ilipaswa kufutwa ktk Zanzibar huru. Kigezo kwamba Sultani wa mwaka 1963 alikuwa amezaliwa Zanzibar hakihalalishi kuwepo kwake.

2.Sote tunajua asili ya Usultani ni wapi na ulikuwepo Zanzibar ktk mazingira yapi. Kama waliamua kupiga vita biashara ya utumwa, kwanini waliacha muhimili wake--Sultani?

3.Kusingekuwa na tatizo kama Jamshid angejiunga na chama cha kisiasa kama raia wa kawaida na kugombea uongozi. Nina hakika coalition ya ZNP/ZPPP wangempa hata Uwaziri Mkuu.

4.Mapinduzi yalikuwa halali kwasababu yalikuwa yakitekeleza azma ya wananchi walio wengi wa Zanzibar ya kumuondoa Sultani. Mapinduzi hayo yalikuwa na lengo la kurudisha heshima ya Wafrika Zanzibar.

5.Ni kweli ktk Mapinduzi yale waliuawa wananchi wasiokuwa na hatia. Serikali ya Mapinduzi inapaswa kuomba radhi kwa hilo na kutafuta njia muafaka wa kufunga ukurasa ule.

6.Sultani naye anapaswa kuomba radhi kwa maovu yote yaliyotokea wakati wa biashara ya Utumwa na utawala wa Kisultani Zanzibar.
 
Kichuguu,

4.Mapinduzi yalikuwa halali kwasababu yalikuwa yakitekeleza azma ya wananchi walio wengi wa Zanzibar ya kumuondoa Sultani. Mapinduzi hayo yalikuwa na lengo la kurudisha heshima ya Wafrika Zanzibar.

tusidanganyane bwana, hiyo heshima ya zanzibar ikowapi ?
 
Kichuguu,
1. Nafasi ya Sultani ilipaswa kufutwa ktk Zanzibar huru. Kigezo kwamba Sultani wa mwaka 1963 alikuwa amezaliwa Zanzibar hakihalalishi kuwepo kwake.

2.Sote tunajua asili ya Usultani ni wapi na ulikuwepo Zanzibar ktk mazingira yapi. Kama waliamua kupiga vita biashara ya utumwa, kwanini waliacha muhimili wake--Sultani?

3.Kusingekuwa na tatizo kama Jamshid angejiunga na chama cha kisiasa kama raia wa kawaida na kugombea uongozi. Nina hakika coalition ya ZNP/ZPPP wangempa hata Uwaziri Mkuu.

4.Mapinduzi yalikuwa halali kwasababu yalikuwa yakitekeleza azma ya wananchi walio wengi wa Zanzibar ya kumuondoa Sultani. Mapinduzi hayo yalikuwa na lengo la kurudisha heshima ya Wafrika Zanzibar.

5.Ni kweli ktk Mapinduzi yale waliuawa wananchi wasiokuwa na hatia. Serikali ya Mapinduzi inapaswa kuomba radhi kwa hilo na kutafuta njia muafaka wa kufunga ukurasa ule.

6.Sultani naye anapaswa kuomba radhi kwa maovu yote yaliyotokea wakati wa biashara ya Utumwa na utawala wa Kisultani Zanzibar.

usidanganywe saana,hata leo siasa ya zanzibar inasema kuna watu wanataka kumrejesha sultani zanzibar.hivi unaamini hili? sultani ni neno ambalo lilitumika na mpaka leo linaendelea kutumika kwa mfumo wa "divide and rule".hata jamshid asingekuwa sultani basi naamini mapinduzi yale yangetokea kwani bado siamini kama mapinduzi yale yalipangwa ndani ya siku 33 baada ya uhuru wa zanzibar. na je sultani alikuwepo miaka mingapi zanzibar? kwanini apinduliwe 1964?na mbona aliepinduliwa ni mzanzibari na mpinduaji ni mganda? na mbona mauaji yaliendelea baada ya mapinduzi kama lengo lilikuwa kumuondoa sultani? na iweje mpaka leo kuna watu waadhibiwe .historia ya zanzibar ni giza na siasa ya zanzibar ni giza, wengi sana wanaendelea kuathirika mpaka leo kupitia historia hiyo kwa kisingizio hicho cha sultani na mwarabu.cha muhimu ni kuirekebisha hii hali,kwani mtanzania asiangaliwe kwa rangi aangaliwe kwa passport na citizenship.
 
....kwani huyo Sultani naye si walimwangalia rangi yake. Kinachotakiwa hapa ni Usuluhishi siyo nani ana haki zaidi.

Binafsi nimeamua kuwasemea upande wa Mapinduzi kwasababu tunajua huku kwenye mtando mumejaa wa-CUF na vibaraka wa Sultani.

Kisasi chenu nyinyi hakiishi. Msipolipiza, basi mtoto atajaribu kulipiza, akishindwa yeye, mjukuu anarithishwa kisasi.

Okello alikwisha shughulikiwa na Iddi Amini, sasa mnataka nini?
 
....kwani huyo Sultani naye si walimwangalia rangi yake. Kinachotakiwa hapa ni Usuluhishi siyo nani ana haki zaidi.

Binafsi nimeamua kuwasemea upande wa Mapinduzi kwasababu tunajua huku kwenye mtando mumejaa wa-CUF na vibaraka wa Sultani.

Kisasi chenu nyinyi hakiishi. Msipolipiza, basi mtoto atajaribu kulipiza, akishindwa yeye, mjukuu anarithishwa kisasi.

Okello alikwisha shughulikiwa na Iddi Amini, sasa mnataka nini?
binafsi yangu sikubaliani na yeyote anaetaka kulipiza kisasi ,ninachotaka ni wazanzibari wawe kitu kimoja kutetea haki zao katika muungano na katika dunia(wasahau yalopita) .baaas.na kuhusu hayo mambo ya vyama ungenijua basi wala usingesemaa maana sina haja na chama cha mtu yeyote ninachojali mimi ni ubinaadamu tu! panapohitajika ubinaadamu.ikiwa chama au ikiwa sultani mie sina habari nao.ninachojali mimi ni kila binadamu apatiwe haki yake.kama maskini tuwe maskini sote au kama matajiri tuwe matajiri sote.tuondoe ubaguzi,tuondoe dhulma,tuondoe unyanyasaji,tusaidie mayatima,tutunze heshima za kinamama na mengineyo,kama vyama tushaviona vingi sana lakini hatujaona lolote la maana,hivyo ninachoongelea mimi siku zote ni mnyonge kutendewa haki,sitaki nitoke nje ya mada,sorry.
 
binafsi yangu sikubaliani na yeyote anaetaka kulipiza kisasi ,ninachotaka ni wazanzibari wawe kitu kimoja kutetea haki zao katika muungano na katika dunia(wasahau yalopita) .baaas.na kuhusu hayo mambo ya vyama ungenijua basi wala usingesemaa maana sina haja na chama cha mtu yeyote ninachojali mimi ni ubinaadamu tu! panapohitajika ubinaadamu.ikiwa chama au ikiwa sultani mie sina habari nao.ninachojali mimi ni kila binadamu apatiwe haki yake.kama maskini tuwe maskini sote au kama matajiri tuwe matajiri sote.tuondoe ubaguzi,tuondoe dhulma,tuondoe unyanyasaji,tusaidie mayatima,tutunze heshima za kinamama na mengineyo,kama vyama tushaviona vingi sana lakini hatujaona lolote la maana,hivyo ninachoongelea mimi siku zote ni mnyonge kutendewa haki,sitaki nitoke nje ya mada,sorry.


...maneno yako yamejaa neema ya u-bin-adam.

...ila dunia sivyo ilivyo!dhambi imezidi!

...watu hubagua hata ndugu zao.

...hiyo ya zanziberi ndo usiseme,haitoisha hiyo dhambi!chuki iko lukuki!

...we serikali mpaka leo yaitwa ya mapinduzi...maana yake unaifahamu weye...hata miye inanitatiza!

...yaani ina maana siku zote ni mapinduzi...sasa mapinduzi yalikuwaje,hilo swali jinginewe!
 
DarsiLamu Na Underage,
Maneno ya underage kweli yana hekima sana- ukiyaangalia kwa undani!
Ingekuwa Mapinduzi ya Uchumi poa! Mbona CCM ni Mapinduzi- (sasa sijua kwa sasa CCM ni mapinduzi gani!!!!!!!!).
Mbona Uganda wana NRM na hata Wabunge juzi tu walikuwa na retreat ana wote walivaa Komabati za Kijeshi?
Huenda Mapinduzi ni jina tu- halimaanishi kuleta chokochoko!
Ila kweli sijui serikali nyingine ya Kimapinduzi ambayo iko mararakani hapa Afrika.
 
....kwani huyo Sultani naye si walimwangalia rangi yake. Kinachotakiwa hapa ni Usuluhishi siyo nani ana haki zaidi.

Binafsi nimeamua kuwasemea upande wa Mapinduzi kwasababu tunajua huku kwenye mtando mumejaa wa-CUF na vibaraka wa Sultani.
Kisasi chenu nyinyi hakiishi. Msipolipiza, basi mtoto atajaribu kulipiza, akishindwa yeye, mjukuu anarithishwa kisasi.

Okello alikwisha shughulikiwa na Iddi Amini, sasa mnataka nini?


Nadhani JokaKuu umekwenda mbali sana hapa. Tunachofanya hapa ni kutafuta ukweli na uhalali wa mapinduzi yale katika msingi wa kihistoria ili kupanua uupeo wetu kuhusiana na mapinduzi yale. Wengi wetu tumekuwa tukiambiwa historia isiyokuwa kamili, hivyo tuna haki ya kutafuta ukamilifu wake kwa njia ya mjadala kama huu. Ubishi kwa msingi wa u-CUF na u-CCM hautusaidii, tafadhali tuendelee kujadiliana kwa kupeana facts tu badala ya kuanza kunyoosheana vidole vya u-CUF na u-CCM.
 
Under_age,
ndugu yangu mimi nakataa kuwa mapinduzi yangekuwepo hata kama Sultan asingekuwepo. Hii inatokana na kwamba mnajaribu kupindisha ukweli kuwa Uhuru wa kwanza wa Zanzibar aliyepewa Utawala ni Sultan. kwa hiyo tutazame kwanza ni nani alikuwa head of the state ambaye alikubalika toka ktk mkutano wa maandalizi ya Uhuru huo huko Lancaster House Uingereza. nani aliyevikwa taji la Utawala Zanzibar ktk Uhuru huo kama sio Sultan!

Kichuguu,
bado nitasisitiza kwamba hata akina Mugabe walipokuwa wakipigania Uhuru wa Rhodesia waliua waafrika wengi kuliko wazungu! Waafrika walokuwa na bega kwa bega na kaburu kama askari, wanajeshi na waajiriwa ma spy wanafiki. South vile vile ukitazama askari walokuwa wakifanyiza zaidi walikuwa weusi pia na kulikuwepo waafrika ktk serikali ya Botha. Yet tunakubali kwamba mapinduzi ya silaha sii solution nzuri lakini ikibidi itumike itatumika, lakini siwezi kukubali kwamba yale mapinduzi hayakuwa halali kwa sababu tu ASP ama CCM wametuweka utumwani tena.... Je, ingekuwa vipi kama tungepata kiongozi kama Mandela badala ya Karume! bado mapiduzi yale yasingekuwa halali?
Nitarudia kusema hata mapinduzi ya kumwondoa Obotte yalishangiliwa na wengi sana bila wananchi wake kufahamu kwamba Idd Amin alikuwa mnyama mwitu alojificha katika ngozi ya kondoo. Sasa kwa sababu Idd Amin alikuwa mnyama hatuwezi kusema ati mapinduzi yake hayakuwa halali!... na Mungu alivyokuwa Mkubwa alimrudisha Obotte yuleyule waliokuwa wakimlilia waingereza na dunia nzima ktk Madaraka... tazama aloyafanya - Unyama mtupu, na karibu afirisi nch kwa muda mfupi sana. Huyu Obotte ndio alimchanganya kabisa Mzee wetu mwl. Nyerere asijue ytena wa kuaminika.
Swala la Muungano pia nitasema ulikuwa lazima kwani tazama mapinsduzi yenyewe ya mapanga na sijui bastola mbili!.. ASP hawakuwa na jeshi wala support yeyote nje zaidi ya Bara na kama utafuatilia sana kuungana huko ndiko kuliko tanguliza kuwaweka ASP na Hizbu kuwa kitu kimoja badala ya kusimamia maslahi ya Sultan ama Washiraz. Huu ndio ulikuwa mpango wa mwalimu kuhakikisha kwamba wananchi wa Zanzibar wanapata protection.
Ni ktk wakati huo huo wafuasi wengi wa Hizbu pia walikimbilia ama kuchukuliwa bara kuondoa hisia za chuki ambazo ziliwahi kujengwa huko nyuma na tazama basi hoja ilobandikwa na mtumwitu kuhusu Sultan utaona kwamba hapa lawama nyingi za Utengano zimepewa Muingereza kwa kuwatenga wananchi kisha report inadai kuwa Muingereza alikuwa akitawala Indirectly kupitia kwa Sultan... Kwa hiyo sii kweli kabisa kuwa Sultan alikuwa sii mtawala kwani hata ukitazama baadhi ya miundombinu, vyuo na kadhalika ilotangulia ilijengwa na Sultan sio Muingereza, siwezi kabisa kusema kitu alichoacha Muingereza Zanzibar zaidi ya magofu ya biashara zake.

Kama alivyosema under age, tuyaache yalopita tugange yaliyopo!... hata leo hii ukinambia kama Zanzibar inahitaji mapinduzi nitasema......YES! mapinduzi ya Tanzania nzima ni Muhimu na halali - lakini sii ya kutumia silaha, unless...
Utajaza mwenyewe.
 
Kama alivyosema under age, tuyaache yalopita tugange yaliyopo!... hata leo hii ukinambia kama Zanzibar inahitaji mapinduzi nitasema......YES! mapinduzi ya Tanzania nzima ni Muhimu na halali - lakini sii ya kutumia silaha, unless...
Utajaza mwenyewe.[/QUOTE]

Mkandara,
Mapinduzi gani hayo- Mbona tayari tuna Chama Cha 'Mapinduzi' na kinatawala kote bara na visiwani miaka 30 sasa?
 
Mapinduzi ya kifikra!...Mapinduzi ambayo yatatanguliza kwanza maslahi ya wananchi mbele ya viongozi na pia kutanguliza Uchumi wetu mbele ya hizi siasa. Wasipokuwa na washabiki hawa jamaa watafunga midomo yao na kusikiliza kwa mara ya kwanza!

Haya ni mapambano makali zaidi ya silaha!... kwanza tufahamu nini haki zetu, malengo ya Uhuru wetu na kisha kutusukuma hadi kukataa Uongizi unaokuja na mbinu za Kifalme!
Kwanza kabisa ni Wazanzibar na wabara wote kwa pamoja kupinga KATIBA ya taifa inayotuendesha leo hii! Kuondoa nguvu na madaraka ya viongozi wasiokuwa na sababu kuwepo kote bara na visiwani.
Zanzibar ifanywe kiungo cha biashara EA kwa kupewa daraja la Free Port. badala ya wafanya biashara wengi wa kiafrika kwenda Dubai tutasema karibu Zanzibar!...
Zao kubwa la Karafuu litajengewa ukuta na kuhakikisha kuwa toka raw hadi finished product inatoka Zanzibar na soko litafutwe kwa udi na Uvumba. Katika mikataba ambayo itawekwa wazi na muhimu ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji ktk Ujenzi wa kiwanda cha matunda ambacho kinaweza kusafirisha hadi nchi za nje. Kituo maalum cha uvuvi ambacho kitakuwa chini ya Union inayotambuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano, samaki ni Utajiri uliolala Zanzibar watu wasisubiri Mungu kumwondoa CCM ama baraza la Mapinduzi.

Wembe wenu mkali na mzidi kumkomalia CCM, ipo siku mtaweza kufanikiwa na hasa kama vyama hivi vinne vitaweza kuungana.
 
Mimi naona kuwa

Mapinduzi yalifofanyika Zanzibar tarehe 12 Januari hayakuwa halali na hayakuwa na ulazima wowote, ila kwa vile yalishatokea hatuwezi kuyafuta. Ni wakati wa serikali kuja mbele na kuwaomba radhi wazanzibar wote waliodhuriwa na mapinduzi yale bila kujali rangi zao. Halafu iwaombe wasahau yaliyopita ili tusonge mbele. Serikali inafanya makosa sana kuchukulia kuwa mapinduzi hayo yalikuwa ya haki; inawezekana ndiyo maana uhasama umeendelea kuwapo baina ya waZanzibari hadi leo kwa vile serikali haijakiri kuwa ilifanya makosa.
 
Mkandara,
Sasa Chama Cha Mapinduzi -tukiiteje? Basi yabidi kibadili jina- kiitwa jina jingine!
Ni mapinduzi ya fikra yale2 aliyoongelea Mwalimu- sema pamoja na Nyerere kujitahidi- hata wakati ule na leo- watu hawakumwelewa kifikra!
Naafikiana na mengi uliyoyasema- ila naona kuna kizazi ambacho hawataki mawazo mapya sana kwa sasa! Changamoto- ni jinsi ya kubadili hizi fikra na kukubali kubadilika!
 
Under_age,

Swala la Muungano pia nitasema ulikuwa lazima kwani tazama mapinsduzi yenyewe ya mapanga na sijui bastola mbili!.. ASP hawakuwa na jeshi wala support yeyote nje zaidi ya Bara na kama utafuatilia sana kuungana huko ndiko kuliko tanguliza kuwaweka ASP na Hizbu kuwa kitu kimoja badala ya kusimamia maslahi ya Sultan ama Washiraz. Huu ndio ulikuwa mpango wa mwalimu


Mkandara,

Suala la kuwa ASP/CCM na HIZBU kuwa ni kitu kimoja baada ya Mapinduzi sidhani kama ni kweli coz mpaka hii leo bado CCM wanawabagua wale wanaowafikiria kuwa ni Mahizbu, mfano mzuri ni wakati wa kutafuta mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005 na nini kilimfika Dr Salim sote tulikuwa ni mashuhuda.

Kwa hiyo kusema kuwa Mapinduzi yaliwaweka wananchi wa Zanzibar pamoja ni uzushi mtupu, ubaguzi hadi hii leo bado upo na ndio huo unaoitwa mpasuko wa kisiasa zanzibar na sababu ya mpasuko huu tusimtafute mchawi - Mapinduzi na matokeo baada ya Mapinduzi ndio sababu kubwa ya mpasuko wa kisiasa Zanzibar.


Suluhisho la mpasuko wa kisiasa Zanzibar ni kuundwa kwa Serikali ya pamoja (mseto) kati ya CCM na CUF na watu kusafisha nyoyo zao na kuvumiliana. Kuhusu hukumu nani kafanya makosa ya kumdhulumu mwenzake katika hayo yanayoitwa Mapinduzi tumuachie M/Mungu yeye ndie mjuzi wa yote yaliyotokea Zanzibar na atahukumu kwa haki baina ya watu.
 
10.3 KUTOKUFAULU MAZUNGUMZO YA MWANZO YA
KATIBA YA UHURU

Baada ya miezi 10 mpaka 11 tokea Serikali ya Muungano wa ZPPP/ZNP
"Serikali Ya Madaraka" kuwa katika mada-raka, Serikali ya Kiingereza ilikubali
baada ya kushikiliwa na serikali hiyo ya madaraka kufanya mkutano wa
mazungumzo ya uhuru. Mkutano huo wa Katiba ya Uhuru ulifanywa ka-
tika miezi ya Machi na April 1962 huko Lancaster House, London. Pande
zote mbili yaani upande wa Serikali na upande wa Upinzani walihudhuria
kwenye mkutano huo. Kwa bakhti mbaya mkutano huo haukuendelea kwa
siku ny-ingi illa ulivunjika bila ya kukubaliana kwa kuwekwa kwa taarikh
ya Uhuru. Waongozi wa Afro-Shirazi walikataa kuzun-gumzwa chochote
kilicho khu-sika na kutolewa taarikh ya Uhuru mpaka kwanza pa-fanywe
uchaguzi mwengine. Baada ya matokeo ya ucha-guzi huo, ndio yafuatie
mazungumzo ya kutolewa kwa taarikh ya Uhuru. Waongozi wa upande wa
Serikali waliwanasihi mwisho wa uwezo wao waongozi wa upande wa Upin-
zani yaani Afro-Shirazi waache ku-leta vizingiti vitavyo sababisha kuchelewa
kwa Uhuru wa Zanzibar. Bali waongozi wa Afro-Shirazi walin'gan'gania uzi
wao huo huo wa kupinga kuzungum-zwa chochote kitacho¯kilia kutolewa
kwa taarikh ya Serikali ya Ndani kabla ya ku-fanywa uchaguzi mwengine.
Waongozi wa upande wa Serikali, walipoona waongozi wa upande wa Up-
inzani hawataki kubadili msimamo wao, walijaribu kuzungumza nao nje
ya mku-tano. Katika mazungumzo hayo, upande wa Serikali waliutaka
upande wa Upinzani wakubali kufanyika serikali ya pamoja, yaani "Gov-
ernment of National Unity" (hii ni mara ya pili ASP kupewa shauri na
wenzao - ZNP/ZPPP kufanya serikali ya pamoja.) Katika serikali hiyo
ya pamoja, upande wa Serikali watawapa ASP wizara tatu kati ya wizara
nane na pia watawapa uwezo wa kutumia "veto" kwa jambo lolote litalo-
tokea nao wakaliona si maslahi kwa upande wao. Yaani ASP watakuwa
na madaraka sawa sawa na ZNP/ZPPP katika uendeshaji wa hiyo serikali
ya pamoja. Waongozi wa Afro-Shirazi baada ya kuyasikia hayo, walitaka
muda wa kuyazungumza na kuyazingatiya wakiwa peke yao, na waliahidi
kutoa uamuzi wao siku ya pili kabla ya kuhudhuria kwenye kikao cha mku-
10.3 KUTOKUFAULU MAZUNGUMZO YA MWANZO YA KATIBA YA UHURU 43
tano wa Katiba. Kwa dalili zote, walionesha kuwa wamevutika na mashauri
hayo, na ilikuwa kuna tamaa kuwa watawa¯k. Upande wa Serikali walin-
gojea kwa hamu na matumainio (pia na wasi wasi) kuwa shauri waliyoitoa
itakubaliwa au sana watataka wazidishiwe wiz-ara moja badala ya tatu ziwe
nne, yaani wawe wao ASP na wizara nne na ZNP/ZPPP wizara nne. Wakati
ulipo¯ka siku ya pili, waongozi wa ASP wakiongozwa na Sheikh Karume
wali¯ka kwa Mawaziri. Walikataa hata kukaa kitako, Karume alisema,
"Tumeyazingatia mashauri yenu. Mazuri! Lakini sisi hatutaki kushirikiana
na nyinyi!" Wakazunguka wakatoka. Kutokana na msimamo huo wa ukoro¯
uliopangwa, waliyoku-wa wakiutumia Afro-Shirazi, Mwenyekiti wa mkutano
huo, Waziri wa Makoloni, aliufunga mku-tano bila ya kuzungumzwa lolote
kukhusu maendeleo ya Katiba. Aliwashukuru wa-jumbe wote kwa kuhud-
huria na aliwataka warejee nyumbani mpaka watapoweza kuwa¯kiana baina
yao, wakati huo Serikali ya Kiingereza itakuwa tayari kufungua tena ma-
zungumzo ya maendeleo ya Katiba. Wajumbe wote wa upande wa Serikali
(isipokuwa Sheikh Ali Muhsin) na wa upande wa Upizani, walirejea Zanz-
ibar bila ya kuwaletea wananchi Uhuru wa nchi yao waliwokuwa wakiun-
gojea kwa hamu kub-wa. Wananchi wa Zanzibar kwa jumla wali-vunjika
moyo na matokeo haya. Baada ya kufuzu hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'
ya Januari 12, 1964, Katibu Mkuu wa Afro-Shirazi, Sheikh Thabit Kombo
alisema wakati akikhu-tubia mkutano wa hadhara mbele ya Makao Makuu
ya Afro-Shirazi, hapo Mapipa ya Ngozi, Kisiwandui:- "Tunamshukuru Mwal-
imu Nyerere kwa kutuvua mtego waliyotaka kutunasa Mahizbu wakati wa
mkutano wa mwanzo wa Katiba, huko Uingereza. Mahizbu walitaka kutu-
fanyia ujanja wa kutaka tuungane pamoja katika kuende-sha serikali na kwa
kutaka kutimiza ujanja wao, walikiri ku-tupa wizara tatu katika serikali
yao. Lakini mzee Karume kabla ya kusema lolote, ali-zungumza na Mwal-
imu kwa simu kumtaka shauri yake juu ya jambo hilo. Mwalimu alimwambia
mzee Karume asikubali kufuata shauri hiyo ya Hizbu kwani huo ni ujanja tu
wakutaka kusiwepo na upinzani. Mkitaka shauri yangu kataeni. Ndipo mzee
alipokataa", alisema Thabit Kombo.
Mara nyingi utamsikia Mwalimu akise-
ma kuwa yeye hakukhusika na lolote ka-tika mizozo ya kisiasa ya Zanzibar.
Hatujui Mwalimu anataka akhusike namna gani zaidi ya hivyo alivyokhusika
(alivyo jikhusisha). Yeye Mwalimu ndiye aliyekiasisi Chama cha Afro-Shirazi
na ni yeye aliyeku-wa, "master mind" katika kuyaandaa hayo yenye kuitwa
'mapinduzi'. Wavamizi walioivamia Serikali ya halali ya Zanzibar wengi wao
wameletwa Zanzibar kutoka katika nchi yake Tanganyika, na huko ndiko wa-
likopewa mafun-zo ya kutumia silaha; na hizo silaha zenyewe zili-toka huko
huko kwake Tanganyika.
Naiwe hakukhusika na ¯sadi zote hizi zilizofanyika
Zanzibar kama adaivyo, bali huo u¯sadi mmoja tu unatosha, nao ni wa huko kuiburura Zanzibar ndani ya huo muungano wake, muungano uhange,
miezi minne tu baada ya kufuzu hayo 'mavamizi' yake. Muungano ambao
leo ni zaidi ya miaka 30 na hapana hata nchi moja za jirani ziliotaka hata



nnaomba ufafanuzi zaidi jee ni kweli Mw Nyerere ndie aliekiasisi chama cha ASP, na yy ndie master mind wa mapinduzi yale?
kuukaribia, licha kujiunga nao. Hili ni janga letu peke yetu!
 
MtuMwitu,
Nyerere alishiriki ktk mapinduzi ya kudai Uhuru wa kweli kwa wananchi wake karibu Afrika nzima hata Mzee Jomo, Obotte wote hawa waliwahi kuzungumza na Nyerere kuhusu Uhuru wa nchi zao.

Haya yote ya Hizbu na ASP hayana maana kabisa ikiwa Uhuru wa mwaka 1963 alikabidhiwa SUltan kama head of the State. Lugha nyingine yoyote ya kutumiwa hapa haiwezi kuleta maana ikiwa Hiizbu walifurahia ushindi wao dhidi ya ASP lakini wakashindwa kumtazama Sultan kwa macho makavu na kumwambia Ufalme wako hauhitajiki tena! For that nawapa mikono yote ASP na Mwl. Nyerere hata kama tumejiingiza ktk janga jingine. Hili janga tuta deal nalo na sasa hivi pamoja na kuwepo miaka 40 vuguvugu la mapinduzi ya kifikra imefika!..Hawana muda mrefu watatia akili kuwa sisi sio tena wale Wadanganyika!

Jembajemba,
Kweli na ndio vita mpya inayotakiwa. Huu ni wakati umefika ambao inabidi tuanze kutazama upya siasa za serikali yetu. Ikiwa wana wabagua hao kina Salim tunataka kuona Salim akipata nafasi ktk vyama vingine kupigania na hata ikibidi awe mgombea binafsi.. acha wananchi wachague nani kiongozi wanayempenda.
 
MtuMwitu,
Nyerere alishiriki ktk mapinduzi ya kudai Uhuru wa kweli kwa wananchi wake karibu Afrika nzima hata Mzee Jomo, Obotte wote hawa waliwahi kuzungumza na Nyerere kuhusu Uhuru wa nchi zao..

mkandara.inategemea na vile neno "uhuru" unavyolitafsiri, kama ni kumuondoa sultani tu,basi nitakubaliana na wewe .lakini kama ni kuwapa wananchi uhuru wa kufanya walitakalo kwa mujibu wa sheria basi nadhani nyerere hilo hakulifanya na acha kulifanya tu bali hata hakukaribia kulifanya.kwa wakati wa nyerere zanzibar kulikuwa na ubaguzi ambao bado utabaki katika historia.kumbuka kwamba kuna wanawake wengi walilazimishwa ndoa mara tu baada ya mapinduzi,kuna walioteswa kutokana na wanavyoonekana,kuna waliopigwa bakora na kuteswa kama kukatwa baadhi ya viungo, mengi hutoyajua mkandara ila nakushauri jaribu kusafiri uende zenji kisha watafute waathirika na jaribu kuwauliza.(nimewaona wengi kwa macho yangu,wala sikuhadithiwa).achana na hapo mara tu baada ya mapinduzi.je unajua kwamba katika utawala wote wa nyerere wananchi wa pemba walidumaishwa kielimu?kimaendeleo?kinadharia?kimadaraka?.na vilipounganishwa tanu na asp hali ndio ilizidi kuvurugika .sipendi sana niizungumzie hii historia kwani nahisi kama kuna mtu atakuja kusoma ninachoandika kisha akute upemba na uunguja katika maelezo yangu jambo ambalo nalichukia sana .nasisitiza kusahau yaliopita na kuanzisha tanzania itakayojali maslahi ya kila upande(tanganyika na zanzibar) na kuanzisha zanzibar itakayojali maslahi ya kila kisiwa(unguja na pemba).binadamu ni binadamu,hivyo vyama vinaundwa na binadamu na wafuasi wake ni binadamu na wanaokufa ni binadamu na wanaodhulumiwa ni binadamu.tusisumbuliwe na utaifa,asili,rangi,lugha.TUTANGULIZENI UBINADAMU KABLA YA UTAIFA.
ni ndugu yenu under_age.
 
Under_age,

sasa naona unamtafuta marehemu Mwl buree kwa mapenzi na ashiki zenu wenyewe!.. Wazanzibar (waunguja)walikuwa na kisasi na waarabu wakiwamezea mate watoto wa kike!.. hakuna sheria yoyote aliyoandika Nyerere kuwaozesha watoto hawa kwa nguvu. NI nyege zenu wenyewe na huyo Karume aliyeanza khabari hizo akiwa mtu mzima!...mbona Sultan alikataza kabisa kwa mwanaume mweusi kumuoa binti wa kiarabu na halizungumzii hili. Ama mwenzangu una rangi.. natania...
Kinachowauma wengi waaarabu ni swala la mweusi kumuao binti wa kiarabu kiarabu! mabinti wetu mliwaoa na hapakuwa na shida tena tuliona sifa na bado ni sifa lakini sio kwa mwarabu yamtokee hayohayo!..Na kwa nini iwe kigezo kikubwa kwenu?.. mbona wengine tumetembe na Wachina, Wajapan, Wazungu na kadhalika nje ya matakwa ya wazazi wao na sijasikia wao kulalamikia Utawala fulani?.

Na sii kweli kabisa kuwa baada ya mapinduzi wananchi wa Pemba walidumaishwa kieleimu. nakumbuka vizuri aloyafanya Seif Sharrif alipokuwa waziri wa Elimu!..nadhani unakumbuka vizuri na scandal ilofuata pale.
Under_age hata kisiwa changu ni kikubwa na pengine kina watu wengi kuliko pemba wakati wote lakini hatukuwa na shule za kutosha! tanzania nzima hatukuwa na shule za kutosha hili sio swala la Pemba.
Nakumbuka wakati wetu kuingia darasa la tisa ilikuwa mbinde! jaribu kuuliza shule za bara ni wanafunzi wangapi waliweza chaguliwa kuingia kidato cha kwanza kama hutakuta wastani ya mwanafunzi mmoja ukipanda sana chini ya 10.

Hili sio swala la Upemba na Uunguja bali ni maslahi ya watu wote kwani zanzibar imejaa wabara, Wangazija na wengine wa kuja kwa hiyo hamuwezi kuleta sheria zenu hali nanyi ni wageni. Zanzibar imesha kombolewa ni jukumu lenu kuiweka ktk hali nzuri kwa kizazi kijacho. Hizi siasa za Uzanzibar na Upemba kusema kweli hazitokani na uzalendo bali ni roho ya kimaskini. Umaskini huja na mengi na moja wapo ni kujenga CHUKI badala ya KIU cha maendeleo.
 
Under_age,

sasa naona unamtafuta marehemu Mwl buree kwa mapenzi na ashiki zenu wenyewe!.. Wazanzibar (waunguja)walikuwa na kisasi na waarabu wakiwamezea mate watoto wa kike!.. hakuna sheria yoyote aliyoandika Nyerere kuwaozesha watoto hawa kwa nguvu. NI nyege zenu wenyewe na huyo Karume aliyeanza khabari hizo akiwa mtu mzima!...mbona Sultan alikataza kabisa kwa mwanaume mweusi kumuoa binti wa kiarabu na halizungumzii hili. Ama mwenzangu una rangi.. natania...

Mkandara,

bwana Mkandara taratibu na maneno yako (ny***).

Bob unaweza kutuwekea ushahidi kuwa sultan alikata mwanaume mweusi kumuoa muarabu?

Kwa sababu kwa mujibu wa historia inaonyesha kuwa hao wafalme wenyewe waliwaowa wanawake wa kiafrika (weusi) tena wengine walikuwa watumwa.
 
Back
Top Bottom